Zitto Kabwe ndani ya Makutano Show: Adai Urais, mabilioni ya Uswisi vinammaliza

TinyMonster

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
248
154
Wadau

Leo Zitto atahojiwa Magic FM kwenye kipindi cha Fina Mango kuanzia saa kumi na moja jioni, kwa mujibu wa tweets za Fina Mwenyewe. Watakaoweza sikiliza kupitia 92.9 Dar, 93.3 Dodoma, 98.6 Arusha, na 101.7 Mwanza na Tanga na online kupitia http://www.ustream.tv/channel/makutanoshow

========

Video ya alichokisema:


Kwa ufupi:

Zitto anasema mifano ya Wangwe na Kabour kuwa walifukuzwa na chama ni hadaa tu ya viongozi wa chadema,na ni kichekesho kwa Dr.Slaa kuufunga mjadala wakati siku 14 hazijaisha...anasema hii ni ajabu sana kwa kiongozi wa nafasi yake kuufunga mjadala wakati hukumu haijatolewa.

Anasema mpaka sasa hajapewa barua,so ataanza kuhesabu hizo siku mara atakapopata hiyo barua yenye mashtaka yake.Wanaompinga ni wale waliokuja juzijuzi ndani ya chama,yeye amekulia na kulelewa ndani ya chama.

Mpaka leo anasikitika kuwa barua aliyoandika kwa Dr.Slaa kuhusu kuthibitisha ule waraka hajajibiwa,wakati yule Dada mjerumani amejibiwa kwa haraka.Anasema polisi amepeleka mashtaka kuwa viongozi wa CHADEMA wa kitaifa wamehusika kumchafua akiwemo Dr.Slaa...na hata alipojitetea ndani ya kamati kuu hakusikilizwa,ila ana ushahidi kuwa Dr.Slaa amehusika kumchafua mitandaoni.
Hajui kwanini amesimamishwa..maana huo waraka anaotuhumiwa nao haujui na hakuwahi kuujua...he is just a beneficiar!!

Tuhuma anazozijua yeye na alizijibu kwa hoja ndani ya kamati kuu ni hizi:
1) kudhalilisha chama kwa kuibua ukaguzi.
2) Kuwadhalilisha viongozi
3) Kuyauza majimbo ya Chadema kwa CCM.

Tuhuma zoote alijibu na wakakosa pa kumkamatia, lkn kwa vile walikusudia kumkomoa kwa kumsimamisha basi wakamuingiza ktk huo waraka, yeye anajua ndio MM, lkn hakushiriki kuuandaa.

Yeye Zitto kama mwanasiasa mzoefu anajua kuwa anaandamwa kwa sbb ameshinikiza ukaguzi wa C.A.G

Kuvuliwa uongozi kuna madhala kwake,fursa ya kusukuma ajenda inakosekana...na hasa ajenda binafsi ambazo baadae zinakibeba chama...kwa mfano ajenda ya Buzwagi ilikuwa yake binafsi lkn ilikibeba chama,imepunguza nguvu ya ajenda ya utoroshaji wa fedha,ajenda hii imefanya aitwe sehemu mbalimbali kama mtaalamu(case study) wa kupinga wizi huu,hali hii ya kusimamishwa imerudisha nguvu zake Kwani amealikwa Lusaka na Argentina...huko Argentina ameitwa kuhamasisha wabunge wa Latin Amerika nao wabebe ajenda ya kupinga utoroshwaji wa pesa nje ya nchi zao,hivyo misukosuko hii ndani ya chama inarudisha nyuma harakati, dhamira na ajenda zake kimataifa za kupinga utoroshaji huu wa pesa.

Kusimamishwa kwake kumesababisha habari za kitaifa kuwa kimya na kubaki kumzungumzia Zitto Zitto....wakati kuna swala la gesi na upandishwaji wa bei ya umeme,watu wameyakalia kimya wamebaki kumzungumzia yeye.

Kufukuzwa ubunge kwake sio mwisho wa maisha...atakachokosa ni platform tu ya kibunge kusukuma harakati na maendeleo, lakini uzoefu na elimu yake vitabakia, na yupo tayari kufukuzwa na ikitokea basi atashika chaki mana ndio kazi anayoipenda na kuiweza.

Amekataa kujibu swali la kama akivuliwa uongozi yupo tayari kuhama?? ....Anaendelea kesema hakujiunga na CHADEMA ili kuwa kiongozi, kwake uongozi ni dhamana tu, alijiunga ili kuleta mabadiliko ktk nchi baada ya yeye na wengine wa Kigoma kuona kama wako "marginalized",na hii ndio Spirit ya watu wa Kigoma na ndio maana hadi sasa ndio mkoa wenye wabunge wa upinzani wengi....anataka spirit hiyo ienee sehemu zote za Tanzania.

POSHO:
Posho ya kujikimu, posho ya kukaa na posho kikao...haya ameyaelezea sana,karudia sana.Ilikuwa ni ajenda ya chama,chama kilikuwa na ajenda mbili...hili la posho na la gari la KUB,Yeye akachukua ajenda ya posho na MBOWE akabeba la gari la KUB.....mambo mengine ni misamaha kodi, ikiwa na ya uagizaji bure wa magari nje ya nchi...na yeye kama waziri kivuri hachukui posho wala msamaha wa kodi, lkn wanaomshangaa ni sbb hawaishi yale wanayoyasema...yeye anaishi kile anachosema.

Wanaomtuhumu ni porojo tu, hawana ushahidi zaidi ya uzushi,wanafikiri kidogo..."they have small minds".... Kwake mtu mwenye mawazo tofauti na yeye ktk siasa si msaliti, bali ni uhuru wa kufikiri. Hana chuki na mtu, yeye hulipa wema kwa ubaya...hivyo hatalipa lolote kwa wanaomsakama!!! Moi alimfukuza Kibaki kazi hadharani,lkn badaye akawa Rais...kwake hajali chama,yupo tayari kwa lolote ili mradi nchi isonge mbele.

Mwisho wa mahojiano, Finna Mango anagundua Zitto ameongea kwa hisia mpaka kulegwa na machozi...anapumzisha kipindi na wanapata fundo la pumzi.

Mwisho anasindikizwa na Kibao cha Bob Marley cha Buffalo Soldier

Magazetini:
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema tuhuma alizosomewa na uongozi wa Chadema katika kikao cha Kamati Kuu sizo zilizoelezwa na chama hicho mbele ya waandishi wa habari na viongozi wa chama hicho.

Aidha, amesema kuwa vita aliyopo siyo kati ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi, akitaja magenge ya watu wanaotaka urais 2015 na walioficha fedha nje ya nchi walioungana wakiona tatizo lao ni yeye hivyo kutaka kumwondoa bungeni.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili kwa njia ya simu, Zitto alisema kuwa hadi sasa bado hajapokea tuhuma 11 anazokabiliwa nazo, hivyo hajui makosa hayo na bado anasubiri akabidhiwe kwa maandishi.

Ana ugomvi gani na viongozi wenzake?

Alipotakiwa kueleza iwapo ana ugomvi na watu ndani ya Chadema, Zitto alisema kuwa huenda mambo hayo yanatokea kwa sababu mahasimu wake wa kisiasa wa ndani na nje wameamua kuungana na kupambana naye ili kumdhoofisha kisiasa kwa masilahi yao.

"Matatizo yaliyopo ni mafanikio yangu, …. nadhani hii siyo vita kati ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi, pengine magenge ya watu wanaotaka urais na wale walioficha fedha zao nje wamekaa pamoja wanaona tatizo lao ni Zitto… wanajua siwezi kusemea nje maana sina kinga…, hivyo wanataka kuniondoa bungeni…" alisema.

Aliongeza kuwa kwenye siasa kinachohitajika ni kusimamia misingi, jambo alilosema binafsi amekuwa akilifanya katika kipindi chake chote cha kisiasa.

Zitto alisema kuwa ni vyema wananchi wakawapima wabunge wao kwa kazi wanazozifanya bungeni akibainisha kuwa kati ya mwaka 2011 hadi 2013, yeye amewasilisha hoja nyingi nzuri zilizo na mashiko ikilinganishwa na wabunge wenzake wanaomtuhumu kutumiwa na CCM.

"Je, mbunge anayetumika na Chama Cha Mapinduzi anaweza kupeleka hoja ya kumng'oa Waziri Mkuu na kumshinikiza Rais mpaka akasimamisha kazi mawaziri wanane? Je, mbunge anayetumika anaweza kushikia bango watu wanaotorosha fedha nje ya nchi?" alihoji Zitto.


Tuhuma za usaliti

"Sizijui hizo tuhuma 11 kwa sababu nilichoelezwa kwenye kikao cha Kamati Kuu sicho kilichoelezwa na chama kwenye mkutano wake na waandishi wa habari… hivyo sijui kabisa hizo tuhuma zangu ni zipi mpaka sasa," alisema.

Alisema kuwa kwenye Kamati Kuu alilaumiwa kwa masuala matatu. Akizitaja: "Nililaumiwa kuwa sifanyi kazi za chama, la pili kuwa nimemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali akague vyama kutokana na kuwa na nia mbaya na chama hicho. Tuhuma ya tatu ni ile ya kukataa kupokea posho bungeni ambapo nadaiwa kulenga kuwadhalilisha wabunge wenzangu."

Zitto alisema kuwa baada ya kuzijibu tuhuma hizo mbele ya wajumbe wa kikao cha Kamati Kuu na katika mkutano wake na waandishi wa habari, akashangazwa na tuhuma alizoziita mpya kuwa anatuhumiwa kutokana na waraka ambao yeye hahusiki nao, licha ya kutajwa kuwa mfaidika tu.

"Mimi sihusiki na waraka wowote, huo unaodaiwa kusambazwa kwenye mitandao wala mwingine wowote… ni wajibu wa chama kueleza mimi nahusikaje na waraka ule," alisema.

Madai ya Mwanasheria wa Chadema kuvunja Katiba

Zitto alisema jambo linalompa shaka kuwa huenda suala lake limelenga kumdhoofisha kisiasa ni kitendo cha mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu kuamua kuvunja katiba ya chama hicho kwa makusudi.

Alifafanua: "Katiba ya chama (Chadema), inasema kwamba kiongozi wa ngazi fulani ataondolewa kwenye uongozi na ngazi iliyomchagua. Mimi nilichaguliwa na Baraza Kuu la Chama, siyo Kamati Kuu… sasa iweje Kamati Kuu iniondoe?"

Alisema kimsingi Kamati Kuu haina mamlaka ya kumvua uongozi bali ina mamlaka ya kuweza kumsimamisha uongozi kusubiri kikao kilichomchagua kufanya uamuzi wa kumwondoa katika uongozi au kumrejesha.

Zitto alidai kuwa Lissu alisema uongo kuwa hata Dk Wallid Kabourou aliondolewa uongozi na Kamati Kuu na kwamba ukweli ni kuwa Dk Kabourou alijiondoa mwenyewe na kuhamia CCM na kwamba hata Chacha Wangwe hakuondolewa na Kamati Kuu isipokuwa alisimamishwa na kusubiri Baraza Kuu ambapo kabla ya Baraza Kuu kuketi alifikwa na mauti.

Kwa nini hapokei posho?

Alipoulizwa ni kwa nini yeye hapokei posho za wabunge alisema suala la posho siyo lake binafsi bali ni suala la imani na msimamo wa chama hicho, ambao waliuweka wakati wa kampeni na ni miongoni mwa mambo waliyowaahidi wapigakura wakati wa kampeni, hivyo yeye anachofanya ni kutimiza tu ahadi.

Aliongeza kuwa wakati wa kampeni za mwaka 2010, walikuwa wakiwaeleza wananchi kuwa wabunge wanapokea fedha nyingi na kuwa wakichaguliwa watapunguza posho hizo na kwamba Chadema ilipofanikiwa kushinda chama kilikubaliana watekeleze ahadi zile.

Alidokeza kwamba walikubaliana kutekeleza kwa kuanza na mambo mawili moja likiwa kukataa kuchukua posho za vikao, maana ni kinyume cha utaratibu na suala la pili ni kuacha kutumia shangingi la Serikali ambalo linatumika na Kiongozi wa Upinzani Bungeni.

Alisema katika kutekeleza uamuzi huo Mbowe alitangaza hatua ya kurudisha shangingi na yeye (Zitto) kama Waziri Kivuli wa Fedha akatangaza kuacha kupokea posho.


"Tulikubaliana wote tutekeleze hayo… lakini wenzangu wakashindwa kuyatekeleza, na mwenzangu akalirudia gari na analitumia mpaka sasa… kwangu mimi mafunzo niliyofundishwa kisiasa ni kwamba unayoyasema, yatekeleze, wenzangu hiyo ‘principal' ya kutekeleza wanayoyasema hawana," alisema.

Kuhusu tuhuma kuwa anakataa posho lakini anapokea rushwa kubwa kubwa, Zitto alisema iwapo kuna mtu aliye na ushahidi na hilo aupeleke vyombo vya dola, wamshtaki na achunguzwe kisha achukuliwe hatua.

Alisema mbali na posho, wabunge wanaongoza kwa kupewa misamaha ya kodi mbalimbali ukiwemo msamaha wa kodi ya uingizaji wa magari.

"Hii nayo tulikubaliana kuikataa… na katika kulitekeleza hili, nilipoagiza gari langu nilikataa msamaha nikalipa kodi hadi nilipoitwa na Kamishna wa Kodi na kuulizwa iweje nilipe kodi wakati nina msamaha wa kodi nikamjibu kuwa ni suala la ‘principal' tu," alisema.

Ruzuku

Kuhusu suala la ukaguzi wa ruzuku ya chama, Zitto alisema yeye anapokuwa Mwenyekiti wa PAC anasimamia taifa, hasimamii chama, hivyo kwa nafasi yake ya PAC na kamati nzima waliona siyo halali vyama vya siasa kukaa bila kukaguliwa.

Alisema alipigania suala hilo tangu mwaka 2011 alipomwandikia barua Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali kumuuliza kwa nini hakagui hesabu za vyama vya siasa wakati sheria inataka vikaguliwe.

Je, ana shaka kuhusu matumizi ya ruzuku ndani ya Chadema?

"Nitaweza kusema jambo hilo kwa uhakika baada ya ukaguzi kufanyika. Mpaka sasa hakuna chama ambacho kimekaguliwa, hivyo inawezekana matumizi mabaya ya ruzuku yako CCM, CUF, NCCR-Mageuzi, Chadema au yako katika vyama vyote…

"Haiwezekani kila mwaka sisi (wabunge) tunaipigia kelele Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, haiwezekani kila mwaka tunaipigia kelele Bodi ya Korosho, halafu vyama vya siasa ambavyo vinapokea zaidi ya Sh29 bilioni kila mwaka, tukisema, tuonekane wasaliti," alisema Zitto.

Chadema yajibu

Alipotakiwa kuzungumzia madai hayo ya Zitto, jana Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa alisema kuwa hawezi kulumbana na mtu kwa njia ya magazeti na kwamba kazi yake yeye ni kufafanua Katiba, kanuni na miongozo ya Chadema pindi inapohitajika.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Last edited by a moderator:
Fina namwminia, hacheki na kima! Atamuhoji maswali yenye kueleweka.
 
NAMSHAURI ZITO KWA KIPINDI HIKI KABLA YA UAMUZI WA CC BAADA YA SIKU ALIZOPEWA KWISHA ajiepushe na matamko na vyombo vya habari kwa ujumla ili kuonyesha ana nidhamu na amedhamilia kwa ukweli kuendelea kuwa CHADEMA

Bilioni mbili sio mchezo, zimemtoa ufahamu ataropoka tu! Harafu ataendelea kuchimba mkwala akisea kuwa "yeye atakuwa wa mwisho kujitoa CHADEMA"
 
NAMSHAURI ZITO KWA KIPINDI HIKI KABLA YA UAMUZI WA CC BAADA YA SIKU ALIZOPEWA KWISHA ajiepushe na matamko na vyombo vya habari kwa ujumla ili kuonyesha ana nidhamu na amedhamilia kwa ukweli kuendelea kuwa CHADEMA

Zitto huwa anataka kushindana na Mbowe muda wote .Kisa kasoma sijui Tanzania ina wasomi wangapi .Wasomi they will deliever na siyo kiwa arrogant kama Muhongo .Na wote wamekutana wapuuzi na Muhongo ndiyo maana Muhongo calls him names .Zitto unaitumikia CCM ina amdhara kumbuka watu walio kuamini ndiyo watakao kumaliza zaidi .Hapa Kigoma mambo yako mengi kijana wangu tunayajua lakini tunakuvumilia kama kionozi .Nje unasema unatuunganisha sirini unatugawa .
 
Wadau

Leo Zitto atahojiwa Magic FM kwenye kipindi cha Fina Mango kuanzia saa kumi na moja jioni, kwa mujibu wa tweets za Fina Mwenyewe. Watakaoweza sikiliza kupitia 92.9 Dar, 93.3 Dodoma, 98.6 Arusha, na 101.7 Mwanza na Tanga na online kupitia MakutanoShow on USTREAM: Makutano na Fina Mango. Radio

Ningeshauri ndugu mpendwa Zitto akaachana na Media kwa sasa .Maana zinakuchanganisha mno na Chadema yako mkuu .
 
1461376_638256166215624_726567862_n.jpg
 
Nadhani kama Chadema hawana cha kuhofia, Wasimshambulie Zitto kwa kutumia uhuru wake wa kuzungumza, bali wamtuhumu kwa kile atakachokizungumza. By the way atahojiwa saa ngapi?
 
kusikia tu kwamba kamanda atahojiwa munaanza kujiharishia hovyo hovyo,mkavae nepi basi kama hamuwezi kuzuia uharo,au mumeharibiwa sana kama lema?
 
Zitto huwa anataka kushindana na Mbowe muda wote .Kisa kasoma sijui Tanzania ina wasomi wangapi .Wasomi they will deliever na siyo kiwa arrogant kama Muhongo .Na wote wamekutana wapuuzi na Muhongo ndiyo maana Muhongo calls him names .Zitto unaitumikia CCM ina amdhara kumbuka watu walio kuamini ndiyo watakao kumaliza zaidi .Hapa Kigoma mambo yako mengi kijana wangu tunayajua lakini tunakuvumilia kama kionozi .Nje unasema unatuunganisha sirini unatugawa .
Mwakeye! Mh unaweza ukatumegea mambo ya Zitto toka huko japo robo tu?
 
Nadhani kama Chadema hawana cha kuhofia, Wasimshambulie Zitto kwa kutumia uhuru wake wa kuzungumza, bali wamtuhumu kwa kile atakachokizungumza. By the way atahojiwa saa ngapi?

Yani wewe ni Gamba la mavi, umetoka kujamba na kujinyea kabla ya kuchamba unarukia thread na kucomment wakati kwenye thread muda wa interview ya Zitto umeandikwa.
 
Zzk umaarufu wake kwisha ati anajaribu kujisafisha ila bado ni sikio la kufa!hata akienda ccm hana nafasi pale akibaki tatizo!aungane na wenzake akina juliana shonza na mtela waanzishe chama cha wasaliti.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom