Eti hatujui... kipimo gani kinatumika?

Eti hatujui... kipimo gani kinatumika?

Meku, ndo pakuwa creative sasa hapo. we kila siku tu utaleta mapera? si utasababisha mwenzio apate tabu ya tumbo? kw anini usitafute manjonjo mengine tofauti tofauti vile....
siku ingine mcheze pamoja (eeh hata wakubwa wanaruhusiwa kucheza), mnakimbizana hadi kijasho kiwatoke kisha muoge maji ya hiliki (yu wapi MJ1 atoe resipi anazomwekea soulmate wake hapa...lol)
Mkeku, kwa hiyo kua creative ndo "mahaba" yenyewe sio?
 
Kuna vitu vingi mbona Kimey ......usiniangushe
Wewe ukisikia nyimbo huko nje ikakukumbushia laazizi, unamtumia ujumbe kumwambia .....thats romantic
Mwalimu taratibu taratibu ntaelewa kutofautisha hivi vitu ngoja nieendelee kuwasoma!
 
Mkeku, kwa hiyo kua creative ndo "mahaba" yenyewe sio?

haswaa Meku! kwanza kununua mapera kila siku wewe mwenyewe si unachoka? yaani kila siku upite kwa mpemba....aaagggrr!! fanya kitu kitakachokufurahisha ukimwona wa ubani anavyokifurahia kwa wewe kumfanyia! mwisho wa siku mmoja wenu kuwa romantic kumpelekee na mwingine kuwa na mwitikio huo huo....

kuna mahali Gee kaandika.....sooo sweeeeeeeeeeeeeet na tha is sweet!!! sikilizia tu tofauti ya hayo matamshi. moja lazima hata wewe likukate stimu
 
Na hiyo creativeness si lazima mwenzio apende sio? ishu inakuja hapo unapeleka pera kumbe yeye anapenda komamanga, kweli kaazi ni kwetu!
Halafu Mwalimu hii mahaba ni one way traffic?

khaa hebu mwaswali basi elekeza na kwa seminar leaders...mwalimu tu???

MEKU, kazi si kwenu tu, ni kwetu sote.
si kwamba ni nyie tu ndo muwe romantic.....its two way traffic aisee!

halafu shurti umsome mwenzio (mpinzani wako kama kloro alivosema) ufahamu mamabo gani hupendelea
 
hapa kloro anaweza saidia kutengeneza the best romantic picture itakavyokuwa lol

nakupa mfano......

Wewe bee ndo wife wangu....umekaa kibarazani unapiga story na wenzio...
Mimi nakuja kwa mbaali...kulia nimeshika kuku na kushoto kuku...wanalia lia...
Unaniona.....unawaambia watoto...kampokeeni baba enu nyi watoto...lol
watoto wanakuja huku wanaimba 'baaba kaleta kuukuu...'majirani wanakuonea wivu.....

Hiyo sio romantic?????? Kumbe je????????lol

.....Uko sahihi mkuu...Umenikumbusha jinsi tulivyokuwa tukimbilia dingi kupokea zigo la nyama, samaki etc...Ila pia ningeongeza vionjo vingine kwenye hiyo package kama vile kapu la ngogwe (nyanya chungu), matunda damu, kokomanga, ubuyu, miwa, mananasi, mapera kidogo, malimau... etc

siku nyingine usinitolee mfano......

daaah Bosi kwa hiyo kuwa romantic kunategemeana na mtu na mazingira pia. mimi ukileta hivyo naona ni sehemu tu ya wajibu wako kama baba wa familia. lakini kuna vijimambo tu vidogo bana ukifanyiwa unajihisi uko ahera wallah tena...

kwa mfano akicheza na jina langu na kuja na jina lingine (yaani hakuna mtu mwingine alishawahi niita hila jina...its so unique) kwa kweli najiskia raha sana, au akinisifia sifia hivi kama nimefanya kitu vizuri au nimeonyesha maendeleo kwenye mambo fulani fulani, that is soo romantic to me!!!!
(does anyone need money to be romantic in such a case?)

Sasa wee Bee, una maanisha hivyo viroba vyetu tuvipeleke wapi kama siyo kwa wandani wetu ili laazizi akatangaze mtaani kwamba store yake haikauki??? Kuna mama mmoja alikuwa akijaziwa store yake anaunda charity chap chap na kuanza kugawa mtaani...Is that not mahaba????


....wakati nikikutayarishia jibu, nami naomba nikuulize swali la kizushi ewe mkuu mstaafu....baada ya kupata hiyo kitu roho inataka, aka 'great' sex....romance/mahaba yanaishia hapo?

Hivi wewe Mbu unatokea dunia gani???? Baada ya kugawa dozi kazi ya mwanamume imefikia kikomo.....Ni jukumu la mama kushukuru kwa chakula murua na kuanzisha hadithi hadithi...Akichelewa unavaa suruali na kuwahi kijiweni kupiga hadithi!!

Generally, mwanamume akishatua mzigo hapendi kusumbuliwa kwa lolote....The chapter is closed till next time!!!

Naamini hawa wajukuu watazingatia maneno yangu...



Loh Mzee DC swali langu mie umelifukia wataka lako nilianike sawa hiyo kweli?
Wewe mwenyewe ushasema kuwa wanaolalamika hivyo kuwa 'hamyajui/hamko romantic ni wake zenu majumbani' ilhali wale mnaokutana nao mara 2 kwa mwaka wanawasifia na kuwaganda. Sasa si ina maana mnajijua na sababu mwaijua??

Mie nlishasema moja, ukasema utajitetea kisha ukakimbia

Mhhh wewe nawe kwa kukaba....huachii hata penalty??? Wazee wenzangu wamenitelekeza. Hata hivyo kwa wale wanaofanya hiyo kitu, ya kukwenda kustua betri zao ili kurudisha charge...watakubaliana na mimi kwamba kule nje ni balaa...Ukipaendekeza hata watoto wako mwenyewe unawaona kama mashetani!! Ila kwa mshikaji wa ndani bwana...ni bora liende na pia kwa sababu ndio kimbilio la uhakika. Otherwise ni ngumu sana kueleza!

Nimekujibu sasa???
 
Na hiyo creativeness si lazima mwenzio apende sio? ishu inakuja hapo unapeleka pera kumbe yeye anapenda komamanga, kweli kaazi ni kwetu!
Halafu Mwalimu hii mahaba ni one way traffic?

Hii kitu kimsingi inatakiwa kuwa pande mbili.

Nafikiri hakuna mamalishi ya kuwa wanawake si romantic kwa sababu they are au? ...Nafikiri ni the same kama ile role ya kuwa mwanamme ndo anaemfata mwanamke, mwanamme anatakiwa a-initiate na mwanamke anafuatia.

Even though sometimes mwanamke anajitahidi mwanamme wala habari hana.
 
DC no, a big NO! not to me!!!!

lakini ukininunulia tu vitu twa kutafuna tafuna huko njiani akiwa anarudi nyumbani hapo poa, akija napokea kimfuko cha vidagaa mchele vya kukaangwa njiani, firigisi za na makanyagio ya kuku pale kwa mtogole basi alimradi mahaba tu!
 
halafu klorokwini baada ya kuandika nikafikiria hivo aisee...lol
usikute sasa na vitasa vingine bana kuna yale mafunguo mengine yenyewe hayana specifications yanafungua tu....hahahaaaaa!
sipo
Kuna mavitasa yanakuwa laini ukiyanunua dukani, kayaweke mlangoni halaf yape mwezi tu utaona yameng'ang'anaa hata hiyo nyundo ukigonga inadunda, ukijifanya kuyapaka girisi sana sana utachafua nguo zako tu. (hapa nimezungumzia romance kifasihi, sjatoka nje ya mada wajameni)
 
According to klorokwin: Kuwa romantic ni kujenga mazingira ya mapenzi ambayo yatamfanya mwenza wako kila wakati ajiskie raha na furaha kuwa karibu yako. Hii inajumuisha majukumu, uchokozi, utundu, Uhashuo (source:gaijin), SRM nakadhalika nakadhalika.

Romantic gauge: Ukitaka kujijua how romantic u are kwa mwenza wako jaribu kumuaga unaenda safari, huzuni yake ukiondoka na mawasiliano yake wakati upo safarini yatakujulisha ni kiasi gani umefanikiwa kuwa romantic kwake.
Ukiona umemuaga waifu, halaf waifu linafurahia na ukiondoka tu limezima simu na ukirejea safari waifu limenenepa ujue romantic gauge yako iko zero au minus. (Dedicationa yako ni wimbo wa "samaki pole")

Nimemaliza

duh, kama kweli vile!
 
Back
Top Bottom