Huyu Dj anajua kuwa na yeye ni dikteta au kwa vile Chadema hawamwambii ukweli? sifa moja ya madictator kung'ang'ania madarakani

Sitaki kuamini kama Chadema wote hawana akili mwenye akili ni Mbowe tu lakini kumbukeni Mbowe ni Binadamu kuna siku atakuwa hayupo leo JPM hayupo lakini CCM ipo na inapata mwenyekiti mwingine kwa amani kabisa kila mtu akitabasamu kwa maana utaratibu ulishatengenezwa siku Mbowe akiondoka tutashuhudia ugomvi na kugombea madaraka ndani ya Chadema .
Afande Selle; ni vyema ukawa na tabia ya kujikita ktk kusoma hoja kwanza badala ya kukurupuka. Anyway, naona ni ile mibange yako na ile albadirr uliyosomewa.
 
Sasa Mkuu ikiwa Mama anasema anafuata nyayo za Magufuli aliyekimbiza wawekezaji lakini wakati huohuo anataka kurudisha imani ya wawekezaje wewe unaelewa nini ?
Hapo ni wewe wa kutakiwa kutumia akili vizuri. Hawezi kumkana Magufuli akiwa ndio aliyemfikisha hapo alipo.

Vile vile akiwa kama rais hawezi kuacha kufanya kile anachokiamini na chenye faida za miaka mingi ijayo kwa Tanzania.

Jiweke wewe kwenye nafasi ya Mama, ungeongea nini pale bungeni mbele ya mamilioni ya watanzania.
 
Mbowe ni CCM puppet. Hawa ndiyo engineers kuhakikisha CCM inashinda na wapo kwenye payroll.....semeni nidadavue
 
Nadhani bado hajamuelewa mama. Mama hawezi kuwa against kabisa na kila kitu. Hiyo system mbovu ndiyo ilyomuweka madarakani. Hebu tu,pe muda tuone atatupeleka wapi. Mi naona kuna tofauti kubwa.
 
Tatizo la Rais Samia Suluhu Hassan ni kuingiwa na hofu ya kuwakwaza wafuasi wa Magufuli. Anaonekana kutaka kuwa mpatanishi wa makundi ndani ya CCM. Yaani Kundi la Mwendazake na Kundi la Samia na wafuasi wake. Kundi la Mwendazake linalituhumu Kundi la Samia kwamba limemuua mtu wao na Kundi la Samia linapinga madai hayo.

Taifa linazidi kuwa njia panda. Ni kweli SSH anateswa vilivyo na kivuli cha JPM. Kila akitaka kujitutumua bado anadidimizwa chini. Ndiyo maana kila alipotajwa JPM makofi bungeni yalizidi, ila akitajwa Kikwete hawapigi makofi maana wanamtuhumu Kikwete kuwa nyuma ya SSH. Wanamtuhumu JK kuwa alikuwa hampendi JPM. Wanamtuhumu SSH kuwa ameshikwa masikio na JK. Kazi bado ipo!

Unalihutubiaje bunge linaloundwa na wabunge wasio kuwa na Chama?
 
Mbowe hajielewi hajawahi kukanusha alipoangushwa na konyagi kusingizia amepigwa na wasiojulikana
 
Huyu Dj anajua kuwa na yeye ni dikteta au kwa vile Chadema hawamwambii ukweli? sifa moja ya madictator kung'ang'ania madarakani

Sitaki kuamini kama Chadema wote hawana akili mwenye akili ni Mbowe tu lakini kumbukeni Mbowe ni Binadamu kuna siku atakuwa hayupo leo JPM hayupo lakini CCM ipo na inapata mwenyekiti mwingine kwa amani kabisa kila mtu akitabasamu kwa maana utaratibu ulishatengenezwa siku Mbowe akiondoka tutashuhudia ugomvi na kugombea madaraka ndani ya Chadema .
Siku hizi umekuwa mganga wa Kienyeji? Naona unaendelea kuagua.

Ni kweli SSH amejitwisha zigo la kupatanisha makundi ndani ya CCM. Kundi moja linalituhumu kundi lingine kwamba limemuua mtu wao. Kundi linalotuhumiwa linajitetea. Ashughulikie Taifa siyo makundi ya CCM. Hata ambao hawamwamini SSH ni hao hao ndani ya CCM.
 
Kiukweli nimemsikiliza mwanzo mwisho lakini sijaelewa anachosimamia
SSH yupo njia panda. Anatamani kukidhi kiu ya watanzania lakini kivuli cha CCM na cha Mwendazake vinamkwamisha mama na nia yake nzuri. Kama hivi wameanza kusema mtu wao aliuawa.
 
Unaishi kwa kujivunia ujinga. Jielimishe, angalao ujie hata ileaana tu ya neno dikteta.

Kwa uelewa wako, Angel kule Ujerumani, ni dikteta? Tony Yam, kule Singapore ni dikteta?
Basi nyumbu mnayofautiana mitazamo maana wenzako wengine wanasema moja ya vigezo vya udicteta ni kung'ang'ania madaraka.
 
kwenye hiyo tweet ya kimombo - hapo Lumumba jamaa wananyan'ganyana dictionary ...teh teh teh
 
Hawa wanasiasa wawili wanaokuwa na tabia ya kujinasibu kuwa wao mabingwa wa uzandiki wa siasa za hapa Tanzania mbona wako Kimya?

Au ndio wanaunga juhudi kimyakimya maana tumeshuhudia miaka mitano chini ya hayati JPM wakiburuzwa na kugarazwa kama kambale kwenye matope.
Kwa viwango tulivyoviona miaka 5 tuliyopita, Mwendazake ameburuza kila mtu Tanzania labda alimshindwa CDF Mabeyo tu. Maana Bunge, Mahakama, Magereza, Tume ya Uchaguzi, CCM yenyewe, viongozi wastaafu nk. Wote hawa Mwendazake aliwadharau na kuwaburuza atakavyo.

Sasa Rais SSH tunaona mpaka anatamka neno Demokrasia, Vyama Vya Siasa, Utawala wa Haki na mengine mengi. Bado haturidhiki? Kama Freeman Mbowe hawezi kushukuru kwa machache ambayo Rais ameahidi.

Mwanadamu yeyote yule anapenda kupata appreciation kwa yale mazuri anayofanya. Kama Mbowe haoni tofauti kati ya SSH na Mwendazake itakuwa ni kwa sababu ya malyenge ya Ubongo.

Hivi kweli SSH yuko sawa na MAGUFULI? Pengine SSH anatumia lugha ya tatsida ya hali ya juu ambyo Mbowe ameshindwa kutambua.
 
Huyu Dj anajua kuwa na yeye ni dikteta au kwa vile Chadema hawamwambii ukweli? sifa moja ya madictator kung'ang'ania madarakani

Sitaki kuamini kama Chadema wote hawana akili mwenye akili ni Mbowe tu lakini kumbukeni Mbowe ni Binadamu kuna siku atakuwa hayupo leo JPM hayupo lakini CCM ipo na inapata mwenyekiti mwingine kwa amani kabisa kila mtu akitabasamu kwa maana utaratibu ulishatengenezwa siku Mbowe akiondoka tutashuhudia ugomvi na kugombea madaraka ndani ya Chadema .
Mbowe na chadema ni kama kanisa la mama lwakatare,kafa na kanisa limekufa.
 
Back
Top Bottom