Dr.Slaa: Zitto anaweza kufukuzwa kabisa

Dr.Slaa: Zitto anaweza kufukuzwa kabisa

Status
Not open for further replies.
Sijaona kosa la kauli hii, zitto anaweza akafukuzwa kabisa uanachama wake, najiuliza maswali sana na sijapata jibu, kwa nini mtetezi wa zitto ni wanaccm na wanachadema wasaliti?

hoja ujibiwa kwa Hoja sio Vioja
 
Kama ni SACCOS kwa nini huyo yuda anang'ang'ania kubaki? si mngemshauri akaacha kupeleka utetezi wake? kwa nini muhangaike kutwa kucha na CDM? Au kama ni saccos inawahusu nini? mlisema imeshakufa lakini wenye akili tunajiuliza kuwa kwa nini muhangaike nayo? huo ni utoto mkikua mtaacha!

Zitto yupo CDM(saccos)kulinda Fedha za walala Hoi,Kodi zetu
 
Hivi wewe shida yako nini? Zitto amepewa nafasi ya kujitetea. Tusubiri. Wakati huo huo Slaa Ana haki ya kutoa maoni yake.
Slaa ana haki ya kutoa maoni lakini Zitto hana haki akitoa maoni anaambiwa atafukuzwa, majanga.
 
Dr.W.Slaa anajaribu kisema kila kinacho fanywa na wanao mpenda na kimuunga mkono zitto basi kime andaliwa na zitto?

Dr.W.Slaa atwambie ni kipengele gani na ni sheria hipi inatoa nafasi mtu kuhukumiwa kwa kosa la mwingine?

Dr.W.Slaa anajaribu kusema kamati kuu yote itakubaliana na mawazo yake ya kumfukuza mtu kwa kuwa wafuasi wake wanataka kuandamana na wameandaa document za kusaini?

Dr.W.Slaa anajaribu kutwambia kamati kuu yote ina fikiri kama yeye na itafanya maamuzi kilingana na matakwa yake?

Dr.W.Slaa anajaribu kusema wafuasi wake wanao mtukana zitto au watu wengine huwa ana watuma?
Dr.W.Slaa kwanini unajaribu kuonesha umeiweka kamati kuu mfukoni.

Tunajali uhai na umoja wa chama
 
Last edited by a moderator:
Mbona Zitto akipanda jukwaani huwa hamtaji,yeye kinachomuwasha ni nini?

NISHAMDHARAU HUYU MZEE kuna siku mtu alisema huyu ndugu anaongozwa na chuki sasa naamini

Zitto hana bifu,Kina Slaa na Mbowe na Vifaranga wao Wana bifu hawapo kufanya Siasa!!Zito ni mwanasiasa!Mbowe na Slaa wameingia kwa bahati mbaya katika Siasa
 
Ni Dr wa ...... Huko kila kitu ndio, no challenges no critics. Siasa haiko hivo babu. You must answers for 5 w's
 
Wewe jamaa bana unafaa sana kwenye vijiwe vya kahawa.
Mimi ni mtu wa kijiweni!, hoja zangu zote ninazoleta humu, nazitoa kijiweni, na pia ni kwa ajili ya watu wangu wa kijiweni na tena haswa vijiwe vya kahawa!. Asubuhi huanzia vijiwe vya kahawa, mchana hushinda kijiwe cha jf, alasiri vijiwe vya jobless, jioni kwenye kahawa tena, usiku saa ya chakula kijiwe cha mama mtilie kukombelezea mabaki, usiku namalizia tena kijiwe cha jf!. Yaani ninazunguka vijiweni kutwa kucha!, nalalia kijiweni, naamkia kijiweni, nashinda kijiweni, nakula kijiweni!.
Pasco
 
Zitto hana bifu,Kina Slaa na Mbowe na Vifaranga wao Wana bifu hawapo kufanya Siasa!!Zito ni mwanasiasa!Mbowe na Slaa wameingia kwa bahati mbaya katika Siasa
Sana tu Mkuu. Ila mwisho wa siku wanachama ndo wanaamua na wanabaini yupi kiongozi wao
 
Mbona hatukuambiwa kama mjadala kuhusu Mh. Zitto umefunguliwa tena kwa sababu katika mazingira ya kawaida, Dr. Slaa alipaswa kutuambia tena kama mjadala ameufungua.

Hii ilikuwa ni sawa na kujifungia ndani ya nyumba wakati wa mvua kubwa inayoambatana na upepo na radi halafu ukaanza kuendelea kufanya mambo mengine ndani ukijiimanisha kuwa hujali kinachotokea nje. HAIWEZEKANI.

Radi ikiunguruma, unaacha kila kitu na kuanza kufikiria matokeo yake. Upepo ukivuma tena kwa kasi, inabidi tena uache kile ulichokuwa unakifanya.

Dr. Slaa can't afford to ignore political gigantic force comes from Zitto. Never!.

Haya ya kusema mjadala umefungwa ilikuwa ni political wishful opine hasa ikichukuliwa kuwa Mh. Zitto hajafika hapo kisiasa by default.

Mh. Zitto anafahamu vizuri sana kuzicheza siasa za Tanzania.
 
Cha kushangaza sana mashabiki na wafuasi wengi wa Bw. Zitto ni WanaCCM. Vyombo vyote vya habari vinavyomilikiwa na CCM na Serikali yake ndivyo vinaendesha utetezi na support kubwa kwa matendo ya Bw. Zitto. Inakuwaje hili liwe hivyo na huyo Zitto asilione?. Kama kweli anakipenda chama chake cha CHADEMA asifuate na kuzingatia taratibu zinazotakiwa badala ya kuendelea kuzunguka huku na huko akiandamana na waandishi wa magazeti kama UHURU yanayonadi na kuripoti kwa nguvu zote mambo yote anayoyafanya? Haoni kuwa mambo anayofanya ni sawa na kuweka tope kwenye kidonda ili kisishambuliwe na inzi ilhal kidonda hicho hicho kinazidi kuoza na kuharibika zaidi?

Ni lazima ifike mahali Zitto aweke bayana kama ameamua kutumika na ktekeleza maagizo ya CCM na watawala wake badala ya kuendelea kuudanganya umma wa Watanzania kuwa yeye ndiyo mtetezi wa demokrasia na shida za wananchi huku inaonekana dhahiri kuwa anayoyafanya yanalenga kunufaisha kundi fulani na yeye binafsi huku mkakati mkuu ukiwa ni kukisambaratisha chama chake.
 
Mbona ndio maisha yake ya kila siku. Unajua hata hizo document wanazo zunguka nazo Tanzania nzima kumchafua Zito wametengeneza Mnyika na Lema.(sauti huru, Dec 11-13 , 2013)
Mnyika ni muadilifu pasi shaka hawezi kushiriki michezo michafu hii, huyo mwingine pia sio yeye, unamsingizia bure, hana kichwa hicho cha kupanga mipango mikubwa ya level ile!.
Pasco.
 
Duh kwa minyukano hii inayoendelea ndani ya chadema, tumaini la kukua kwa demokrasia nje ya ccm kwa sasa ni ndoto
 
Hivi ni kwanini Chadema!?kwanini iwe Slaa na Mbowe?kama ni suala la uongozi Mbona Cuf tangia ianze Lipumba mpaka leo bado ni mwenyekiti na Seif bado katibu!?vp kwa TLP!vp kwa Cheo na wengine?Kweli hi ni njama zlizopangwa na ccm kudhoofisha nguvu ya Chadema!Chadema chukueni uamuzi mgumu!mfukuzeni Zito!!tupeni kule!embu tusiyumbishwe sisi wanchama!!huyu jamaa ni mzadiki mnafiki!hafai!Chadema simamen imara!hali ya bahari siyo nzuri
 
Mbona hatukuambiwa kama mjadala kuhusu Mh. Zitto umefunguliwa tena kwa sababu katika mazingira ya kawaida, Dr. Slaa alipaswa kutuambia tena kama mjadala ameufungua.

Hii ilikuwa ni sawa na kujifungia ndani ya nyumba wakati wa mvua kubwa inayoambatana na upepo na radi halafu ukaanza kuendelea kufanya mambo mengine ndani ukijiimanisha kuwa hujali kinachotokea nje. HAIWEZEKANI.

Radi ikiunguruma, unaacha kila kitu na kuanza kufikiria matokeo yake. Upepo ukivuma tena kwa kasi, inabidi tena uache kile ulichokuwa unakifanya.

Dr. Slaa can't afford to ignore political gigantic force comes from Zitto. Never!.

Haya ya kusema mjadala umefungwa ilikuwa ni political wishful opine hasa ikichukuliwa kuwa Mh. Zitto hajafika hapo kisiasa by default.

Mh. Zitto anafahamu vizuri sana kuzicheza siasa za Tanzania.
Hizi ni double standards za Chadema, wasiposimamia haki, watakuwa haunted na udhalimu wao hadi kuzimu!.
Pasco.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom