Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Serikali imesema watu kumi tu ndo walokufa?

Amini ni mara kumi yake ...😡
 
Siyo chumvi ni Magadi hayo !!!!watu miambili???unadhani nipadogo??
 
JK must resign, this country is heading to the black point. Pls JK step down otherwise, tuingie barabarani mtuue wote ili mjiongoze wenyewe.
 
Kuna mzazi alikuwa anaongea asubuhi anasema bomu limemkata mtoto wake mkono,amekimbia nyumbani ameliacha bomu liko nyumbani hajui afanyeje yeye yuko hosiptali na mtoto
 
Serikali ya Tanzania sijui ikoje jamani watu wanakufa 200+ wao wanasema 10?? Kama moto upo watakiona.
 
Jana mimi hawa jamaa wa TV stesheni walinikera sana kutoonyesha habari hizi hata japo picha za tukio.

ITV walionyesha usiku wa saa saba kidogo tu kabla ya kuondoa (sijui kwa amri ya nani) na kurudisha Aljazeera.
 
uwajibikaji ndio nalosubiri kwa sasa... some people has to answer for this

tatizo la hii nchi utasikia wameshaunda tume, hakika mtasikia tu leo tume kuundwa
 
mi nashauri jeshi lisimiliki silaha za mlipuko kwa kuwa hawawezi kuzihifadhi. Utasikia tume imeundwa kuchunguza majibu ya tume iliyoundwa ya mabomu ya Mbagala.
 
TUJIKUMBUSHE MABOMU YA APRILI 2009 MBAGALA
8D6U0041.JPG




Picha tu inatosha kuonyesha kuwa huyu prezident sio makini.........Huwezi kuwana na furaha katika mazingira kama hayo hayo, inaonyesha kuwa jamaa ni kama alionekana kutoguswa kabisa na hilo tukio huwezi kutabasamu wakati watu wamepoteza maisha!
SI HAKI KUMUHUKUMU NGIRI KUWA ANACHEKA MUDA WOTE HATA KWENYE MSIBA YEYE ANACHEKA, "JAMANI NGIRI MENO KUWA NJE SI KUCHEKA NI MAUMBILE YAKE TU"

Hivyo tusimuhukumu JK inawezekana kuchekacheka ni maumbile yake, kiongozi wetu ajaumbwa kukasirika. 'Hila ukidai tu niongeza ya mshahara ndipo utakapojua kuwa anakasirika'
 
mbagala waliunda tume......... ripoti wamezikalia na wala hakuna lolote lililofanyika...na leo g'mboto ndo hivyo watu wamekufa na bado tume itaundawa
 
Hongera Kimilidzo :clap2:
Kama madaraka tunapeana kiswahiba mtawajibishana vipi?? Inabidi tuseme ni bahati mbaya ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Hivi kweli JK anaweza kumuwajibisha mtoto wa Mwinyi?? Si Mwinyi naye aliwahi kumpa JK uwaziri na JK kalipa kwa kumpa mtoto wa Mwinyi... Kwanza tujiulize sakata la Mbagala kuna mtu hata mmoja alijiuzuru?? Kama hakuna then nani angechukua taadhari wakati hakuna issue yoyote kubwa nchii hii hata kama watu wanakufa. Kosa lilishafanyika kuruhusu Mkwere achakachue kura na kubakia kuwa rais then tuendelee tu kubeba msalaba manake ndo adhabu zenyewe hizo na laana toka kwa Mungu
 
Mabomu yanalipuka Gongo la Mboto polisi....

Taarifa zaidi kufuatia.

UPDATES: (by Invisible)

1. Hali ni mbaya jijini Dar, nyumba zinabomoka, watu wanakimbia ovyo!

2. Barabara ya Nyerere haitembei (kama unafikiria kwenda uwanja wa ndege ahirisha mapema), magari yameingiliana watu wanakimbia ovyo mitaani na barabarani kulikimbia eneo la maafa.

3. Dalili zinaashiria mabomu ni mengi zaidi na milipuko itaongezeka, kuna uwezekano wa kupoteza raia na watumishi (wanajeshi) wengi kufuatia milipuko hii

4. Watu kadhaa wamekufa kwa kugongwa na magari

5. Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Abdulrahman Shimbo amesema:

"Hali ni mbaya Kikosi namba tano maghala yamelipuka ni hatari, watu wahame, maghala yako karibu karibu sana, tunaomba wananchi wahame sasa hivi, tunajitahidi kuzuia moto unaotokana na hilo unaweza kwenda mbali sana hadi Kilomota kumi, wananchi walioko karibu na maghala ya kikosi Gongo la Mboto wasogee mbali sasa hivi.

6. Kwa mujibu wa FikraPevu, anga limefungwa kwa muda na ndege hazitaweza kutua uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.

7. Mkono wa mtu (mwanamke), moyo na viatu (na khanga) vimeokotwa... - Radio One

8. Picha ya tukio kwa mbali sana...

obhbd.jpg


183908_188361264530414_100000696254336_536897_2719650_n.jpg


184277_188361657863708_100000696254336_536909_7097881_n.jpg


VIDEOS:



Wahusika lazima waachie ngazi. Uzembe huu utaendelea hadi lini? Mbagala tulisema ni bahati mbaya. Ina maana baada ya Mbagala wahusika hawakuchukua hatua katika kambi nyingine za jeshi? Au ndio hivyo tena nchi yetu acha kila kitu kijiendee.

Kwa kuanzia Rais, Mkuu wa majeshi na Waziri wa ulinzi WAJIUZULU, kwani ndio hao hao ambao walikua katika nafasi hizo wakati wa ulipukaji wa mabomu ya Mbagala, na sasa kinatokea kitu cha aina hiyo hiyo miaka michache baada ya Mbagala.
 
Last edited by a moderator:
Unakumbuka Mbagala walisema wangapi wamekufa?

Alafu si walisema haya mabomu yaliyo zeeka wanayaharibu?

leo asubuhi 12.00am BBC walikuwa wanasema 10 na Radio one saa 1 asubuhi wamesema 13 kutoka Hospital ya Amana

Lakini inawezekana wakafika 200 maana waliokufa kwenye tukio hawajahesabika
 
Nafikiri haya mabomu yangelipuka IKULU labda watu ndio watawajibishwa lakini hili tutaendelea kusikiliza story tu.

Baada ya tukio la Mbagala, na kisha serikali kuutangazia umma kuwa tukio kama hilo lisingetokea tena, halafu likatokea - Ni hapa kwetu tu ambapo uhai wa mwananchi hauna thamani, ndiyo mambo haya yanaweza kuvumilika lakini kwa mataifa ambayo huthamini uhai wa wananchi wao, na serikali ipo kwaajili ya kuwatumikia, HAKIKA tukio hili lingelazimu serikali kuondolewa madarakani maana wameshindwa kutekeleza jukumu kuu la msingi la serikali ambalo ni kulinda usalama wa Raia na mali zao.

Lakini kwetu hapa kiongozi anaweza leo kutoa kauli hii, kesho ile na kusitokee lolote. Walisema bado muda kidogo tatizo la umeme litakuwa historia, na juzi wamesema tatizo la umeme litakwisha 2030, na hakuna anayewajibishwa kwa kauli za uwongo za huko nyuma.

Ndugu zetu wa Gongolamboto poleni sana, waliopoteza maisha, Mwenyezi Mungu awarehemu, Muumba uwasamehe makosa yenu, na awapokee katika ufalme wake. Wale waliosababisha kufa kwenu kabla ya mpango wake, Bwana awalipie kadiri ya mapenzi yake. Tunajua hapa Tanzania hawatafanywa chochote lakini siku zote haki mwenye kujiona mwenye nguvu na mamlaka huadhibiwa na Muumba, Amen.
 
Rais,Waziri wa ulinzi na Mkuu wa majeshi wanapaswa kuwajibika kwa kujiuzulu nyadhifa zao mara moja.Hii ni kulitia hasara taifa...kupoteza kunguvu kazi sio kitu cha mchezo.Watanzania hatupaswi kulifungia macho hili...Juzi ilikua mbagala leo gongolamboto na kesho litatokea kawe na kunduchi....Watanzainia tuamke sasa......tuandamane hadi ikulu kuishinikiza serikali ya CCM itoke madarakani.

Poleni sana wahanga wa mabomu gongolamboto na Dar es salaam kwa ujumla.
 
Kwa maeneo kama gongolamboto inawezekana kutokana na ujenzi wa nyumba ulivyo na mitaa kukosa barabara, kwa maana hiyo idadi hiyo inawezekana kabisa
 
Najiuliza haya mambo yatakuwa hivi mpaka lini??
Ni lini tutaona afadhali leo, manake kila siku ni afadhali ya jana ku ya leo,, mpaka lini??

Ni nani jamani anayetutesa hivi, manake hata kama tumetenda dhambi kupitiza bado Mungu sio gaidi hivo hata asisikie kilio chetu. Ni nani huyu jamani, jamani, Mpaka lini sasa. Tumchoka!!
 
Back
Top Bottom