Lema akiongea na radio one.."nimepigikiwa simu tangu jana kuhusu uamuzi huu...na hata H.Mdee amenitaarifu mapema asubuhi kuwa amepata habari kwa mtu nyeti kuwa nimeshindwa kesi...polisi wamezingira ofisi ya mbunge alfajiri na hata mahakamani kabla ya uamuzi hii inaonyesha ilishapangwa...makamba aliongea na mtu wa ccm kumtaarifu ajiandae kwa kura za maoni....hata wakirudia uchaguzi bado nitashinda...nasubiri tamko la chama ndio niwajuze wananchi nini cha kufanya".
Wilbrod Slaa
We shall overcome.!
LikeUnlike · · @wilbrodslaa on Twitter · 21 minutes ago via Twitter ·![]()
Pole Lema.
Pole CHADEMA.
Kwa wanaotaka kufahamu, Jaji Rwakibarila hakunadika Hukumu ya kesi hii; imeandikwa na Dr. Masumbuko Lamwai. Chadema wakitaka kuzuia mvua hii ya Mahakama kutoa ushindi CCM, basi mkakati wao unapaswa kumshughulikia Lamwai. Majimbo mengine ambayo matokeo ya uchagzi yatatenguliwa ni Ubungo, siyo Segerea.
Hivi ccm watamsimamisha nani Arusha ashinde?
Hii nimeipenda .
Mh.Lema pamoja na Chadema Makao Makuu hakuna kukata rufaa.Waacha uchaguzi ufanyike August 2012.Muhimu kuanda timu nzuri ya Kampeni na pia kudai marekebisho katika daftari la wapiga kura ili vijana waliofikia umri wa 18yrs baada ya 2010 nao wapate haki ya kupiga kura.Katika hili inafaa kuwa andikisha kata hadi kata vijana wote ambao wamefikia umri wa kupiga kura na kufungua madai katika tume ya Uchaguzi mapema kabla ya muda wa Kampeni
dats a heroic decision he has made..Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupitia CHADEMA, amepoteza kiti hicho kwa kuenguliwa na Mahakama katika kesi iliyokuwa inamkabili ya kupinga ubunge wake.Kesi hiyo iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Mollel (44) ambao walikuwa wanamtuhumu Mbunge huyo kwa kutoa kauli za udhalilishaji, matusi na kashifa kwa aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Dkt. Batilda Buriani.Hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila.Katika hukumu hiyo, Lema hakuondolewa haki ya kugombea ubunge huo kwa kuwa kosa lililomtia hatiani ni matumizi mabaya ya lugha tofauti na ilivyodhaniwa kuwa ni vitendo vya rushwa. Uamuzi wa kugombea ama kutokugombea kiti hicho tena utatokana na maamuzi yake mwenyewe na ridhaa ya chama chake ikiwa kitamteua na kumpitisha kugombea.Taarifa za watu wa karibu zinasema kuwa Lema hatakata rufaa mahakamani juu ya hukumu ya kesi hiyo, bali atakata rufaa kupitia kura ya wananchi wa Arusha Mjini wakati wa kugombea kiti hicho. Hivyo tutarajie uchaguzi mpya ndani ya siku 90. Tanzania, nchi ya uchaguzi kila uchao...!
Mnafikiri mtashinda uchaguzi wa marudio!! Mnapoteza muda tu...
Ooh no!
Lakini tukumbuke kwamba, hizi ndio harakati za ukombozi, zinakuwa na njia ngumu sana na zenye maumivu makali hata wakati mwingine umwagaji wa damu.
Mwaka huu naona kama mapambano ya ukombozi wa kweli wa Tanzania ndio yameziduliwa rasmi na CDM.
Naomba sana CDM isije kukata rufaa, kwani kufanya hivyo mahakama hizi za magamba zitatumia delaying tacts ili uchaguzi usirudiwe.
Aibu kubwa kuliko ie ya ARMR inakuja kwa ccm.
Aluta continua!!
Hii nimeipenda .
Mh.Lema pamoja na Chadema Makao Makuu hakuna kukata rufaa.Waacha uchaguzi ufanyike August 2012.Muhimu kuanda timu nzuri ya Kampeni na pia kudai marekebisho katika daftari la wapiga kura ili vijana waliofikia umri wa 18yrs baada ya 2010 nao wapate haki ya kupiga kura.Katika hili inafaa kuwa andikisha kata hadi kata vijana wote ambao wamefikia umri wa kupiga kura na kufungua madai katika tume ya Uchaguzi mapema kabla ya muda wa Kampeni
kaka n ya upendeleo mwanzo mwisho!NA Kifup Tuwaonee Huruma Ccm Kwan Watapigwa mara7 ya uchaguz wa Awal!EE MUNGU SIKIA KILIO CHETU WATANZANIA TUMECHOKA KUDANGANYIKA!Ni hukumu ya upendeleo na haina msingi!