Godbless Lema avuliwa ubunge

Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
Hamna kupinga uchaguzi urudiwe LEMA agombee tena tuone CCM kama watashindwa halafu serikali inapata faida gani kama sio hasara ya kugharamia uchaguzi ambao hauna faida maana hata kama kusoma hujui lakini picha huwezi kushindwa kuona hapa nadhani mmenielewa ARUSHA ni LEMA na LEMA ni ARUSHA.
 
hali ni shwari....mji upo salama.....polisi ndio wanazungukazunguka sijui wana kizunguzungu......ila hakuna mtu anafanya fujo wala anaetaka kufanya fujo.......tunaamini mbunge wetu yupo likizo ya muda......
Tutakutana battle field....

preta,wana wa nchi wansemaje,i mean wananchi wa kawaida
 
Usikate tamaaa maadamu wamekuruhusu kugombea tena nguvu ya umma itawadhihirishia kuwa wewe kamanda na wanaarusha wanakukubali
 
1 - 1 = 0

Arumeru Mashariki - toa - Arusha Mjini = sifuri.

Biashara kichaa hii, wanaoiweza ni magwanda tu.
 
Wana JF nimeona nika fukue Katiba ya Nchi hii....

========================================================================
67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu
yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-
(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(a) ikiwa mtu huyo anao au kwa hiari yake amejipatia uraia wa nchi nyingine yote; au
(b) ikiwa kwa mujibu wa sheria inayotumika katika Jamhuri ya Muungano imethibitishwa rasmi kwamba mtu huyo ana ugonjwa wa akili; au
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi
miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu; au
(d) ikiwa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(e) bila ya kuingilia haki na uhuru wa mtu kuwa na maoni yake, kuamini dini atakayo, kushirikiana na wengine na kushiriki shughuli za umma kwa mujibu wa sheria za nchi, ikiwa mtu huyo si mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
(f) ikiwa mtu huyo ana masilahi yoyote katika mkataba wa Serikali wa aina yoyote aliyowekewa miiko maalum kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na iwapo amekiuka miiko hiyo;
(g) ikiwa mtu huyo ameshika madaraka ya afisa mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais aweza au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa mujibu wa Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge;
(h) ikiwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inayoshughulikia makosa yanayohusika na uchaguzi wa aina yoyote mtu huyo amezuiliwa kujiandikisha kama mpiga kura au kupiga kura katika uchaguzi wa Wabunge.

===============================================================

Kwa Nguvu ya UMMA Lema anaendelea kuwa mbunge..
 
katika kile kinachooneka kama judgment za mahakama kuliki.hili limetokana na vyombo vingi vya habari jana kuandika hukumu ambayo imesomwa leo na jaji katika kesi ya uchaguzi iliyokuwa inamkabili Lema.Hili lililotokea leo katika mahakama kuu kanda ya Arusha alijawastua wala kuwashanga wanaArusha coz nikitu ambacho walishakijua kutokana na habari zilizokuwa zimezaaga kuwa kuna watu ambao walikuwa wamemshikisha mlungula hakimu ili atoe maamuzi haya kwa faida yao.
Mytake:Mahakama zetu zimefikia hatua ya kuwa kama rubber stamp.safari bado ni ndefu
 
Ameshindwa kwa kosa lipi? Naomba mwenye taarifa kamili atujuze.
 
Baada ya kuenguliwa ubunge wa Arusha,sasa bwana GODLESS LEMA anakabiliwa na pigo lingine kubwa ambalo wadadisi wa mambo wanaamini linaweza likamfanya ashindwe kutetea kiti chake na hivyo kushindwa kuingia bungeni!

PIGO hilo linahusiana na yeye kuwaambia WANAARUSHA tangu achaguliwe miaka miwili iliyopita ameshawafanyia nini wanaARUSHA mpaka sasa? LEMA amekuwa akihaha huku na huko,kushiriki maandamano yasiyo na TIJA baada ya kujikita katika kuleta maendeleo na kutimiza ahadi, inadaiwa mpaka sasa lema hajafanya chochote arusha, utalii umeshuka kutokana na maandamano yake ya mara kwa mara,hili kwa kweli ni PIGO SANA KWAKE NA CHAMA KWA UJUMLA!

MYTAKE: KAMA CHADEMA WANAWEZA WAMSIMAMISHE MTU MWINGINE ARUSHA
 
Huyu jaji ni CHADEMA, ameifanyia CHADEMA bonge la favor kwa kuitisha uchaguzi mwingine ambao anajua kabisa CHADEMA inachukua tena back to back, na ku build momentum toward 2015.

Walikuwa moja bila, juzi wamesawazisha, sasa itakua mbili moja, na mpira wenyewe baaado, kuna mpira wa kona unaenda kupigwa kwa Mpendazoe Segerea halafu kuna penati inakuja kwenye jimbo la Tundu Lissu huko, by the time mchezo unaisha uchaguzi mkuu huo, fainali!.
 
Ina maana NEC hawakurudia uchaguzi wa Madiwani wa Arusha Mjini kwa sababu ya hii hukumu?,
 
hali ni shwari....mji upo salama.....polisi ndio wanazungukazunguka sijui wana kizunguzungu......ila hakuna mtu anafanya fujo wala anaetaka kufanya fujo.......tunaamini mbunge wetu yupo likizo ya muda......
Tutakutana battle field....

Pole dada yangu Preta...ndio siasa zilivyo kuna kipindi unapata furaha na kuna kipindi unapata udhuni.
 
Baada ya kuenguliwa ubunge wa Arusha,sasa bwana GODLESS LEMA anakabiliwa na pigo lingine kubwa ambalo wadadisi wa mambo wanaamini linaweza likamfanya ashindwe kutetea kiti chake na hivyo kushindwa kuingia bungeni! PIGO hilo linahusiana na yeye kuwaambia WANAARUSHA tangu achaguliwe miaka miwili iliyopita ameshawafanyia nini wanaARUSHA mpaka sasa? LEMA amekuwa akihaha huku na huko,kushiriki maandamano yasiyo na TIJA baada ya kujikita katika kuleta maendeleo na kutimiza ahadi, inadaiwa mpaka sasa lema hajafanya chochote arusha, utalii umeshuka kutokana na maandamano yake ya mara kwa mara,hili kwa kweli ni PIGO SANA KWAKE NA CHAMA KWA UJUMLA!
MYTAKE: KAMA CHADEMA WANAWEZA WAMSIMAMISHE MTU MWINGINE ARUSHA

Ushauri wako peleka CCM, CDM inamsimamisha Lema...
 
Hizi ni hadithi za abunuasi.
CCM kushinda Arusha ni sawa na ngamia kupenya katika tundu la sindano.

Formula ni piga kura, linda kura.
 
1 - 1 = 0

Arumeru Mashariki - toa - Arusha Mjini = sifuri.

Biashara kichaa hii, wanaoiweza ni magwanda tu.

Unamaanisha magamba maana waliopoteza ni Magamba... Swali Mbunge wa Arusha ni nani? kwa kina Ritz na Rejao jbu ni ....... Lakini kwa Mtu wa A town jibu na CDM jibu ni LEMA
 
Kuna haja ya kuanzisha mahakama za uchaguzi baada hizi kushindwa na kuona pia zinapeleka ujumbe kwa watu vibaya jaribu kutazama hata wakina Kafulila, na wengine hatuwezi kuwa na chaguzi kila wakati na hilo lipo wazi. CCM wajiandae kushindwa maana watashindwa vibaya sana huko na kelele zao nitashangaa sana kuona kama kuna mtu atapeleka pua yake kula Arusha
 
Naamini cdm hawana haja hata kupiga kampeni wasubiri tu siku ya kupiga kura tutapigia "movement 4 change"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom