Gaijin
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 11,812
- 5,303
Ahsante sana Mwalimu wangu,
Siwezi kuacha kuwa na wasi wasi ndugu.. Unajua, enzi zetu wanawake walifundwa na kufundishwa kusema maneno mawili makubwa kwa mume wake ..."NDIYO" na "AHSANTE"!!! Sasa inawezekana mama DC bado anaaply hayo mafunzo na mimi nakenua mijino kwamba ninaweza kumbe patupu!!!
Hata hivyo huwa anafurahia migunia yangu ya mikaa na kuku wa Boss,... ingawa maji simsaidii kubeba!!
Kuna kitabu kimoja nilisoma mwandishi Mzungu anasema
"Waafrika ni masikini mno, na kwa nadharia ya Kimagharibi umasikini ule lazima ukufanye unhappy, lakini kwa vile Waafrika hawana/hawajui zaidi ya kile wanakuwa maskini na happy vya kutosha pengine zaidi ya hata Mzungu tajiri kiasi"
So falsafa hiyo inaweza kuwa inahusika. Kwa wale walotizama Egoli sana na kuishi ughaibuni hata wakifundwa vipi unakuta system ishachakachuliwa. LOL ....Lakini wa enzi hizo, vitu simple anafurahia vya kutosha, hamna kukwazana na mwenza wake kwa vitu viso msingi