Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Kikwete atoe majeshi Congo ili waasi wakae na serikali ktk meza ya mazungumzo, sisi kama wa Tanzania hatutaki vita yasije yakawa ya kama ya kumpeleka Obote UGANDA, au wamezidiana kwa mademu? make raisi wetu kwa kupenda chini hajambo kilamtoto na mama
Mkuu upeo wako upo kwenyekizibo cha soda mbona unaongea kirahisi sana kama mtoto vile naomba ukumbuke kuwa majeshi yetu hayakopekeake na hayajaenda magizo ya jk pekee yake ila wameenda kwa mwamvuli wa un.
 
Hapa sioni mwenye nafuu. Naona wote hali kadhalika. Nikimtizama huyu naona bora yule. Nikimsikiliza yule naona bora huyu. 2015 ifike mapema.
 
ratel_16.jpg


WASWAHILI WANASEMA 'IGA UFE!'
KITENDO CHA SLAA KUM'ATTACK' Mr. PRESIDENT HAKINA TOFAUTI NA KUMUIGA 'HONEY BADGER' KULINA ASALI MCHANA KWEUPE, TENA PASIPO NA NYENZO YEYOTE!

JAPO WATZ WENGI TUNAKUHESHIMU, LAKINI KWA HILI UME'BUGI!' UMEONYESHA JINSI UNAVYOFANYA MAMBO YAKO KWA MISIMAMO 'PERSONAL' NA SIO 'BUSSINESS!' BE REMINDED THAT OUR BUSSINESS IS, AND WILL REMAIN, 'TANZANIA DAIMA!' (Not the Newspaper!)

POLE KWA YALIYOKUPATA MZEE! JIREKEBISHE NA UWEKE UZALENDO MBELE!
 
Never expecting such a low comment coming from Dr Slaa
Ni upuuzi kufanya cheap politics kwenye issues ambazo hazi hitaji siasa

Hivi Dr anadhani yeye hawezi kumshauri mtu kwenye mambo ya ndoa kwasababu ya mahusiano yake mabovu kwenye mahusiano yake

Hivi Dr Slaa anajua JK alikua anaongea kama nani?

Watu kama Ben Saanane wameonyesha ni jinsi gani wameshikiwa akili zao wala hawamaanishi wanachoongea zaidi ya kuongea wanavyopenda mabosi wao

Labda nimkumbushe Dr Slaa kwamba waswahili wanasema kuchamba kwingi..................


u hv nailed it

kwa sababu slaa ana mchumba hawezi kumpa ushauri wa ki-mke ben saanane????
 
Dr Slaa ameanza kuzeeka ubongo au ameanza kuvuta aina fulani ya tumbaku. Sikutegemea Slaa akose uzalendo kiasi hiki.

Nalaumu waandishi wa habari pia kwa kukosa uzalendo. Hivi nini kiliwasukuma kuandika matapishi ya Slaa? Habari kama hizi hazikutakiwa zimfikie Kagame.

Anyways Dr Slaa umesomeka vizuri na Kagame. Amekutumia friend request kwenye Facebook yako.
 
Mr. Man ninaona mambo ni mazuri kama umeweza kuona makosa katika maandishi yangu mambo yanakwenda vizuri. Karibu sana kwani IQ yako imetoka 10% na kufikia sasa 10.5 % karibu sana. Kuhusu mawazo yako ya kwamba kuwa mzalendo nafikiri inabidi niwe nasubira kwani tunavyo endelea utabadirika tu. Lbd kwa kukumbusha ni kwamba wewe ni kti ya watu walio okotwa kutoka huko vijijini na kutafutiwa mahali pa kujibana na baadae ndiyo ukaaanza kufagia pale lumumba na sasa unafikiri UDC utaupata! Lkn jitahii uongeze IQ yako kwani ya UDC hata ukiwa na 40% bado kwa nguvu ya mag utapata tu! karibu sana

mbulula wewe nani kakwambia nautaka udc? Natetea nchi yangu toka kwa mafisi kama nyie ambao mmekosa kabisa uzalendo na kutumiwa na maharamia wanaoisaliti nchi kwa kulipwa ujira mdogo sana. Mmemwaga hapa hamna cha maana mnachoandika zaidi ya upuuzi katika kutetea maharamia na magaidi.
 
Hapo mkuu naona ume hit a bull's EYE - well said "Kufanya cheap politics kwenye issues ambazo hazi hitaji siasa" Personally have a feeling Dr.Slaa & Co have no slightest idea how ruthless/dangerous M7 and PK are, these guys are capable of wreaking havoc in Eastern and Central Africa region at opportune time, don't U underrate their resolve....

Rwanda na Uganda hawana kitisho chochote kwa Tanzania acheni kukuza haya mambo.Naamini kijeshi tupo vizuri zaidi kuliko hao majirani zetu.Na kwa taarifa yenu hakuna watu wenye misimamo mikali katika siasa za nje kama tulioko CHADEMA.Kagame asingethubutu kutoa matusi anayoyatoa kwa JK kama Slaa angekuwa Rais.Angeanzaje kwanza?Ili kwenye ukweli lazima tuseme Rais wetu amechemsha na hili halihusiani na Uzalendo kabisa.
 
Dr.W.Slaa,

..u definetely need to do more research kuhusu mgogoro wa DRC kabla ya kuanza kuchukua upande wa Kagame au Kikwete.

..ningeshauri uwe na timu ya vijana wako wanaofanya kazi ya utafiti na kukupatia taarifa ya mambo mbalimbali.

..zaidi timu hiyo inatakiwa ukishauri kuhusu misimamo na mitizamo ambayo unapaswa kuchukua huku ukizingatia sera rasmi za CDM.

..I think u r doing too much. U have too much on your plate. kwa nafasi kama yako unahitaji timu ya wataalamu kukushauri, kukuelekeza, na kukuongoza, kwani masuala ambayo unashughulika nayo ni mengi.
JokaKuu nakubaliana nawe kabisa kuhusu hili. Dr.W.S.Slaa anatakiwa awe katika nafasi ya kuelewa kuwa kuna kuzungumza kama mtu binafsi na kuzungumza kama kiongozi wa chama. Nadhani anahitaji washauri katika hili.

Slaa aelewe kuna vitu vutatu hapa, kauli ya Kagame, ushauri wa JK na ugomvi wa PK na Ntarahamwe.

Alitakiwa aeleze kwa ufasha na wala si suala la kuonyesha hasira zake dhidi ya JK.
Hili ni tatizo la kimataifa na approach yake si sawa na kuwaita CDM kuongea nao Ikulu.

By the way mara ngapi tumeona wakiwa wamezunguka majagi ya jusi na Togwa pale Ikulu, mara ngapi amekutana nao katika mikutano na ufunguzi wa barabara .

Dr aelewe tofauti ya kukutananishwa na kuzungumza. JK anaposema PK azungumze na wapinzani ni kwamba amefungua milango ya ima yeye au mtu mwingine kukutanisha pande hizo kwa kuwasuluhusisha. Kitu cha muhimu ni kupata ridhaa ya pande husika kwanza ndio maana JK alisema wazungumze., si kuchukua jukumu kwasababu yoyote anaweza kuwa msuluhushi.

Standard ya opposition party lazima iwe juu sana na isiache doubt kwa namna yoyote.
Kuna umuhimu wa kuangalia washauri wa mzee hasa katika mambo ya kimataifa.
Kitila Mkumbo Jasusi Ben Saanane
 
Last edited by a moderator:
Yaani wewe ndugu yangu mwanaukonga mwenzangu nimesoma hoja yako nilipoimaliza nikakuhurumia huenda hujui kinachoendelea duniani.

Jana Marekani imetangaza kufunga ofisi zake za balozi zipatazo 21 katika nchi za Afrika Kaskazini pamoja na Middle East kufuatia kitisho cha mashambulizi ya Al Qaeda. Sasa sijui unaizungumzia al qaeda ipi iliyodhoofika lakini hapo hapo inaweza kuwa kitisho kwa nchi kubwa super power kama marekani hadi inaamua kufunga balozi zake.

Kwahiyo ndugu yangu hoja yangu iko palepale kwamba Kikwete angekuwa muungwana sana kama angetoa ushauri ambao yeye mwenyewe ana u-practice. Wananchi wa Mtwara tu ameshindwa kuongea nao na kuwatumia batallion ya JWTZ sasa huo uungwana/huruma kwa majirani zake ameutoa wapi?

Mwita Maranya, two wrongs can not make one right! Wakati tunakosoa kauli ya JK katika suala hili, lakini pia tusiache kukosoa kauli ya Dr. Slaa iliyopelekea kuwepo kwa thread hii. Hii ni busara itakayopelekea kuwa na chama kinachokosoana na si vinginevyo. Binafsi mimi pia nakuonea huruma mwanaukonga mwenzangu na pia najionea huruma kwa sababu najua repercussion ya kauli ya Dr. Slaa. Bahati tu haitaonekana sana tu kwa kuwa kiwango cha watanzania kupoteza matuamaini kwa Serikali ni kikubwa sana ndiyo maana watu watapata uvumilivu kidogo, lakini kauli ya Dr. Slaa "inayumba" sana kuweza kuielewa. Tunapozungumzia siasa, ni vema tutofautishe baina ya siasa za ndani na nje. Siku zote siasa ya ndani inajengwa kwa siasa za nje kupitia "Diversionary incentives" na si kinyume chake. Na hii huenda ndicho kinachofanywa na hawa marais wawili. Nimesema hapo juu kuwa ushauri wa Kikwete kimantiki uko sawa, labda kimazingira. Hata hivyo naweza kusema pia hata kimazingira ilikuwa ni sahihi kwa sababu lengo ni kupata "Global attention" na pia haukutolewa kwa Kagame pekee, je ni nini kilichofanya Kagame ndio aonekane kama ndiyo pekee aliyepewa ushauri huu? Na je ulifatilia kikao kilichopita cha Baraza la Usalama la UN mwezi uliopita ambapo Rwanda ni mjumbe wa kudumu kwa sasa kwenye Baraza hilo na kuiona hali aliyokuwa nayo Foreign Minster wake? Nilifuatilia live mwanzo mwisho na yule mama alikuwa kama yu mgonjwa kwenye mkutano ule.

Kuhusu Marekani na balozi zake, nadhani pia huna budi kuzingatia kuwa kilichoifanya Marekani kufunga Balozi zake si Alqaeda ile ya Osama, no. Ni kutokana na intervention yake katika vita ya Syria na Libya, machafuko yanayoendelea ktk arab countries ambazo zimetoa mwanya wa minimal movement control kwa kutumia kigezo cha machafuko pamoja na wale mamia ya wafungwa waliotoroka ambao kutokana na mateso waliyoyapata, Marekani inaamini kuwa wale watu watalipiza kisasi kwa kufanya mashambulizi, lakini pia inaamini baada au siku chache kabla ya Mfungo wa Ramadhan, radical muslims wanakuwa na highest morality ya kufanya attack. Lakini si Alqaeda as Alqaeda kwa sababu (narudia tena kiasi fulani imedhoofika baada ya kuwa Marekani amebaini njia zake za mawasiliano kitu ambacho awali hakuwa akijua, kiasi cha kuamini AAlqaeda walikuwa na teknolojia ya juu sana ya mawasiliano). Kwa sasa, marekani inatumia neno ALqaeda kama ni justification na supports kutoka kwa wananchi wake kwa sababu ndio jina ambalo wanalielewa sana. Lakini hoja yangu katika hili nilisema kuwa Alqaeda ni mtandao si kikundi tofauti na kesi ya Rwanda. Ni kutokana na kuwa ni mtandao ndio maana hadi wanafunga hizo Balozi hawana hakika exactly wapi hizo attacks zinaweza fanywa. Mwita ndugu yangu, nafuatilia kwa karibu sana siasa za nje hususan Marekani.

Nimalizie maelezo haya marefu kwa mwanaukonga mwenzangu kwamba, Dr. hana budi kuwa well informed katika anga za kimataifa kwa sababu hiyo ndiyo hali ambayo Tanzania inayo kutokana na strategic environment zinazotokana na resources zilizopo. Hakuna namna yoyote ya Tanzania kuwa "dumb" katika siasa za nje kwa sasa. Nitumie fursa hii kuiomba kurugenzi ya mambo ya nje ya Chadema kuiangalia nafasi ya Tanzania kwa sasa katika International political arena kwa umakini mkubwa kuliko ilivyokuwa one year before kwa sababu inaweza kuisumbua katika kipindi cha uchaguzi. Ni rahisi kwa UK na US kuiachilia mbali Zimbabwe, lakini si rahisi kwa Congo, Tanzania na Nigeria.
 
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo kwa vile wanatambulika kama wauaji.

Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Alimshangaa kuwataka kuzungumza na watu ambao Kagame anawaita wauaji wenye asili ya kundi la jeshi la Nterahamwe, lililokuwa linaangamiza Watutsi.

“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani, hajachukua hatua dhidi wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi, alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda, amempandisha cheo,” alisema.

Alisema Rais alitakiwa kuwaambia waje awapatanishe lakini si kuwaambia wazungumze na watu anaowatuhumu kuua Watutsi.

Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.


CHANZO: NIPASHE

Slaa na wewe ka meza moja umalize tofauti zako na ex wife wako kabla ya kuanza kuwaambia wenzako....
 
JokaKuu nakubaliana nawe kabisa kuhusu hili. Dr.W.S.Slaa anatakiwa awe katika nafasi ya kuelewa kuwa kuna kuzungumza kama mtu binafsi na kuzungumza kama kiongozi wa chama. Nadhani anahitaji washauri katika hili.

Slaa aelewe kuna vitu vutatu hapa, kauli ya Kagame, ushauri wa JK na ugomvi wa PK na Ntarahamwe.

Alitakiwa aeleze kwa ufasha na wala si suala la kuonyesha hasira zake dhidi ya JK.
Hili ni tatizo la kimataifa na approach yake si sawa na kuwaita CDM kuongea nao Ikulu.

By the way mara ngapi tumeona wakiwa wamezunguka majagi ya jusi na Togwa pale Ikulu, mara ngapi amekutana nao katika mikutano na ufunguzi wa barabara .

Dr aelewe tofauti ya kukutananishwa na kuzungumza. JK anaposema PK azungumze na wapinzani ni kwamba amefungua milango ya ima yeye au mtu mwingine kukutanisha pande hizo kwa kuwasuluhusisha. Kitu cha muhimu ni kupata ridhaa ya pande husika kwanza ndio maana JK alisema wazungumze., si kuchukua jukumu kwasababu yoyote anaweza kuwa msuluhushi.

Standard ya opposition party lazima iwe juu sana na isiache doubt kwa namna yoyote.
Kuna umuhimu wa kuangalia washauri wa mzee hasa katika mambo ya kimataifa.
Kitila Mkumbo Jasusi Ben Saanane

Shukrani sana Nguruvi3 na JokaKuu.Hatutawaangusha katika hili....!

Pia suala la kukutana Ikulu lilikua mara moja tu, je rais alitekeleza makubaliano?Maana chanzo kikubwa cha mifarakano kwa mataifa mengi ni kwa serikali kukataa kutekeleza makubaliaano yao waliyoafikiana na wapinzani.
 
Last edited by a moderator:
mi nadhani slaa yuko sahihi. Huo ushauri ulitakiwa uwaendee serikali ya congo wakae na waasi wao wakubaliane kuhusu amani ya nchi yao pia wawarudishe Rwanda wahutu wa Fdlr au km wanabaki kongo wawanyang'anye silaha wabaki kuwa wakimbizi wa kawaida na ikiwezekana wawape uraia. Hawa Fdrl wanafanya nn Kongo na Rwanda hakuna vita? Kagame alishawaambia warudi rwanda na kuna wenzao 20,000 walisalimu amri wakarudi na kuingizwa jeshini. Tatizo kurudi hawataki wanaogopa kuchukuliwa hatua wengi wao ni wauaji wana kesi za kujibu nyingi tu.
 
Never expecting such a low comment coming from Dr Slaa
Ni upuuzi kufanya cheap politics kwenye issues ambazo hazi hitaji siasa

Hivi Dr anadhani yeye hawezi kumshauri mtu kwenye mambo ya ndoa kwasababu ya mahusiano yake mabovu kwenye mahusiano yake

Hivi Dr Slaa anajua JK alikua anaongea kama nani?

Watu kama Ben Saanane wameonyesha ni jinsi gani wameshikiwa akili zao wala hawamaanishi wanachoongea zaidi ya kuongea wanavyopenda mabosi wao

Labda nimkumbushe Dr Slaa kwamba waswahili wanasema kuchamba kwingi..................

Slaa ni "mfa maji haishi kutapatapa".

Na huyu Ben Saanane ni mnafiki mwingine, msome hapa, leo kishabadilika baada ya boss wake kudandia treni kwa mbele.

Hivi kuna watu wenye akili timamu wanaounga mkono msimamo wa Kagame pamoja na Matusi yake?The guy is such a disgrace.....!

Tayari watanzania tunajua JK si kiongozi Shupavu.Lakini mimi kama Mtanzania sitavumilia kuona Kagame anamtukana kwa sababu tu kaambiwa aongee na waasi kwa maslahi mapana ya Rwanda,DRC na ukanda wa Maziwa makuuu.Bloodthirsty tyrant!

Huu ni msimamo wangu binafsi.Wale wenye mpango wa kunisuta wanapoteza muda tu.Sitaubadilisha hata kwa mtutu wa Bunduki.
 
Kikwete alisomea wapi.Nina shahada 2 za uzamili.Nimezisotea kamwe sitawahi kutamka jina "Dr.Kikwete" hata kwa mtutu.

Basi wewe ni mbumbumbu mzungu wa reli, unazisotea shahada wakati watu wanaonekana kazi zao duniani na magwiji wa vyuo vikuu wenyewe wanaamuwa kuzitoa hizo shahada kwa kazi tu ya mtu. Hapo ndio ujuwe tofauti yako wewe na wenye vichwa.
 
We are paying the price of denying Kwame Nkrumah idea of African unity. Sahv tungekuwa na united states of africa (USA). Matokeo yake ni vita kila mahali africa kwa sababu ya selfshness ya viongozi wetu
 
What is the correlation?Je JK ali-stick kwenye agreement?

Mtu ambaye hatekelezi makubaliano ni chanzo cha mifarakano na kutpaminiana kama tulivyoshuhudia uasi kutoka nchi nyingi.

Asingeshiriki kwenye agreement mbona hatukuwasikia viongozi wako kupinga tena mchakato wa katiba mpya wala kusema kuwa Kikwete kakiuka mkataba? Unanshangaza.
 
Back
Top Bottom