Dr. Slaa: Pinda anapaswa kujiuzulu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,018
144,377
Katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),Dr.Wilbroad Slaa amesema serikali nzima na Baraza la Mawaziri linapaswa kujiuzulu na kwamba kitendo cha kujiuzuru kwa mawaziri wanne tu hakitoshi na badala yake amesema Pinda kama "kiranja" mkuu anapaswa kuwajibika.

Dr.Slaa ametoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara huko mkoani Tabora.

CHANZO:ITV
 
Ukweli Mhe. Waziri Mkuu kashindwa kazi yake, Jana alitakiwa kwa heshima AJIUZULU MARA MOJA, kwa aibu iliyofanywa na watendaji wake anaowaongoza.
 
Ni ajabu wengine wanajiuzulu kwa matendo ya juniors wao lakini pm ameuchuna tu.
 
Dr.Slaa ameenda TABORA kufanya nini? Mbona hajawaambia wanatabora kilichompeleka huko? badala yake amedakia topic ya mawaziri waliojiuzulu na kuifanya ndio ajenda kuu kwenye mikutano yake, huyu BABU sasa ameishiwa nyimbo!
 
mzee wa ajabu kweli huyu ubaguzi unawasumbua wamemuonea zitto sasa anahangaika na kudandia mambo hata hayajui yeye kwa nini asijiuzulu wakati chama chake kimemshinda kimevurugika kabisa.
 
Hali ya Tabora ni mbaya!, heri ya mwaka 1980 kuliko ya sasa!

slaa ndiyo kaenda kuichafua na kuiharibu tabora haikuwa na shida hata kidogo leo slaa kashindwa hata kusema nini kimempeleka tabora.
 
Kuwaeleza uozo wa pm ni moja ya mambo nyeti yakuwaambia wana tabora na akifika kaliuwa awaonyeshe na picha za yule mbakaji. Hiyo nayo ni agenda nzuri maana wananchi bila kuwapata taarifa za ukweli mabadiliko yatachukua muda sana
 
Dr.Slaa ameenda TABORA kufanya nini? Mbona hajawaambia wanatabora kilichompeleka huko? badala yake amedakia topic ya mawaziri waliojiuzulu na kuifanya ndio ajenda kuu kwenye mikutano yake, huyu BABU sasa ameishiwa nyimbo!
chooni upo? Hongera kwa jina lako kuitwa chooni
 
Dr.Slaa ameenda TABORA kufanya nini? Mbona hajawaambia wanatabora kilichompeleka huko? badala yake amedakia topic ya mawaziri waliojiuzulu na kuifanya ndio ajenda kuu kwenye mikutano yake, huyu BABU sasa ameishiwa nyimbo!

....nafasi za kazi loliondo!!!
 
Sasa hivi ndo tunaona hasara za kupeana vyeo kwa kulipana fadhila na madhala ya kuwa na baba mwenye madhambi katika familia, hawezi kupata nguvu za kuwakemea watoto wake kwa sababu wanajua madhambi yake
 
Mzee wa gongo...
Mnajua wakati mwingi pro-CCM najidhalilisha kwa uzaifu wa akili zenu. Hicho ulichosema kina uhusiano gani na hoja ya Pinda kutakiwa kujiuzulu. Mnaonyesha janga tulilonalo kwa kuwa na CCM madarakani. Imagine mtu kama wewe unapewa dhamana na kuongoza.
 
Mkuu,

Hiyo ni sera mpya ya Slaa ambayo anazunguka mikoani kuitangaza...
 
mzee wa ajabu kweli huyu ubaguzi unawasumbua wamemuonea zitto sasa anahangaika na kudandia mambo hata hayajui yeye kwa nini asijiuzulu wakati chama chake kimemshinda kimevurugika kabisa.

:thumbup:
 
Tatizo la Slaa yeye anasubiri matukio halafu akienda vijijini anaona kama watu wale hawana habari ndo kwanza analeta porojo mpya. Uchovu huo Dr wa silaha. Na ndio maana sasa hii hata hakuna anayeshangilia, hana jipya
 
Back
Top Bottom