Buriani Edward Lowassa, Rais wa mioyo ya Watanzania

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Sitasahau Mei 2015 uwanja mzima wa Sheikh Amri Abeid, Arusha ukiimba "Lowassa Lowassa, Lowassa Lowassa, sitasahau ile picha Dr. Emmanuel Nchimbi na wengi wa wanachama wa CCM wakiimba "Tuna imani na Lowassa" kwenye mkutano wa NEC 2015.

Kipindi cha mchujo hakijanitoka akilini, Edward Lowassa alikuwa strategist mkuu ndani ya CCM, Edward Lowassa alikuwa Kiongozi mwerevu tuliowahi kujaaliwa lakini waovu wakamchafua na issue ya Richmond, Edward Lowassa akakatwa kwenye mchujo wa Wagombea Urais, wao walidhani mchezo ulikuwa umeishia pale, lakini kilichotokea Edward Lowassa aliujaza uwanja wa Jangwani alipotangaza kuhamia Chadema na kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

-Edward Lowassa mwanzilishi wa falsafa ya Maamuzi magumu.

Watanzania siku zote hupenda watu wenye misimamo na maamuzi magumu, rejea Hayati Rais John Pombe Magufuli alivyopendwa kwa misimamo yake na maamuzi magumu, Mwaka 2015 nchi ilikuwa imetoka katika uongozi wa hovyo ambao wananchi walishauchoka, Wananchi waliamua liwalo na liwe, bora kumchagua yeyote aliyekinyume na CCM au kumchagua mtu ndani ya CCM mwenye maamuzi magumu ataebadili mfumo wa hovyo ndani ya CCM.

Edward Lowassa alikuja tena kuonyesha maamuzi magumu kipindi cha maji ya ziwa Victoria pale Misri waliposema tusitumie maji ya Ziwa Victoria sababu ni chanzo chao cha mto Nile, Edward Lowassa aliwaambia tutatumia maji hayo ya Ziwa Victoria kwa maana ni urithi wa Mtanzania na akiwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa alionyesha maamuzi magumu kwa kujenga shule za kata Tanzania nzima.

Sitasahau alipotoa siku saba kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Yusuph Makamba kumaliza ujenzi wa barabara ya Temeke, Nayakumbuka maneno yake; "Mwaka 1978 tulichelewa kuchukua hatua dhidi ya Idi Amin, tukavumilia na kufikiri tutashauriana naye kama jirani yetu. Lakini tukaja kujikuta ameharibu mambo mengi tukaingia kwenye madhara makubwa sana na tumepoteza watu wetu. Hatuwezi kurudia makosa kumchekea mtu yeyote anayetuchokoza, tutawashughulikia bila kusita."

Sitasahau uamuzi wake mgumu wa kujiuzuru Uwaziri Mkuu baada ya kuchafuliwa kwa kashfa ya Richmond.

-Mwanzilishi wa Falsafa ya Mabadiliko.

Sitaisahau kauli ya Mh. Edward Lowassa aliyoitoa pale jangwani wakati wa uzinduzi wa kampeni za Urais mwaka 2015 alisema Watanzania huu ndio wakati wa kufanya MABADILIKO, nimekuja ili mfanye mabadiliko, mkishindwa sasa itawachukuwa miaka 50 kuipata Bahati hii tena".

Nitamkumbuka Mzee Edward Lowassa kwa style aliyokuja nayo ya Tulizungusha sana Mikono😁Mabadilikoooo🤜🔄🤛...* (Lowassa)... Lowassa...🤜🔄🤛...Mabadilikoooo, kusema na ukweli mwaka 2015 CCM ndio ilikuwa mwisho kutawala hii nchi ya Tanzania, Watanzania walihitaji sana Mabadiliko ni bahati mbaya sana huyu Edward Lowassa alihamia upinzani ungali dhaifu sanaa nchini na ukiwa upinzani wenye wahuni wengi wasiojua jasho la wapigania uhuru wa nchi hii.

Hivyo basi isingekuwa rahisi kuachia dola kwa upinzani dhaifu kama wa kina Tundu Lissu ambaye kila kukiacha yupo Ulaya kwa wajomba zake, au kuicha nchi kwa Mwenyekiti Freeman Mbowe ambaye ni mfanyabiashara na the like utabomoa nchi iliyojengwa kwa ujamaa kwa miaka mingi ndani ya muda mfupi tu.

Mwaka 2015 kipindi Edward Lowassa anatangaza nia ya kugombea urais nchi ilikuwa imetoka katika uongozi wa hovyo ambao wanachi walishauchoka, Watanzania walihitaji sana Mabadiliko hivyo kuamua liwalo na liwe bora kumchagua yeyote ambaye yuko kinyume na uongozi wa CCM.

Karibu kila mtu kipindi hicho alikuwa kinyume na utawala wa awamu ya nne, wana CCM walizomewa ilionekana lazima mabadiliko yafanyike kwa hali na Mali kwa maslahi ya Taifa la Tanzania, pamoja uongozi wa awamu ya nne kuchokwa Watanzania walichokwa na CCM na mifumo yake ndio jambo lililofanya wengi wahamie upande wa kusapoti upinzani.

The same way kama ilivyokuwa 2010 kwa Dr Slaa alivyopita na nyomi la wafuasi wengi waliochoshwa na utawala wa CCM, hapo hakuna cha uchawi,dawa wala mvuto bali uhalisia wa maisha unaowafanya watu kuchoshwa na aina ya mfumo na kuamua kuhamia/kutamani mfumo wa upande wa pili(upinzani).

Nani ataongoza wimbi hili la Mabadiliko ndipo alipoonekana Edward Lowassa mwenye maamuzi magumu kufaa kuongoza wimbi hili la Mabadiliko, baada ya Edward Lowassa kushindwa uchaguzi, matumaini ya walioupinga mfumo wa CCM yalirudi baada ya kuona utendaji wa Rais mteule, Pombe Magufuli.

Watanzania wakasema kumbe kuna matumaini hata huko CCM pale Magufuli alipobadili mfumo mzima wa kipuuzi ndani ya CCM, hapo ndipo hata baadhi ya wapinzani walianza kumsapoti na hata wale waliokuwa wamechoshwa na utawala wa CCM kabla ya 2015 walirudisha matumaini na kurudi CCM na hata Edward Lowassa nae alirudi CCM na kumsupport Rais John Pombe Magufuli kuubomoa mfumo ovu ndani ya CCM.

Hii sio hadithi, sio stories, haya Watanzania waliyashuhudia wenyewe baada ya Magufuli kuapishwa tu,alianza ziara za kushtukiza, kutumbua wazembe/wala rushwa, kuinua maisha ya walala hoi,kupambana na wakwepa kodi, haya aliyafanya ndani ya muda mfupi jambo lililorudisha matumaini kwa Watanzania, wanamabadiliko na wana Ukawa.

-Safari ya Matumaini inaendelea.

Ikaja zamu ya Watanzania kufanya uamuzi mgumu, je, utaunga mkono uamuzi wowote wa kumfanya Lowassa awe mgombea uraisi kwa ticket ya CHADEMA/UKAWA endapo uamuzi huo utafikiwa? Majibu ya Wananchi kwenye mitandao yalikuwa hivi, kama hiyo Kama ndio njia pekee iliyobaki ili kuitoa ccm madarakani i would rather say YES.

Lowasa aje Ukawa tuifute kwanza CCM kwenye masikio ya watanzania na kuunda taifa huru lenye kujali uhuru wa watu na ustawi wao kiuchumi, wanyonge nao wapumue wale keki ya nchi.

Hata kama ili kuiondoa ccm inabidi kumkodi Lowassa mie nasema ndio kwani hatuwaondoi watu bali mfumo mbovu, Uongozi wa Ukawa unaweza kuingia madarakani na yeyote yule lakini kwa mfumo wao atadhibitiwa tuu,muhimu kwa sasa ni CCM kuondoka tuu.

Lowassa aje Chadema kwa sababu Lowassa na timu yake wanamtandao wa kuweza kunyamazisha vyombo vya usalama visichakachue kura kwa maslahi ya Taifa. Mwisho tuliona Matokeo ya uchaguzi na utofauti wa Matokeo ulikuwa mdogo, hili lilionesha hamu ya Mabadiliko iliwajaa Watanzania, rejea kura zilizo pigwa kati ya Edward na John zimepishanaje, hili alilijua Hayati Rais John Pombe Magufuli, ndio maana John Pombe Magufuli alikuwa akimheshimu sana Edward Ngoyai Lowassa.

Suala la Lowasa kuwa na wafuasi wengi lilitokana na Watanzania kuchoshwa na utawala wa kihuni wa CCM ndiomaana wakatamani na kushawishika na upande wa Upinzan wakifikili kutakuwa na unafuu au kutaman Uongozi mpya nje ya CCM.

Siasa za upendo na kusaidia watu, wakati mwana siasa unapanga safu ndio unakuwa umetoa fursa kwa wenzako kwa kuwapa msaada katika kujipachika kwenye nafasi za kisiasa na kiserikali, ndio maana aliweza kusumbua chama katika uchaguzi wa 2015, alikuwa ana watu wengi ambao aliwagusa maisha yao moja kwa moja kwa nafasi walizokuwepo.

Sifa za Edward Lowassa ni Ukimya, Uvumilivu, Maamuzi magumu, usiri, kujali maslahi ya Taifa, kujali marafiki.

Nachukua nafasi hii kutoa pole sana kwa Familia ya Hayati Edward Lowasa. Kwa maumivu niliyonae juu yake yeye ambae ni ndiye chanzo cha mimi kuingia kwenye siasa na kufuatilia siasa.

Adios Amigos Edward Ngoyai Lowassa.

Nikiishia hapa, mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Mafuriko ya watu waliomsindikiza Edward Lowassa kuchukua form ya Urais.
 
Attachments

  • IMG-20240211-WA0308.jpg
    IMG-20240211-WA0308.jpg
    106.9 KB · Views: 3

R.I.P Laigwanan EL
 
Kama Kuna kipindi Kikwete alikuwa na hali mbaya ni kipindi Lowassa anatafuta urais kuanzia kupitia ccm Hadi ukawa akiwaza ufedhuli alomfanyia mwenzie versus ukarim aloutenda Lowassa Kwa kikwete na endapo atachukua nchi kupitia huko alikokwenda
 
Back
Top Bottom