Eti hatujui... kipimo gani kinatumika?

Eti hatujui... kipimo gani kinatumika?

nafikiri hakuna kipimo ni namna tu utakavyoweza kumrithisha huyo mwenzio makafurahia mapenzi yenu si dhani kama kuna kipimo, hivyo tunaweza kusema mapenzi ni subjective, kila mmja ana namna yake alafu pia utamaduni una mchongo mkubwa wa jinsi mapenzi ya jamii yatakavyokuwa
 
kuna mavitasa yanakuwa laini ukiyanunua dukani, kayaweke mlangoni halaf yape mwezi tu utaona yameng'ang'anaa hata hiyo nyundo ukigonga inadunda, ukijifanya kuyapaka girisi sana sana utachafua nguo zako tu. (hapa nimezungumzia romance kifasihi, sjatoka nje ya mada wajameni)

lol........
 
halafu klorokwini baada ya kuandika nikafikiria hivo aisee...lol
usikute sasa na vitasa vingine bana kuna yale mafunguo mengine yenyewe hayana specifications yanafungua tu....hahahaaaaa!
Sipo

specification ya nini?lol
hivyo hivyo tu lol
 
nafikiri hakuna kipimo ni namna tu utakavyoweza kumrithisha huyo mwenzio makafurahia mapenzi yenu si dhani kama kuna kipimo, hivyo tunaweza kusema mapenzi ni subjective, kila mmja ana namna yake alafu pia utamaduni una mchongo mkubwa wa jinsi mapenzi ya jamii yatakavyokuwa
Hapo red hapo mkuu umeleta hoja nzito sana, takriban sote katika huu mjadala tumelifumbia macho hilo.
 
mkuu majukumu ni kwa mkeo au mpenzi wako tayari....
But mahaba yanaanza hata kabla hajawa wako....
Yanaweza kuwa chanzo hivi....

Tena hapo ndio yanafika maximu...Mtu akiyakosa wakati huo basi tena, imekula kwake!!

The Boss

Kwa kijijini labda ukirudi home mama watoto ukisikia yupo kisimani, kwenda kumfata huko, na kumpokea ndoo ya maji ukabeba wewe

Mwanamume wa kiafrika hawezi kubeba ndoo ya maji au kutwanga makande akabaki kuitwa mwanamume...Enzi zetu mtu wa namna hiyo haruhusiwi kabisa kukaa kwenye vikao vya wazee!! Anakuwa amejipiga ban mwenyewe!

umeona ehhh?
Dark city umeona hii?
Wanajua kuwa tuko romantic ile mbaya...but wanataka.....the hollywood type.....
Hili ndio tatizo nowadays....

Kweli ila siyo kwa kubeba ndoo ya maji....Hapana mkuu!!

hapa kazi ipo! kwa hiyo romantic ni lazima iishie kwenye sex?? mtu hawezi kuwa romantic kwa mama yake, baba yake, watoto wake, na wengineo?

Hii ni version mpya ya mahaba...Kama dot com wamefika huko basi wana hatari isiyo na kipimo!!

Niwe na mahaba na mama yangu mzazi kweli, halafu hapo watu wasema akili yangu haijapata fracture???

kichwa chako bado kabisa kina chemka mwayego!!!
khaa, unakuwaje romantic kwa kutimiza wajibu wako kama mke/mume? (ndo maana wanaambiwa hawako romantic maana kumbe hata hawajui unakuwaje romantic....lol!!!)

The other way round...Unaweza kuwa romantic wakati hutimizi wajibu wako kama mume???

Unabeba ma-apples, chorcolates, hugs za kukata na shoka wakati nyumbani hakuna hata nusu kilo ya unga....Hapo utakuwa romantic kweli wakati la azizi wako ana njaa au anaenda kuomba chumvi kwa jirani???
 
Mkuu unaweza kuwa romantic wakati nyote mna njaa.....

Na unaweza kuwa mtimiza wajibu kwa asilimia mia lakini usiwe romantic

Na unaweza laazizi wako akawa na njaa na wewe ukawa romantic (hasa wakati wa kuchumbiana) ....maana jukumu la njaa yake si lako
 
Hapo red hapo mkuu umeleta hoja nzito sana, takriban sote katika huu mjadala tumelifumbia macho hilo.

Klorokwini

Post yangu ya kwanza ya thread hii nilieleza kuwa neno Romantic asili yake ni maana ya "Relating to Rome", (and it was more on art and beuaty) kwa hiyo kwetu tusio na asili ya Roma au tusioguswa na utamaduni wa Roma haliwezi kuwa na maana sawa na wa huko Magharibi, na ndo maana hata neno lenye maana halisi ya Romance kama wanavyolitumia wenyewe hakuna kwetu
 
mi naona kwamba wangeweka vigezo ambavyo vinaeleweka halafu tungeweza kujua tatizo

Sijaona mwenye vigezo ambavyo ni universal hata mmoja...Ila naona wanachokubaliana ni kuwa ukiwa zoba zoba kidogo basi mahaba yanakuwa >100%

....kwa mara nyingine tena, tupo ukurasa mmoja!....safi sana,.....hata kumletea mke zawadi (bila kutegemea/kukusudia sex in return!) iwe ni peremende au kitenge ndiyo mahaba yenyewe hayo....

...itafsiri romantic kwa kiswahili----mahaba!----mapenzi!-----, utagundua inawezekana sana tu...
tatizo nilionalo hapa, wengi wetu tukisoma romance tayari mawazo yanahamia ndani ya shuka, mmefunga mapazia, taa mmezima, na nyie wawili mnanong'ona....----

Hahahahah,

Kwangu mimi mahaba ambayo hayaishia kwenye burudani ya baba na mama siyataki..Labda kama tunaigiza!

Hata hivyo suala la maandalizi nakubaliana nalo, siyo kusubiri baada ya taa kuzimwa!!

umeona eh... ndi maana nikamwambia DC kuwa hao wanaowasifia na kuwang'ang'ania nje wanafanya hivyo kwa kuwa huwa wanafanya extras!! Akifika kwa bi mdogo DC atatoa tabasamu la nguvu; atatoa hug la mpaka anazunguka naye kama si kumbeba juu juu kuonyesha alivyofurahi; atambusu na wengine atamshikia mpaka nyama wakati wa kupika jikoni huku wakipiga vistory vya hapa na pale wakati akija nyumbani kwake anafikia kukumbati a remote na kugandisha macho kwenye TV akisubiri Mkewe amalize kupika ale akaoge. Hakuna cha kukumbatia, kukiss wala kusaidia nyama jikoni na story.

Hizo extraz hizo, hivyo vya ziada hivyo ndo mahaba yenyewe!.

Naona sasa unaanza kupotoka...Hizo package za London, Paris, na kwingine huko umezitoa wapi? Mwanamume wa kiafrika hawezi kufanya hayo ila bado atakuwa romantic in his own way.....!!
 
Klorokwini

Post yangu ya kwanza ya thread hii nilieleza kuwa neno Romantic asili yake ni maana ya "Relating to Rome", (and it was more on art and beuaty) kwa hiyo kwetu tusio na asili ya Roma au tusioguswa na utamaduni wa Roma haliwezi kuwa na maana sawa na wa huko Magharibi, na ndo maana hata neno lenye maana halisi ya Romance kama wanavyolitumia wenyewe hakuna kwetu

Niliona hiyo post lakini hakuna aliobase argument yake kwenye tradition zetu except ambae amekuwa close kidogo ni The Boss na gunia lake la mkaa.
Mfano ulizungumzia mwanaume kubeba ndoo za maji, kwa baadhi ya maeneo mwanaume kubeba ndoo za maji anadharaulika hata katika jamii ya wanawake wenyewe, sasa hapa unakuta utamaduni unaathiri romantic ways of life.
 
Hoja hii imesimamiwa vizuri na DC pia.

Basi tukubali kuwa Mtanzania si romantic by nature ......lol ...kwa sababu wanaotetea bado hawajatu convince kuwa wanavyofanya ni romantic.

Inawezekana ikawa tatizo ni kuwa tuna define romance kwa mentality ya Magharibi ndo maana.
 
Kuna mavitasa yanakuwa laini ukiyanunua dukani, kayaweke mlangoni halaf yape mwezi tu utaona yameng'ang'anaa hata hiyo nyundo ukigonga inadunda, ukijifanya kuyapaka girisi sana sana utachafua nguo zako tu. (hapa nimezungumzia romance kifasihi, sjatoka nje ya mada wajameni)

heheeeee la hivyo dawa yake libadilishe kabisa, utakuwa lazima ulikosea funguo au uliipoteza!
 
specification ya nini?lol
hivyo hivyo tu lol

specifications si ndo sifa ya kufungua kitasa husika? vinginevyo uktakuwa unafosi, matokeo yake ndo kama hayo ya kuweka grisi na oil chafu mwishowe uchafuke bure!
 
Mkuu DC, unanikimbusha thread moja hapa ya "Keep the flame burning" yaani kwa mitazamo yao bila uzungu hakuna cha flame burning hapo!

Tatizo ninaloliona ni kutaka kuchukua tamaduni za nje kisha kulazimisha iwe na sisi tunazo. Kama hatuna tamaduni ya kufanya romance ndio hatuna, lakini tuna nyengine labda. Culture hazifanani, tukubali

Wazungu wana tamaduni wa kufanya mbwa pets wanaingia ndani wanafanya kila kitu kama binaadamu, sisi hiyo hatuna kwa mfano .......
 
mkuu unaweza kuwa romantic wakati nyote mna njaa.....

Na unaweza kuwa mtimiza wajibu kwa asilimia mia lakini usiwe romantic

na unaweza laazizi wako akawa na njaa na wewe ukawa romantic (hasa wakati wa kuchumbiana) ....maana jukumu la njaa yake si lako

gaijin
hili la njaa ya mchumba kuwa halituhusu wakati wa kuchumbiana
linahitaji thread yake peke yake aisee lol
 
Njoo huku nikufundishe, hakika hautojutia.
Wanasayansi wamesema romance ukizijulia hauzeeki mapema na hata ukizeeka hautang'oka meno ya mbele.
Zisije kuwa zile za kuigiza mpaka mwenzako anaona aibu, yaani wanaume waigizaji wananiudhi, hata utamwona amekaa mahala na mpenzi wake anataka kufanya mambo ya kwenye movie, kasahau wenzake wamelipwa pale,
 
Back
Top Bottom