Rais SSH anateswa na kivuli cha JPM. JPM & CCM mlitaabisha sana Taifa. Rais anaendelea kujisifu kuwa sehemu ya utesi huu. Hajutii. Bila kukiri & kutubu ni ubatili. Bunge haramu nalo giza! Rais kachagua kutafuta suluhu ya CCM siyo Taifa. Kazi bado ipo. Tusibweteke. Muda uongee!

 
Hawa wanasiasa wawili wanaokuwa na tabia ya kujinasibu kuwa wao mabingwa wa uzandiki wa siasa za hapa Tanzania mbona wako Kimya?

Au ndio wanaunga juhudi kimyakimya maana tumeshuhudia miaka mitano chini ya hayati JPM wakiburuzwa na kugarazwa kama kambale kwenye matope.
 
Hicho kikao cha Mbowe na Samia kikitokea kitanoga sana, nimejiuliza inakuaje Rais anasema atalinda demokrasia kwa kutaka sheria ifuatwe, lakini bado anakuwa mgumu kuruhusu mikutano ya kisiasa iendelee sababu ipo kisheria mpaka wakakutane ikulu, hiyo kauli ya Mbowe hapo juu ndio inatoa majibu ya doubt yangu.
 
Kama ulitegemea akupe uongozi sahau.
 
Huyu Dj anajua kuwa na yeye ni dikteta au kwa vile Chadema hawamwambii ukweli? sifa moja ya madictator kung'ang'ania madarakani

Sitaki kuamini kama Chadema wote hawana akili mwenye akili ni Mbowe tu lakini kumbukeni Mbowe ni Binadamu kuna siku atakuwa hayupo leo JPM hayupo lakini CCM ipo na inapata mwenyekiti mwingine kwa amani kabisa kila mtu akitabasamu kwa maana utaratibu ulishatengenezwa siku Mbowe akiondoka tutashuhudia ugomvi na kugombea madaraka ndani ya Chadema .
 

Baba moja mama moja labda ana wasiwasi mwendazake atarudi kuja kumfurumusha Ikulu
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kama kutakua na korosho na juice ya embe tafadhali ACT au CHADEMA msiniache nyuma nitawasindikiza huko kwenda kuongea na Rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…