Miezi 30 ya Rais Samia madarakani: Pamoja na kujikwaa kwenye Bandari, bado ni Rais mwenye record bora ya kukuza uchumi wa Tanzania kwa kipindi kifupi

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,603
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Unapozungumzia masuala ya kiuchumi, huwa mara zote tunaangalia Zaidi ‘numbers’. Kwenye uchumi hakuhitaji porojo na mihemko. Waweza kumchukia mtu lakini kamwe huwezi kujidanganya kwamba eti hakuna lolote alilofanya, kwasababu namba huwa hazidanganyi.

Lengo haswa la uzi huu ni kuweka record sawa na kuhabarisha umma kuhusiana na mwenendo wa kiuchumi wa nchi yetu na ‘performance’ ya Rais Samia Suluhu kwa miezi hii Takribani thelathini aliyokuwepo madarakani.

Kwa kuangalia takwimu ambazo zinaweza kuthibitishwa na vyanzo mbali mbali, nitagusia performance ya Rais Samia kwenye ‘real sector’ na ‘non-real sector (sekta ya kibenki)’. Nitatumia Zaidi viashiria ‘indicators’ kuelezea mwenendo wa uchumi katika miaka hii miwili ya Rais Samia na kufananisha na miaka Zaidi ya kumi iliyopita.

1. Sekta ya ajira
Kwa miaka miwili iliyopita, kuna mabadiliko makubwa sana yametokea kwenye suala la ajira – kote kote kwenye sekta binafsi na ya umma, kuna ajira nyingi sana zimetengenezwa. Mimi binafsi kwa miaka miwili iliyopita nimebadili ajira mara mbili. Mke wangu alikuwa Jobless tangu amalize chuo 2016 ila kwa huu mwaka ameambulia nafasi ya kazi.

Ukitaka kuthibitisha hili suala la ajira kwenye kipindi cha Rais Samia, kuna uzi hapa Jamii Forum unaitwa Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini? huu uzi umekuwa maarufu tangu kuanzishwa kwake tarehe 26 July 2022 na umekuwa ni uzi ambao upo active sana hususani kwa wale wanaotafuta ajira za serikalini, na kwa udadisi wangu uzi umekuwa upo active kwa muda wote ukienda sambamba na trend ya ajira za serikalini jinsi zinavyotoka. Mpaka ninavoandika sasa, uzi huu umeshapata views karibu ‘2 Millions’ pamoja na comment ‘39k’ Na hiyo haijawahi kutokea kwa kipindi cha miaka takribani kumi iliyopita.

Kwenye upande wa ajira za private sector nako hakukua vibaya, ajira zimetangazwa nyingi sana na ukitaka ku prove hilo angalia sites za ajira kwa hii miaka ukifananisha na kipindi kile cha ‘uchumi kilema’ hali ilivokuwa, watu walikaa miaka 5 bila kuhudhuria hata interview moja.

2. Sekta ya viwanda
Ukiangalia viashiria vya takwimu kwa upande wa sekta ya viwanda, ni wazi kumekuwa na ongezeko la haraka kwa muda wa miaka miwili iliyopita. Mfano kwa takwimu zilizokuwepo za uzalishaji wa Cement nchini pamoja na ujazo wa gesi zinazotumika viwandani, inakuonesha kabisa mwaka 2021, 2022, na miezi michache ya mwaka 2023, vinaonesha ongezeko la haraka ukilinganisha na kipindi kabla ya hapo.

1. Cement consumption.JPG


Hapo kwenye cement consumption, pamoja na kuwa kwamba ni kiashiria kinachoonesha kuendelea kupanuka kwa viwanda vya uzalishaji wa cement nchini, pia inaakisi Zaidi pia hali ya soko la ununuzi wa Cement. Na hapa unawazungumzia Zaidi walaji wa Cement ambao Zaidi ni wananchi na serikali. Maana yake ki nadharia, kama kunakuwa na ongezeko la uzalishaji wa Cement, pia inaonesha hali iliyopo kwenye sekta ya ujenzi, na hii inaweza kukuambia kuwa, sekta ya ujenzi na yenyewe inaenda ikipanuka.

Sasa huwezi kuwa na kupanuka kwa sekta ya ujenzi kusikoendana na kuboreka kwa hali ya uchumi.

2. Industries Gas Consumption.JPG


3. Monthly Gas Consumption.JPG


Kiuchumi, unavokuwa na trend inayoongezeka kwenye viashiria kama vilivyotumika hapo juu, maana yake ni kwamba kumekuwa na ongezeko la shughuli za uzalishaji. Mfano mdogo tu, kama wewe ni mama ntilie na kipindi cha nyuma ulikuwa ukiweka mkaa wa elfu moja kwa sababu ulikuwa unahudumia wateja watano kila siku, endapo tukiona kwamba sasa unaanza kutumia mkaa wa elfu nne, ni wazi kwamba utakuwa umeongeza idadi ya wateja.

Hiyo ndio mantiki haswa ya kuangalia viashiria na mwenendo wa uchumi.

3. Sekta ya usafirishaji
Ukiangalia zama za Kikwete kwa miaka 5 ya mwisho sekta ya usafirishaji (Transit - Freight Business) iliweza ku generate kutoka wastani wa USD 40 Million mpaka USD 60 Million kwa mwezi (USD 20 Million gain in 5 Years). Magufuli akatutoa kutoka wastani wa USD 60 Million kwa mwezi mpaka 100 Million (USD 40 Million gain in 5 years). Samia ametutoa kutoka USD 100 Million mpaka kufikia range ya USD 150 Million – 160 Million (Ongezeko la Zaidi ya USD 50 Million in 2 Years).
5. Usafirishaji mwezi.JPG


4. Mfumuko wa bei
Hapa Rais Samia emeendeleza legacy ya Rais Magufuli, ambayo kwa kipindi chake mfumuko wa bei uliweza kudhibitiwa. Ila tofauti kubwa ya kudhibitiwa kwa mfumuko wa bei wa kipindi cha Rais Magufuli na hiki cha Rais Samia ni kwamba, wakati wa Magufuli, mfumuko wa bei ulidhibitiwa lakini hakukuwa na ongezeko kubwa la Money Supply (ujazo wa fedha kwenye uchumi), wakati kwa Rais Samia, mfumuko wa bei umedhibitiwa wakati at the same time, kuna ongezeko kubwa la ujazo wa fedha kwenye uchumi.

6. Inflation.JPG


Hiyo maana yake inampa credit Zaidi Rais Samia, kwasababu kiuchumi tulitegemea Money Supply ikiongezeka kwa kasi basi, mfumuko wa bei nao ungeongezeka kwa kasi, ila kwa hichi kipindi cha Rais Samia bado haijawaha hivo. Ukiangalia kwa sasa, monthly reported inflation ipo below 5% ambayo BOT wanasema ndo target rate yao ya inflation, ila credit growth kwa miezi 12 iliyopita nadhani ipo above 18% kitu ambacho ni maajabu.

Na penginepo nadhani hii ndo sababu kubwa ni kwanini Benki Kuu bado wameacha policy rate iwe chini, japo mimi mtizamo wangu ni kwamba policy rates inatakiwa kuwa juu kidogo ya level iliyokuwepo kwa sasa.


Hatari pekee ninayoiona kwenye mfumuko wa bei ni madhara ya kupandisha bei ya mafuta kusikoendana na bei iliyopo duniani. Na hii nimeshaiweka wazi kwenye huu uzi ambapo kwa kweli mpaka sasa sijui ni kwanini EWURA na Makamba wamechukua uamuzi wa ajabu kiasi kile Makamba na genge lake wamekurupuka kwenye bei ya mafuta, na benki kuu nao wapo kwenye usingizi wa pono


5. Sekta ya kibenki na ujazo wa fedha kwenye uchumi
Sekta ya kibenki au masuala ya mikopo ndo kichocheo kikubwa cha kuongezeka kwa ujazo wa fedha kwenye uchumi au ‘Money supply’.

Kwa hii miaka miwili ya Rais Samia, hakujawahi kuwa na performance ya kibenki niliyoishuhudia kwa nchi ya Tanzania, haswa haswa ya mwaka 2022. Kipindi cha Kikwete, mwaka 2014 Pia ulikuwa na performance ya kibenki inayokaribiana na hii, lakini hii ya Rais Samia imevuka.

Nadhani ukuaji wa sekta ya kibenki na ujazo wa fedha kwenye uchumi ambao mimi huwa napenda kuiita hii sekta ya kibenki kwamba ni ‘non – real sector’ ni kiashiria pia kwamba growth tuliyoiona kwenye real sector ni valid. Yaani kwa maana nyingine, unavokuwa na growth kwenye monetary variables kama credit growth, money supply, currency in circulation, hiyo ni validation kwamba kuna mambo yanatendeka kwenye ‘real-economy’ ya viwanda, kilimo, na biashara.

Ndo maana pia utaona ya kwamba sekta ya kibenki ilivopitia uchungu kipindi cha Rais Magufuli hususani mwaka 2017, hali ya private sector na real economy pia ilikuwa taabani.

8. Private sector credit.JPG


Ukiangalia level ya credit au mikopo kwa sekta binafsi kuanzia mwaka 2000 mpaka June 2023, unaweza kuona ni mlima ambao una slope au miinuko tofauti tofauti. Bila kuzama kwenye technicality zozote za kiuchumi, kwa kuangalia kwa macho ni wazi kwamba kwa miaka miwili ya Rais Samia, unaweza kuona muinuko ulivokuwa mkali.

Tukia assume kama huu ni mlima, na tupo kwenye mbio za kupanda mlima, ni wazi kwamba kipindi cha Mkapa miaka ya 2000 mpaka 2005 mlima ungekuwa ni rahisi kupanda kwasababu ni kipindi ambacho watanzania wengi walikuwa na tongotongo na uchumi haukuwa complicated.

Kipindi cha JK kama kinavyojionesha hapo (kulikuwa na growth ya kama ya 17 Trillion kwa miaka 10) na slope ya mlima ilikuwa kali kuonesha hali ya kibenki na money supply ilikuwa kwa trend nzuri.

Magufuli era, kama inavoonekana kwenye picha (credit growth ya almost 3 Trillion in 5 Year) na hata slope ya mlima ilikuwa almost flat.

Samia era, unaweza kuona hali ya mikopo ilivokuwa a very steep slope ambayo haijawahi kuonekana. (credit growth ya almost 9 Trillion ndani ya miaka 2). Na hata ukiona slope ya mlima, ni wazi kwamba ingekuwa ngumu sana kuupanda huu mlima.

Mzunguko wa fedha

Hapa pia unaweza kuona ni namna gani Rais Samia anaweza kufananishwa na wengine.

9. Currency in circulation.JPG


10. net increase in currency in circulation.JPG


11. change in currency in circulation.jpg


All in all, performance bado kwa kuangalia namba bado inambeba rais Samia.

Hatari ninayoiona kwenye uchumi kwa sasa
Hatari pekee ninayoiona kwenye uchumi kwa kipindi hichi ni issue ya kuadimika kwa dola ambayo imepelekea bei ya dola dhidi ya shilingi kupanda thamani kwa haraka hususani kuanzia huu mwaka uanze. Na hii imepelekea shilingi kupoteza thamani kwa karibu asilimia saba tangu mwaka uanze.

dola.JPG


Madhara ya hichi kitu ni kwamba kitasababisha cost of importation kwenda juu, na kwasababu Tanzania bado ni nchi tegemezi kwenye importation, kutaweza kuwa na mabadiliko ya shughuli za kiuchumi kwenye real sectors, kitu ambacho kitapelekea baadhi ya matokeo mazuri yaliyoonekana kwenye uchumi kuanza kudorora, hususani kwenye sekta ya viwanda na pia kwenye biashara.

Pia kunaweza kuwa na pressure ya bei za vitu kuanza kuongezeka kiholela, vile vitu ambavyo huagizwa nje ya nchi.

Kwa nadharia za kiuchumi, kudhibiti kuporomoka thamani kwa shilingi na kupanda haraka kwa bei ya dola, itabidi benki kuu ya Tanzania iangalie namna ya kupunguza money supply kwenye uchumi, japo hii itakuwa na madhara hasi kwenye ukuaji wa uchumi, lakini inaonekana ndio maamuzi muhimu ya kuchukua ili kuinusuru shilingi.

Hapo juu nilisema kwamba, kwa miezi ya hivi karibuni, Tanzania imekuwa na ongezeko la money supply ambalo halijawahi kushuhudiwa, ambayo kwa kiasi kikubwa imechochewa na ongezeko la kasi la utoaji wa mikopo kwa upande wa benki za kibiashara.

Kwenye dhana ya kiuchumi ya monetarists, kwakuwa kwa dunia ya sasa, dola ya Marekani inachukuliwa kama bidhaa, unavokuwa na ongezeko la haraka la ujazo wa fedha katika nchi yako, maana yake, itasababisha mahitaji ya dola kuongezeka, kitu ambacho ndio naona kimetokea Tanzania. Kwamba ‘too much shillings chasing few dollars’ na ndo maana tunaona outcome ya kupanda haraka kwa bei ya dola.

Ushauri na matazamio yangu kwa serikali na benki kuu ili kuilinda shilingi kwenye hatari
Hivyo kwa matazamio yangu, na kwa hali ya uchumi ilivo kwa sasa – ambao ni strong kwa viashiria vingi, nategemea kabisa benki kuu wafikirie suala la kuongeza kiwango cha riba. Na hii nadhani ni hatua ilipaswa kuchukuliwa miezi karibu miezi saba iliyopita.

7. Interest rate.JPG


Ukiangalia wastani viwango vya riba ya ukopeshaji na policy rate (Discount rate) ya benki kuu, utagundua ya kwamba, mebenki ya kibiashara yameweza kuvuna faida kubwa sana kwasababu gharama zao za kununua pesa ni ndogo sana wakati wao gharama zao za kukopesha almost zimebaki zile zile.

Hili suala nilijaribu kulizungumzia kwenye uzi wangu wa kumpongeza gavana mpya wa benki kuu mnamo January ya huu mwaka <<Mitihani mikuu mitano kwa gavana mpya wa BOT – Emmanuel Tutuba>> lakini sioni kama ni kitu ambacho kinamulikwa kwa jicho la tatu.

Na ndio maana ukiangalia hiyo chart ya interest rate landscape, utaona ya kwamba, sasahivi kuna gap kubwa kati ya lending rates na policy rates’ maana yake ni kwamba mabenki yanapata pesa kwa unafuu na wanakopesha kwa bei kubwa. Na hii ndio sababu haswa ongezeko kubwa la faida za mabenki kwa mwaka 2022 (abnormal profits).

Na kwenye hili ukiangalia mfano mdogo wa benki za NMB na CRDB kama sample ya benki zote nchini. Kwa mwaka 2022 benki ya CRDB ilitengeneza faida ya bilioni 351 ikiwa ni ongezeko la asilimia 30 kutoka faida ya bilioni 268 mwaka 2021. Upande wa NMB, yenyewe mwaka 2022 ilitengeneza faida ya bilioni 429 ambayo ni ongezeko la asilimia 47 kutoka faida ya bilioni 292 kwa mwaka 2021. (Hiyo ndiyo tafsiri ya abnormal profits kwa mabanki).

Kama nilivosema hapo juu, benki au taasisi za kifedha, sio ‘real sector’, hizi huwa tunaziita intermediaries, yaani vipo hapo kurahisisha operation ya real sector kama kilimo, viwanda, na biashara.

Kwahiyo unavokuwa na mebenki ambayo yanatengeneza mabilioni ya faida kutokana na low rates kama ilivokuwa faida za benki nyingi kwa mwaka 2022, maana yake hilo tayari ni tatizo kwenye uchumi. Kwa trend, banks are overly lending, yaani sasa wanakopesha kupita kiasi which good kwa sababu real economy kweli nayo inakuwa, lakini is also bad, kwasababu kwenye ongezeko hili kubwa la mikopo ambalo lipo kwa sasahivi, huwa kunakuwa pia na viashiria vya mikopo chechefu ambayo nayo pia ni mibaya kwenye uchumi.

Na hiyo ndio dhana ya ni kwanini huwa inabidi benki kuu kufanya ‘policy tightening’ wakati kunavokuwa na ukuaji wa uchumi wa haraka. Ni kama vile unavokuwa unaendesha gari, ukiwa kwenye mteremko mkali, lazima kuna point Fulani utakuwa unashika breki, kwa maana ya kwamba usipofanya hivo unaongeza hatari ya kupata ajali. It works the same way even in economics.

Hata wana falsafa wanakuambia, ukiona kila kitu kinakuendea vizuri kwenye maisha, usifurahi sana kupitiliza, kuwa na fikra ya ambacho kinaweza kukuendea kombo. Na huo ndio muongozo wa kufanya maamuzi yenye busara.

Hitimisho
Kwahiyo ukiniiuliza mimi kwa darubini yangu ya hawa marais kwa jicho la kiuchumi, naweza kusema kwamba Rais Samia amekuwa na record safi sana ya kiuchumi ikifuatiwa kwa karibu na Rais Jakaya Kikwete, na Magufuli.

Sijamuweka Rais Mkapa kwakuwa kwa kipindi chake watanzania walikuwa ni kama bado wana tongotongo usoni, na ni kipindi ambacho taasisi nyingi na mifumo ya kiuchumi ilikuwa bado haijakaa kwenye reli.

Vivo hivyo upande wa Magufuli pia, japo hakuwa mzuri kwenye sekta binafsi ambao ndo ukweli, ila Magufuli kuna kitu ameongeza kwenye tasnia ya uongozi Tanzania. Magufuli ametufunulia kwenye issue ya ‘tactical infrastructures’ na issue nzima ya ‘nationalism’ ambayo mimi naamini hayo mambo mawili kama yakiwekewa sera murua, yatakuwa chachu kwa uchumi wa Tanzania kwa miongo inayokuja.

Hapo kwenye kuendeleza legacy ya Magufuli kwenye tactical infrastructures, Rais Samia anaonesha pia mfano mzuri kwa vitendo. Ila kwenye issue nzima ya ‘nationalism’ au kupigania rasilimali za nchi hili ndo eneo ambalo naona Rais Samia anataka kukwama kitu ambacho kinaweza kuathiri performance ya uchumi in the long run.

Wasalaaam

N. Mushi.
 
Back
Top Bottom