(PICHA) Lowassa atua Arumeru kwa kishindo: Chadema waparaganyika

busar

JF-Expert Member
Dec 22, 2011
1,068
1,061
Wenye taarifa tupeni, tujuzuzeni Kama kamanda wetu yupo ndani ya meru?
 
Nilikuwa sijui kama Lowassa nae ni Comrade / Kamanda!
Hata mimi mkuu,
Comrade ni mpiganaji asiye na makundi wala makuu
Mpiganaji wa principles za kuwaokoa wanyonge
Mpiganaji aliyeweka maisha Yake rehani kwa ajili ya haki ya umma
Mpiganaji anaye amini katika haki zote za usawa na kukomesha dhuluma kwa masikini
Mpiganaji anyegawa chochote alichonacho kwa ajili ya wapiganaji wenziwe ili kutimiza lengo la umoja, usawa na maendeleo ya wote.

Simuoni Lowassa katika kundi hilo.
Lowassa ni tajiri
Hive kuna kitabu chochote cha kuelezea filosofia ya Lowassa?
 
Huyo ni mbipi,akipanda jukwaani leo hata kura 2000 za sioi zitapungua.LEMA anamsubiri kwa hamu
 
Kifupi ni kwamba anaenda kuwaharibia ccm! Ni mtu mchafu ambaye hawezi kusafishwa! Ni kama mavi yanayopuliziwa pafyumu! Anaenda kuchafua hali ya hewa na kukamilisha anguko la ccm huko.

Wakati eneo analofanyia mkutano leo, yaani Kikatiti, hakuna maji kabisa, Lowasa akiwa waziri wa maji aliyakusanya maji huko Meru na kujenga bomba kubwa kuyapeleka Monduli huku wananchi wa vijiji vya Meru hawaruhusiwi hata kulisogelea.

Wakazi wa Meru ambao walitaka Sarakikya akawawakilishe bungeni, EL alitumia jeuri ya fedha kuhakikisha anampitisha Mkwe wake kwenda kumuongezea mtandao wake!

Nitakuwepo mkutanoni Kikatiti kusikiliza tutaelezwa nini na fisadi huyu, akiwa na Mtoto aliyezunguka nchi nzima akimwita gamba huku akisisitiza kwamba lazima ajiondoe kwenye nyazifa za chama! Wakati wanaccm wakisubiri ajiondoe, leo watamwona akimsaidia mkwewe aingie!

Yangu macho!?
 
Hapa ndipo CCM inanichekesha kiasi cha kuhatarisha usalama wa mbavu zangu. Yaani wamekaa na kuamua kumtumia Lowassa kumpigia kampeni mkwewe Sioi! Hiyo haitoshi huyu ndiye kwenye vikao vya juu vya chama ametakiwa kujiondoa kwa hiari yake leo wanampa jukumu la kukipigania chama! Hakika ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni .... hapa kuna firauni ingawa nashindwa kujua ni nani hasa!
 
Open picha hii hapa kuona kinachoendelea arumeru
 

Attachments

  • 548074_2907954614869_1140685357_32122931_83426049_n.jpg
    548074_2907954614869_1140685357_32122931_83426049_n.jpg
    18 KB · Views: 463
safi sana mkuu endelea kutupa taarifa .
Mkuu, we umefika Arusha na mafuriko ya uchaguzi wa Arumeru!
Utaondoka, utatuacha na bahati mbaya utakuwa mpole sana siku ya kupanda saibaba pale stendi ya CHAWOTE!
 
Back
Top Bottom