Dr.Slaa: Zitto anaweza kufukuzwa kabisa

Dr.Slaa: Zitto anaweza kufukuzwa kabisa

Status
Not open for further replies.
Nilishasema sana jamani,hii ni saccos ya watu,hamkunielewa, haya sasa mnayaona wenyewe!

Kama ni SACCOS kwa nini huyo yuda anang'ang'ania kubaki? si mngemshauri akaacha kupeleka utetezi wake? kwa nini muhangaike kutwa kucha na CDM? Au kama ni saccos inawahusu nini? mlisema imeshakufa lakini wenye akili tunajiuliza kuwa kwa nini muhangaike nayo? huo ni utoto mkikua mtaacha!
 
Sijaona kosa la kauli hii, zitto anaweza akafukuzwa kabisa uanachama wake, najiuliza maswali sana na sijapata jibu, kwa nini mtetezi wa zitto ni wanaccm na wanachadema wasaliti?
Hivi dogo wasaliti ni kina nani? Wana ccm ni wepi? Kwa hiyo kila anayesimama kwenye kweli ni ccm ? Ni msaliti? Jibuni maswali magumu mkuu acheni kujificha kwenye kichaka kisicho na nyasi, unafukia kichwa wakati kiwiliwili chote kipo nje.
 
Kama ni SACCOS kwa nini huyo yuda anang'ang'ania kubaki? si mngemshauri akaacha kupeleka utetezi wake? kwa nini muhangaike kutwa kucha na CDM? Au kama ni saccos inawahusu nini? mlisema imeshakufa lakini wenye akili tunajiuliza kuwa kwa nini muhangaike nayo? huo ni utoto mkikua mtaacha!
Kwanini hii saccos inaendeshwa kiimla?
 
Tatizo ni anakotokea zitto na dini yake. Zitto as haukufunga ndoa ya kikatolik na cdm ya kutenganishwa na kifo kuwa mtulivu.
 
Last edited by a moderator:
Kiitifaki dr slaa ni mtu wa tatu kitoka kwa mwenyekiti, na kwa sasa ambapo hakuna makam mwenyekiti, yeye ni mtu wa pili.lakini yeye ndio mtendaji mkuu kabisa wa chama.

Dr slaa amekaririwa akiwa tabora jana akisema kuwa "zitto atafukuzwa kabisa uanachama" je kwa kauli hii kuna haja ya kusubiri siku 14? Je hukumu ndio hiyo imeshatolewa? Je hiyo ndio demokrasia ndani ya chadema? Ndio utaratibu wa chadema kuhukumu majukwaani??

my take: tuenende tunayoyahubiri. Unayopenda kufanyiwa mtendee mwenzio, usiyopenda kufanyiwa usimtendee mwenzio

Tupe source kwanza,ina maana wewe ulikuwa kasulu na Igunga? Ulijigawaje?
 
Kiitifaki dr slaa ni mtu wa tatu kitoka kwa mwenyekiti, na kwa sasa ambapo hakuna makam mwenyekiti, yeye ni mtu wa pili.lakini yeye ndio mtendaji mkuu kabisa wa chama.

Dr slaa amekaririwa akiwa tabora jana akisema kuwa "zitto atafukuzwa kabisa uanachama" je kwa kauli hii kuna haja ya kusubiri siku 14? Je hukumu ndio hiyo imeshatolewa? Je hiyo ndio demokrasia ndani ya chadema? Ndio utaratibu wa chadema kuhukumu majukwaani??

my take: tuenende tunayoyahubiri. Unayopenda kufanyiwa mtendee mwenzio, usiyopenda kufanyiwa usimtendee mwenzio
Kwanza wewe ni muongo kabisa Slaa hajasema Zitto lazima afukuzwe yeye kasema Zitto anaweza kufukuzwa kabisa kama ataendelea na ukaidi wake kwa chama na viongozi.
 
Slaa angekuwa ndiye mwalimu Nyerere enzi zile za akina bibi titi mohamed akina mirisho sarakikya angefanyaje. Dr akili imeishia kwenye vitobo. I hate u dr slaa i hate u cdm.
 
Viongozi waandamizi wa CHADEMA wana uwezo wa kumfukuza Zitto hata bila kuwa na sababu yeyote ile ya maana yenye kuwapa nguvu ya kufanya hivyo.Kwa lugha rahisi ni kwamba wana uwezo wa kumfukuza Zitto huku wanafunja sheria walizoziweka wenyewe.
Wasichoweza kabisa ni kumfukuza kwa kufuata katiba yao wenyewe.
Namna tu walivyolishughulikia suala la Zitto wamevunja katiba ya CHADEMA.
Kile kipengele cha kumwandiakia barua na kuhakikisha ameipata na kuisoma kabla ya kuanza aina yeyote ya kikao chenye nia ya kuhoji na hata kutoa hukumu kilivunjwa. Na nina aamini kilivunjwa kwa makusudu kwa sababu ya kuamini kwamba mahali walipo kama viongozi na heshima waliojijengea kama viongozi wa CHADEMA hakuta kuwa na mtu yeyote wa kudodosa sembuse kupayuka.
Kwa Kitila na Mwigamba, ambao wamekubali kuhusika moja kwa moja ule Mzalendo wenye maswali na hoja nzito nao pia naona hawajatendewa haki.
Tangu lini kupanga mikakati ya siri ya kushinda katika kubsdili uongozi wa juu ni UHAINI??

Zamni nilidhani naelewa sana maana ya neno UHAINI lakini kwa hii Definition mpya ya uongozi wa CHADEMA sidhani kama bado naelewa maana ya UHAINI.

UHAINI ni neno kubwa sana ambalo kama sikosei linahusu watu au kundi la watu kula njama dhidi ya Jamhuri.
Sioni rangi wala kusikia harufu yeyote ya UHAINI Kwa kundi la viongozi au wanachama wa CHADEMA kupanga mkakati wa kubadili uongozi kwa kutumia sanduku la kura.

Kilichopo hapa ni kwamba uongozi wa juu wa CHADEMA unajaribu kwa nguvu zote kuficha aina ya UVUNDO sawa na ule ulioko CCM kwa kutumia viganja huku wakichoma ubani na kujaribu kuwatoa watu kadhaa kafara ya dhambi zao.

Pamoja na mengi mazuri yaliyofanyika kupitia uongozi huu, hili la kujaribu kumg'oa Zitto bila kufuata utaratibu linaleta maswali mengi sana.
Kama CHAMA chenye nia ya kuleta mageuzi, tunahoji uvunjifu mwingi wa sheria za nchi unaofanywa na Chama tawala. Lakini je?
Mbona sisi akina Madela tukihoji kifungu kwa kifungu juu ya namna suala la Zitto linavyoshughulikiwa naona tunapewa majibu yanayo fanana na yale ya uongozi wa CCM?????
Tuna nia ya dhati ya kuleta mabadiliko ya kweli?? Au ni namna tu ya kuvaa viwalo vya kondoo lakini mioyoni mwenu na ndani ya akili zenu ni mbweha ambao wako Full armed na Makucha makali, meno ya kuchongoka na uchu wa kihayawani wa kusambaratisha??

Inaweza kuwa ni kweli MH Zitto kanunuliwa na CCM, na ana nia ya kuharibu CHADEMA, hata hivyo sioni sababu ya kutoa hukumu au kuendesha vikao bila kufuata na kuzingatia katiba ya chama.

Kwa kuamua kuvunja katiba kwa makusudi kabisa, sisi akina Madela Wa Madilu tutashindwaje kuwatuhumu ninyi viongozi wa juu wa CHADEMA kwamba nia zenupia ni mbaya hata kuliko nia ya huyu mnaye taka kumtimua bila kufuata katiba??

Endapo vifungu vya katiba vinanyofolewa katika katiba bila kujadiliwa ili kutoa kinga ya Kifalme kwa uongozi wa juu! Hii haitoshi kufanya tuwatuhumu kwamba huenda mnataka kumwondoa Zitto ili kutoa message kali kwa wale wote wanaotaka kuhoji mienendo yenu michafu ya kunajisi katiba na CHADEMA??

Kadi yangu ya CHADEMA sirudishi kwa sababu ndiyo TURUFU pekee niliyo nayo,na wala sina mpango wa kuhama chama. Ila nipo tayari kabisa kutumia akili yangu yote kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya CHADEMA. Hii ndiyo ahadi kwa chama changu.
 
Tatizo ni anakotokea zitto na dini yake. Zitto as haukufunga ndoa ya kikatolik na cdm ya kutenganishwa na kifo kuwa mtulivu.

Hapana. Msipotoshe watu. Tatizo ni arrogance ya Zitto na kujiona yeye ni muhimu kuliko chama.
 
Last edited by a moderator:
Tokea afariki chacha wangwe Hakuna kiongozi wa Chadema amewahi kumkumbuka sasa Mzimu wake umebisha hodi chezea Mzimu wewe...

Mizimu ipo kuzimu,wenye akili timamu hawasumbuliwi na mizimu,wanaokumbuka mizumu ni wapuuzi kama wewe.
 
Kiitifaki dr slaa ni mtu wa tatu kitoka kwa mwenyekiti, na kwa sasa ambapo hakuna makam mwenyekiti, yeye ni mtu wa pili.lakini yeye ndio mtendaji mkuu kabisa wa chama.

Dr slaa amekaririwa akiwa tabora jana akisema kuwa "zitto atafukuzwa kabisa uanachama" je kwa kauli hii kuna haja ya kusubiri siku 14? Je hukumu ndio hiyo imeshatolewa? Je hiyo ndio demokrasia ndani ya chadema? Ndio utaratibu wa chadema kuhukumu majukwaani??

my take: tuenende tunayoyahubiri. Unayopenda kufanyiwa mtendee mwenzio, usiyopenda kufanyiwa usimtendee mwenzio

Dr slaa amekusaidia kujua majukumu ya kila siku ya mtendaji mkuu wa taasisi ,sasa unaweza kujua utofauti wa pinda na dhana nzima ya utendaji by the way mfano mzuri ni Kinana vs Mawaziri mizigo hata kabla ya kuwahoji?
 
Dr Slaa ni mtu ambaye hafikirii kabla ya kutamka. Huwezi kumfananisha na Zitto ambaye hutafakari na wakati mwingine huomba ushauri kabla ya kutamka
 
tulishasema chadema kinaongozwa kibabe hakuna demokrasia nadani ya chadema.
 
Mbona Zitto akipanda jukwaani huwa hamtaji,yeye kinachomuwasha ni nini?

NISHAMDHARAU HUYU MZEE kuna siku mtu alisema huyu ndugu anaongozwa na chuki sasa naamini
 
Japo sisi wengine sio madaktari, lakini dalili za early stages za mind incapacitation zimeanza kujitokeza kwa baadhi ya viongozi wa Chadema, nadhani kuna baadhi yao wameanza kufunguka macho kuwa kinachoendelea dhidi ya Zitto ni some kind of vendatta ndio maana wamejinyamazia!. Sasa kama hizi ndizo early stages, later stages zitakuwaje?!.

Kama hawatatokea watu imara ndani ya CC ya Chadema kuhakikisha haki inatendeka, mzee wetu huyu, atakipeleka chama kusiko!, na hivi kufuatia kuwa ni msomi wa divinity aliyebobea, kuna baadhi ya wafuasi wake ni wanakondoo, sio tuu kwa utii, hadi kukaribia kumuabudu, chochote atakachosema hapana, wao hukiona kama dhambi, na kosa kubwa la Zitto ni kuonyesha interest ya 2015!, hii ni dhambi ya mauti na ndicho pekee kinachomsubiri Zitto ndani ya Chadema, hii kauli ya "eti anaweza" as if maamuzi hayajaamuliwa, ni zuga tuu!, nashukuru Zitto mwenyewe hili ameishalijua, na kaamua kufa nao!.
Pasco.

Wewe jamaa bana unafaa sana kwenye vijiwe vya kahawa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom