Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

TPDF nao wamechoka tu... mabomu mpaka yana expire wanayaangalia tu!!!!:twitch::twitch:

Mwanangu mabomu huwa hayana expire hata siku moja hizo ni visingizio na kukwepa uwajibikaji.
Kusema askari wamechoka hapo nakupa tano.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya waziri mkuu aliyoitoa leo asubuhi bungeni anasema tayari mpaka sasa jumla ya watu 17 wamepoteza maisha katika hospitali za muhimbili, amana na temeke. Kutokana na tukio hilo la milipuko spika wa bunge ameahirisha bunge hadi kesho. Source: star tv
 
Mungu wa Rehema na Neema tunaomba uwaponye majeruhi wote kwa haraka, wale waliopotewa na ndugu, jamaa na marafiki uwape faraja kuu na waliopoteza maisha uwape mwanga wa milele na raha ya milele uwaangazie.

Mungu wa haki tunakuomba unyoshe mkono wako kwa wale wote waliohusika kwa kukusudia au kwa zembe wao na maafa haya katika nchi yetu. Mungu wewe ni adui wa maadui zetu na hawa watu ni adui wa uhai wetu na watoto wetu. Washughulikie mmoja mmoja kwa kadiri ya uhusika wake katika hili.

Mungu tumechoka tuteteee mwenyewe sasa!! Usinyamaze Mungu tunataka kuuona mkono wako. Amen!!
Amen!!!😛ray2:
 
Amana hospital,pugu kajungen majohe,wamekataa kupokea tena waathirka hospital full na majeruhi na maiti mungu tuepushe na balaa hii hi inaonyesha kuna watu awajafanya kazi zao vizuri amuwezi kuudanganya umma na vifo vya mbagala na sasa mtudanganye na gongolamboto..kama mlisema mmethibiti mbagala na alitatokea tena haya ya jana upupu ama\???kwa nini watanzania ni wagumu kuwajibika wapendwa lini tutaheshimu matakwa ya wananchi
 
Nichukue fursa hii kuwapa pole ndugu jamaa na watu wote kwa ujumla wao walioguswa kwa namna moja ama nyingine na ajali hii iliyotokea Gongolamboto!
 
Taarifa aliyoitoa Pinda Bungeni inasema 19 wamefariki!
 
Najiuliza haya mambo yatakuwa hivi mpaka lini??
Ni lini tutaona afadhali leo, manake kila siku ni afadhali ya jana ku ya leo,, mpaka lini??

Ni nani jamani anayetutesa hivi, manake hata kama tumetenda dhambi kupitiza bado Mungu sio gaidi hivo hata asisikie kilio chetu. Ni nani huyu jamani, jamani, Mpaka lini sasa. Tumchoka!!
Ni uzembe tu uliokithiri hakuna jingine kuna watu wanapaswa waadabishwe na sio kuwajibishwa
 
Hakuna namna yoyote ya kutetea Uzembe huu uliotokea Ukonga,Ni kweli tukio zima ni ajali,lakini ni ajali ambayo ingeweza kuzuilika...Haiwezekani katika kipindi kisichozidi mwaka kutokee ajali zinazofanana,ina maana next month likitokea tukio kama hili Lugalo bado tutasema ni bahati mbaya?Inabidi Viongozi wetu wajifunze kutoa majibu sahihi kwa maswali magumu.Waziri Wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inabidi atoa maelezo ya kina kwa Umma wa watanzania na kutafuta suluhu ya kuyaangamiza mabomu chakavu...kwa kutumia ujuzi na uwezo ndani ya jeshi lake au kuomba msaada nje ya nchi...Hatuwezi kuona Raia wasio na hatia wanapoteza maisha yao,na sababu inayotolewa na serikali ni ya kizembe eti "ni ajali tu".....hali ya joto kali imesababisha mabomu kulipuka,majibu hayo ni dharau na matusi kwa waathirika na raia wa Tanzania,imefika wakati sasa Viongozi wetu wajifunze kujiuzulu,ikitokea kashfa ndani ya mamlaka yao...Waziri Mwinyi jiteteee!Utetezi wako uandamane na KUJIUZULU!
 
wale panya wa sua vipi tena walishindwa kutoa taarifa za mabomu kulipuko? au walidisco?
 
Mizahamizaha tu na maisha ya watu...inasikitisha kwa serikali kutojali namna hii!
 
Kuna mzazi alikuwa anaongea asubuhi anasema bomu limemkata mtoto wake mkono,amekimbia nyumbani ameliacha bomu liko nyumbani hajui afanyeje yeye yuko hosiptali na mtoto

Nimetaarifiwa na ndugu yangu wa huko Gongolamboto ambaye anasema ameshuhudia mabomu mengi yakipita juu ya nyumba yake. Moja lilipiga nyumba ya jirani yake na kusambaratisha kabisa, bahati nzuri walikuwa wamekwishakimbia. Mabaki ya bomu hilo yamechukuliwa asubuhi. Bomu moja kubwa lilipiga sehemu ya nyumba yake na kwenda kuanguka kwenye choo chake cha nje, hilo halikulipuka. Askari wamekuja mara mbili asubuhi hii lakini wameshindwa kulichukua maana ni kubwa sana, na halijalipuka.

Familia yake yote ilitawanyika usiku, ni yeye pekee yake alibaki hapo nyumbani, akisali usiku kucha. Mmoja wa wanafamilia alikuwa mgonjwa, alikutwa na wasamaria wema njiani akijikongoja wakamsafirisha kwa ndugu zetu huko Mikocheni. MMoja wa wanafamilia kabla ya kukimbia alikuwa ameumia mkono lakini haukukatika. Namshukuru Mungu kwa kuwanusuru, na ninawapa pole sana wale waliopoteza ndugu, kuumia na kuharibiwa mali na nyumba zao.
 
Husein Mwinyi Ajiuzuru, kutokana na kushindwa kwake kazi nitamshangaa sana maana viongozi wa kitanzania hatuna utaratibu mpaka maji yakufike shingoni kabisa. Inasikitika sana kusikia eti walio fariki ni kumi tu huku kukiwa na taarifa za uhakika familia mbili zimethibitisha kupoteza watoto sita,
 
The gov.must step down.
we are tired of ur absurd staffs.
 
tumeshindwa kuandamana basi wameona watufanyizie kabisa.
Kwani tungeandamana hata kama wangeua watu wasingefika hao 200+
na tungekuwa tumeshafanya historia nyingine ya Tanganyika.
hatuna hulka hiyo
 
Somen hii pinda kaongeza tena 10-27 wamekufa
 
Nimetaarifiwa na ndugu yangu wa huko Gongolamboto ambaye anasema ameshuhudia mabomu mengi yakipita juu ya nyumba yake. Moja lilipiga nyumba ya jirani yake na kusambaratisha kabisa, bahati nzuri walikuwa wamekwishakimbia. Mabaki ya bomu hilo yamechukuliwa asubuhi. Bomu moja kubwa lilipiga sehemu ya nyumba yake na kwenda kuanguka kwenye choo chake cha nje, hilo halikulipuka. Askari wamekuja mara mbili asubuhi hii lakini wameshindwa kulichukua maana ni kubwa sana, na halijalipuka.

Familia yake yote ilitawanyika usiku, ni yeye pekee yake alibaki hapo nyumbani, akisali usiku kucha. Mmoja wa wanafamilia alikuwa mgonjwa, alikutwa na wasamaria wema njiani akijikongoja wakamsafirisha kwa ndugu zetu huko Mikocheni. MMoja wa wanafamilia kabla ya kukimbia alikuwa ameumia mkono lakini haukukatika. Namshukuru Mungu kwa kuwanusuru, na ninawapa pole sana wale waliopoteza ndugu, kuumia na kuharibiwa mali na nyumba zao.

Poleni sana.

Kinachosikitisha ni kwamba hakuna taarifa rasmi na za uhakika kuhusu haya mabomu. Halafu kama hilo jingine halijalipuka na hawajalichukua. Hii ni uzembe na hatari.
 
Back
Top Bottom