Thread hii inanikumbusha shairi nililosoma nikiwa darasa la tatu mwaka 1983
na shairi lenyewe sijalisahau mpaka leo hii linasomeka hivi :-
Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia,
Hadithi uliyongoja leo ninakuletea,
Alitoka siku moja njaa aliposikia,
njaa aliposikia,sungura nakuambia.
Siku ile akaenda porini kutembelea,
Akayaona matunda mtini yameenea,
sungura akayapenda mtini akasogea,
Mtini akasogea,sungura nakuambia.
Sungura karukaruka,
Lakini hakufikia,matunda hakuyashika,
Mikononi hakutia hakika alisumbuka nguvuze zikapungua ,
nguvuze zikapungua,sungura nakuambia.
SIZITAKI MBICHI HIZI,
Sungura akagumia naona nafanyakazi bila faida kujua,
yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia sungura nakuambia,
Sio kama hakutaka sasa nakupasulia,
Matunda liyataka ndio kisa akalia,
Tunajua hakufika alichoka kurukia,
alichoka kurukia,sungura nakuambia.