Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

UNAFIKI mbaya jamani.

Huyu mzee uroho wa pesa na madaraka unampeleka kubaya sana kiasi kwamba anawalaghai wafuasi wa chadema waache kuomba Mungu!

Huyu ndio anasema Kikwete haongei na wapinzani?!!!

kikwete anasikiliza.jpg
 
Unadhani Dr Slaa bila kumkosoa Rais Kikwete ataendeshaje siasa zake.

Dr Slaa anatoa mifano ya kitoto sana analalamika kuwa mbona JK kashindwa kuongea na wapinzani.

Dr.W.Slaa, ziara zenu pale Ikulu mlikuwa mnakwenda kuongea na nani au tuweke picha.
 
Last edited by a moderator:
Dr.Slaa anaweza kuongea hivyo
kwa sasa. Lakini hata Dr. Slaa angekuwa Rais wa nchi,maisha yake binafsi
na mipaka ya nchi yake ikitishiwa,angeanza kwanza ku deal na
wanaotishia mipaka ndipo angekuja kutatua ya ndani. Ukiwa unagombana na
mkeo/mumeo ndani,ukasikia watu wanataka kuvunja gate wavamie kwako,cha
kwanza utaenda kupambana na wanaivunja gate lako ukisha wasambaratisha
ndio utarudi ndani kupatana na mkeo/mumeo.

Huu mfano wa Geti ... Nafikiri si mbaya ... nimzuri... ingepaswa uingie ndani ya vichwa na mioyo ya Watanzania wote ... Bila kumsahau Diktete Paul Kagame ambaye nina Bif naye personaly. Namhakikishia hata wakiptana Jk nitamchakaza tu!
 
Kinadharia ushauri wa Kikwete unaweza kuonekana kama mzuri lakini haukuwa na action plan au road map ya utekelezaji kushauri bila action plan ni sawa na kuropoka hasa unapomshauri mkuu wa nchi nyingine.

Kama Kikwete ataanzisha vita na Kagame binafsi nitakuwa wa mwisho kwenda vitani, kwa sababu naamini Kikwete hakuwa sahihi kuwaambia Rwanda wakutane na waasi alichotakiwa ni ku-mediate mkutano kwa kuwakutanisha mahasimu na sio kuwaambia wakutane, kwanza wakutane wapi na nani awe mlalamikaji na mlalamikiwa.

Kushinda vita kunahitaji umoja wa kitaifa.Uzalendo ni kigezo kimojawapo katika sababu za kushinda au kushindwa.Kiongozi mkuu wa Nchi ni lazima aunganishe taifa dhidi ya common enemy ambaye ni adui wa nje.Wahenga walisema kamba hukatika......!

Uongozi wa JK na brutality dhidi ya wapinzani wa serikali yake unaliweka taifa katika precarious situation.Nyerere alishinda vita ya Kagera kutokana na ushawishi wa ndani.Rais anatakiwa amfanye mtanzania ajisikie proud anaposimama mbele ya raia wa mataifa mengine.Pride na national values ndizo zinazolitofautisha taifa kubwa na dogo.We have what it takes to make Tanzania a giant Nation in Africa and beyond!
 
Dr.Slaa anaweza kuongea hivyo kwa sasa. Lakini hata Dr. Slaa angekuwa Rais wa nchi,maisha yake binafsi na mipaka ya nchi yake ikitishiwa,angeanza kwanza ku deal na wanaotishia mipaka ndipo angekuja kutatua ya ndani. Ukiwa unagombana na mkeo/mumeo ndani,ukasikia watu wanataka kuvunja gate wavamie kwako,cha kwanza utaenda kupambana na wanaivunja gate lako ukisha wasambaratisha ndio utarudi ndani kupatana na mkeo/mumeo.
Huku ndio kunaitwa kupamba maandishi tu, kama kasema hivyo kweli anaji expose tu as vuvuzela. Ina maana Dr.Slaa aliomba kazi kwa watanzania ya kuwaongoza bila ya kujua job description, can we really afford another learn as you go leader in our politics.

Kuna wakati inabidi ajue the meaning of national interest politics na si kila kitu kupinga tu kama mwanasiasa mwenye kiwewe. Naanza kuichukulia kwa umakini sana kauli ya mchungaji Mtikila ya kuwa Kagame katupandikizia wanyarandwa tayari, na huko ndani ya CDM naona waanze mchakato wa kuangalia historia za watu wanaowapa nafasi za kutoa ushauri kwa viongozi wajuu.

Maana with Slaa and Mbowe both without clear national visions and already are willing to take advise from members in the social media. What it shows there are not many brains in that party, no wonder majimbo, majimbo my foot.
 
Kwa hili Babu umepotoka,naona unazeeka vibaya.JK alikuwa sahihi kabisa kusema hilo,Kagame hataki kupambana kwa sababu zake binafsi ni mkweli usiopingika hataki mupinzani nchini kwake ndo maana wapinzani wengi wamefungwa Rwanda na Jenerali Nyamwasa kutaka kuuwwawa na agent wa serikali yake kwa kuanza kumpinga akiwa kama balozi wa nchi ya Rwanda

Serikali ya Tanzania inwapa uhuru nyinyi akina Silaa Uhuru wa kupita kiasi ambao humom kwenu Chadema haupo,nani asiye jua kuwa Kafulila alifukuzwa CDM kwa suala la kuhoji demokrasia,na pia mlitaka kumfukuza ZITO kwa kuwa alitaka kugombea uenyekiti wa CDM

Nini chanzo cha kifo cha Chacha Wangwe ambaye alikuwa amejipanga kugombea uenyekiti wa CDM

Acha hizo,na kwa sasa Tanzania tunahitaji Rais mwenye muono wa mbali kiuchumi na sio mpiga kelele
 
Aliyoyaongea Dr Slaa ndio yalikuwa kichwani mwangu.Namuunga mkono Dr Slaa kwa hili.Tanzania hatuwezi kuingizwa Vitani kwasababu ya matatizo binafsi ya JK na Kagame.

Yaani wee hata fikra zako huzijuwi zinataka nini...we ni kijana acha kuamini na kushabikia kila kitu tafakari kwanza kabla hujapost ndio ukomavu wa fikra, sio kwasababu kaongea Dr Slaa basi naunga mkono.... Lol pole sana
 
Nadhani sasa kwa wakati tulionao hatuna budi kuchagua kipi cha kusema na kuandika kuhusu Rwanda.Hali ni mbaya tofauti na tunavyofikiri.
 
Kweli kabisa Mkuu. Mimi naona kama vile wanataka kutengeneza tu habari, basi hakuna zaidi ya hilo. Au ndiyo tumeshaanza kuchonganishwa makusudi?


Jk anatuabisha tu. Rwanda is just too a small country to argue with. Wote tunaoneka wehu kama wao. what is the difference ?
 
Kosa kubwa la Rais Kikwete ni kutamka maneno hayo hadharani angeweza kumwita kagame wakaongea naye badala ya kukimbilia kutoa matamko hadharani ni kama anamwona kagame hana akili
 
Jamani upinzani si kupinga kila kinachosemwa au kufanywa na ruling party. Kama swala linahusu ustawi na usalama wa nchi yetu ni vyema kuweka uzalendo mbele kuliko maslahi binafsi. Slaa busara imemtoka now anaonyesha wazi kuwa hafai kuwa rais kwa sababu hataweza kuilinda nchi yetu.kikwete hakuitishia rwanda bali ametoa ushauri ili kukomesha vita rwanda na hata kama hao waasi ni wauaji tujiulize ni bora waendelee kuwa waasi au kagame azungumze nao kusudi warudi kuwa wananchi wa kawaida? Angola na burundi uasi ulikwisha kwa mazungumzo na si kwa mapigano.naunga mkono ushauri wa jk na kama kagame hataki ni yeye na nchi yake
 
Kwakweli nadhani dr slaa anaheshimika sana sana,namm nilitegemea kama mtu wa busara angejiepusha kuzungumzia maswala ya rwanda kama hawezi kuunga mkono,mh rais alivyo jibu baada yakutukanwa,angeweka uzalendo kwanza,mambo yandani yabaki kama yalivyo ila swala la rwanda hata yeye angekuwa rais angetoa ushauri,sasa ushauri unapogeuka matusi yeye cjui angefanyeje,swala hili lakila siku kudanganya dunia kwa propaganda,ndo madhala yake,rwanda wanaishi kwa propaganda,je mtoto aliyezaliwa baada ya mauji ya 1994 naye nimwuuliaji?ukweli ubaki kama ukweli tuache ushabiki,mm nampongeza kikwete kwa msimamo naukomavu wakisiasa,niwachache wanao dhalilishwa kama yeye wanakaa kimya.tufaham historia zamajirani zetu.
 
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo kwa vile wanatambulika kama wauaji.

Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Alimshangaa kuwataka kuzungumza na watu ambao Kagame anawaita wauaji wenye asili ya kundi la jeshi la Nterahamwe, lililokuwa linaangamiza Watutsi.

“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani, hajachukua hatua dhidi wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi, alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda, amempandisha cheo,” alisema.

Alisema Rais alitakiwa kuwaambia waje awapatanishe lakini si kuwaambia wazungumze na watu anaowatuhumu kuua Watutsi.

Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.


CHANZO: NIPASHE

Huyu dk. Slaa nadhani naye sasa ana matatizo ya kisaikolojia, sijui ni kwa sabaubu ya mapenzi ya uzeeni? Ras Kikwete ni mtu makini. Alipotoa ushauri ule siyo kwamba alikurupuka, ila ni kwa maana historia ya Rwanda anailewa vizuri. Rwanda haitakuja kuwa tulivu bila wanyarwanda wote kukaa chini na kuzungumza kwa pamoja. KAGAME anahusika moja kwa moja na mauaji ya kimbali kwa kuwa yeye ndiye chanzo cha mapinduzi yaliyomwaga damu lakini pia kuna wahutu wengi nao waliuawa. Ni kwa kuwa jumuia ya Kimataifa ilimnyamazia Kagame ili kuleta amani nchini Rwanda. Hivyo FDRL na KAGAME wote walipaswa kufikishwa katika mahakama ya kimataifa. Sasa kama wote walishiriki katika mauaji na wote ni wanyarwanda kwa nini wasikae chini wakazungumza na nchi yao ikawa na amani? FDRL na KAGAME wote ni wauaji wa binadamu wasio- kuwa na hatia. Hivyo Dr. Slaa usikurupuke! au tushawishike kuamini kwamba unapewa misaada na Kagame? maana Kagame alisema anajua ni wakati gani atampata JK, sehemu mojawapo tunayojua ni kupitia M23 ambayo atashindwa vibaya, lakini pia kupitia vyama vya upinzani ambako nako ameishashindwa kabla hajatimiza malengo yake. Kagame asijidanganye kama ana jeuri hata chembe ya kuiyumbisha Tanzania aidha kupitia vibaraka wake walioko nchini ama kwa njia yeyote. Ameamua "naturaly" kujiandalia mwisho wake na lazima adhoofike na kupotea.
 
Dr. Slaa sio kosa lake. Uwezo wake wa kufikiri umekuwa wa kiwango cha Josephine Mushumbusi.

Anasema Kikwete haongei na wapinzani wakati Slaa ameonekana mara kadhaa Ikulu akinywa juice. Sasa sijui walikuwa wanakunywa juice kimyakimya!!!

View attachment 105628

si busara kutukana wanaume wenzio namna hii watu hawakosoani kwa kutukanana. no wonder unataka kuwa mbunge mimi mwenyewe sijakubaliana na wazo la DR slaa maana aijaona kosa kwenye ushauri wa mh jk. lakini matusi yako haya yana kuaibisha na kukushushia hadhi.
 
Back
Top Bottom