Eti hatujui... kipimo gani kinatumika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti hatujui... kipimo gani kinatumika?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dark City, Sep 26, 2011.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Jana nimesoma makala ya Freddy Macha kwenye gazeti la Mwananchi iliyokuwa inaongelea mijadala inayoendelea kwenye mitandao mbali mbali ikieleza kuwa wanaume wa Kitanzania (na labda Waafrika wote) hatujui mahaba (romance)!

  Nimeguswa sana na makala hiyo. Si kwa sababu napingana na hoja za hao wanaosema hivyo, bali nina wasi wasi kwamba vigezo vinavyotumiwa vinaweza kuwa siyo sahihi.

  Inawezekana hii mada ilishajadiliwa hapa pia, ila naomba tu kupata maoni ya wadau wa jukwaa letu hili tukukufu kuhusiana na issue hii.

  1. Ni kweli wanaume wa Kitanzania hawajui mahaba??

  2. Kama hawajui, ni kosa lao peke yao au na wenzi wao (wanawake)???

  3. Na vigezo gani vinatumiwa ku-judge kama mtu anajua mahaba au la?

  Naomba maoni yenu!!

  Babu DC
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  its complicated......

  ukiwauliza wadada wa kenya na uganda watakwambia wanaume wa tanzania ndo best.....
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  but nionavyo mimi ni kuwa tumegawanyika

  wapo ambao hawajui au tuseme hawana mahaba ya tamthilia za akina alejandro
  ,hasa wa mikoani na vijijini......na hapa namaanisha romance...na sio love.....

  dunia imebadilika mno.....juzi hapa kuna thread ilianzishwa na afrodenzi kuhusu siku ya ku propose

  nikajiuliza....am i old fashioned guy or what?

  kwangu mimi ku kneel down na ku propose imekaa ki hollywood zaidi...
  but wadada wa sasa wanataka hizo pia....go figure....
   
 4. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tatizo ukilinganisha sana ndio unajikuta unaona nani ni best, mie pia
  kuna mambo naona kabisa watu ni ya kuiga sana kama hilo la
  kupiga magoti na kuomba mkono wa ndoa, ile ni mila yao, wanafata
  na sie bila hata kuuliza ina maana gani utakuta jibaba la kibongo
  eti nae anaiga hiyo, mie kwanza ukipiga tu goti natoka mbio, nitaona
  aibu hata sielewi

  Wanaume wetu wa kibongo wanajua sana mapenzi in their own way
  kazi kwao wanaolinganisha na kina tom cruise
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280

  we mtoto umeandika pointi hapa
  au ndo unanitega aisee lol
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kweli mkuu,

  Baada ya kusoma hiyo makala ya Macha, nilitamani kumuuliza bibi yangu (about 90yrs old) hilo swali. Bahati mbaya niko mbali naye...Whatever the case,....nadhani bado tuna safari ndefu ya kuji-define kama Watanzania wa karne hii!!
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  BB, umegonga home kabisa....

  Hivi kweli mtu ukilikuta jitu kama Babu DC limepiga magoti linaomba uchumba wa mke wa 4 au liko pale kwenye viwanja vya Posta ya zamani linampiga piga busu mke wake utaliewa kweli???

  May be kama alivyosema Boss, tunasumbuliwa na hang-over ya maisya yetu ya 1947!!
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  au unaongea kwa sauti laaini huku mdomoni unatafuna ncha ya miwani
  na mrembo anakutazama kwa tabasamu hivi lol
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ukifikia hapo itakuwa kasheshe...

  Enzi zetu kijana wa namna hiyo alikuwa automatically anahesabiwa kuwa ni fungu la kukosa! Tulizoea kuwaona wachumba wakitafuna kucha au kuandika kwenye udongo maandishi ambayo hayasomeki.

  Kumbe siku hizi vijana ndio wanafanya hivyo........???

  Ngoja niishie hapo kwani ninaweza kutoa machozi nikipiga picha na kuwaona wajukuu zangu (boys) wanafanya upuuzi kama huo!!
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mkuu dunia imebadilika mno
  ni kweli yapo mambo inabidi twende nayo but mengine mimi naona ni upuuzi...

  ukitazama relationship za watoto wa shule wa siku hizi ni tamthilia tupu....

  unakuta wengine wanatoka familia duni mno but wanaangushiana birthday party
  za nguvu na kumbi zinakodishwa hadi unashangaa,wakati wazazi wao home wanakopa
  mchele kwa wapemba madukani....yote kuiga wanachoona kwenye tv.....

  its complicated......mfano sasa wadada kkama huna culture ya kumpigia simu kila siku
  wana tafsiri humpendi...sasa jaribu kujiuliza hizi simu zimeanza lini?????/
   
 11. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #11
  Sep 26, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nilibahatika kuuona huu mjadala kupitia wanabidii.........it was hot. Watu wanajibu hoja kwa references jamani ah. kuna points zilizungumziwa kule nikabaki kumwomba mwenzi wangu abakie wa kibantu kama alivyo.
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Tupe basi uhondo kidogo ndugu yangu,

  Hiki kizazi inawezekana kimeshatuacha mbali sana!
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mjone zilete hizo pointi hapa...tujadili

  wadada siku hizi mnataka wanaume wa kuwanunulia maua.....

  hiyo ndo romantic kwenu....

  wakati sisi tumefundishwa na mababu na mababu kuwa romantic ni kubeba kikapu
  na kupitia ferry na kukijaza samaki wa kutosha halafu huyo unaelekea kwa mwenzio na kiroba cha mchele pembeni....lol
   
 14. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwani na ww unategwa?hapo naelezea ukweli, kwa mfano eti kuna rafiki yangu kaachana na bf wake, kisa anaona shida anapoongea kiswahili wakati wa majambo, nikamshangaa sana, mie napenda full kiswahili,wasichana tunatofautiana
   
 15. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,722
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  the boss naona una utani na wapemba wewe, hivi mkurya unaweza kumbebesha kikapu akakubali,zaidi ya kauli ya rara chini nikurenge mama wankuru,mura!
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni mtazamo.

  Kila mtu ana mtazamo wake wa nini haswa ni romantic na mwanamke/mwanaume wa aina gani ni romantic. Kuna mtu mumewe kumpikia ni romantic na mwingine anaona kwa kufanya vile mumewe anajishusha. Kuna mwanaume mkewe kumpigia simu three times a day ni romantic na mwingine anaona ni pure usumbufu. Kwahiyo kwa vyovyote vile...kwa kutumia kipimo chochote kile hamna mtu ambae atakubalika na kila mtu (watu wenye background na mategemeo tofauti ) kwamba yeye ni romantic universally.

  Kujibu maswali yako
  1. Wanaume wa Tanzania ni romantic. Just not to everybody.
  2.Kama sio kwa baadhi ya watu sioni kwanini kosa liwe la yeyote yule. Ni vizuri kila mtu akawa vile alivyo...wanaopenda his kind of romantice watakuwepo na ikitokea bahati nzuri akawa na mahusiano na mmoja wao hakutakua na malalamiko kati yao.Akikutana na ambae ni tofauti basi ni jukumu la huyo mwenza kumjulisha mwenzake kwamba ningependa kitu fulani na fulani ili nifurahi na iwapo hicho kitu kiko ndani ya uwezo na matakwa ya mwanaume basi kitafanyika.
  3. Vigezo vinaofautiana kati ya mtu na mtu/sehemu na sehemu.Hamna kipimo ambacho ni universal amabcho majibu yake kila mtu atakubaliana nayo.
   
 17. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,722
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  kwa hiyo wakati wa ku do kingereza kwake ndio mshiko? huyo shost wako mjinga sana inaelekea ni tamthilia hizi za akina marichui na second chance zimemharibu,lol! mpe pole zake manake siku akikutana na ambaye mizuka ikimpanda anaomgea kilugha sijui atasema ana mashetani.
   
 18. Salma osman

  Salma osman Senior Member

  #18
  Sep 26, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmmmh!!! I don't believe so!
   
 19. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Watu wanapenda mapenzi ya kuigiza sana
   
 20. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,722
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  hiyo point ya tatu imesimama sana lizy for sure hamna kipimo universal na sijui kingekuwepo SI unit yake sijui ingeitwaje
   
Loading...