Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

moja limetua tabata kwa Swai na kuua mtoto mdogo so + 10 wa Amana 11. Habari toka kwa rafiki yangu aishie maeneo hayo. RIP wote waliofaliki na poleni waadhirika wote tunamuomba Mungu awape uvumilivu. I hope this time Serikali itawawajibisha waliohusika. Ila ningependa waziri Mwinyi akajiuzuru mana hili limetokea chini ya uongozi wake.
 
Pinda kasema kuna maiti 13 amana, 2 temeke, 2 Muhimbili na nyingine 3 gongolamboto so jumla ya Pinda ni 20 hadi anataarifiwa.
 
Mungu wa ibrahim isak na yakobo lazima amwadabishe kikweete na wapuuzi wake kwa kuondoa maisha ya watu dunian
 
Nawapa pole wakazi wote wa Gongo la Mboto waliofikwa na msiba huu mkubwa tupo nanyi katika wakati huu mgumu.
 
Jamani tunaomba detail za uhakika wengine jamaa yetu kubwa ipo huko Gongolamboto...
 
Itabidi Marehemu hawa nao wapatiwe mazishi ya kishujaa kama wale Mashujaa waliouawa katika maandamano january 5 Arusha kwani wote source ya vifo vyao ni moja, JK kushindwa kuiongoza nchi.
 
wale panya wa sua vipi tena walishindwa kutoa taarifa za mabomu kulipuko? au walidisco?

mkuu hawa panya na mapanya buku si walìhitimu shahada na walipata skolashipu ya kufanya masters mbele!? Wako mbele mkuu,na nasikia wamefanya press Conference Bbc na kueleza masikitiko yao kuhusu mlipuko wa jana. Wakihitimu masters watarudi bongo kutusaidia.
 
Wanajeshi wetu walivyokosa uzalendo walishindwa hata kulielekeza bomu moja magogoni ili Mkwere naye aone uchungu wa watu kuondokewa na wapendwa wao kwa uzembe wa shimbo.
 
Wanajeshi wetu walivyokosa uzalendo walishindwa hata kulielekeza bomu moja magogoni ili Mkwere naye aone uchungu wa watu kuondokewa na wapendwa wao kwa uzembe wa shimbo.


Magogoni asingeumia sana wange yaelekeza kule BAGAMOYO wasambarratishe kile kijiji alichojengewa na wale wapuuuuuuuu mmba vu wajapan..na familia yake..hana adabu kabisa huyurais kama anavyoema mh pk j mzaha mzaha kila sehemu inamcost sasa anakosa pa kutokea...laana wa mlaaniwa
 
Hali ilivyo serikalini ni kuwa kuna wakuu wengi wa vitengo na idara mbali mbali ambao wameteuliwa kuongoza idara na vitengo hivyo ila hawajui kabisa vitengo vyao na idara zao zinafanya kazi gani na zinafanyaje kazi hizo! Ni ajabu na ukweli lakini ndo ukweli halisi. Kwa mtaalamu na Msomi aliye mkuu wa kitengo, tukio hili hawezi kuliita ajali! Haiwezekani tukio hili likawa ajali.

Wale waliopitia mafunzo ya uhandisi, naamini madude hayo yaliyolipuka yalikuwa chini ya kitengo hicho, siku ya kwanza kabisa kitu cha kwanza kujifunza au kufundishwa ni kuwa hakuna ajali inayotokea tu. Ajali zote husababishwa na uzembe na sababu nyingine nyingi ambazo zote zinafanana na uzembe. Sasa likitokea jambo kama hili mkuu wa kitengo hicho akasema ni ajali tu, na bosi wake akakubali kuwa ni ajali, na bosi wake naye akakubali, ........ hadi rais ambaye ndiye mkuu wa majeshi na bosi wa wote akakubali ... Ni wazi Rais hajui anafanya nini kwenye urais, waziri wa ulinzi hajui kuwa waziri wa ulinzi maanake ni nini, mkuu wa majeshi hajui kuwa mkuu wa majeshi manake nini, .... Na kuendelea.

Hali iko hivyo. Watu wengi wameteuliwa, wanafika ofisini wanakaa. Wanaletewa makaratasi ya kusaini kila siku wanasaini. Wanaalikwa kwenye vikao kufunga na kufungua vikao wanakwenda. Wanasafiri kwenda sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi. Wanarudi wanakaa ofisini. basi. Lakini ukimuuliza kwa undani kabisa wewe majukumu yako nini, hawajui! Pengine anaweza kukuambia majukumu yake ni kusafiri na kuiwakilisha taasisi anayoiongoza kwenye vikao mbali mbali!!!

Ndo maana unakuta sehemu nyingi wakuu wa idara au wakuu wa vitengo wanasafiri hadi asilimia 80 ya muda wao wote wa kazi. Vinginevyo hakuna kiongozi wa sehemu anayejua majukumu yake anayeweza kusafiri safiri sana namna viongozi wetu wanavyosafiri. Kifupi ni kuwa hakuna raisi wa nchi anayejua majukumu yake kama raisi anayeweza kuwa anasafiri safiri kama afanyavyo rais wetu.

Hali ikiwa hivi, tutarajie mambo mabaya zaidi!
 
ndugu wapendwa
kwa walio karibu na gongo la mboto wanaweza kwenda kwenye hospital na mdk waaminifu awafichi ukweli wengi wamekufa tofauti na serikali kuudanganya umma watu kumi tu .....,akika imefika wakati serikali ya tanzania kuwajibika kwa hili kama ni kuhujumiana basi wasituadhiri wananchi na kama mabomu yaliletwa yame expire kwa nini watu wasiwe responsible na hiili????

Wewe mtoto wa mwinyi embu jiuzul naona kazi imekushinda nilijua ya mbagala bahati mbaya nikaandika nahisi sasa naona wazi kazi imekushinda..na kwa taarifa mbaya hakuna hata kiongozi alieenda mahospitalini si waziri wa ulinzi wala mageneral wake...............,

huu ni upuzi tusiukubali hata kidogo watanzania na this time tutaandamana kumpunguzia kazi huyu rais asiejua madaraka yake

kikwete mwenyewe hujishtukii kwanini mambo kama haya hayajajitokeza kwa marais watatu waliomtangulia?wakat sasa umefika kukubali uongoz umekushinda na sio fan yako jaribu jingine
 
Walipouwa Arusha wakasema hali hiyo haitajirudia tena, mara wakajisahau, wakaenda kuua tena Mbarali....!
Ni wakati sahihi wa kuacha kuwaamini kabisa hawa...Ni bora kichaa, maana at least anakumbuka njia ya kwao!

WAPO vichaa wengine hakyamungu hawakumbuki njia waliyotoka.... JK
 
Tunawapa pole ndugu zetu waliofiwa Mungu awape faraja, majeruhi wote pia tunawaombea Mungu awaponye haraka, but walioko responsible na hii kitu ni lazima wawajibishwe tutaendelea kuumia hivi hadi lini and the government is not even caring its real bad.
 
Poleni ndugu zangu GongolaMboto. Niko Tarime na familia yangu iko Tabata Segerea lakini nimelala saa 7 usiku kutokana na kizaa zaa hiki maana nilikuwa na kazi kubwa kuwasihi familia yangu warudi nyumbani.Yalikuwa yakitua pia mita chache kutoka nyumbani kwangu. Hataaari kweli kweli.
 
RAIS,
WAZIRI WA ULINZI, MKUU
WA MAJESHI must resign,
we hv had it, this z too
much they must ol GO
nw. Yes, I said it...!
 
Hakuna namna yoyote ya kutetea Uzembe huu uliotokea Ukonga,Ni kweli tukio zima ni ajali,lakini ni ajali ambayo ingeweza kuzuilika...Haiwezekani katika kipindi kisichozidi mwaka kutokee ajali zinazofanana,ina maana next month likitokea tukio kama hili Lugalo bado tutasema ni bahati mbaya?Inabidi Viongozi wetu wajifunze kutoa majibu sahihi kwa maswali magumu.Waziri Wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inabidi atoa maelezo ya kina kwa Umma wa watanzania na kutafuta suluhu ya kuyaangamiza mabomu chakavu...kwa kutumia ujuzi na uwezo ndani ya jeshi lake au kuomba msaada nje ya nchi...Hatuwezi kuona Raia wasio na hatia wanapoteza maisha yao,na sababu inayotolewa na serikali ni ya kizembe eti "ni ajali tu".....hali ya joto kali imesababisha mabomu kulipuka,majibu hayo ni dharau na matusi kwa waathirika na raia wa Tanzania,imefika wakati sasa Viongozi wetu wajifunze kujiuzulu,ikitokea kashfa ndani ya mamlaka yao...Waziri Mwinyi jiteteee!Utetezi wako uandamane na KUJIUZULU!

Nawasikitikia sana wanaoamini kinachoendeleea kwenye kambi za Jeshi ni AJALI??? Jamani fikirieni kwa undani zaidi ruhusuni vichwa vyenu vifanye kazi .... hakuna ajari hapo
 
Back
Top Bottom