Godbless Lema avuliwa ubunge

Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
Baadhi ya picha za matukio yanayoendelea hapa Arusha kufatia kuvuliwa ubunge Kamanda Godbless Lema. IMG_0794.JPG IMG_0788.JPG IMG_0787.JPG IMG_0781.JPG IMG_0773.JPG





IMG_0770.JPG IMG_0765.JPG
IMG_0764.JPG
 
Ndiyo Lema amevuliwa ubunge,ndiyo amekutwa na hatia,ndiyo jaji ametumiwa na akatumika na chama cha kina Livingston Lusinde.Kwa mara nyingine tena mahakama zetu zimedhihilisha kuwa bado zipo kaktika ile minyororo ya CCM.Aliyekashifiwa hakuona kama amekashifiwa lakini kada mfu aliumia sana kwanini mgombea wake amekashifiwa. Dr.Burian alijua asingeshinda ndiyo maana hata mahakama ilipo mhitaji mahakamani mawakili wake walijenga hoja dhaifu kuwa anajaza form za ubalozi huko kenya.
Lakini taarifa zilizo chini ya kapeti zinasema mkulu hakuwa anafurahishwa na jiji la Arusha kuwa mikononi mwa CHADEMA hivyo amri imetolewa katika hatua za mwisho kabisa kumtaka jaji atoe hukumu ya kutengua ubunge wa Lema. Na mawasiliano yamekuwa ya kifanywa na mkuu wa mkoa wa Arusha bwana Magesa.
Lakini CCM wameshindwa kufahamu kuwa ni kiasi gani fedha za walipa kodi zitakavyotekea kwa uchaguzi wa ARUSHA. Mimi siyo mtabiri lakini naona kwambali vifo vya wananchi wa Arusha n a hapa ndipo ninaumia sana.Ndiyo huenda CCM wakalazimisha ushindi kwa mgombea wao(Kama Shinyanga).
Lakini ifahamike wazi kuwa Arusha siyo kama SHINYANGA. Arusha kuna watu jasiri,kuna watu wanaojitambua,kuna watu huru. Kwa mara nyingine CCM inakwenda kuaibika tena na CHADEMA inakwenda kuwa imara mara dufu mkoani Arusha na kaskazini kwa ujumla. Ndugu zangua wapenda Mabadiliko lazima tujipange kuhakikisha Lema anarudi tena kwa kishindo.

Jambo la faraja nikuwa hadi mda huu hakuna mwanaCCM mwenye ushawishi Mkoani Arusha kufikia hatua ya kumtisha Lema... PEOPLES POWER
 
Nafikiria hivyo pia. Sidhana kama CCM ni wajinga kiasi hicho. Either walalamikaji watakata rufaa kuomba Lema asigombee tena kama njia ya ku-delay uchaguzi. Au Wanaweza kumwacha Lema agombee tena halafu CCM watoe pingamizi. Au wanaweza kuchelewesha uchaguzi kwa njia yoyote ile.

CCM ni chama cha wahuni,wajinga,mazezeta,mafisadi na majambazi waliokubuhu.
Hayo yote yanawezekana maana wao ndiyo wameshika makali. Wanaweza kuchelewesha Uchaguzi kwa kudai kuwa hawana fedha za kuendeshea Uchaguzi mdogo wa Jimbo hili au wakaweka pingamizi pindi Lema atakapoamua kugombea tena. Ilimradi tu ni hujuma za kutaka kumkomoa Lema na CHADEMA.

Mpaka sasa kuna kesi nyingi tu za kupinga Ubunge wa Wabunge wa CDM sehemu mbalimbali nchini na inaelekea kuwa Mahakama zimepewa maelekezo maalumu na Serikali ya Magamba kutengua Ubunge wowote wa CHADEMA ulioko Mahakamani! Yote hii ni kujaribu kupunguza idadi ya Wabunge wa CDM Bungeni na hivyo kutaka kudhoofisha nguvu ya CDM ndani na nje ya Bunge. Huo ndo mpango kamili.

CDM lazima ichukue hatua za kimkakati kuzuia ujinga huu.Vinginevo mpaka 2015 Wabunge wa CDM wanaweza kuwa wamepunguzwa zaidi ya nusu na hakutakuwa na kurudia Chaguzi hizo kwa kisingizio cha ukata wa Serikali which is not true. Wanaweza kuruhusu chaguzi kurudiwa pale tu ambapo wana uhakika wa KUSHINDA KWA KUIBA KURA na si vinginevo.
 
Mahakama kuu kanda ya Arusha imetengua matokeo ya ubunge. Source TBC.

Mkuu tangu saa nne kasoro watu tuna information humu JF kabla ya Blog zingine.. Next time pitia post kabla ya kupost information...
 
Walete uchaguzi mdogo angalau hizo bilioni 4 zitasaidia kutuongezea kamzunguko ka hela hapa na kupunguza umaskini japo kiduchu. Tutapata wateja wa soda, maji ya kunywa, michemsho, mitura, guest houses, na hata dada poa pale Shivers. Mshkaji wa Raha Promotions atapata tenda ya matangazo ya kampeni na wapangaji wetu watapata pesa ya kutulipa kodi ya pango. Tutauza nyama choma kwa wingi (hizo wapambe watakazokuwa wanahonga wapiga kura tangu kwenye kura za maoni), waarusha watapata soko la mbuzi wao. Wapambe watapata pesa za kumalizia nyumba zao Moshono, kambi ya chupa, Kwa Mromboo nk, na vijana wetu watapata kazi za ujenzi. Na kadhalika na kadhalika. Asanteni kwa uchaguzi huu mdogo mnaotuletea.
 
Haki ya mtu haipotei.
Mungu atawapigania watu wa ARUSHA!
 
MMMMMMMhhhh kwa style hii maamuzi mengine ya mahakama yanaitaji busara sana na sio ushabiki,hiki ni kiberiti cha gesi kinachezewa kwenye kituo cha mafuta ya petrol tena super.Hiyo ni hala hala kidole na jicho zinabaki ni busara za CDM walipo nadhani wanasali CDM isibadilishe mawazo
 
duh....
Wananchi wanataka kujua nini hatma ya Lema na jimbo lake?//
 
Safi sana sioi aje ajaribu bahati yake hapa!asikate tamaa apambane!anaweza kupata

Wa Arusha siyo mazezeta wa kuchagua mkimbizi na domo zege kama huyo magamba,Arusha town ni ya machalii na wanataka pure hip hop aka chalii mwenzao kama lema na siyo mbana pua kama sioi au magamba yeyote!.
 
Kaka asante sana. Waache CCM wacheke sasa hivi, na sisi tutacheke hivi kalibuni. Ya Meru ni cha mtoto. CCM hawakufikiri kawa kawaida yao na kipigo watakachokipata kama kura itarudiwa basi patachimbika CCM
 
Tunataka haki pia itendeke kwenye kesi ya jimbo la Segerea maana ushahidi upo wazi kuwa Mahanga wa CCM hakushinda kihalali,wakitoa hukumu ya kweli ndo nitakuwa na imani na mahakama zetu.I mheshimiwa Lema kaonewa,ila Mungu yu pamoja naye hata uchaguzi ukirudiwa CHADEMA watalichukua tena hilo jimbo.
 
Hiyo delay tactic watakayotumia CCM sijui wataitumia kwa muda gani.
 
wanacho fanya ni kumpiga chura teke tuu, ccm chalii, na ndo haita inuka teeena
 
Hii ni nafasi nyingine nzuri ya kuudhihirishia umma wa watanzania kuwa cdma ni moto wa kuotea mbali
 
Serikali ya tanzania inatakiwa iwaonee hurumu watanzania wanaolala njaa ili kulipia kodi ambazo wanaamini zitapelekea maendeleo ya nnchi yao,kurudi uchaguzi ni gharama kubwa sana na ni mzigo mkubwa kwa watanzania ambao ni walipa kodi! poleni CHADEMA lakini ninaamini jimbo bado ni la CHADEMA kwa kuwa watu wa arusha wana imani kubwa sana kwa MR LEMA
 
I wish ningekuwepo jamani hapoo

hali ni shwari....mji upo salama.....polisi ndio wanazungukazunguka sijui wana kizunguzungu......ila hakuna mtu anafanya fujo wala anaetaka kufanya fujo.......tunaamini mbunge wetu yupo likizo ya muda......
Tutakutana battle field....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom