Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
Mabomu yanalipuka Gongo la Mboto polisi....

Taarifa zaidi kufuatia.

UPDATES: (by Invisible)

1. Hali ni mbaya jijini Dar, nyumba zinabomoka, watu wanakimbia ovyo!

2. Barabara ya Nyerere haitembei (kama unafikiria kwenda uwanja wa ndege ahirisha mapema), magari yameingiliana watu wanakimbia ovyo mitaani na barabarani kulikimbia eneo la maafa.

3. Dalili zinaashiria mabomu ni mengi zaidi na milipuko itaongezeka, kuna uwezekano wa kupoteza raia na watumishi (wanajeshi) wengi kufuatia milipuko hii

4. Watu kadhaa wamekufa kwa kugongwa na magari

5. Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Abdulrahman Shimbo amesema:

"Hali ni mbaya Kikosi namba tano maghala yamelipuka ni hatari, watu wahame, maghala yako karibu karibu sana, tunaomba wananchi wahame sasa hivi, tunajitahidi kuzuia moto unaotokana na hilo unaweza kwenda mbali sana hadi Kilomota kumi, wananchi walioko karibu na maghala ya kikosi Gongo la Mboto wasogee mbali sasa hivi.

6. Kwa mujibu wa FikraPevu, anga limefungwa kwa muda na ndege hazitaweza kutua uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.

7. Mkono wa mtu (mwanamke), moyo na viatu (na khanga) vimeokotwa... - Radio One

8. Bunge limeahirishwa kufuatia tukio hili

9. Waziri Mkuu Mizengo Pinda anadai idadi ya waliokwisha kufa ni zaidi ya 19 lakini tunaarifiwa kuwa idadi halisi huenda ni zaidi ya 100.

10. Jeshi la Polisi linawaarifu wale wanaotafuta watoto wao na hawawaoni kwenda kwenye vituo vya polisi jijini kwani kuna watoto wengi wamepelekwa huko.

11. Wananchi wanaombwa kukaa mbali na eneo la tukio kwani hali haijawa shwari.


Picha ya tukio kwa mbali sana...

obhbd.jpg


183908_188361264530414_100000696254336_536897_2719  650_n.jpg


184277_188361657863708_100000696254336_536909_7097  881_n.jpg


VIDEOS:

 
Last edited by a moderator:
Tupe hata hizo habari ndogo ulizonazo ...
sababu ni nini?
wewe umesikia wapi?
please anything...
 
Kuna milipuko mikubwa inaendelea sasa hivi maeneo ya Airport au Gongo la Mboto, walio karibu na tukio kulikoni?
 
Wakuu habari za sikuu kuu. Jamani kuna milipuko Kama ya mabomu inalipuka. Mi nipo ukonga. Mpaka sasa kuna miale ya moto. Labda watu husika wangechukua tahadhari Kama ndege zinazotua
 
Hayo mabomu bora yalipuke kwenye matawi ya ccm ya Intelejensia (Polisi) Kuliko kulipuka huku kwa walalahoi tena mimi nataka yalupike na magogoni maana tumechoshwa na Ufisadi uliokithiri Ikulu:clap2:
 
moto una waka vibaya sana mabomu yanalipuka Gongo la Mboto kwenye kambi ya JESHI!
 
Milipuko ipo na inasemekana inatoka katika maeneo ya kambi za jeshi, source tbc taifa radio imetangazwa sasa hivi saa 3.02 usiku huu.
 
Ni mabomu kwenye kambi ya jeshi Gongo la Mboto, nyumba nyingi za raia jirani na eneo hilo zimeathirika.
Tunafuatilia wahanga wa ajali hiyo, inaelekea ni zaidi ya Mbagala!
 
CONFIRMED: nimeongea na mtu , ame confirm hali ni mbaya moto unaonekana kutokea mbali!
 
Watu walio karibu hebu tuelezeni, au drill ya kawaida ya moto na milipuko
 
Nini tena bongo? Utashangaa badala ya kudeal na chanzo halisi serikali ya ccm itasema cdm ndo wamesababisha!
 
Back
Top Bottom