Dr.Slaa: Zitto anaweza kufukuzwa kabisa

Dr.Slaa: Zitto anaweza kufukuzwa kabisa

Status
Not open for further replies.
Mimi ni mtu wa kijiweni!, hoja zangu zote ninazoleta humu, nazitoa kijiweni, na pia ni kwa ajili ya watu wangu wa kijiweni na tena haswa vijiwe vya kahawa!. Asubuhi huanzia vijiwe vya kahawa, mchana hushinda kijiwe cha jf, alasiri vijiwe vya jobless, jioni kwenye kahawa tena, usiku saa ya chakula kijiwe cha mama mtilie kukombelezea mabaki, usiku namalizia tena kijiwe cha jf!. Yaani ninazunguka vijiweni kutwa kucha!, nalalia kijiweni, naamkia kijiweni, nashinda kijiweni, nakula kijiweni!.
Pasco
Pasco, mimi nipo kijiweni kwangu hapa nakunywa kahawa na kashata nakusoma.
 
fukuzeni hilo joka mmelichelewesha sana tu.....

ona anavyovimba makalio kwa kuendeleza misuguano ndani ya chama.
futa...... delete...... ondoa kabisa huyo kenge.
 
Dr.Slaa anaendesha Chadema kwa mkono wa chuma.
 
Hizi ni double standards za Chadema, wasiposimamia haki, watakuwa haunted na udhalimu wao hadi kuzimu!.
Pasco.

Mkuu Pasco kinachoisumbua chadema hapa ni uchaguzi wa mwenyekiti!

Kwa bahati mbaya sana chadema ilidhani ikimvua zitto nyadhifa zake basi wanachama watakubali kirahisi rahisi!

Matokeo yake yamekuja kinyume saivi wanaanza kujikanyaga ,kuna watu ndani ya chama huwa ni roho ya chama unapomtikisa chama chote kinatikisikq!

Hiki ndicho kilichojitokeza kwa zitto,kuna wengi wamefanyiwa hivyo na chadema na ikafanikiwq kwa hiyo ilidhani ni mazoea tu!
 
Hivi ni lazima kuwa mwanachama wa chama unachoona hakina misingi ya chama kama vile demokrasia n.k?, kama kweli hakuna demokrasia ndani ya cdm kwa nn watu wanang`ang`ania kuendelea kuwepo/, si watoke waanzishe chama/, harafu watu wanakuja na theory kibao hapa, wote tunajua, issue hizo theories hata mnaozileta mnazifanyia kazi?,kumbe siasa wakati mwingine inaweza kukufanya uwe mjinga kwa sababu tu unataka kujipambambanua bila kujali wenzio wanajua nini
 
Hivi ni kwanini Chadema!?kwanini iwe Slaa na Mbowe?kama ni suala la uongozi Mbona Cuf tangia ianze Lipumba mpaka leo bado ni mwenyekiti na Seif bado katibu!?vp kwa TLP!vp kwa Cheo na wengine?Kweli hi ni njama zlizopangwa na ccm kudhoofisha nguvu ya Chadema!Chadema chukueni uamuzi mgumu!mfukuzeni Zito!!tupeni kule!embu tusiyumbishwe sisi wanchama!!huyu jamaa ni mzadiki mnafiki!hafai!Chadema simamen imara!hali ya bahari siyo nzuri
Kwa hiyo umwinyi uliopo kwenye vyama vya upinzani ni kwa sababu hivi vyama ni baba mmoja mama mmoja? Akili ndogo kuongoza akili kubwa? Kweli ww ni mnyamighunda
 
Halafu mbona maccm yanahaha sana na zzk??mission failed nini saizi mpaka kina mtela mwampamba nao wamekuwa wasemaji wa zito.think louder!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
... je kwa kauli hii kuna haja ya kusubiri siku 14?...
Kwani bado siku 14 zinasubiriwa? Mbona zilishaisha na hukumu ndio kama hiyo? JK amewang'oa mawaziri wanne akiwa USA, akisharudi Dar ni utekelezaji tu, wala haihitaji utetezi hapo!
 
Mkuu Pasco kinachoisumbua chadema hapa ni uchaguzi wa mwenyekiti!

Kwa bahati mbaya sana chadema ilidhani ikimvua zitto nyadhifa zake basi wanachama watakubali kirahisi rahisi!

Matokeo yake yamekuja kinyume saivi wanaanza kujikanyaga ,kuna watu ndani ya chama huwa ni roho ya chama unapomtikisa chama chote kinatikisikq!

Hiki ndicho kilichojitokeza kwa zitto,kuna wengi wamefanyiwa hivyo na chadema na ikafanikiwq kwa hiyo ilidhani ni mazoea tu!
Chadema kwa sasa iko "in between the devil and the deep blue sea!", inahitaji busara kidogo kujiokoa, au hiyo busara kidogo ikikosekana, then inaweza ikaanza kujipotezea!. Tatizo ni kuchezea "powers" za watu!.
Ili mtu uchezee powers za mtu, lazima kwanza ujipime, unazo powers za kukabiliana na huyo unaeshindana nae!, kwa upande wa Zitto, ule ni msuli kweli!, Dr hafui dafu!. Waabudio watu hawaamini mungu wao hawezi!. Watu wanamtegemea Mungu kweli sio hawa miungu watu!.
Soon Chadema inapaswa kutenda yakipasayo kutenda, the sooner the better!, vinginevyo itajuta na majuto siku zote ni mjukuu!.
Pasco.
 
Hivi ni lazima kuwa mwanachama wa chama unachoona hakina misingi ya chama kama vile demokrasia n.k?, kama kweli hakuna demokrasia ndani ya cdm kwa nn watu wanang`ang`ania kuendelea kuwepo/, si watoke waanzishe chama/, harafu watu wanakuja na theory kibao hapa, wote tunajua, issue hizo theories hata mnaozileta mnazifanyia kazi?,kumbe siasa wakati mwingine inaweza kukufanya uwe mjinga kwa sababu tu unataka kujipambambanua bila kujali wenzio wanajua nini
Akili ya gongo hii
 
kauli ya katibu mkuu wetu wa chama DK WILBROAD SLAA imekuja wakati wanachama bado tukiwa na shauku ya kupata ufafanuzi wa kamati kuu na hatua ambazo zitachukuliwa juu ya mbunge zito kabwe, nimeona nilizungumze suala hili kwani KATIBU MKUU wetu nimeona kama analipalilia suala hili kwa kudai kwamba wanaweza kumfukuza ZITO KABWE je DK SLAA INAMAANA KATIBA INASEMAJE? SHERIA NA KANUNI ZINASEMAJE?? JE KWELI KAMA ZITO ATAFUKUZWA DK SLAA HUTAJIWEKA PABAYA KWAMBA HUENDA ULIKUA UNAJUA KWAMBA MNAENDA KUMFUKUZA MH ZITO?? wewe kama mtendaji mkuu wa chama ulipaswa ukae kimya ukusanye ushahidi ili kwenye kikao uweze kumsulubu mtuhumiwa kwa ushahidi uliokusanya, kwa kutumia kanuni,sheria na katiba ya chama, je na wewe ukiwa biased kama mtendaji mkuu wa chama unatuweka rehani wanao.
 
Tatizo ni anakotokea zitto na dini yake. Zitto as haukufunga ndoa ya kikatolik na cdm ya kutenganishwa na kifo kuwa mtulivu.
we bibi si nilikuambia baki MMU na chitchat udiscuss mapenzi?ona unavyoandika u.ha.ro,hebu lea wajukuu acha ujinga.
 
Yaani kila siku nikisikia Mwigamba, Kitila au Zitto anapata audience ya kuongelea mambo yao tumbo linanikata mie. Najiuliza hivi ni kwa nini Baraza kuu CDM msichukue uamuzi wa kuwafukuzilia mbali hawa wasaliti mapema kadri iwezekanavyo? Nini kinawafanya kuwa na kigugumizi hicho? Hamwoni kwamba hawa watu wanazidi kupata huruma ya jamii? Kwa nini msifanye haraka? Kwani nini kinawashinda kuwatimua, hata kama bila kufuata taratibu, wawe nje ya CDM wakajaribu kutafuta haki yao ya kurudishwa CDM huko huko mahakamani ilimradi wawe nje. Yaani napata hasira sana ninapoona hawa wasaliti bado wamo CDM na wanatamba wapendavyo!
 
Aisee, yaani hawa jamaa wanatakiwa kutolewa baru, kivibaya.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom