Haijapata kutokea: Ndani ya Miezi 2 mastaa ya mpira duniani wanafurika Tanzania. Hongera Samia wewe ndo Deng Xiaoping wangu

Inaonekana una uelewana uzoefu kwenye hii sekta

Kuanzia mwaka 2007 nimekuwa nikisafiri kutokea KIA.

Maendeleo ya KIA na changamoto zake nazifahamu sana.

Ninafanya biashara ya Utalii,huu ni mwaka 13.

Watalii wengi wanaokuja sasa ni wale walio cancels Safari zao kipindi cha Covid 19.

Utalii Tanzania umekua ukikua mwaka hadi mwaka.Sababu ni hizi.

Mosi mawakali wa utalii duniani wengi hawakujua vivutio vya utalii kwasababu ya siasa zetu na uwekezaji duni.Uwekezaji kuanzia hotel,lodge & camp site ni mkubwa mno.

Pili technology imekuwa msaada mkubwa sana.Huwezi kumdanganya mgeni eti Kilimanjaro ipo Kenya na ikawa kazi rahisi !.Jambo hili zamani liliwezekana sana.

Tatu Mbuga kama Masai mara Kenya imezidiwa na Ujenzi wa Lodge,Hotel & Camp Site ukuwa Serengeti gotogonja ukiitaza Masaimara usiku utafikiri unaangalia Jiji la Nairobi taa na msongamano wa Hotel hali ni tofauti ukiwa Serengeti.
 
Wanaopinga wana sababu hizi

1) Ni Mzanzibari
2) Ni Muislam
3) Ni Jinsia Yake
Kwa uislamu gani wa mke wa mtu kwenda kushikwa shikwa na yule mzungu Peter? Ule ndio uislamu na uzanzibar wake unaouzungumzia au ndio katumia uwanamke wake kunogesha ile filamu yake na Peter?
 
umeshawai ona wakija kwa wingi huu ndani ya muda mfupi kama sasa?

Kwa sasa hasa hao wachezaji huko ulaya msimu umeisha na hivyo ni muda wao wa kula Bata. Usisahau watu walikuwa kwenye lockdown, hii inapelekea wetu kutembea kwa wingi ili kurefresh. Hakuna uhusiano wowote na royal tour. Labda kama mnataka kutumia hiyo royal tour kama sehemu ya kuhadaa umma.
 
Kwa sasa hasa hao wachezaji huko ulaya msimu umeisha na hivyo ni muda wao wa kula Bata. Usisahau watu walikuwa kwenye lockdown, hii inapelekea wetu kutembea kwa wingi ili kurefresh. Hakuna uhusiano wowote na royal tour. Labda kama mnataka kutumia hiyo royal tour kama sehemu ya kuhadaa umma.
kwa nini wasiende kwenu Kenya wanakuja Tanzania?
 
wanadakwaje juu juu wakati wanapost wenyewe kwenye pages zao za social media?

Au unataka waje Nairobi na Narok?

Wanapost picha zao kila waendapo na sio Tanzania tu. Je huko kwingine wanaenda kutokana na royal tour?
 
Ni kama ndoto ila ndo yanatokea kweli! Ndani ya miezi miwili mastaa wa mpira duniani wanaotambulika na kufahamika duniani kote wanamiminika Tanzania kwa fujo sana!

Mastaa hawa wanapiga picha kwenye mbuga zetu za Serengeti na Ngorongoro na maeneo ya Zanzibar na wanazipost kwenye pages zao kwenye mitandao ya kijamii, wanasema wako Tanzania, wanaitangaza Tanzania kwa dunia!

Tanzania tunaingiza madolali sio tu kwa hawa kuja ila kwa namna nchi yetu inavyozidi kuliteka soko la utalii la dunia

Hongera sana Rais wangu mahiri Samia Suluhu Hassan, uongozi ni maarifa, uongozi ni busara , uongozi ni kutumia exposure yako katika kukamata fursa zilizopo duniani. Tanzania sasa inaonekana, watu wanaisema Tanzania, wanaijua Tanzania.

Naiona Tanzania tukifikisha watalii Mil 5 mwaka 2025. Naiona sekta ya Utalii ikiwa kinara tena kwenye kuchangia pato la Taifa na kuingiza fedha za kigeni

Huyo ndo Samia, ninayemuita Deng Xiaoping, The father of modern China. Kwangu Samia ndo" THE MOTHER OF MODERN TANZANIA"

Angalizo
Uzi huu ni ndimu kwa wale vibaraka wa Kenya mnaotaka kuua industry yetu ya Utalii ili Tanzania ife kiuchumi. Naomba mpite tu bila ku comment

Kwa wale pingapinga fc na Burundi gang hii ndo maana halisi ya uongozi uliojaa maarifa! Sijui kama mna swali lingine kuhusu Royal Tour?
View attachment 2272689View attachment 2272693View attachment 2272694View attachment 2272694View attachment 2272696View attachment 2272698View attachment 2272736


I think ww ni mgeni kwenye haya mambo ya utalii, miezi hii ndio uwa wanakuja watu mashughuli wengi kila mwaka

Ukienda huko nungwi ndio utashangaa movies stars kutoka Hollywood walivyojaa
 
Nadhani sijui niseme ni ushamba au upotishaji wa maksudi.

Miaka yote Kanda ya kaskazini miezi hii ndio high season.

Wamekuja kina Abromovic,Beckham,Bill Gate,Oboma & ......... bila hiyo royal tour.

Kabla ya ujio wa Covid 19 KIA zilikuwa zinashuka ndege 17 za mashirika mbali mbali ya kimataifa eg Turkish,Ethiopia,Quatar,Rwanda,Kenya, KLM .......... Israel wamewahi kuleta ndege 6 kwa mara moja na nk.

Royal tour haina lolote na ujio wa watalii Tanganyika.


Tena hawa wote wamefanya booking bfr movie ya Royol Tours so faida ya Ile movie tutaanza kuiona mwakani
 
Hao masupestar huwa wanakuja tu miaka yote, ila safari hii wakitokea tu wanadakww juu kwa juu ili kusaka kiki za kisiasa. Hawajaja kwasababu ya roho tua, bali mnataka kujustfy ile filamu ya Roho Tua kitu ambacho si kweli.

Umeongea ukweli kabisa
 
Back
Top Bottom