Freeman Mbowe, Said Issa na Tundu Lissu, washinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu CHADEMA

Nanyaro Ephata

Verified Member
Jan 22, 2011
1,165
2,000
Matokeo ya uchaguzi mkuu Chadema yametangazwa ambapo Freeman Mbowe amepata ushindi wa Tsunami. Mbowe ambaye amekiongoza chama hicho kwa miaka kumi na tano sasa alishangiliwa mno na wajumbe wakati matokeo yakitangazwa na msimamizi wa uchaguzi Sylivester Masinde.

Mbowe amepata ushindi wa asilimia 93.5 ya kura zote huku mpinzani wake Cecil Mwambe akiambulia kura 59.Tundu Antipass Lissu amezoa kura karibu zote kwa asilimia 98.8.
1576730085632.png

Matokeo yote ya uchaguzi CHADEMA ni kama yanavyoonyesha chini.

MWENYEKITI WA TAIFA
1.Freeman Mbowe-886-93.5✔
2.Cecil David Mwambe- 59
3.HARIBIKA -3

MAKAMU MWENYEKITI BARA
1.Tundu Antipas Lissu-930-98.8%✔

2.Sophia H.Mwakagenda-11- 1..2%
HARIBIKA 9

MAKAMU MWENYEKITI ZANZIBARI
SAID ISSA MOHAMED
NDIYO 859-88.7%✔
HAPANA 95
HARIBIKA 12

Zaidi, soma:

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,510
2,000
Matokeo ya uchaguzi mkuu Chadema yametangazwa ambapo Freeman Mbowe amepata ushindi wa Tsunami. Mbowe ambaye amekiongoza chama hicho kwa miaka kumi na tano sasa alishangiliwa mno na wajumbe wakati matokeo yakitangazwa na msimamizi wa uchaguzi Sylivester Masinde.

Mbowe amepata ushindi wa asilimia 93.5 ya kura zote huku mpinzani wake Cecil Mwambe akiambulia kura 59.Tundu Antipass Lissu amezoa kura karibu zote kwa asilimia 98.8.

chadematzofficial_20191219_2.jpg

Matokeo yote ya uchaguzi CHADEMA ni kama yanavyoonyesha chini.

MWENYEKITI WA TAIFA
1.Freeman Mbowe-886-93.5✔
2.Cecil David Mwambe- 59
3.HARIBIKA -3

MAKAMU MWENYEKITI BARA
1.Tundu Antipas Lissu-930-98.8%✔
2.Sophia H.Mwakagenda-11- 1..2%
HARIBIKA 9

MAKAMU MWENYEKITI ZANZIBARI
SAID ISSA MOHAMED
NDIYO 859-88.7%✔
HAPANA 95
HARIBIKA 1

Uchaguzi umefanyika kwa utulivu mkubwa huku wagombea wakipewa nafasi ya kujinadi kwa wajumbe bila hofu yoyote na kwa uhuru mkubwa.

Wajumbe kadhaa wa mkutano mkuu wakitoa maoni yao baada ya matokeo kutangazwa wamepongeza kwa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa kwa demokrasia na kusema hiyo ni heshima kubwa kwa chama chao ndani na nje ya nchi.

Baraza Kuu linatarajiwa kukutana leo kumchagua Katibu Mkuu wa chama hicho na manaibu wake wawili watakaopendekezwa na Mwenyekiti aliyechaguliwa Freeman Mbowe.

#NoHateNoFear

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,543
2,000
Hongera zao mashujaa wetu Freeman Mbowe na Tundu Lissu na hakika "wishes" za jamaa zetu wa Lumumba za kutupenyezea wasaliti wao zimeshindwa!

Hakika uwepo wa chama cha CHADEMA ni mpango wa Mungu na yeyote anayetamani kukiua chama hicho atapambana na hasira za Mungu wetu aliye Mkuu kuliko kitu chochote hapa duniani
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom