Kada wa CCM anena kuhusu Zitto na ubia wa CCM

Status
Not open for further replies.

daniel merengo

JF-Expert Member
Aug 19, 2011
277
98
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameuweka njia panda uanachama wake ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kukubali pingamizi lake la kuizuia Kamati Kuu (CC) ya chama hicho isimjadili hadi kesi yake ya msingi itakapokuwa imesikilizwa. Kwa uamuzi huo, Zitto sasa atabaki kuwa mwanachama kwa nguvu ya mahakama hadi hapo itakapoamriwa vinginevyo.
Sasa Zitto ataungana na wabunge wenzake wawili, David Kafulila wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) na Hamad Rashid Mohammed wa Wawi (CUF) ambao pia ubunge wao upo kwa nguvu ya mahakama.
Zitto alifungua kesi mahakamani hapo siku moja kabla ya CC kuanza vikao vyake ambavyo vilikuwa vijadili utetezi wa tuhuma zake za kuendesha mkakati wa siri wa kusaliti chama, akiomba mahakama izuie suala la uanachama wake lisijadiliwe hadi kesi yake isikilizwe.
Akitoa uamuzi wa awali, Jaji John Utamwa, alisema kuwa mahakama imeridhia ombi la Zitto kuwa CHADEMA au chombo chochote kisijadili uanachama wake hadi kesi ya msingi itakapomalizika.
Akisoma maelezo ya awali, Utamwa alisema kuwa wakili Peter Kibatala anayewakilisha Bodi ya Udhamini ya CHADEMA na Katibu Mkuu ambao ndio washtakiwa, alikula kiapo kwa niaba yao jambo ambalo si sahihi.
Utamwa alisema kuwa kwa mazingira ya kesi kuhusisha Bodi ya Udhamini ya CHADEMA na Katibu Mkuu, ilikuwa si sahihi kwa wakili kula kiapo kwa niaba yao.
Wakizungumza baada ya kutoka mahakamani, mawakili wa upande wa CHADEMA, Kibatala na Tundu Lissu walisema kuwa kuhusiana na hati ya kiapo, ipo sheria inayoruhusu wakili kula kiapo kwa ajili ya mteja wake.
Walisema kuwa wanaheshimu uamuzi wa mahakama japo hawajaridhika, na hivyo watachukua hatua za ziada.
Wakili wa Zitto, Albert Msando, aliomba uamuzi wa mahakama uheshimike kwani ni hatua za haki kutendeka na mteja wake kupata nafasi ya kusikilizwa.
Katika kesi ya msingi, Zitto anaiomba mahakama ikizuie chama hicho kumchukulia hatua, ambapo kesi hiyo inatarajiwa kutajwa Februari 13, mwaka huu.
Zitto aliwasilisha maombi dhidi ya Baraza la Wadhamini la CHADEMA pamoja na Katibu Mkuu wa chama, Dk. Willibrod Slaa, akiiomba mahakama itoe zuio la muda kwa Kamati Kuu kutojadili uanachama wake.
Katika kesi hiyo, Zitto anaiomba mahakama iizuie Kamati Kuu kujadili uanachama wake hadi rufaa yake itakaposikilizwa na Baraza Kuu la chama na kuomba mahakama imwamuru Dk. Slaa ampe nakala za taarifa za vikao vilivyomvua uongozi ili akate rufaa.

Hali ilivyokuwa
Zitto alipokelewa na wanachama wa CHADEMA kwa kuzomewa kuanzia hoteli ya Hyatt Kempisky hadi katika lango kuu la kuingia Mahakama Kuu.
Sauti hizo zilisikika zikimba na kuzomea; "Zitto kibaraka wa CCM; CCM huyo…"
Zitto ambaye aliongozana na walinzi wanne wenye miili mikubwa (mabaunsa), alikuwa ameinamisha sura chini na kutembea haraka kuingia mahakamani.
Hata hivyo, kabla ya kuingia lango kuu la mahakama, alipepesuka na kuvuka kiatu kimoja cha mguu wa kushoto.
Baada ya kadhia hiyo ya nje, alikutana na wanachama wengine wa CHADEMA ndani ya mahakama, ambao walimzomea hadi kwenye mlango wa vyumba vya mahakama.
Nako nje, mamluki wanaodaiwa kukodiwa na Zitto tangu kuanza kwa kesi hiyo, jana hali ilikuwa ni tofauti kutokana na kufika kwa uchache huku wakizomewa na wanachama wa CHADEMA.
Tanzania Daima ilidokezwa kuwa walinzi waliokuwa wanamlinda Zitto, walifahamika kwa jina moja moja la Tino, Evans na Ziggy.
Ndani ya mahakama, kabla ya kesi kuanza baadhi ya wanachama wa CHADEMA walimtambua mtu mmoja aliyevaa suti nyeusi na kuanza kumshambulia kwa maneno kuwa ni kibaraka wa Ridhiwani Kikwete hadi mtu huyo alipojitetea akidai ni wakili.

Vituko vya Zitto kisiasa
Zitto ambaye anahaha kila kona ili asivuliwe uanachama wa CHADEMA, amekuwa na mtiririko wa matukio mengi ya kauli ambazo zimechangia wananchi kumtilia shaka mwenendo wake ndani ya chama.
Mwaka 2010 wakati nchi ikielekea uchaguzi mkuu, Zitto alitishia kutowania tena ubunge katika jimbo lake la Kigoma Kaskazini kwa madai kuwa ameombwa kugombea katika majimbo ya Kigoma Mjini, Kinondoni, Geita na Kahama.
Lakini dakika za mwishoni kabisa, Zitto alirudi kugombea jimboni kwake akidai ameshauriwa na wazee.
Baada ya uchaguzi mkuu, mwanasiasa huyo alitangaza kutogombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2015, akidai kuwa ataachana na siasa ili akafanye kazi ya kitaaluma chuo kikuu.
Muda mfupi baadaye, akakaririwa na vyombo vya habari kwamba anaandamwa ndani ya chama, kiasi cha kufikia hatua ya kutembea na barua ya kutaka kujiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.
Machi mwaka jana, mbunge huyo alitangaza nia ya kuutaka urais wa Tanzania, lakini baada ya kuibuka mjadala mkubwa ndani na nje ya chama chake akielezwa kuwa umri wake hajakidhi matakwa kikatiba, Septemba mwaka huo, alitengua nia hiyo.
Akiwa katika ziara ya kichama mkoani Tabora Novemba mwaka jana, Zitto pia alitengua kauli yake ya kutogombea ubunge mwaka 2015 akisema anaitafakari upya baada ya kuona kero nyingi zinazowakabili wananchi.
Kauli tatanishi za Zitto zimezidi kuongeza shaka hasa katika majibu yake hivi karibuni kupitia mtandao wake wa kijamii wa facebook wakati akifafanua tuhuma zilizoelekezwa kwake na mwanasheria wa CHADEMA, Lissu.
Lissu alidai kuwa Zitto amehongwa magari mawili na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ili amwezeshe kupita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Hata hivyo, katika utetezi wake wa maandishi kupitia ukurasa wake, Zitto aliandika kuwa; "Lissu amenituhumu kuwa nimehongwa magari 2 na mheshimiwa Nimrod Mkono. Mimi ninamiliki gari mbili, Freelander ninayotumia Dar es Salaam na Toyota Carina ninayotumia jimboni."
Majibu ya Zitto yalitofautiana na Mkono ambaye katika taarifa yake alisema kuna magari mawili yanayohusishwa na Zitto na kuyataja kuwa ni Toyota Land Cruiser na Nissan Patrol.
"Sijawahi kumpatia Zitto magari, isipokuwa kuhusu hiyo Land Cruiser, nilitoa msaada wa kuwanusuru Zitto na Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe), kule Tarime kwenye msiba wa marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CHADEMA), kwani walikuwa wakitishiwa kupigwa.
"Walipofika Mwanza, Zitto aliwasiliana na mimi kuhusu ununuzi wa gari hilo na kupitia wakala wangu nilimuuzia," alisema Mkono.
Kuhusu Nissan Patrol, Mkono alisema lilikodishwa kwa Zitto na hadi sasa bado analipa gharama za kulikodisha.
Utata katika suala hili uko kwenye aina za magari zilizotajwa na wanasiasa hawa wawili. Wakati Zitto akitaja kumiliki Freelander na Toyota Carina bila kufafanua kama anayo magari mengine, Mkono anasema amemuuzia Land Cruiser na Nissan Patrol.

Kada CCM anena
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro, David Mgesi, amesema yanayotokea sasa kwa Zitto ni kile alichokuwa akikisema kwa muda mrefu kuhusu mbunge huyo.
Mgesi ambaye kwa sasa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisema wakati akiwa CHADEMA, alishaonya mienendo ya Zitto kwa kuona kwamba ni mtu ambaye anaweza kukisaliti chama wakati wowote.
Kwamba viongozi wa juu wa CHADEMA waliweza kumuamini Zitto na kumuona kuwa ni mtu mwenye busara.
Akitolea mfano, alisema ilikuwa mwaka 2005, Zitto alipewa dhamana ya kutengeneza bajeti ya chama, na baada ya kuwagawia taarifa ya wajumbe wa Kamati Kuu alitaka wazirudishe kwa madai kuwa hawaamini kwani wanaweza kuvujisha siri nje.
"Baada ya kauli ile nilimuomba Mwenyekiti, Freeman Mbowe tujadili kauli hiyo, lakini lilifunikwa na Zitto akatetewa kuwa aliteleza.
"Sasa ukiangalia leo nani msaliti kama sio yeye ambaye amekuwa akipokea fedha kwa muda mrefu kwa lengo la kukivuruga chama?" alihoji.
Akizungumzia hatua ya Zitto kwenda mahakamani, Mgesi alisema sio sahihi na badala yake alitakiwa kwanza kujibu tuhuma zote zilizoelekezwa kwake ili kuwaelewesha Watanzania na kuwahakikishia anachotuhumiwa si sahihi.
Hata hivyo, Mgesi alisema inasikitisha kuona hadi sasa Zitto na CCM wanaotuhumiwa katika kupeana fedha ili kukiharibu CHADEMA wameshindwa kujitokeza kukanusha taarifa hizo.
"Zitto anapaswa ajitokeze akane kama hakupokea fedha hizo zinazodaiwa kupitia benki ya CRDB, vile vile Serikali ya CCM ilipaswa kuthibitisha kama akaunti zilizotajwa kuwa za Idara ya Usalama wa Taifa ni za kweli au hapana," alisema.
Mgesi alisema kitendo cha pande zote kukaa kimya wakati suala tajwa likiendelea kushika kasi, kunaibua maswali mengi kwa wananchi.
Alisema mgogoro huu ni wa muda mrefu na umetengenezwa huku akikumbushia namna ambavyo Waziri Stephen Wasira alikuwa akisisika akisema kuwa CHADEMA itakufa kabla ya mwaka 2015.
Mgesi pia alitaja matukio ya kubambikiwa kesi ya ugaidi kwa Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare na vijana wengine watano kuwa ulikuwa ni mwendelezo wa mkakati wa kukiua chama hicho.
Aliwaonya vingozi wa CCM ambao wamekuwa wakizungumzia mgogoro huo wa CHADEMA majukwaani, akiwataka kuachana na kazi hiyo kwa kuwa sio iliyowaweka madarakani.
"Wakati CCM inapewa dhamana na wananchi kuongoza, katika ahadi zake hakuna mahali wanasema watakuwa wakijadili mgogoro wa CHADEMA," alisema.
 
Huyu Ndugu naona yupo CCM kimwili lakini Kiroho yupo CHADEMA.
 
RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE KWA CHADEMA
UCHUNGUZI WA MWENENDO WA KISIASA WA ZITTO Z. KABWE NDANI NA NJE YA CHADEMA.
UTANGULIZI:
Tangu mwaka 2008 mwenendo wa kisiasa wa Zitto Zuber Kabwe ulianza kutiliwa shaka na wanachama wa CHADEMA ndani na nje ya chama, Hili lilipelekea kuibuka maneno ya chini kwa chini kuwa anakisaliti chama.

Hilo liliilazimu timu ya kijasusi ya chama kuanza kufuatilia nyendo zake kwa ukaribu zaidi usiku na mchana ili kujiridhisha pasipo kuacha chembe ya mashaka. Ifahamike kuwa chama kina idara ya ulinzi na usalama wa chama na viongozi wake yenye uwezo wa kufuatilia nyendo za majasusi wa nje na viongozi na wanachama wake popote walipo kwa masaa 24. Baada ya kujiridhisha kuwa mwenendo wake ni wa mashaka, bila kusita timu ya ujasusi ilianza kazi rasmi ya ujasusi dhidi ya nyendo zote za Zitto Zuberi Kabwe
MAMBO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI DHIDI YA ZITTO KABWE.

  • Kumfuatilia yeye binafsi nyendo zake.
  • Kufuatilia mawasiliano yake ya simu.
  • Kufuatilia mawasiliano yake ya barua pepe.
  • Kufuatilia pato lake nje ya kazi zake halali za kibunge.
SEHEMU YA KWANZA 2008
Chombo chetu cha ujasusi tulichokipandikiza kwa siri katika nyendo zote za Zitto Kabwe na ndani ya vikao vya mwanzo kabisa vya Zitto na viongozi serikalini, nahata vile vikao muhimu vya idara ya ujasusi ya chama cha mapinduzi (ccm), kinatupa fursa ya kuweka msingi wa kuimarisha chama cha CHADEMA na kutenda haki kidemokrasia kwa maslahi ya chama na Taifa kwa ujumla:

Mnamo Jumatatu ya tarehe 16/6/2008 saa 09:46 asubuhi, Mh Zitto Kabwe kupitia simu yake ya kiganjani namba +255754787550 alipokea simu kutoka kwa Ramadhani Ighondu mwenye namba +255717760473 ambaye ni afisa Usalama wa Taifa anayefanya kazi ikulu hivi sasa. Alijitambulisha kuwa yeye ni Usalama wa Taifa ametumwa na mkuu wake wa kazi aje aongee na Zitto, Maelezo ya msingi katika simu hii ilikuwa ni bwana Ramadhani Ighondu kuomba miadi ya kuonana kutokana na agizo la mkuu wake wa kazi.
Siku sita baadae yaani Jumatatu ya tarehe 23/6/2008 saa 07:52 asubuhi, Zitto alipigiwa tena simu na Ramadhani Ighondu akimkumbusha maongezi yao waliyo fanya siku 6 zilizopita na kumuomba siku hiyo jioni waonane, ingawa Zitto alionekana kusita kidogo lakini baadae alikubali, Walikubaliana wakutane Sea Cliff Hotel, ilipofika jioni ya siku hiyo Zitto akiwa na marafiki zake wawili Omar Lyasa na Abdalah Said walifika Sea Cliff Hotel wakaketi na kuagiza vinywaji, Baada ya kama dakika kumi hivi Zitto alipokea simu ikimuelekeza alipo bwana Ramadhani Ighondu kisha Zitto akawaambia marafiki zake wamsubiri kidogo, akaondoka kuelekea aliko elekezwa…..
Mashariki mwa lango kuu la kuingilia Sea Cliff Hotel mita kama tatu tu kuna mlango mdogo unaoelekea kwenye vyumba maalumu (VIP), chumba namba 8 ndicho Zitto alichokuwa anaelekezwa kwa simu kuingia, chumba hiki kina meza moja na sofa zilizo zunguka meza ile zenye uwezo wakukaliwa na watu watano hadi sita, Ndani ya chumba kile Zitto anakutana na watu watatu ambao ni Steven Wasira, Ramadhani Ighondu na Abdalla Punja (hawa wote ni TISS)
Mazungumzo yao ndani ya chumba hiki yalianza maramoja, akianza Mr Ighondu kueleza sababu za wao kumuita Zitto, kikubwa ilikuwa ni "bwana Zitto, serikali (ikulu) inakutaka uache kuibana na kuishurutisha hasa kwa hili suala la Buzwagi". Tunaomba kujua shida yako kubwa ni nini?" Ighondu alihoji, Katika majibu yake Zitto anajibu, "Mimi napigania haki za watanzania, nimechaguliwa na wanakigoma na watanzania wameniamini ni wawakilishe hivyo", Lakini mashambulizi ya ushawishi yalipozidi Zitto alilegeza msimamo wake.
Katika kikao hiki kilichochukua masaa mawili, Zitto anaonekana kusita sana na anaomba apewe muda akafikirie aliyoitiwa, wote wanaafiki na kukubali ombi la Zitto na kikao kinaahirishwa.
Siku tatu tu baada ya kikao cha Hotel ya Sea Cliff, yaani tarehe 27/6/2008 Zitto anakutana na Naibu Mkurugenzi wa TISS Ndugu Jack Zoka jijini Arusha, hiki sio kikao chao maalumu bali wamekutana kwa mara ya kwanza wote wakiwa kwenye shughuli za kitaifa, Katika mazungumzo yao wanaonekana ni watu wanaofahamiana japo si kwa undani, Baada ya maongezi ya dakika kadhaa wakiwa wamesimama, Mr Zoka alimuuliza "Vipi vijana wangu walikupa ujumbe, umefikia wapi?" Zitto aliitikia kwa kucheka na kusema "yap nipo tayari, lakini nihakikishieni usalama wangu" Katika maongezi haya, Zoka anasikika akisema "Ondoa shaka" Kisha Mr Zoka anamuagiza Zitto kuwa kesho kutwa yake aende kwa Charles Kimei (Mkurugenzi CRDB Benki) pale Makao makuu, atayakuta maagizo yake huko.
Tarehe 30/6/2008 majira ya saa 12:22 za alasiri, Zitto akiwa ameongozana na kijana mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Rajabu Abdala anaingia eneo la CRDB Benki mtaa wa Azikiwe, na kwenda moja kwamoja kuonana na Bw Kimei, baada ya salamu haikuchukua muda mrefu, Zitto akapelekwa katika moja ya vyumba maalumu vya bank hiyo kwenye jengo hilohilo la Azikiwe, baada ya kufika katika chumba hicho Zitto alihamaki kuwakuta watu wawili katika chumba hicho, mmoja alikuwa ni mfanyakazi wa bank hiyo aliyetambuliwa kwa jina laMaselina K. Kombe na mwingine hakuwa mgeni machoni mwa Zitto, alikuwa ni Ramadhani Ighondu yule wa TISS waliyekuwa naye kwenye kikao cha awali kule Sea Cliff Hotel wiki chache zilizopita, Zitto alikabidhiwa Briefcase nyekundu iliyokuwa imesheheni pesa halali za kitanzania kiasi cha Shilingi milioni 250.
Wakati hayo yakitendeka yule kijana aliyekuja na Zitto alikuwa kwenye gari aina ya Toyota Mark 11 No T 134 AAB yenye rangi nyeupe na vioo vyeusi (Tinted). Baada ya makabidhiano yaliyochukua kama dakika 10 tu, Mr Ighondu alimwambia Zitto, "tunataka utulivu, mengi mazuri yanakuja utafurahia kijana," Na kisha Zitto akatoka na begi lake (Briefcase) na kuingia nalo katiga gari ile na kutokomea.
Uchunguzi umeonyesha kuwa pesa ile aliyokabidhiwa ndugu Zitto, ilitoka katika akaunti Namba 0J56708968923 yenye jina la Shani Maya, ambapo inaonyesha kuwa akaunti hii ilifunguliwa CRDB tawi la azikiwe tarehe 25/6/2008 saa 10:14 asubuhi, kisha tarehe 27/6/2008 iliingizwa kiasi cha pesa za kitanzania milioni 400. Na tarehe 30/6/2008 pesa hizo zilitolewa zote na akaunti hii ilifungwa. Madhumuni ya pesa hii kutoka CRDB kwenda kwa Zitto yanathibitishwa na kikao cha 23/6/2008 pale Hotel ya Sea Cliff kuwa ni kupunguza kasi ya Zitto kuibana serikali hasa anapo kuwa bungeni. Na kweli kasi yake iliyozoeleka kwenye kuibana serikali akiwa bungeni ikapungua na kuweka msingi wa ujenzi wa mashaka juu ya mwenendo wake wa kibunge.
SEHEMU YA PILI 2009
Mnamo Jumatatu ya tarehe 30/11/2009 saa 04:30 asuhuhi wakati wa maandalizi ya uchaguzi wa mkuu wa 2010, idara ya ujasusi ya ccm ilikutana kwa siri pale Moven Pick/SERENA Hotel, ndani ya idara hii wakiwamo Jack Zoka, Wilson Mkama, Kingunge Ngombale Mwiru, Jakaya Kikwete, Nape Nnauye, Fred Kimati, Steven Wasira, Ramadhani Ighondu, Martin Palakyo, Mwigulu Nchemba, Ahamed Msangi na Abdalla Punja. Katika kikao hiki yalijadiliwa mengi sana, lakini kubwa lilikuwa nikukabiliana na vyama vya upinzani hususani CHADEMA, zilipangwa mbinu nyingi sana juu ya Chadema, Mbinu hizo ni kama ifuatavyo:

  1. Kuwanunua wagombea ubunge na Udiwani (Mtakumbuka wagombea wetu kadhaa walikuja kununuliwa na chama kina ushahidi kwenye hili).
  2. Kuwanunua VIONGOZI wajuu wa CHADEMA.
  3. Kutumia TISS kutisha wagombea na wanachama wa Chadema (Hii ilikuwa ni kuwakamata au kuvuruga mikutano).
  4. Kuwaua baadhi ya wafuasi wa Chadema, viongozi wa Chadema na wabunge.
Lakini walitilia mkazo zaidi njia ya kwanza ,ya pili na ya tatu ambapo kikao kilijiridhisha kuwa mmoja wa VIONGOZI wa Chadema ambae ni Zitto Kabwe ni mtu wao ambaye wamesha anza kumtumia, kikubwa liandaliwe fungu tu kwa ajili yakuanza mikakati yao, Waliafikiana mambo mengi kwaajili ya uchaguzi wa mwaka ambao ungefuata, na wakakubaliana mambo kadhaa ambayo walimuagiza Mr Zoka akamwambie Zitto nini cha kufanya ili kupunguza nguvu ya upinzani.
Kwa upande wake Zoka alikiambia kikao kuwa Zitto amemthibitishia kuwa yeye anawafuasi wakutosha ndani ya chama ambapo watamuunga mkono kwa lolote hivyo kikubwa ni pesa tu. Lakini kwanza kikao hicho kilimtaka Mr Zoka amwambie Zitto kuwa taarifa zote zinazoihusu Chadema na za kila vikao vya ndani vya chama zinatakiwa pia ziifikie timu hiyo ya kijasusi ya ccm, pili walitaka Zitto apunguze ushiriki katika majukwaa ya chama na shughuli nyingine za chama. Baada ya kikao sasa ulikuwa ni utekelezwaji wa maadhimio yao.
Zoezi la kikao cha tarehe 30/11/2009 linaonyesha kuzaa matunda hasa baada ya kubainika mawasiliano ya karibu sana kati ya Zitto na Jack Zoka, Kwamfano: Jumamosi ya tarehe 6/12/2009 saa 03:43 asubuhi Zoka kupitia namba yake ya simu +255756809535 alimpigia simu Zitto kupitia simu yake ya kiganjani ambayo ni +255754787550, wakati wa mawasiliano yao haya ya simu Zitto alikuwa Tabata na maongezi yao yalihusu kikao cha 30/11/2009 na kile walichoamua timu ya kijasusi ya chama (ccm) na matakwa yao kwa Zitto. Ndani ya maongezi yao yaliyochukua dakika 68, Zitto anasema, "Mr kazi hii ni nzito, vipi mmeongeza hela? Isije kuwa kama ile ya mwaka jana." Anajibiwa na Zoka kuwa "ondoa shaka una dili na Jamhuri, hela sio tatizo"
Lakini zaidi Zitto anamshauri bwana Zoka kuwa utaratibu wa uchukuaji wa pesa ubadilike, "Mr Jack ile staili ya uchukuaji pesa kule CRDB mwaka jana ilinitisha kidogo halafu hii isije ikabumburuka vyombo vya habari vipo makini kweli sasa hivi" Anajibiwa na Bwana Zoka kuwa "Tunazo njia nyingi sana ambazo si TAKUKURU wala polisi wanaoweza kubaini, tusikilize sisi, tutakacho kuambia ujue ni salama, Haya Mr (Zitto) wewe unayajua mazingira vizuri katika nchi moja ya Ulaya?, au unaweza kutafuta mtu unae mwamini huko ili atumiwe yeye hiyo pesa na awe wa kuaminika ili tumtumie kwa vipindi hivi vyote, kisha uifuate huko au uangalie mwenyewe njia sahihi ya kuichukua huko" Suala la kumpata mtu Ulaya lilionekana kama zito kidogo kwa Zitto, kwani aliomba wawasiliane kesho yake ili awe na jibu la uhakika.
Tarehe hiyo hiyo 6/12/2009 ya Jumamosi saaa 23:05 usiku, Zitto kupitia simu yake ya mkononi namba +255754787550, alipiga namba +4915739444853, kimaongezi walionekana ni watu wanafahamiana sana, alikuwa anaongea na mwanamke ,waliongea mengi lakini kubwa lilikuwa ni Zitto kuomba kupitisha hela yake kwenye akaunti ya huyu mtu. Mwanamke huyu alihoji kama pesa hiyo ni nyingi na haina madhara? Lakini alijbiwa sio nyingi na haina madhara kwakuwa inatoka serikalini na chama tawala, Mwanamke huyo alizidi kuhoji zaidi, "sasa vyombo vya dola vya hapa Berlin vikinihoji nitasema nimepata wapi?" Anajibiwa kuwa "Darling huniamini? Nimesoma na wewe na nimefanya kazi na wewe, lakini huniamini? Utasema umelipwa nchini Tanzania kwa kazi yako", kisha katika maongezi ya hapa na pale dada akakubali na baada ya dakika kumi akamtumia akaunti namba 033B 33093101 Berliner Bank German.
Baada ya kuipata akaunti hii Zitto hakuchelewa, akaipeleka kwa Mr Zoka kwa njia ya ujumbe wa maandishi (sms), baada ya dakika 5, Zoka akampigia simu Zitto kupitia namba +255756809535 nae Zitto akapokea kupitia namba +255754787550, na mazungumzo yao yaliyochukua dakika 6 yakaendelea, Zoka aliuliza swali kuwa "Mwenye akaunti hiyo huko Ujerumani unamwamini na unamjua vema?" Majibu ya Zitto yalikuwa "Ondoa shaka Mr Jack nafanya kazi ya hatari na wewe , siwezi kukuangusha au kujiangamiza, huyu mtu nimesoma nae na ninamfahamu in and out" Zoka akajibu "ok".
Jumatano ya tarehe 16/12/2009 majira ya saa 13:12 za mchana kwa Ujerumani akaunti namba 033B 33093101 Berliner Bank, ziliingizwa dola za kimarekani 266,000 pesa hizi katika uchunguzi zimebainika kuwa zilitoka Tanzania katika Benki ya NMB tawi la NMB House jiji Dar katika akaunti namba 2231604658 yenye jina la TSA, hii ni moja ya akaunti za siri za TISS, ambapo wao ndio huzisimamia akaunti zao zote kwa kutumia mawakala (TISS) walio ndani ya benki hiyo.
Kujiridhisha kuwa pesa hiyo ilifika Ujerumani, kunabainishwa na mawasiliano ya barua pepe kati ya Zitto Kabwe na yule mwanamke wa kijerumani aliyemtumia akaunti ya benki, anafahamika kwa jina la Andrea Cordes, mawasiliano yaliyofanywa tarehe 17 alhamisi saa 20:34 usiku ambapo Andrea kupitia barua pepe yake aco…@gmail.com anamwandikia Zitto kupitia barua pepe ya Zitto iitwayozitto…@gmail.com , Andea anasema "Hey sweet, mzigo yako imefika, can we talk?" Ujumbe huu unajibiwa na Zitto saa 21:03 usiku huo kwakusema, "I'm so sorry my darling, nimechelewa kukujibu, I will call you soon"
Saa 23:23 Zitto Kabwe kupitia simu yake ya kiganjani namba +255754787550, alimpiga Andrea Codes kupitia namba +4915739444853, akimweleza kuwa anashukuru kwa mzigo kumfikia, lakini anataka kumpa utaratibu wa kuichukua hiyo pesa, ambapo alimweleza kuwa atakuwa anaichukua kidogo kidogo kila mwezi kwa njia ya Western Union kuanzia dola 20,000 hadi dola 50,000, wakati huo Andea Codes atakula kamisheni ya dola 25,000.
Uchunguzi wa ndani umebaini pesa hiyo ilitumwa kwa Zitto ndani ya miezi 8 kwa vipindi tofauti kupitia Western Union kama alivyoomba, na alikuwa anachukulia maeneo tofauti tofauti hapa jijini Dar, vilevile uchunguzi umebaini kuwa mwanamke huyu ni Mjerumani aliyewahi kuishi Tanzania na amezaa mtoto mmoja hapa Tanzania, Mwanamke huyu anaitwa Andrea Cordes, anaishi Mechernich Ujerumani, mtaa namba 134, nyumba namba 141, anafanya kazi UN Women Nationales Komitee Deutschland e.V. Shirika ambalo shughuli zake huendeshea pia Tanzania. Katika uchunguzi zaidi imebainika kuwa akaunti aliyomtumia Zitto ni ya kwake binafsi, katika ushahidi tuliobaini kupitia benki iitwayo Berliner Bank yenye Code No Hardenbergstraße 32, 10623 iliyopo mjini Berlin nchini Ujerumani.

SEHEMU YA TATU 2010
Uhusiano usio wa kawaida na wa karibu wa Zitto na viongozi wa ccm, serikali na wale wa Usalama wa Taifa uliendelea kushamiri hasa kipindi cha kampeni na kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2010, Mfano tarehe 7/9/2010 siku ya jumanne saa 11:21 asubuhi, Ahmed Msangi kupitia namba yake ya simu ya kiganjani +255784277884, alimpigia Zitto kupitia simu ya kiganjani namba +255754787550 waliongea mambo mengi japo kwa muda mfupi, na jambo kubwa lilikuwa ni "vipi kuna kipya ndani ya Chadema?" Zitto alijibu "yapo mengi lakini hayana impact kwa ccm" Msangi anajibu "Ok mr nikutakie siku njema"

Lakini mawasiliano ya simu yaliyochukua mda mrefu zaidi yalikuwa kati ya Zitto na Zoka yaliyofanywa tarehe 10/9/2010 siku ya ijumaa saa 07:04 jioni na mazungumzo yao yalichukua dakika 71, Mazungumzo haya yalifanywa wakati huo Zitto akiwa katika hoteli ya Blue Pearl Ubungo, Mr Zoka alitaka kujua mambo kadhaa kuelekea Uchaguzi mkuu, kwanza alimuuliza "Mr Zitto umejiandaaje, una timu ya kazi?" Zitto akajibu "nipo fiti kiakili na kimwili na nina timu ya kutosha, ondoa shaka juu yangu, kama ipo hiyo hela tumeni tu Ujerumani kwenye ile akaunti, na ningeomba kukutana na mwenyeti wenu (rais JK)" Zoka lijibu "hilo halina tabu nitalifikisha sehemu husika bwana Zitto",
Uchunguzi umebainisha kuwa akaunti namba 033B 33093101 Berliner Bank ya German iliendelea kuingizwa pesa kwa nyakati tofauti kutoka Tanzania kupitia NMB akaunti namba 2231604658 yenye jina la TSA ambayo ni moja ya akaunti za siri za TISS.
Mfano: tarehe 29/9/2010 siku ya juma tano, kiasi cha dola 250,000 kiliingizwa kwenye akaunti hii 033B 33093101 ya Ujerumani, kutoka akaunti namba 2231604658 NMB Tanzania,
Tarehe 06/01/2011 siku ya alhamisi, kiasi cha dola 240,000 kiliingizwa kwenye akaunti hii 033B 33093101 ya Ujerumani, kutoka akaunti namba 2231604658 NMB Tanzania,
Tarehe 21/6/2011 siku ya jumanne, kiasi cha dola 240,000 kiliingizwa kwenye akaunti hii 033B 33093101 ya Ujerumani, kutoka akaunti namba 2231604658 NMB Tanzania,
Tarehe 09/12/2011 siku ya ijumaa, kiasi cha dola 255,000 kiliingizwa kwenye akaunti hii 033B 33093101 ya Ujerumani, kutoka akaunti namba 2231604658 NMB Tanzania,
Tarehe 02/02/2012 siku ya alhamisi, kiasi cha dola 260,000 kiliingizwa kwenye akaunti hii 033B 33093101 ya Ujerumani, kutoka akaunti namba 2231604658 NMB Tanzania,
Tarehe 14/05/2012 siku ya jumatatu, kiasi cha dola 250,000 kiliingizwa kwenye akati hii 033B 33093101 ya Ujerumani, kutoka akaunti namba 2231604658 NMB Tanzania,
Tarehe 13/12/2012 siku ya alhamisi, kiasi cha dola 255,000 kiliingizwa kwenye akati hii 033B 33093101 ya Ujerumani, kutoka akaunti namba 2231604658 NMB Tanzania,
Uchunguzi umebainisha kuwa pesa zote zilimfikia Zitto kwa njia ya Western Union akitumiwa dola 50,000 mpaka dola 20,000 kati ya wiki mbili mpaka mwezi mmoja.

SEHEMU NNE: MATUMIZI YA PESA HIYO
Uchunguzi umezidi kubaini kuwa kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2011, kutoka kuugwa mkono na wanachadema kama mwanasiasa makini, Zitto aliamua kuunda kundi la uasi ndani ya chama. Baadhi ya waliounda kundi hili ni:

Zitto Z. Kabwe +255754787550/756809535/713730256
Juliana Shonza +255714669850/756359073
Habib Mchange +255762178678
Mtela Mwampamba +255718037358/755178927
Gwakisa Burton +255713316790
Eddo Makata +255757149043/655148758
Greyson Nyakarungu +255755023503
Adams Chagulani +255767137831
Deogratius Kisandu +255655025609
John M. Shibuda +255754465597
Kitila Mkumbo +255754301908
Exaud Mamuya +255767160685
Ben Saanane +255768078523

Timu ya upelelezi imebaini kuwa kundi hili lilikuwa linapokea fedha kutoka kwa Zitto kwa njia ya M-Pesa, Uchunguzi umebaini kuwa kuanzia 2011 kundi hili lilianza kutumiwa pesa na Zitto kwa njia ya M-Pesa kila mwezi, ambapo kila mwanakundi alikuwa akipokea kati ya 150,000/= mpaka 200,000/= , na ilipofika mwishoni mwa mwaka 2012 kundi hili sasa likawa linalipwa karibu kwa wiki,
Takwimu za malipo ya wafuasi wa kundi hili kutoka kwa Zitto kwa mwaka 2012 zinaonyesha walilipwa kwa njia ya M-PESA No+255756809535 hii ni namba mojawapo ya Zitto Zuberi Kabwe:
Tarehe 25/2/2012 saa 10:09 asubuhi, Zitto Kabwe kupitia +255756809535 aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake, Juliana Shonza +255756359073, Habib Mchange +255762178678, Mtela Mwampamba +255755178927, Gwakisa Burton +255713316790, Eddo Makata +255757149043, Greyson Nyakarungu +255755023503, Deogratius Kisandu +255655025609, Adams Chagulani +255767137831, Exaud Mamuya +255767160685, Ben Saanane +255768078523,
Baada ya hapo saa 10:32 asubuhi hiyohiyo Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255756809535 aliwatumia shilingi 200,000/= Mkumbo Kitila +255754301908 na John Shibuda +255754465597
Tarehe 26/3/2012 saa 11:12 asubuhi, Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255756809535 aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake, Juliana Shonza +255756359073, Habib Mchange +255762178678, Mtela Mwampamba +255755178927, Gwakisa Burton +255713316790, Eddo Makata +255757149043, Greyson Nyakarungu +255755023503, Deogratius Kisandu +255655025609, Adams Chagulani +255767137831, Exaud Mamuya +255767160685, Ben Saanane +255768078523, Baada ya hapo saa 11:43 asubuhi hiyohiyo Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255756809535 aliwatumia shilingi 200,000/= Mkumbo Kitila +255754301908 na John Shibuda +255754465597
Tarehe 20/4/2012 saa 09:11 asubuhi, Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255756809535 aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake, Juliana Shonza +255756359073, Habib Mchange +255762178678, Mtela Mwampamba +255755178927, Gwakisa Burton +255713316790, Eddo Makata +255757149043, Greyson Nyakarungu +255755023503, Deogratius Kisandu +255655025609, Adams Chagulani +255767137831, Exaud Mamuya +255767160685, Ben Saanane +255768078523, Baada ya hapo saa 10:30 asubuhi hiyohiyo Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255756809535 aliwatumia shilingi 200,000/= Mkumbo Kitila +255754301908 na John Shibuda +255754465597
Tarehe 22/5/2012 saa 10:15 asubuhi, Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255756809535 aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake, Juliana Shonza +255756359073, Habib Mchange +255762178678, Mtela Mwampamba +255755178927, Gwakisa Burton +255713316790, Eddo Makata +255757149043, Greyson Nyakarungu +255755023503, Deogratius Kisandu +255655025609, Adams Chagulani +255767137831, Exaud Mamuya +255767160685, Ben Saanane +255768078523, Baada ya hapo saa 11:02 asubuhi hiyohiyo Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255756809535 aliwatumia shilingi 200,000/= Mkumbo Kitila +255754301908 na John Shibuda +255754465597
Tarehe 28/6/2012 saa 13:51 mchana, John M. Shibuda kupitia namba yake ya simu +255754465597 aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wenzake, Habib Mchange +255762178678, Mtela Mwampamba +255755178927, Gwakisa Burton +255713316790, Eddo Makata +255757149043, Deogratius Kisandu +255655025609, Adams Chagulani +255767137831, Exaud Mamuya +255767160685, Ben Saanane +255768078523, Greyson Nyakarungu +255755023503, Juliana Shonza +255756359073,
Baada ya Shibuda kuwalipa 28/6/2012 saa 13:51 mchana, sasa Zitto alibadili mfumo wa malipo ukawa wa TIGO PESA +255713730256 lakini viwango vilevile na mtiririko ulele.
Tarehe 22/7/2012 saa 08:17 asubuhi, Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255713730256 aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake, Ben Saanane +255768078523, Adams Chagulani +255767137831, Juliana Shonza +255756359073, Habib Mchange +255762178678, Mtela Mwampamba +255755178927, Gwakisa Burton +255713316790, Eddo Makata +255757149043, Greyson Nyakarungu +255755023503, Deogratius Kisandu +255655025609, Exaud Mamuya +255767160685, Kisha saa 09:38 asubuhi hiyohiyo Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255713730256 aliwatumia shilingi 200,000/= Mkumbo Kitila +255754301908 na John Shibuda +255754465597
Tarehe 24/8/2012 saa 09:06 asubuhi, Zitto Kabwe kupitia ++255713730256 aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake, Ben Saanane +255768078523, Adams Chagulani +255767137831,Juliana Shonza +255756359073, Habib Mchange +255762178678, Mtela Mwampamba +255755178927, Gwakisa Burton +255713316790, Eddo Makata +255757149043, Greyson Nyakarungu +255755023503, Deogratius Kisandu +255655025609, Exaud Mamuya +255767160685, Kisha saa 09:23 asubuhi hiyohiyo Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255756809535 aliwatumia shilingi 200,000/= Mkumbo Kitila +255754301908 na John Shibuda +255754465597
Tarehe 02/09/2012 saa 09:52 asubuhi, Zitto Kabwe kupitia +255713730256 aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake, Ben Saanane +255768078523, Adams Chagulani +255767137831, Juliana Shonza +255756359073, Habib Mchange +255762178678, Mtela Mwampamba +255755178927, Gwakisa Burton +255713316790, Eddo Makata +255757149043, Greyson Nyakarungu +255755023503, Deogratius Kisandu +255655025609, Exaud Mamuya +255767160685, Kisha saa 10:43 asubuhi hiyohiyo Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255713730256 aliwatumia shilingi 200,000/= Mkumbo Kitila +255754301908 na John Shibuda +255754465597
Tarehe 20/09/2012 saa 10:19 asubuhi, Zitto Kabwe kupitia +255713730256 aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake, Ben Saanane +255768078523, Adams Chagulani +255767137831, Juliana Shonza +255756359073, Habib Mchange +255762178678, Mtela Mwampamba +255755178927, Gwakisa Burton +255713316790, Eddo Makata +255757149043, Greyson Nyakarungu +255755023503, Deogratius Kisandu +255655025609, Exaud Mamuya +255767160685, Baada ya hapo saa 10:53 asubuhi hiyohiyo Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255713730256 aliwatumia shilingi 200,000/= Mkumbo Kitila +255754301908 na John Shibuda +255754465597
Tarehe 24/10/2012 saa 11:18 asubuhi, Zitto Kabwe kupitia +255713730256 aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake, Ben Saanane +255768078523, Adams Chagulani +255767137831, Juliana Shonza +255756359073, Habib Mchange +255762178678, Mtela Mwampamba +255755178927, Gwakisa Burton +255713316790, Eddo Makata +255757149043, Greyson Nyakarungu +255755023503, Deogratius Kisandu +255655025609, Exaud Mamuya +255767160685, Kisha saa 11:52 asubuhi hiyohiyo Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255713730256 aliwatumia shilingi 200,000/= Mkumbo Kitila +255754301908 na John Shibuda +255754465597
Tarehe 25/11/2012 saa 10:34 asubuhi, Zitto Kabwe kupitia +255713730256 aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake, Juliana Shonza +255756359073, Habib Mchange +255762178678, Mtela Mwampamba +255755178927, Gwakisa Burton +255713316790, Eddo Makata +255757149043, Greyson Nyakarungu +255755023503, Deogratius Kisandu +255655025609, Adams Chagulani +255767137831, Exaud Mamuya +255767160685, Baada ya hapo saa 10:56 asubuhi hiyohiyo Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255713730256 aliwatumia shilingi 200,000/= Mkumbo Kitila +255754301908 na John Shibuda +255754465597
Tarehe 29/11/2012 saa 12:12 mchana, Zitto Kabwe kupitia +255713730256 aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake, Juliana Shonza +255756359073, Habib Mchange +255762178678, Mtela Mwampamba +255755178927, Gwakisa Burton +255713316790, Eddo Makata +255757149043, Greyson Nyakarungu +255755023503, Deogratius Kisandu +255655025609, Adams Chagulani +255767137831, Exaud Mamuya +255767160685, Baada ya hapo saa 12:32 mchana huohuo Zitto Kabwe kupitia namba yake ya simu +255713730256 aliwatumia shilingi 200,000/= Mkumbo Kitila +255754301908 na John Shibuda +255754465597
Kundi hili lilikuwa na mipango mingi sana, lakini lengo/shabaha/dhamira ilikuwa ni moja tu nayo ni kukidhohofisha Chadema kwa manufaa ya ccm. Uthibitisho wa lengo la kundi hili unabainishwa katika mawasiliano ya simu kati ya Zitto na wanakikundi hicho, katika ujumbe wa maandishi (sms) aliousambaza kwa wanakikundi hiki Zitto anasisitiza umakini ili wasije kujulikana na Chama, vilevile anawasisitiza kukisajili kikundi hiki ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti ya benki ya kikundi hiki,
Ujumbe mwingine aliousambaza tarehe 30/11/2012 saa 08:21 kwa wafuasi wa kundi hili kupitia namba +255713730256, unasema, "Ni lazima tukidhibiti hiki kibabu vile vile lazima tumng'oe Mbowe, Tunadanganyana tu kuwa chadema itaingia ikulu, kwanza simamieni harakati za kushinikiza kadi ya kibabu irudishwe ccm".
Timu ya kijasusi imejiridhidha kuwa Ben Saanane alikuwa kwenye kundi hilo kwa kazi maalumu na ameisaidia sana timu hii ya ujasusi kupata habari muhimu za ndani za kundi hilo la uasi lililokuwa limejipanga kwa ustadi likitumia mbinu za kuwagombanisha viongozi wa juu wa chama hasa likilenga Mwenyekiti na Katibu mkuu, huku juhudi za kumkwamisha mwenyekiti wa BAVICHA nazo zikipamba moto na kusukwa kwa ustadi mkubwa, Kikundi hiki hakikuishia hapo tu kwani kilianzisha mradi wa kuwatukana viongozi wa Chadema na familia zao, kuanzisha tuhuma za uongo na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii. Lilianzisha mradi wa kuhubiri udini, ukanda na ukabila ndani ya chama kwa kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Likaanzisha tena harakati za kumpindua mwenyekiti kupitia kifupi cha jina PM7 (Pindua Mbowe 7) nk.
MAPENDEKEZO YA HATUA ZA KUCHUKUA
Baada ya kujiridhisha kuwa Zitto Zuber Kabwe Mbunge wa Chadema na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, ameasi Chama na ameunda kundi ndani ya chama linaloendesha vuguvugu la mapinduzi kwa viongozi halali wa chama kwa ufadhiri wa chama tawala ccm, ikiwa ni kinyume cha katiba na itifaki za chama, Timu ya ujasusi inapendekeza yafuatayo:

Chama kijiridhishe bila ya kuacha chembe ya mashaka kutoka kwa wahusika wa kikundi hiki ambao ni Zitto na wenzake, Ikiwa watakiri kuhusika, Chama kiwaamuru wawaombe radhi wanachama.
Naibu Katibu mkuu ndugu Zitto Kabwe na Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA ndugu Julina Shonza wapime wenyewe kama wanastahili kuendelea na nafasi zao za uongozi ndani ya Chama.
Ikiwa Chama kitaamua kuunda tume ya uchunguzi wa haya, wahusika wote hasa wenye vyeo kama Zitto Kabwe na Juliana Shonza wawekwe pembeni na shughuli za Chama ili kupisha uchunguzi huru.
Chama kiwavue uanachama Zitto Kabwe na kundi lake lote bila kusita, hii inatokana na mikakati ya kukiangamiza chama inayoendelea ndani ya CCM kwa ushirikiano wa Zitto Kabwe na viongozi waandamizi wa ccm.
Kuelekea 2015, Idara ya ujasusi ya chama iongezewe nguvu na mafunzo, ikiwezekana kiundwe kikosi maalumu nje ya timu ya kijasusi iliyopo sasa na kipewe mafunzo na vitendea kazi vya kutosha kwaajili ya ulinzi wa chama na viongozi wake.
Chama kianzishe utaratibu wa semina au mafunzo ya kipindi kifupi na kati kwa makada wake jinsi ya utumiaji wa mitandao ya kijamii.
Kiundwe kitengo cha propaganda za kisiasa chenye watu weledi wa mambo na masuala mbalimbali na kipewe uwezo ili kukabiliana na propanda za chama tawala na vyama vingine.
Chama kizidi kuchukuahatua stahiki za kimaamuzi dhidi ya viongozi au wanachama wanao dhoofisha harakati za mabadiliko kuelekea 2015 na baada ya 2015
Mwisho tunawashukuru baadhi ya maafisa wa kijasusi wa mjini Berlin Ujerumani waliosaidia kupata baadhi ya taarifa muhimu kutoka Ujerumani
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameuweka njia panda uanachama wake ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kukubali pingamizi lake la kuizuia Kamati Kuu (CC) ya chama hicho isimjadili hadi kesi yake ya msingi itakapokuwa imesikilizwa. Kwa uamuzi huo, Zitto sasa atabaki kuwa mwanachama kwa nguvu ya mahakama hadi hapo itakapoamriwa vinginevyo.
Sasa Zitto ataungana na wabunge wenzake wawili, David Kafulila wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) na Hamad Rashid Mohammed wa Wawi (CUF) ambao pia ubunge wao upo kwa nguvu ya mahakama.
Zitto alifungua kesi mahakamani hapo siku moja kabla ya CC kuanza vikao vyake ambavyo vilikuwa vijadili utetezi wa tuhuma zake za kuendesha mkakati wa siri wa kusaliti chama, akiomba mahakama izuie suala la uanachama wake lisijadiliwe hadi kesi yake isikilizwe.
Akitoa uamuzi wa awali, Jaji John Utamwa, alisema kuwa mahakama imeridhia ombi la Zitto kuwa CHADEMA au chombo chochote kisijadili uanachama wake hadi kesi ya msingi itakapomalizika.
Akisoma maelezo ya awali, Utamwa alisema kuwa wakili Peter Kibatala anayewakilisha Bodi ya Udhamini ya CHADEMA na Katibu Mkuu ambao ndio washtakiwa, alikula kiapo kwa niaba yao jambo ambalo si sahihi.
Utamwa alisema kuwa kwa mazingira ya kesi kuhusisha Bodi ya Udhamini ya CHADEMA na Katibu Mkuu, ilikuwa si sahihi kwa wakili kula kiapo kwa niaba yao.
Wakizungumza baada ya kutoka mahakamani, mawakili wa upande wa CHADEMA, Kibatala na Tundu Lissu walisema kuwa kuhusiana na hati ya kiapo, ipo sheria inayoruhusu wakili kula kiapo kwa ajili ya mteja wake.
Walisema kuwa wanaheshimu uamuzi wa mahakama japo hawajaridhika, na hivyo watachukua hatua za ziada.
Wakili wa Zitto, Albert Msando, aliomba uamuzi wa mahakama uheshimike kwani ni hatua za haki kutendeka na mteja wake kupata nafasi ya kusikilizwa.
Katika kesi ya msingi, Zitto anaiomba mahakama ikizuie chama hicho kumchukulia hatua, ambapo kesi hiyo inatarajiwa kutajwa Februari 13, mwaka huu.
Zitto aliwasilisha maombi dhidi ya Baraza la Wadhamini la CHADEMA pamoja na Katibu Mkuu wa chama, Dk. Willibrod Slaa, akiiomba mahakama itoe zuio la muda kwa Kamati Kuu kutojadili uanachama wake.
Katika kesi hiyo, Zitto anaiomba mahakama iizuie Kamati Kuu kujadili uanachama wake hadi rufaa yake itakaposikilizwa na Baraza Kuu la chama na kuomba mahakama imwamuru Dk. Slaa ampe nakala za taarifa za vikao vilivyomvua uongozi ili akate rufaa.

Hali ilivyokuwa
Zitto alipokelewa na wanachama wa CHADEMA kwa kuzomewa kuanzia hoteli ya Hyatt Kempisky hadi katika lango kuu la kuingia Mahakama Kuu.
Sauti hizo zilisikika zikimba na kuzomea; “Zitto kibaraka wa CCM; CCM huyo…”
Zitto ambaye aliongozana na walinzi wanne wenye miili mikubwa (mabaunsa), alikuwa ameinamisha sura chini na kutembea haraka kuingia mahakamani.
Hata hivyo, kabla ya kuingia lango kuu la mahakama, alipepesuka na kuvuka kiatu kimoja cha mguu wa kushoto.
Baada ya kadhia hiyo ya nje, alikutana na wanachama wengine wa CHADEMA ndani ya mahakama, ambao walimzomea hadi kwenye mlango wa vyumba vya mahakama.
Nako nje, mamluki wanaodaiwa kukodiwa na Zitto tangu kuanza kwa kesi hiyo, jana hali ilikuwa ni tofauti kutokana na kufika kwa uchache huku wakizomewa na wanachama wa CHADEMA.
Tanzania Daima ilidokezwa kuwa walinzi waliokuwa wanamlinda Zitto, walifahamika kwa jina moja moja la Tino, Evans na Ziggy.
Ndani ya mahakama, kabla ya kesi kuanza baadhi ya wanachama wa CHADEMA walimtambua mtu mmoja aliyevaa suti nyeusi na kuanza kumshambulia kwa maneno kuwa ni kibaraka wa Ridhiwani Kikwete hadi mtu huyo alipojitetea akidai ni wakili.

Vituko vya Zitto kisiasa
Zitto ambaye anahaha kila kona ili asivuliwe uanachama wa CHADEMA, amekuwa na mtiririko wa matukio mengi ya kauli ambazo zimechangia wananchi kumtilia shaka mwenendo wake ndani ya chama.
Mwaka 2010 wakati nchi ikielekea uchaguzi mkuu, Zitto alitishia kutowania tena ubunge katika jimbo lake la Kigoma Kaskazini kwa madai kuwa ameombwa kugombea katika majimbo ya Kigoma Mjini, Kinondoni, Geita na Kahama.
Lakini dakika za mwishoni kabisa, Zitto alirudi kugombea jimboni kwake akidai ameshauriwa na wazee.
Baada ya uchaguzi mkuu, mwanasiasa huyo alitangaza kutogombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2015, akidai kuwa ataachana na siasa ili akafanye kazi ya kitaaluma chuo kikuu.
Muda mfupi baadaye, akakaririwa na vyombo vya habari kwamba anaandamwa ndani ya chama, kiasi cha kufikia hatua ya kutembea na barua ya kutaka kujiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.
Machi mwaka jana, mbunge huyo alitangaza nia ya kuutaka urais wa Tanzania, lakini baada ya kuibuka mjadala mkubwa ndani na nje ya chama chake akielezwa kuwa umri wake hajakidhi matakwa kikatiba, Septemba mwaka huo, alitengua nia hiyo.
Akiwa katika ziara ya kichama mkoani Tabora Novemba mwaka jana, Zitto pia alitengua kauli yake ya kutogombea ubunge mwaka 2015 akisema anaitafakari upya baada ya kuona kero nyingi zinazowakabili wananchi.
Kauli tatanishi za Zitto zimezidi kuongeza shaka hasa katika majibu yake hivi karibuni kupitia mtandao wake wa kijamii wa facebook wakati akifafanua tuhuma zilizoelekezwa kwake na mwanasheria wa CHADEMA, Lissu.
Lissu alidai kuwa Zitto amehongwa magari mawili na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ili amwezeshe kupita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Hata hivyo, katika utetezi wake wa maandishi kupitia ukurasa wake, Zitto aliandika kuwa; “Lissu amenituhumu kuwa nimehongwa magari 2 na mheshimiwa Nimrod Mkono. Mimi ninamiliki gari mbili, Freelander ninayotumia Dar es Salaam na Toyota Carina ninayotumia jimboni.”
Majibu ya Zitto yalitofautiana na Mkono ambaye katika taarifa yake alisema kuna magari mawili yanayohusishwa na Zitto na kuyataja kuwa ni Toyota Land Cruiser na Nissan Patrol.
“Sijawahi kumpatia Zitto magari, isipokuwa kuhusu hiyo Land Cruiser, nilitoa msaada wa kuwanusuru Zitto na Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe), kule Tarime kwenye msiba wa marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CHADEMA), kwani walikuwa wakitishiwa kupigwa.
“Walipofika Mwanza, Zitto aliwasiliana na mimi kuhusu ununuzi wa gari hilo na kupitia wakala wangu nilimuuzia,” alisema Mkono.
Kuhusu Nissan Patrol, Mkono alisema lilikodishwa kwa Zitto na hadi sasa bado analipa gharama za kulikodisha.
Utata katika suala hili uko kwenye aina za magari zilizotajwa na wanasiasa hawa wawili. Wakati Zitto akitaja kumiliki Freelander na Toyota Carina bila kufafanua kama anayo magari mengine, Mkono anasema amemuuzia Land Cruiser na Nissan Patrol.

Kada CCM anena
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro, David Mgesi, amesema yanayotokea sasa kwa Zitto ni kile alichokuwa akikisema kwa muda mrefu kuhusu mbunge huyo.
Mgesi ambaye kwa sasa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisema wakati akiwa CHADEMA, alishaonya mienendo ya Zitto kwa kuona kwamba ni mtu ambaye anaweza kukisaliti chama wakati wowote.
Kwamba viongozi wa juu wa CHADEMA waliweza kumuamini Zitto na kumuona kuwa ni mtu mwenye busara.
Akitolea mfano, alisema ilikuwa mwaka 2005, Zitto alipewa dhamana ya kutengeneza bajeti ya chama, na baada ya kuwagawia taarifa ya wajumbe wa Kamati Kuu alitaka wazirudishe kwa madai kuwa hawaamini kwani wanaweza kuvujisha siri nje.
“Baada ya kauli ile nilimuomba Mwenyekiti, Freeman Mbowe tujadili kauli hiyo, lakini lilifunikwa na Zitto akatetewa kuwa aliteleza.
“Sasa ukiangalia leo nani msaliti kama sio yeye ambaye amekuwa akipokea fedha kwa muda mrefu kwa lengo la kukivuruga chama?” alihoji.
Akizungumzia hatua ya Zitto kwenda mahakamani, Mgesi alisema sio sahihi na badala yake alitakiwa kwanza kujibu tuhuma zote zilizoelekezwa kwake ili kuwaelewesha Watanzania na kuwahakikishia anachotuhumiwa si sahihi.
Hata hivyo, Mgesi alisema inasikitisha kuona hadi sasa Zitto na CCM wanaotuhumiwa katika kupeana fedha ili kukiharibu CHADEMA wameshindwa kujitokeza kukanusha taarifa hizo.
“Zitto anapaswa ajitokeze akane kama hakupokea fedha hizo zinazodaiwa kupitia benki ya CRDB, vile vile Serikali ya CCM ilipaswa kuthibitisha kama akaunti zilizotajwa kuwa za Idara ya Usalama wa Taifa ni za kweli au hapana,” alisema.
Mgesi alisema kitendo cha pande zote kukaa kimya wakati suala tajwa likiendelea kushika kasi, kunaibua maswali mengi kwa wananchi.
Alisema mgogoro huu ni wa muda mrefu na umetengenezwa huku akikumbushia namna ambavyo Waziri Stephen Wasira alikuwa akisisika akisema kuwa CHADEMA itakufa kabla ya mwaka 2015.
Mgesi pia alitaja matukio ya kubambikiwa kesi ya ugaidi kwa Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare na vijana wengine watano kuwa ulikuwa ni mwendelezo wa mkakati wa kukiua chama hicho.
Aliwaonya vingozi wa CCM ambao wamekuwa wakizungumzia mgogoro huo wa CHADEMA majukwaani, akiwataka kuachana na kazi hiyo kwa kuwa sio iliyowaweka madarakani.
“Wakati CCM inapewa dhamana na wananchi kuongoza, katika ahadi zake hakuna mahali wanasema watakuwa wakijadili mgogoro wa CHADEMA,” alisema.

Vita kati ya wanademkrasia asilia vs demokrasia mabadiliko. CDM chali, hoi bini taabani!!!!!!
 
Sombetini na Bunda CHADEMA wameisha wanyang'anya CCM kata 2 za udiwani ktk uchaguzi wa Feb 18!Wewe endelea kujipa moyo hivyo hivyo!

Kata 2 tayari CHADEMA wanazo kibindoni na likely wataongeza zingine!Feb 18 usikimbie kuja hapa na Feb 18 sio mbali toka sasa!
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameuweka njia panda uanachama wake ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kukubali pingamizi lake la kuizuia Kamati Kuu (CC) ya chama hicho isimjadili hadi kesi yake ya msingi itakapokuwa imesikilizwa. Kwa uamuzi huo, Zitto sasa atabaki kuwa mwanachama kwa nguvu ya mahakama hadi hapo itakapoamriwa vinginevyo.
Sasa Zitto ataungana na wabunge wenzake wawili, David Kafulila wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) na Hamad Rashid Mohammed wa Wawi (CUF) ambao pia ubunge wao upo kwa nguvu ya mahakama.
Zitto alifungua kesi mahakamani hapo siku moja kabla ya CC kuanza vikao vyake ambavyo vilikuwa vijadili utetezi wa tuhuma zake za kuendesha mkakati wa siri wa kusaliti chama, akiomba mahakama izuie suala la uanachama wake lisijadiliwe hadi kesi yake isikilizwe.
Akitoa uamuzi wa awali, Jaji John Utamwa, alisema kuwa mahakama imeridhia ombi la Zitto kuwa CHADEMA au chombo chochote kisijadili uanachama wake hadi kesi ya msingi itakapomalizika.
Akisoma maelezo ya awali, Utamwa alisema kuwa wakili Peter Kibatala anayewakilisha Bodi ya Udhamini ya CHADEMA na Katibu Mkuu ambao ndio washtakiwa, alikula kiapo kwa niaba yao jambo ambalo si sahihi.
Utamwa alisema kuwa kwa mazingira ya kesi kuhusisha Bodi ya Udhamini ya CHADEMA na Katibu Mkuu, ilikuwa si sahihi kwa wakili kula kiapo kwa niaba yao.
Wakizungumza baada ya kutoka mahakamani, mawakili wa upande wa CHADEMA, Kibatala na Tundu Lissu walisema kuwa kuhusiana na hati ya kiapo, ipo sheria inayoruhusu wakili kula kiapo kwa ajili ya mteja wake.
Walisema kuwa wanaheshimu uamuzi wa mahakama japo hawajaridhika, na hivyo watachukua hatua za ziada.
Wakili wa Zitto, Albert Msando, aliomba uamuzi wa mahakama uheshimike kwani ni hatua za haki kutendeka na mteja wake kupata nafasi ya kusikilizwa.
Katika kesi ya msingi, Zitto anaiomba mahakama ikizuie chama hicho kumchukulia hatua, ambapo kesi hiyo inatarajiwa kutajwa Februari 13, mwaka huu.
Zitto aliwasilisha maombi dhidi ya Baraza la Wadhamini la CHADEMA pamoja na Katibu Mkuu wa chama, Dk. Willibrod Slaa, akiiomba mahakama itoe zuio la muda kwa Kamati Kuu kutojadili uanachama wake.
Katika kesi hiyo, Zitto anaiomba mahakama iizuie Kamati Kuu kujadili uanachama wake hadi rufaa yake itakaposikilizwa na Baraza Kuu la chama na kuomba mahakama imwamuru Dk. Slaa ampe nakala za taarifa za vikao vilivyomvua uongozi ili akate rufaa.

Hali ilivyokuwa
Zitto alipokelewa na wanachama wa CHADEMA kwa kuzomewa kuanzia hoteli ya Hyatt Kempisky hadi katika lango kuu la kuingia Mahakama Kuu.
Sauti hizo zilisikika zikimba na kuzomea; "Zitto kibaraka wa CCM; CCM huyo…"
Zitto ambaye aliongozana na walinzi wanne wenye miili mikubwa (mabaunsa), alikuwa ameinamisha sura chini na kutembea haraka kuingia mahakamani.
Hata hivyo, kabla ya kuingia lango kuu la mahakama, alipepesuka na kuvuka kiatu kimoja cha mguu wa kushoto.
Baada ya kadhia hiyo ya nje, alikutana na wanachama wengine wa CHADEMA ndani ya mahakama, ambao walimzomea hadi kwenye mlango wa vyumba vya mahakama.
Nako nje, mamluki wanaodaiwa kukodiwa na Zitto tangu kuanza kwa kesi hiyo, jana hali ilikuwa ni tofauti kutokana na kufika kwa uchache huku wakizomewa na wanachama wa CHADEMA.
Tanzania Daima ilidokezwa kuwa walinzi waliokuwa wanamlinda Zitto, walifahamika kwa jina moja moja la Tino, Evans na Ziggy.
Ndani ya mahakama, kabla ya kesi kuanza baadhi ya wanachama wa CHADEMA walimtambua mtu mmoja aliyevaa suti nyeusi na kuanza kumshambulia kwa maneno kuwa ni kibaraka wa Ridhiwani Kikwete hadi mtu huyo alipojitetea akidai ni wakili.

Vituko vya Zitto kisiasa
Zitto ambaye anahaha kila kona ili asivuliwe uanachama wa CHADEMA, amekuwa na mtiririko wa matukio mengi ya kauli ambazo zimechangia wananchi kumtilia shaka mwenendo wake ndani ya chama.
Mwaka 2010 wakati nchi ikielekea uchaguzi mkuu, Zitto alitishia kutowania tena ubunge katika jimbo lake la Kigoma Kaskazini kwa madai kuwa ameombwa kugombea katika majimbo ya Kigoma Mjini, Kinondoni, Geita na Kahama.
Lakini dakika za mwishoni kabisa, Zitto alirudi kugombea jimboni kwake akidai ameshauriwa na wazee.
Baada ya uchaguzi mkuu, mwanasiasa huyo alitangaza kutogombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2015, akidai kuwa ataachana na siasa ili akafanye kazi ya kitaaluma chuo kikuu.
Muda mfupi baadaye, akakaririwa na vyombo vya habari kwamba anaandamwa ndani ya chama, kiasi cha kufikia hatua ya kutembea na barua ya kutaka kujiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.
Machi mwaka jana, mbunge huyo alitangaza nia ya kuutaka urais wa Tanzania, lakini baada ya kuibuka mjadala mkubwa ndani na nje ya chama chake akielezwa kuwa umri wake hajakidhi matakwa kikatiba, Septemba mwaka huo, alitengua nia hiyo.
Akiwa katika ziara ya kichama mkoani Tabora Novemba mwaka jana, Zitto pia alitengua kauli yake ya kutogombea ubunge mwaka 2015 akisema anaitafakari upya baada ya kuona kero nyingi zinazowakabili wananchi.
Kauli tatanishi za Zitto zimezidi kuongeza shaka hasa katika majibu yake hivi karibuni kupitia mtandao wake wa kijamii wa facebook wakati akifafanua tuhuma zilizoelekezwa kwake na mwanasheria wa CHADEMA, Lissu.
Lissu alidai kuwa Zitto amehongwa magari mawili na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ili amwezeshe kupita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Hata hivyo, katika utetezi wake wa maandishi kupitia ukurasa wake, Zitto aliandika kuwa; "Lissu amenituhumu kuwa nimehongwa magari 2 na mheshimiwa Nimrod Mkono. Mimi ninamiliki gari mbili, Freelander ninayotumia Dar es Salaam na Toyota Carina ninayotumia jimboni."
Majibu ya Zitto yalitofautiana na Mkono ambaye katika taarifa yake alisema kuna magari mawili yanayohusishwa na Zitto na kuyataja kuwa ni Toyota Land Cruiser na Nissan Patrol.
"Sijawahi kumpatia Zitto magari, isipokuwa kuhusu hiyo Land Cruiser, nilitoa msaada wa kuwanusuru Zitto na Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe), kule Tarime kwenye msiba wa marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CHADEMA), kwani walikuwa wakitishiwa kupigwa.
"Walipofika Mwanza, Zitto aliwasiliana na mimi kuhusu ununuzi wa gari hilo na kupitia wakala wangu nilimuuzia," alisema Mkono.
Kuhusu Nissan Patrol, Mkono alisema lilikodishwa kwa Zitto na hadi sasa bado analipa gharama za kulikodisha.
Utata katika suala hili uko kwenye aina za magari zilizotajwa na wanasiasa hawa wawili. Wakati Zitto akitaja kumiliki Freelander na Toyota Carina bila kufafanua kama anayo magari mengine, Mkono anasema amemuuzia Land Cruiser na Nissan Patrol.

Kada CCM anena
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro, David Mgesi, amesema yanayotokea sasa kwa Zitto ni kile alichokuwa akikisema kwa muda mrefu kuhusu mbunge huyo.
Mgesi ambaye kwa sasa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisema wakati akiwa CHADEMA, alishaonya mienendo ya Zitto kwa kuona kwamba ni mtu ambaye anaweza kukisaliti chama wakati wowote.
Kwamba viongozi wa juu wa CHADEMA waliweza kumuamini Zitto na kumuona kuwa ni mtu mwenye busara.
Akitolea mfano, alisema ilikuwa mwaka 2005, Zitto alipewa dhamana ya kutengeneza bajeti ya chama, na baada ya kuwagawia taarifa ya wajumbe wa Kamati Kuu alitaka wazirudishe kwa madai kuwa hawaamini kwani wanaweza kuvujisha siri nje.
"Baada ya kauli ile nilimuomba Mwenyekiti, Freeman Mbowe tujadili kauli hiyo, lakini lilifunikwa na Zitto akatetewa kuwa aliteleza.
"Sasa ukiangalia leo nani msaliti kama sio yeye ambaye amekuwa akipokea fedha kwa muda mrefu kwa lengo la kukivuruga chama?" alihoji.
Akizungumzia hatua ya Zitto kwenda mahakamani, Mgesi alisema sio sahihi na badala yake alitakiwa kwanza kujibu tuhuma zote zilizoelekezwa kwake ili kuwaelewesha Watanzania na kuwahakikishia anachotuhumiwa si sahihi.
Hata hivyo, Mgesi alisema inasikitisha kuona hadi sasa Zitto na CCM wanaotuhumiwa katika kupeana fedha ili kukiharibu CHADEMA wameshindwa kujitokeza kukanusha taarifa hizo.
"Zitto anapaswa ajitokeze akane kama hakupokea fedha hizo zinazodaiwa kupitia benki ya CRDB, vile vile Serikali ya CCM ilipaswa kuthibitisha kama akaunti zilizotajwa kuwa za Idara ya Usalama wa Taifa ni za kweli au hapana," alisema.
Mgesi alisema kitendo cha pande zote kukaa kimya wakati suala tajwa likiendelea kushika kasi, kunaibua maswali mengi kwa wananchi.
Alisema mgogoro huu ni wa muda mrefu na umetengenezwa huku akikumbushia namna ambavyo Waziri Stephen Wasira alikuwa akisisika akisema kuwa CHADEMA itakufa kabla ya mwaka 2015.
Mgesi pia alitaja matukio ya kubambikiwa kesi ya ugaidi kwa Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare na vijana wengine watano kuwa ulikuwa ni mwendelezo wa mkakati wa kukiua chama hicho.
Aliwaonya vingozi wa CCM ambao wamekuwa wakizungumzia mgogoro huo wa CHADEMA majukwaani, akiwataka kuachana na kazi hiyo kwa kuwa sio iliyowaweka madarakani.
"Wakati CCM inapewa dhamana na wananchi kuongoza, katika ahadi zake hakuna mahali wanasema watakuwa wakijadili mgogoro wa CHADEMA," alisema.

ala! kumbe ni tanzania daima!!! hebu nijiendee zangu shamba mie kwani kila aliye hai hata kama awe hana akili sawasawa anaelewa kuwa gazeti hili kwenye sakata kama hili litazusha na kuandika kitu gani!!!! boooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Sina shaka kabisa na msimamo wala maamuzi ya cdm juu ya Zitto na ninaunga mkono hilo kwa 100% kumuondoa ndani ya CDM. Shaka niliyonayo ni moja tu, kwamba taratibu na katiba ya kumchukulia hatua zzk huenda zilikuwapo na ndio zinazotugharimu CDM leo na katika kesi hii, lakini pia nna imani hatimae tutashinda. Tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu....

Toka awali nimekuwa na imani kubwa sana kwa mwenyekiti na katibu wake, na tukio hili linaidhihirisha imani yangu kwao zaidi kwani yale niloyajengea imani sqasa yanathibitika, vivyo hivyo toka awali nilikua na shak sana juu ya mwenendo thabiti wa zzk na leo hili pia linathibitsha kwangu kuwa zzk si mkweli na hapaswi kuungwa mkono asilani.

Mh. Mbowe, ni mtu ambaye kweli amejitoa kihali na mali kumpigania Mtz ambapo inasikitisha kuwa leo wapo ndani yetu wanaombeza..... of course ni kwawaida kwani mara zote unapoishi duniani lazima wawepo wanaokupenda na wanaokuchukia kinyume cha hapo basi lazima una tatizo. Big up Mh. Mbowe, Big up Mh. Slaa, Big up CC CDM na wengine wote wenye mapenzi mema na wanaotaka ukombozi wa kweli CDM

Kwa tahmini yangu ya haraka haraka juu ya utendaji wa viongozi wangu, ni Mkiti na Katibu amabo utendaji wao unazidi wenyeviti na makatibu wote east and central Africa. Chini yao chadema imepata mafanikio makubwa na kuongeza mizizi yake mpaka kwenye grass root level. Hili linajidhihirisha katika namna mbalimbali, 1. idadi ya wabunge toka 5 - zaidi ya 45 hivi sasa, kuongezeka kwa utawala wa CDM mpaka kiwango cha vitongoji, mabadiliko ya haraka na kazi kama vile CDM kuongoza halmashauri ndogo Arumeru muda mfupi tu toka uchaguzi mkuu lakini pia kwa mtidno uleule kuchukua Jimbo la Arumeru magharibi kwa kishindo kikubwa na kutoa upinzani mkali igunga pamoja na hujuma kubwa zilizofanyika huko, lakini moja kati ya mafanikio ya uongozi huu ni hamasa/ari kubwa nadani ya wananchi hivi sasa Tanzania ya kujua na kudai haki zao, jambo ambalo Mkiti wakati wote amekuwa akiliosema kama moja ya vitu ambavyo anavisimamia kuvijenga, ili hata kama CDM itachukua madaraka isiswaburuze wananchi bali iwajibike kwao. Yapo mengi ya kurejea kama mafanikio ya uongozi huu, wana JF wema hebu sasa tupate muda wa kuyaorodhesha yote ili malumbano haya yasiendelee kwa watu kuzomeana tu ila pia yatoe somo na watu wauone ukweli, nina imani kuwa ukweli huongea vizuri zaidi kuliko matusi au kuzomeana?????, nilichogundua hapa ni kwamba watu hawasomi hata magazeti kujua dhana fulani fulani, ni muhimu sana sasa tuusome waraka ule wa akina zitto wa kutaka mabadiliko ya uongozi na kuu critic kwa hoja bila hivyo tutapoteza muda na kutoka bila elimu wala kupanuana mawazo.

Kuhusu ZZK kwa kweli nimekuwa mfuasi wake bali wa mashaka (Urafiki wa mashaka) nimempenda kwa hoja zake mbali mbali japo mara zote nimekuwa nikikatishwa tamaa na namna ambavyo amekuwa akikosa udhati wa kuonyesha nia halisi ya kushughulikia yale anayodai kuyasimamia, nilimpenda sana kipindi alipotolewa nje ya bunge na kufanya Operesheni sangara, labdas hili ndilo pekee lililonikosha zaidi juu yake. Vinginevyo anaonekana zaidi katika mazingira yenye mashaka mashaka na kwa haraka haraka namuona Zitto Akiwasiliana sana na Mkurugenzi TISS 2010 katika kipindi kigumu CDM ikichakachuliwa juu ya matokeo ya urais/ubunge wakati ambapo Dr Slaa akilalamikia matokeo ya urais; Namuona zzk akitweet haraka sana kwa urahisi wakati wa matokeo kule Igunga akikiri CDM kushindwa eti kwa sababu chama hakijajengeka vijijini (Hata kwa matokeo yale yaliyochakachuliwa usemi wa zzk hauna ukweli na hasa ukizingatia ndio kwa mara ya kwanza CDM ilisimamisha mgombea), namuona zzk akifanya bidii kuahakikisha Pinda, Dewji, Mkono n.k akipambana kukihujumu CDM na wagombea wake ili CCM na maswahiba wake wapite bila kupingwa, namuona zzk akigoma kutoka nje ya Bunge rais alipokwenda kulihutubia eti kwa vile amemjengea barabara nk (Hapa uanaona ubinafsi wa dhahiri wa mbunge ambae leo nataka zugukia sehemu zote tanzania ati Mzalendo), namuona zzk ikulu akigonga glasi na rais kumpongeza kwa baraza jipya la mawaziri wakati M/kiti wake yupo Arusha akilaani kitendo cha katiba kuvunjwa kwa kuchguliwa baadhi ya mawaziri, Mh Mwinyi kushika wizara ambazo si za muungano, namuona zzk akiwa mabli na viongozi wenake nyakati zote - Akijitenga, Namuona zzk akiwa mbele kwenye ajenda ya kutaka uongozi wa juu kwa udi na uvumba bila staha- Urais, uenyekiti, uongozi wa upinzani bungeni (taamaa ya madaraka; namuona zzk akienda Anticlockwise wakati wenzake wakienda clockwise nk. Nabaki mwenye mashaka makubwa juu ya uzalendo na ukweli wake na sasa namuona ni msalitit anaepaswa kufukuzwa chama tu.

Ukweli hapa kulingana na mtazamo wangu ni kuwa zzk kwa kutofautina na uongozi wote amepoteza sifa na hawezi kubaki cdm, this does not need rocket sayansi kulitambua, ni wazi kuwa atatapata wana cdm wanaomuunga mkono lakini wale ambao hwapo uongozini kumbe itakuwa ngumu kwake kuongoza cdm, haiwezekani wewe peke zako ukaongoza chama katika mazingira ambayo cdm imefikia, hilo linawezekana UDP, TLP, UDP etc etc.

Ukweli ni kwamba M/kiti na katibu CDM wamekuwa mwiba kwa CCM kwani wamevaaa sura ya serikali mbadala inyojihidhirisha ndani ya uongozi thabiti wa kutohongeka na kujitolea kwa hali na mali, lakini pia muamko na ari kubwa ya watanzania juu ya CDM uliotokana na uongozi wao. Wote tutakiri jinsi ambavyo watanzania wamekuwa mbele kuichangia cdm hata kwa mpesa mpaka hujuma ya kukata kodi ya mabilioni toka CDM m-pesa ilipotungwa. Mh. Mbowe hakuzivaa combat kwa bahati mbaya au kifasheni zaidi kama ambavyo inaonekana sasa bali vazi lile liliendana fika na mwandani wake, ukweli, nia, thirika na utendaji wake. Niliwahi safiri na dada mmoja ambae aliwahi fanya kazi na mbowe, akanithibitishia hilo, kwamba Mbowe ni mtu ambae akishaamua kufanya kitu akaanza basi ni mpaka akimalize/akikamilishe, akanimabia kwamba wakati akijenga Bilicanas alikesha usiku na mchana site aliondoka asubuhi tu tena kwa muda mfupi kwenda kwa Bfast kubadili nguo na kurudi site kwa mkesha mwingiine, alipokuta mkewe anadunduliza ili ajenge nyumba yao kisiri, aliingilia kati plan hiyo kuanza na kujenga nyumba nadni ya mwezi mmoja nk, hii ilinikumbusha muda wote hata kabla chadema haijafika hapa Mbowe akizunguka kwa kampeni zake za urais akitumia Helikopta kuhutubia vijijini pamoja na kukijenga chama akiibua hamasa ya mabadiliko.
Hakika sura yake na Dr. Slaa katika siasa za tz inatisha ccm ndio maana wanatafuta mamluki ili kile kilichotokea NCCR kijirudie....Tulianza na mungu tutamaliza na mungu.

Wana JF, mkakati wa zzk, kitila na Mwigamba haupaswi kuungwa mkono kwa namna yeyote sio tu na CDM au wanachama wake bali wanamageuzi wote Tz. Ni kweli katka chama au jamii kwa ujumla hakukosekani makundi lakini makundi hayo yasiwe ya mafungate au kimtandao bali ya hoja na yenye afya kwa chama kwa maana watu watafungama na hoja sio mtu fulani. Hili ndilo linalowasumbua ccm hata leo, ndio maana wanashindwa kuwajibishana, kujivua magamba nk. Raisi Kikwete alipokutana na makatibu wa Wilaya/Mikoa dodoma aliongea kama analia tu hana meno kwa ajili ya mtandao ndani ya ccm akaishia kuwalalamimikia kwamba mtindo wao wa kuchukua posho za simu kila mwezi wa laki mbili kila mwezi utakiua chama, haya ndio matokeo ya Mitandao. Katika mtindo wa mitandao watu hawatahoji CDM imesema nini bali nani kasema ndani ya cdm, kiwe cha ujinga au busara ili mradi kasema zzk sawaaaaa!!!! akasema mbowe holaaaaaaa!!!!!!!! Slaa mjinga!!!!!!!!!!!!!, tusifike hukoooo hakuna maslahi ya taifa hili.

Mh. Mbowe & Slaa, zzk na waheshimiwa wote wenye nia nzuri, ukiona unapingana na wengi ndani ya CDM its time to quit, ndio taratibu za siasa!!!! Mwl. Nyerere aliwahi kumshangaa Mh. Kawawa kwamba anadai hwezi toka ccm!!! yeye akaweka bayana kabisa kuwa ccm sio babake wala mama kwamba huwezi mbadili na kwamba kwamba ccm haitatekeleza kile anachoamini ataondoka....!!! Lyatonga Mrema laifanya hivyo mara kadhaa na wakati wote wafuasi wake walimfuata. Mh zzk ni wazi kwangu wewe unapingana na wenzako na kwa hali hii nakushauri utoke na wafuasi wako watakufuata tuu...... Vinginevyo hisia za watu kwamba --------- na ccm zitaongezeka kwani itakuwa kama vile kukimbia kazi ambayo umeshalipwa kumbe uanang'ang'ania ili kuikamilisha...... Tazama Damu za watu zimeshamwagika kuipigania CDM na ukombozi wa taifa hili sehemu nyingi, kkwa mzalendo halisi angekubali kupoteza maslahi yake ili chama hiki kifike mahali kutoa heshima ya damu iliyomwagika, na mungu afurahie hilo, usikatize mapango wa mungu laana itakufuata kwani damu ya wanyonge hawa bado inalia juu ya taifa hili

Aluta Continua CDM

Mungu ibariki CDM... Mungu ibariki TZ

Tulianza na mungu.... Tutamaliza na Mungu, Amen.

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameuweka njia panda uanachama wake ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kukubali pingamizi lake la kuizuia Kamati Kuu (CC) ya chama hicho isimjadili hadi kesi yake ya msingi itakapokuwa imesikilizwa. Kwa uamuzi huo, Zitto sasa atabaki kuwa mwanachama kwa nguvu ya mahakama hadi hapo itakapoamriwa vinginevyo.
Sasa Zitto ataungana na wabunge wenzake wawili, David Kafulila wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) na Hamad Rashid Mohammed wa Wawi (CUF) ambao pia ubunge wao upo kwa nguvu ya mahakama.
Zitto alifungua kesi mahakamani hapo siku moja kabla ya CC kuanza vikao vyake ambavyo vilikuwa vijadili utetezi wa tuhuma zake za kuendesha mkakati wa siri wa kusaliti chama, akiomba mahakama izuie suala la uanachama wake lisijadiliwe hadi kesi yake isikilizwe.
Akitoa uamuzi wa awali, Jaji John Utamwa, alisema kuwa mahakama imeridhia ombi la Zitto kuwa CHADEMA au chombo chochote kisijadili uanachama wake hadi kesi ya msingi itakapomalizika.
Akisoma maelezo ya awali, Utamwa alisema kuwa wakili Peter Kibatala anayewakilisha Bodi ya Udhamini ya CHADEMA na Katibu Mkuu ambao ndio washtakiwa, alikula kiapo kwa niaba yao jambo ambalo si sahihi.
Utamwa alisema kuwa kwa mazingira ya kesi kuhusisha Bodi ya Udhamini ya CHADEMA na Katibu Mkuu, ilikuwa si sahihi kwa wakili kula kiapo kwa niaba yao.
Wakizungumza baada ya kutoka mahakamani, mawakili wa upande wa CHADEMA, Kibatala na Tundu Lissu walisema kuwa kuhusiana na hati ya kiapo, ipo sheria inayoruhusu wakili kula kiapo kwa ajili ya mteja wake.
Walisema kuwa wanaheshimu uamuzi wa mahakama japo hawajaridhika, na hivyo watachukua hatua za ziada.
Wakili wa Zitto, Albert Msando, aliomba uamuzi wa mahakama uheshimike kwani ni hatua za haki kutendeka na mteja wake kupata nafasi ya kusikilizwa.
Katika kesi ya msingi, Zitto anaiomba mahakama ikizuie chama hicho kumchukulia hatua, ambapo kesi hiyo inatarajiwa kutajwa Februari 13, mwaka huu.
Zitto aliwasilisha maombi dhidi ya Baraza la Wadhamini la CHADEMA pamoja na Katibu Mkuu wa chama, Dk. Willibrod Slaa, akiiomba mahakama itoe zuio la muda kwa Kamati Kuu kutojadili uanachama wake.
Katika kesi hiyo, Zitto anaiomba mahakama iizuie Kamati Kuu kujadili uanachama wake hadi rufaa yake itakaposikilizwa na Baraza Kuu la chama na kuomba mahakama imwamuru Dk. Slaa ampe nakala za taarifa za vikao vilivyomvua uongozi ili akate rufaa.

Hali ilivyokuwa
Zitto alipokelewa na wanachama wa CHADEMA kwa kuzomewa kuanzia hoteli ya Hyatt Kempisky hadi katika lango kuu la kuingia Mahakama Kuu.
Sauti hizo zilisikika zikimba na kuzomea; “Zitto kibaraka wa CCM; CCM huyo…”
Zitto ambaye aliongozana na walinzi wanne wenye miili mikubwa (mabaunsa), alikuwa ameinamisha sura chini na kutembea haraka kuingia mahakamani.
Hata hivyo, kabla ya kuingia lango kuu la mahakama, alipepesuka na kuvuka kiatu kimoja cha mguu wa kushoto.
Baada ya kadhia hiyo ya nje, alikutana na wanachama wengine wa CHADEMA ndani ya mahakama, ambao walimzomea hadi kwenye mlango wa vyumba vya mahakama.
Nako nje, mamluki wanaodaiwa kukodiwa na Zitto tangu kuanza kwa kesi hiyo, jana hali ilikuwa ni tofauti kutokana na kufika kwa uchache huku wakizomewa na wanachama wa CHADEMA.
Tanzania Daima ilidokezwa kuwa walinzi waliokuwa wanamlinda Zitto, walifahamika kwa jina moja moja la Tino, Evans na Ziggy.
Ndani ya mahakama, kabla ya kesi kuanza baadhi ya wanachama wa CHADEMA walimtambua mtu mmoja aliyevaa suti nyeusi na kuanza kumshambulia kwa maneno kuwa ni kibaraka wa Ridhiwani Kikwete hadi mtu huyo alipojitetea akidai ni wakili.

Vituko vya Zitto kisiasa
Zitto ambaye anahaha kila kona ili asivuliwe uanachama wa CHADEMA, amekuwa na mtiririko wa matukio mengi ya kauli ambazo zimechangia wananchi kumtilia shaka mwenendo wake ndani ya chama.
Mwaka 2010 wakati nchi ikielekea uchaguzi mkuu, Zitto alitishia kutowania tena ubunge katika jimbo lake la Kigoma Kaskazini kwa madai kuwa ameombwa kugombea katika majimbo ya Kigoma Mjini, Kinondoni, Geita na Kahama.
Lakini dakika za mwishoni kabisa, Zitto alirudi kugombea jimboni kwake akidai ameshauriwa na wazee.
Baada ya uchaguzi mkuu, mwanasiasa huyo alitangaza kutogombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2015, akidai kuwa ataachana na siasa ili akafanye kazi ya kitaaluma chuo kikuu.
Muda mfupi baadaye, akakaririwa na vyombo vya habari kwamba anaandamwa ndani ya chama, kiasi cha kufikia hatua ya kutembea na barua ya kutaka kujiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.
Machi mwaka jana, mbunge huyo alitangaza nia ya kuutaka urais wa Tanzania, lakini baada ya kuibuka mjadala mkubwa ndani na nje ya chama chake akielezwa kuwa umri wake hajakidhi matakwa kikatiba, Septemba mwaka huo, alitengua nia hiyo.
Akiwa katika ziara ya kichama mkoani Tabora Novemba mwaka jana, Zitto pia alitengua kauli yake ya kutogombea ubunge mwaka 2015 akisema anaitafakari upya baada ya kuona kero nyingi zinazowakabili wananchi.
Kauli tatanishi za Zitto zimezidi kuongeza shaka hasa katika majibu yake hivi karibuni kupitia mtandao wake wa kijamii wa facebook wakati akifafanua tuhuma zilizoelekezwa kwake na mwanasheria wa CHADEMA, Lissu.
Lissu alidai kuwa Zitto amehongwa magari mawili na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ili amwezeshe kupita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Hata hivyo, katika utetezi wake wa maandishi kupitia ukurasa wake, Zitto aliandika kuwa; “Lissu amenituhumu kuwa nimehongwa magari 2 na mheshimiwa Nimrod Mkono. Mimi ninamiliki gari mbili, Freelander ninayotumia Dar es Salaam na Toyota Carina ninayotumia jimboni.”
Majibu ya Zitto yalitofautiana na Mkono ambaye katika taarifa yake alisema kuna magari mawili yanayohusishwa na Zitto na kuyataja kuwa ni Toyota Land Cruiser na Nissan Patrol.
“Sijawahi kumpatia Zitto magari, isipokuwa kuhusu hiyo Land Cruiser, nilitoa msaada wa kuwanusuru Zitto na Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe), kule Tarime kwenye msiba wa marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CHADEMA), kwani walikuwa wakitishiwa kupigwa.
“Walipofika Mwanza, Zitto aliwasiliana na mimi kuhusu ununuzi wa gari hilo na kupitia wakala wangu nilimuuzia,” alisema Mkono.
Kuhusu Nissan Patrol, Mkono alisema lilikodishwa kwa Zitto na hadi sasa bado analipa gharama za kulikodisha.
Utata katika suala hili uko kwenye aina za magari zilizotajwa na wanasiasa hawa wawili. Wakati Zitto akitaja kumiliki Freelander na Toyota Carina bila kufafanua kama anayo magari mengine, Mkono anasema amemuuzia Land Cruiser na Nissan Patrol.

Kada CCM anena
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro, David Mgesi, amesema yanayotokea sasa kwa Zitto ni kile alichokuwa akikisema kwa muda mrefu kuhusu mbunge huyo.
Mgesi ambaye kwa sasa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisema wakati akiwa CHADEMA, alishaonya mienendo ya Zitto kwa kuona kwamba ni mtu ambaye anaweza kukisaliti chama wakati wowote.
Kwamba viongozi wa juu wa CHADEMA waliweza kumuamini Zitto na kumuona kuwa ni mtu mwenye busara.
Akitolea mfano, alisema ilikuwa mwaka 2005, Zitto alipewa dhamana ya kutengeneza bajeti ya chama, na baada ya kuwagawia taarifa ya wajumbe wa Kamati Kuu alitaka wazirudishe kwa madai kuwa hawaamini kwani wanaweza kuvujisha siri nje.
“Baada ya kauli ile nilimuomba Mwenyekiti, Freeman Mbowe tujadili kauli hiyo, lakini lilifunikwa na Zitto akatetewa kuwa aliteleza.
“Sasa ukiangalia leo nani msaliti kama sio yeye ambaye amekuwa akipokea fedha kwa muda mrefu kwa lengo la kukivuruga chama?” alihoji.
Akizungumzia hatua ya Zitto kwenda mahakamani, Mgesi alisema sio sahihi na badala yake alitakiwa kwanza kujibu tuhuma zote zilizoelekezwa kwake ili kuwaelewesha Watanzania na kuwahakikishia anachotuhumiwa si sahihi.
Hata hivyo, Mgesi alisema inasikitisha kuona hadi sasa Zitto na CCM wanaotuhumiwa katika kupeana fedha ili kukiharibu CHADEMA wameshindwa kujitokeza kukanusha taarifa hizo.
“Zitto anapaswa ajitokeze akane kama hakupokea fedha hizo zinazodaiwa kupitia benki ya CRDB, vile vile Serikali ya CCM ilipaswa kuthibitisha kama akaunti zilizotajwa kuwa za Idara ya Usalama wa Taifa ni za kweli au hapana,” alisema.
Mgesi alisema kitendo cha pande zote kukaa kimya wakati suala tajwa likiendelea kushika kasi, kunaibua maswali mengi kwa wananchi.
Alisema mgogoro huu ni wa muda mrefu na umetengenezwa huku akikumbushia namna ambavyo Waziri Stephen Wasira alikuwa akisisika akisema kuwa CHADEMA itakufa kabla ya mwaka 2015.
Mgesi pia alitaja matukio ya kubambikiwa kesi ya ugaidi kwa Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare na vijana wengine watano kuwa ulikuwa ni mwendelezo wa mkakati wa kukiua chama hicho.
Aliwaonya vingozi wa CCM ambao wamekuwa wakizungumzia mgogoro huo wa CHADEMA majukwaani, akiwataka kuachana na kazi hiyo kwa kuwa sio iliyowaweka madarakani.
“Wakati CCM inapewa dhamana na wananchi kuongoza, katika ahadi zake hakuna mahali wanasema watakuwa wakijadili mgogoro wa CHADEMA,” alisema.
 
Ukiona mtu anautafuta na kuupigania uongozi kwa nguvu zake zote ni wa kumuogopa kama ukoma!
 
Daaaaaaah! Ya kweli haya jamani au ndo propaganda? Kama ni kweli basi Zitto kageuka ibilisi ndani ya chama.
When people are greedy, all natures are insufficient.
 
Hata siku moja gazet ka mbowe haliwez kumsifia Zitto. Na mtahangaika sana tu. Polen team ms.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom