Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

sina uhakika kama ni 200 nadhani hii ifanyiwe uchunguzi, na ww usituletee habari zisizo na chanzo
 
Unaona sasa??? Mnaogopa nini kuandamana? Kufa ni kitu kidogo sana, tutokeni jamani, tutokeni tulete tafrani hawa manyang'au waondoke. Jamani wanatutoa kafara, tunawapa mno nafasi!! Ah!!:sick:
 
Wahusika lazima waachie ngazi. Uzembe huu utaendelea hadi lini? Mbagala tulisema ni bahati mbaya. Ina maana baada ya Mbagala wahusika hawakuchukua hatua katika kambi nyingine za jeshi? Au ndio hivyo tena nchi yetu acha kila kitu kijiendee.

Kwa kuanzia Rais, Mkuu wa majeshi na Waziri wa ulinzi WAJIUZULU, kwani ndio hao hao ambao walikua katika nafasi hizo wakati wa ulipukaji wa mabomu ya Mbagala, na sasa kinatokea kitu cha aina hiyo hiyo miaka michache baada ya Mbagala.


walimshusha yule mama wa watu cheo baada ya yale ya Mbagala bila kujali ni report ngapi alizowatumia kuhusu hilo suala wanasema ni uzembe, sasa watujuze ni nani mzembe na walivyomshusha mama wa watu na Kanali mzima akastaafu bila heshima yeyote watamlipa ... mi naona sisi hatuna Rais tujiandae tu kumtoa madarakani, tatizo la kuweka mashoga kwenye vyeo unashindwa kutatua tatizo unatafuta wa kumuadhibu na wasipo angalia vizuri yatalipuka mpaka Kibaha ... Kama Mungu hataki tuandamane atusaidie basi kwa kutumia ile njia yake raisiiiiiiiiiiiii............
 
jamani mimi nimeshuhudia watu watano(5) , baada ya bomu kuanguka kwenye nyumba na kuangukiwa na ukuta, Gari Haice ya Jirani imeteketea kwa moto.


Niko tayari kwa maandamano, kwani nina kira sababu , yakufanya hivyo. Hawa wapuuzi wanataka kutumaliza sasa kwa kunywa damu yetu. hatuna sababu ya kuendelea kuwaweka madalakani. Hii maksudi naamini si uzembe, kama kujifunza wangesha jifunza siku nyingi. Naona, Temeke na Ilala tayari. tusubili na kinondoni (lugalo au Kunduchi) wananchi inabidi tuchimbe mahandaki.

Mafisadi wameamua kutubadilishia Biti na Korasi maana waliana musiki wa dowan unawanyima usingizi!!


Shenzi Hawa!!!&^&&^!##!%&*
 
Ni hatari kuwa na serikali ya watu mbumbu, wapuuzi lakini wenye kiburi na dharau kwa watu waliowaeweka madakani.


Je, watanzania kwanini bado tunakuwa na vichwa ngumu ya kutotaka kujifunza?

''WE SHALL NOT BLAME OUR ENEMIES FOR OPPRESSING US BUT LET'S BLAME OURSELVES FOR DOING
NOTHING''


 
Pinda kasema kuna maiti 13 amana, 2 temeke, 2 Muhimbili na nyingine 3 gongolamboto so jumla ya Pinda ni 20 hadi anataarifiwa.

Kwa nini asiende mwenyewe asubiri kupewa taarifa? Hayo anayoyaongea ana uhakika nayo?
 
Ndugu wapendwa
kwa walio karibu na gongo la mboto wanaweza kwenda kwenye hospital na mdk waaminifu awafichi ukweli wengi wamekufa tofauti na serikali kuudanganya umma watu kumi tu .....,akika imefika wakati serikali ya tanzania kuwajibika kwa hili kama ni kuhujumiana basi wasituadhiri wananchi na kama mabomu yaliletwa yame expire kwa nini watu wasiwe responsible na hiili????

WEWE MTOTO WA MWINYI EMBU JIUZUL NAONA KAZI IMEKUSHINDA NILIJUA YA MBAGALA BAHATI MBAYA NIKAANDIKA NAHISI SASA NAONA WAZI KAZI IMEKUSHINDA..NA KWA TAARIFA MBAYA HAKUNA HATA KIONGOZI ALIEENDA MAHOSPITALINI SI WAZIRI WA ULINZI WALA MAGENERAL WAKE...............,

HUU NI UPUZI TUSIUKUBALI HATA KIDOGO WATANZANIA NA THIS TIME TUTAANDAMANA KUMPUNGUZIA KAZI HUYU RAIS ASIEJUA MADARAKA YAKE

Source pls, not hearsay
 
Pinda anasema at least 20 poeple have died and mroe than 140 have been injured. wati4,000 wamepewaq hifadhi uwanja wa taifa. Bunge limeahirishwa kutokana na disaster hiyo. Tundu Lissu anataka waziri wa Ulinzi ajiuzulu
 
Nafikiri hayo yanayoruka na kupita juu za nyumba ni risasi za mizinga na maroketi ya kupigia mizinga ukichanganya na high speed bullets ,nijuavyo mabomu huwa hayaruki hulipukiana papo kwa papo ila hayo niliyoyata yakiunguza fuse tu huelkea kusikojulikama kama lililofyetuliwa kutoka kwenye mzinga,ila kama kuna wakuu wanaojua habari za mabomu yanayoruka watueleze. Sidhani kama kuna mtu anatakiwa ajiuzulu huo utakuwa ni uzezeta kutaka kiongozi wa juu ajiuzulu ,mbona sehemu nyingi tu duniani kulipuka kwa maghala ya silaha ni jambo la kawaida.

Nawapa pole wenyeji wa eneo hilo na wajeshi waliokuwa kwenye zamu.
 
Hii ndiyo hasara ya kuteua watu kwa misingi ya kindugu, na kidini...
 
Poleni sana ndugu zetu wote waliofiwa....tunawaombea Mungu awatie nguvu na kuwafariji. Wazembe wote wawajibishwe...!
 
Taarifa aliyoitoa Pinda Bungeni inasema 19 wamefariki!

Hawa wabunge nawashangaa wanaendelea na mipasho bungeni kwa ajili ya posho ya leo huku waajiri wao wanaangamia £öéßù.
Si ombi ahirisheni bunge ASP Mje mjionee hali halisi huku G/Mboto. angalau kuwafariji hawa walalahoi jamani hamna hata huruma?j
 
Kweli mtu amefika sehemu yenye kuhuzunisha anadiriki kupiga picha na tabasamu kana kwamba yupo kwenye sherehe fulani. Embu cheki hii pic

kituko.jpg
 
Ndugu wapendwa
kwa walio karibu na gongo la mboto wanaweza kwenda kwenye hospital na mdk waaminifu awafichi ukweli wengi wamekufa tofauti na serikali kuudanganya umma watu kumi tu .....,akika imefika wakati serikali ya tanzania kuwajibika kwa hili kama ni kuhujumiana basi wasituadhiri wananchi na kama mabomu yaliletwa yame expire kwa nini watu wasiwe responsible na hiili????

WEWE MTOTO WA MWINYI EMBU JIUZUL NAONA KAZI IMEKUSHINDA NILIJUA YA MBAGALA BAHATI MBAYA NIKAANDIKA NAHISI SASA NAONA WAZI KAZI IMEKUSHINDA..NA KWA TAARIFA MBAYA HAKUNA HATA KIONGOZI ALIEENDA MAHOSPITALINI SI WAZIRI WA ULINZI WALA MAGENERAL WAKE...............,

HUU NI UPUZI TUSIUKUBALI HATA KIDOGO WATANZANIA NA THIS TIME TUTAANDAMANA KUMPUNGUZIA KAZI HUYU RAIS ASIEJUA MADARAKA YAKE

...Mwongo mkubwa, kabisa.
 
poleni sana wahanga wa hayo mabom! Something must be done!
 
Mie kwa kweli machozi yananitoka kwa uchungu ninaoupata. Sio kwa sababu tu ndugu zangu wanaoishi karibia na meneo hayo wamepona lakini pia ni kwa sababu ya uzembe wa hali ya juu na jinsi ambavyo serikali yetu hii haichukulii suala hili na uzito wake. Ni janga la taifa na tunapaswa kuomboleza kwa kweli. ikiwezekana na bendera iwekwe nusu mlingoti. This is too much for us tanzanians to just swallow it in like its nothing big.............
 
Tukio la jana la mlipuko wa makombora kwenye kambi ya JWTZ Gongolamboto limenifanya nitafakari ni somo gani serikali yetu ililipata baada ya tukio la milipuko ya Mbagala,hii inanifanya nizidi kuconfirm ule wasi wasi wangu kuwa nchi hii inaongozwa na vichwa maji wasio na uwezo wa kufikiri wala kujifunza kutokana na yanayotutokea.,baada ya maafa ya Mbagala sikutegemea kama tukio kama lile lingetokea tena katika nchi hii na kinachosikitisha ni kwamba hakuna atakayewajibika kwa hili kama ilivyo kawaida ya viongozi wetu,na hakika damu ya watanzania inayoendelea kumwagika itadumu mikononi mwao na kwa hiyo kama wanashindwa kuwajibika tutawawajibisha sisi wananchi wenye uchungu na mustakabali wa taifa hili.
 
Hawa wabunge nawashangaa wanaendelea na mipasho bungeni kwa ajili ya posho ya leo huku waajiri wao wanaangamia £öéßù.
Si ombi ahirisheni bunge ASP Mje mjionee hali halisi huku G/Mboto. angalau kuwafariji hawa walalahoi jamani hamna hata huruma?j

Bunge limeAHIRISHWA NDUGU! kUNA WABUNGE WENYE UTU SIYO WOTE WALIO BINAFSI
 
jamani tunapoandika threads ni lazima kuzingatia uandishi pia kuwa na uhakika, sio kweli hiyo idadi uliyotaja...
watchout!!!!
 
Back
Top Bottom