Edward Lowasa, jina lako si dogo hata kidogo, historia siyo fupi, mchango wako kwa Taifa siyo mdogo, hekima yako si ndogo, uvumilivu wako siyo mdogo, upendo wako kwa binadamu wenzako siyo mdogo.

Nayakumbuka maneno yako siku ile nilipokuona ana kwa ana kwa mara ya kwanza na ya mwisho uliposema, "Kinachonipa hofu siyo kutotangazwa kuwa mshindi wa kiti cha Urais, bali ni nini vijana hawa wanaoniunga mkono watafanya baada ya mimi kutotangazwa mshindi. Ni aheri niukose Urais kuliko uhai wa mtu upotee kwaajili yangu".

Kitabu chako ni kirefu na kumbukumbu rejea yenye mafunzo mengi.

Mzee Edward Lowasa, mwendo umeumaliza, tunamwomba Mungu wa huruma akujalie pumziko jema la milele, na pale ulipopungukiwa, basi mema uliyoyatenda yakalipie hayo mapungufu.

Poleni sana wanafamilia, jipeni moyo kwani hampo pekee yenu. Na wala msipungumiwe imani badala yake mjawe na ujasiri wa kuyapokea mapenzi yake Mungu wetu.
 
R.I.P EN Lowassa

Viongozi wa Umma wanapofariki wanaandikwa kwa mema na mabaya, waliishi kwa ''privilege' ya Umma

Katika mazuri aliyofanyia Taifa ni kuongoza nchi za ukanda wa mto Nile (Riparian states) kupinga Mkataba wa Waingereza na Egypt wa mwaka 1929 kuhusu matumizi ya maji ya mto Nile.

Akiwa Waziri wa Maji na Mifugo ,Lowassa alisimama kidete kuhakikisha maji ya Ziwa Victoria yananufaisha Taifa. Mpango wa Maji ya Victoria Dodoma ni matokeo ya kazi hiyo.
Waanaofaidika na miradi wa maji ya Ziwa Victoria ni kazi ya Lowassa, tunamkumbuka na kumshukuru kwa hilo

Katika mambo mabaya aliyofanya ni kusimama Bungeni kama Waziri Mkuu kupinga KATIBA MPYA akisema iliyopo inatosha ingawa alijua si kweli. Alisimama kutetea Uwaziri mkuu wake na si masilahi mapana ya nchi.

Pili, akiwa Bungeni kama Waziri Mkuu alitetea Richmond kwamba hakuna Wizi. Leo tunajua kulikuwa na wizi ya kutisha si kwa Richmond n.k. Lowassa aliogopa sana Uwaziri mkuu wake kuliko masilahi mapana ya nchi. Hakutetea nchi alitetea hali yake ya baadaye ya Urais

Tatu, ENL alikuwa na matamanio zaidi ya uongozi kuliko wito.
Katika hilo, alifanya makosa mengi kwasababu tu alilenga Urais wake na si masilahi ya nchi.

Muda wake umetimu, tumtakie safari njema, kwamba kuna cha kumkumbuka sana!! linabaki swali

JokaKuu Pascal Mayalla Mag3
 
My feeling ni kwamba aliondoka siku nyingi Sana SEMA Protokali za kikubwa ndio.zilichekewesha kumtangaza!!


Nafsi yangu inaniambia yupo mwingine hatangazwi Hadi Hawa kwanza watangazwe ndio huyo atafuata coz yeye ni mkubwa zaidi kuliko Hawa wanaotangulia Sasa hivi!!

Ngoja tuone!!
Master NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

1. Unadhani alifariki mwezi wa gapi?

2. Huyo mkubwa ambaye hatangazwi ni nani huyu mkubwaaaa?

3. Kuna huyu Mzee EL, na Huyo Mkubwa na vipi hao wengine wanaofanya kuwa na wingi wa kutangazwa hawa kwanza hawa kabla ya Mkubwa hao ni akina nani? Wako wagapi?
 
Taifa liko gizani hatuna umeme kauchuna! Kaibukia kwingine kana kwamba suala la umeme halimhusu!
Mtu alijiuzulu kwa kashfa ya ufisadi, sasa huo uwazir mkuu hiyo heshima inatokana na nini, mtu anasifika kwa wizi wa mali za umma, bado anapewa heshima eti ya bendera kupepea nusu mlingoti.
 
pia ishu ya anoutoglo kuuzwa Lowasa aliamuru ukuta uvunjwe na wananchi fasta waliuvuja.
lowasa pumzika kwa amani baba
Najua alokusababishia gonjwa hili alokuwa rafiki yako mpenzi BOYZ 2 MEN aka JK ataleta unafiki mkubwa kwenye mazishi yako.
Ndo watanzania mjue Wakwere na wazaramo wana unafiki mkubwa sana.
wanakuua huku wakikuchekea
Emmanuel Nchimbi na Hussein Bashe, Iddy Zungu walikuwa bado ni watiifu kwa mzee au walishamsaliti na kuunga juhudi Msoga Gang?
 
Huyo katoka kwenye familia ya kitajiri tangu akiwa mtoto na biashara amefanya sana tu, si aina ya watu ambao walihitaji kujitafuta sana ili watoboe kama ilivyo kwa makupuku wengi hapa Tz.

Ni kama ilivyo kwa Mbowe tu.

Mtu wa pekee ambaye utakuwa sahihi kushangaa utitiri wa mali alizojilimbikizia ni JK kwasababu hata historia ya familia yake inakataa.
Hzi huwa ni fix tuu wanasiasa ni wezi
 
Hili nalo litazamwe
IMG-20240211-WA0000.jpg
 
Lowasa angekuwa Rais haya yanayotendeka Loliondo yasingefanyika. Na hata angekuwa na afya njema haya yasingetokea. Walisubiri Sokoine aondoke wakavuruga Azimio la Arusha, wamesubiri Lowasa aondoke wakauza urithi wa Wamasai wakiwa na lengo la kuzima ndoto za viongozi strong kuzaliwa katika jamii hii.

In absence of Sokoine politicians signed contract to sell part of Serengeti and Ngorongoro to Arab companies; in absence of Lowasa the eviction of maasai will set the strip to fly Dubai
 
Back
Top Bottom