Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Aliyoyaongea Dr Slaa ndio yalikuwa kichwani mwangu.Namuunga mkono Dr Slaa kwa hili.Tanzania hatuwezi kuingizwa Vitani kwasababu ya matatizo binafsi ya JK na Kagame.

CCM otewalipo + Kikwete + Mwiguru =janga la taifa
 
“Mimi sipendi nchi zetu ziingie vitani kwa sababu ya kauli za viongozi wawili, hapa tunazungumzia kushambulia na kushambuliwa, hawa marais wawili wangekutana kumaliza tofauti zao, maana wananchi wa mataifa haya ni ndugu,” alisema...
Huyu ndie Dr Slaa, anasema hakuna haja ya kuingia vitani kwa sababu ya tofauti tu ya kauli za viongozi.....we hutaki! unataka kagame apigwe tu!
Jk aliongea vizuri sana hakuna mahara alipotaka vita tena katumia kauri nzuri sana ila slaa ndiyo kaharibu kwa kumuona jk kaksea na kumsapoti kagame ambaye amekuwa akitukana kila kukicha hivi jk angetoa kauri kama za kagame slaa angesemaje naona angeenda moja kwa moja icc kumshitaka jk huyu mzee kwa nini anamchukia sana jk na kwa nini akawa na roho mbaya kiasi hiki kwa jk na taifa.
 
Na hii ndiyo LOGIC YA DR W.P. SLAA mkuu iwapo umemsoma kwa kina!..Tatizo ni moja tu kwa wana CCM wanaojipambanua kwa michango yao humu jamvini, ni kwa sababu tu hayo yamesemwa na Dr Slaa ambao kwao ni adui yao mkuu na kikwazo kikubwa kwao!!

Alichokifanya JK ni kosa tu la kiufundi kwani inawezekana nia yake ni njema (mimi sina hakika) hata kama ni kiongozi wa AU au SADC au EAC. Kamwe hawezi kuongea jambo lolote linalohusu Rwanda na Wanyarwanda na Kagame Rais wao kana kwamba anaongea na mkuu wake wa mkoa wa KIGOMA. Rwanda ni nchi huru ni lazima iheshimiwe hata kama ina matatizo yake kama hayo.Na wale wanaosema kuwa wanaweza kuipiga Rwanda kama upigavyo mwanao wa miaka mi5 ni KUJILISHA UPEPO TU kwani ukubwa wa pua si uwingi wa kamasi.....Hatujui wanawaunga mkono Rwanda ni kina nani.Na je, sisi tunawajua marafiki na maadui zetu??...JK kama kaamua kuwa mpatanishi,basi afanye hivyo kwa uwazi na kuyaheshimu makundi yote!!

.
Unajua kama sisi watanzania tumeamua kujipumbaza wacha tu-face consequences za --------. Huwezi kusema kwamba utaichakaza kwa kipigo nchi nyingine kwa kigezo cha udodo kama ingelikuwa ni hivyo mataifa 11 ya kiarabu yasingesalimu amri kwa Israel ndogo au Daudi mdogo asingekata kichwa cha Goliat giant. Tujaribu ku-reason logically maana hata kama usalama wa taifa wa kagame watakuwa wanajaribu kufuatilia comment za watanzania katika hii mitandao ya kijamii wanaweza kuhitimisha hukumu ya ni vichwa vya namna gani wanavyojihusisha navyo. Ushindi wa vita siku zote huanzia pale mtu anapotambua kuwa adui yake hana uelewa wa kile kinachomkabili. Rais wetu pamoja na kujitetea kuwa ushauri ni ama anaeshauriwa akubali au kuukatae kuuchukua pia anapaswa kufahamu kuwa anaeshauri/patanisha ana kanuni na sheria zinazomuongoza. Sii tu kwamba anaropoka popote pale kwa kisingizio cha kujificha katika kivuli cha ushauri.
.
 
sASA ndugu Morinyo kama unafahamu kuwa wapinzani wote wa Kagame wako nje ya nchi, na hao FDLR wako misituni sasa Kikwete anawezaje kumshauri Kagame akazungumze nao? kundi la FDLR limeshatajwa kuwa ni kundi la kigaidi na ndivyo dunia inavyolitambua, sasa Kikwete anaanzaje kumshauri Kagame aafanye mazungumzo na magaidi? mbona asiishauri marekani kuingia kwenye meza ya mazungumzo na al qaeda? au ameshindwa nini kumshauri Kenyata aondoe majeshi yake somalia na kukaa na al shabab katika meza ya mazungumzo? Ushauri mwingine kabla hujaautoa ni vizuri ukajipima kwanza kama ungekuwa wewe ungeuchukuliaje.


Mkuu umesahau kua Marekani wameshakaa mezani na Talebani, na wamewafungulia ofisi Qatar. Wapinzani wa kagame wamekimbia nchi kuokoa maisha yao na waliobaki kama akina Bizimungu wako gerezani. Ukikosoa utawala wa PK usipouawa ni kifungo. Kauli ya Kikwete imesharudiwa na viongozi wa SADC na wakati ukifika itatolewa na jumuia nyingine kubwa kuliko hiyo. Genoside ilishatokea na dunia inajua kua ilitokea, lakini mda wa kuitumia genoside kama panga la kuchinjia wapinzani wake umeisha. Nani yaliyofanywa na Makaburu dhidi ya watu weusi, je ilimzuia Mandela kukaa nao mezani?
 
Mzee slaa anamatatizo na wanawake zake na bado hajayamaliza kwa nini anadandia mambo ya wengine wakati ya kwake hajayamaliza kama hoja yake ndiyo hiyo.
Bado tu utakataa nikisema wewe ni mjinga?onyesha wapi wake wa Dr slaa waliwahi kutamka kuwa watam Hit slaa at any given chance,kama hawajafikia huko basi hali ni shwari!ila kagame alitamka wazi kuwa ata m hit kikwete!!hapo ndiyo tatizo lilipo,we hata hujui kama jk na familia yake wanaishi kwa amani.
 
Huyu mzee anasaliti nchi yake kwaajili ya urais. Sasa ndio nimedharau kabisa. Yote hii ni kujipendekeza kwa kagame.

Yaani urais ni bora kuliko kila kitu!? Kwakweli siasa za vyama vingi ni 'REACTIONARY!' Japo vyama vinasaidia kwa kiasi fulani kudhibiti madhambi ya watawala lakini kwa asilimia kubwa vyama hivi vinakwaza maendeleo kwa siasa za kujipendekeza hata pasipostahili!
 
sASA ndugu Morinyo kama unafahamu kuwa wapinzani wote wa Kagame wako nje ya nchi, na hao FDLR wako misituni sasa Kikwete anawezaje kumshauri Kagame akazungumze nao? kundi la FDLR limeshatajwa kuwa ni kundi la kigaidi na ndivyo dunia inavyolitambua, sasa Kikwete anaanzaje kumshauri Kagame aafanye mazungumzo na magaidi? mbona asiishauri marekani kuingia kwenye meza ya mazungumzo na al qaeda? au ameshindwa nini kumshauri Kenyata aondoe majeshi yake somalia na kukaa na al shabab katika meza ya mazungumzo? Ushauri mwingine kabla hujaautoa ni vizuri ukajipima kwanza kama ungekuwa wewe ungeuchukuliaje.

Hapana, kosa kubwa linalofanywa na pro-CCM ni kushindwa kusema hii siyo na hii ndiyo; Wewe kuwa Chadema na Dr. Slaa kuwa Chadema haina maana kwamba chochote atakachosema ni ndiyoooooo, litakuwa kosa la magamba hili. Labda magazeti au habari namna ilivyoletwa imepotoshwa. lakini ukweli ni kwamba ushauri wa JK hauna kosa kimantiki labda kimazingira. Marekani haiwezi kuzungumza na Al-qaeda ni kwa sababu kuu mbili. Kwanza Alqaeda ni mtandao wala si kikundi ambao haupo msituni wala mjini wala popote. 2. Nguvu za Alqaeda zimeshadhoofika sana, kwa hiyo marekani hana sababu ya kuzungumza na watu ambao tayari ni dhaifu. Lakini je? umepata kujiuliza kama Taliban ni nini? Ni Serikali au ni nini? Na kwa nini Marekani pamoja na huko nyuma kuitambua Taliban kama kikundi kinachosapoti ugaidi (na hivyo wao pia magaidi) hivi sasa kuonyesha nia ya kuzungumza nao? Halafu tukubali kwamba, Tanzania haiwezi kumshauri Marekani kwa sababu mgogoro wa Marekani na maadui zake hauiathiri Tanzania Directly kama namna mgogoro wa majirani wa Tanzania (Rwanda, Burundi) unavyoathiri Tanzania kwa kila nyanja. Mwita Maranya najua sote ni waathirika wa yule mama aliyeua Ukonga yetu lakini sitakuwa mtumwa wa kukubali kauli iliyokosa substance kwa kuwa tu ni chama kimoja. Hii ni tabia ya kulindana, tabia ambayo siku zote tunagombana na wana Lumumba humu JF.
 
Hivi huyu Slaa ndo tunategemea aje eti ashike urais??? CDM kwa usawa huu watasubiri 50 years..this guy is not a presidential material...hii alioongea ni pumba at a higher level...CDM itabidi wajipange upya huyu hata udiwani hapati maana ni dhaifu kuliko udhaifu wenyewe...
nani hajui chuki mliyonayo kwa CDM ni kwa vile mnajua siku wameingia ikulu UWT wote nje! ndio maana mmejiapiza kutetea ujinga hata asiyejua siasa hawezi kutetea ili mfie ikulu..hata rumi empire ilianguka kumbuka hilo ucsahau kabisa..mtatoka tu hata mkeshe jf na mauza uza yenu!
 
Kikwete atoe majeshi Congo ili waasi wakae na serikali ktk meza ya mazungumzo, sisi kama wa Tanzania hatutaki vita yasije yakawa ya kama ya kumpeleka Obote UGANDA, au wamezidiana kwa mademu? make raisi wetu kwa kupenda chini hajambo kilamtoto na mama
 
Huyu Dr Slaa kadri siku zinavyokwenda nadhani ameanza kujisahau na kujiona Mungu mtu kwakuwa tu kuna watu wamekuwa brainwashed kwa kuamini Dr hakosei na wanaunga mkono kila atakalo tamka
Kama wanadhani wanamjenga basi wajue kabisa wana mbomoa, hakuna busara wala mantiki yoyote kwa Dr kutoa kauli za kipuuzi kama hizi just simple kwakuwa zinamlalia mpinzani wake kisiasa.

Hivi kwa akili ya kawaida kabisa kama unamwambia tu mtu kutana na mpinzani wako myamalize anaanza kukutolea matusi na kejeli, jaribu kujenga picha ukimwambia nimeongea na FDRL wamekubali naomba uje tukae meza moja niwapatanishe unadhani ata react vipi? si ataingiza majeshi kabisa..............umekaa na maadui zake mkaongea? anaweza kuzusha lolote

Hakuna tofauti yoyote ya alichoongea JK na mapendekezo ya Dr Slaa
The issue was no room for negotiation with killers......huu ndio msimamo wa Kagame
Namuhakikishia Dr Slaa hata kama yeye kwasasa ndio angelikuwa Rais wa TZ na akafanya hayo anayoyasema JK afanye he will face the same fate from Kagame simply because there is no room for negotiation with killers

Lakini pia Dk labda sio kosa lake ni ufahamu mdogo wa mambo ya kimataifa na ndio maana anaanza kuingiza mambo ya Mwangosi, EPA nk.......This is something else Brother
Kagame ameongea upuuzi mara ngapi na viongozi wenzake, lakini JK alikuwa kimya. na angeendelea kukaa kimya tungesema mbona haongei chochote, ameongea tunaanza kuita majibizano

Jambo kubwa kwenye hili ni busara kubwa aliyotumia JK, Hatataki kuyaamini tunayoysikia lakini hatuta yapuuzia,
 
Kikwete alisomea wapi.Nina shahada 2 za uzamili.Nimezisotea kamwe sitawahi kutamka jina "Dr.Kikwete" hata kwa mtutu.
slaa amesomea wapi? Halafu na wewe msomi wa india unajisifu ni msomi wakati watu wananunua degree kama njugu huko india.acha zarau kijana wakati elimu ulio nayo ni ya kidosi.
 
kama kikwete aliongea kama msimamo wa nchi ya tanzania naamini alikosea coz ameingilia mambo yasiomuhusu. Pia kama alitoa tamko la AU yupo sahihi kabisa maana hawezi kuwa upande wa kagame au hao waitwao Fdrl. Mkuu wetu anatupa mzgo wa kutupiana mipa&ho na mtu wa nyumba ya pil kwakweli hatuna ma&ilah hapo labda kiu&alama kama yapo. Mtu hawezi kuja tz na kutueleza nn cha kufanya labda kam tumeomba m&ada &o &izani kama tuliombwa u&hauri
 
Slaa ameshindwa kukaa na Zitto na kumaliza tofauti zao. Ameshindwa kukaa na mke wake wa ndoa na kumaliza tofauti zao Halafu anakuja na kutoa ushauri njaa kwa amiri jeshi.
 
Hapana, kosa kubwa linalofanywa na pro-CCM ni kushindwa kusema hii siyo na hii ndiyo; Wewe kuwa Chadema na Dr. Slaa kuwa Chadema haina maana kwamba chochote atakachosema ni ndiyoooooo, litakuwa kosa la magamba hili. Labda magazeti au habari namna ilivyoletwa imepotoshwa. lakini ukweli ni kwamba ushauri wa JK hauna kosa kimantiki labda kimazingira. Marekani haiwezi kuzungumza na Al-qaeda ni kwa sababu kuu mbili. Kwanza Alqaeda ni mtandao wala si kikundi ambao haupo msituni wala mjini wala popote. 2. Nguvu za Alqaeda zimeshadhoofika sana, kwa hiyo marekani hana sababu ya kuzungumza na watu ambao tayari ni dhaifu. Lakini je? umepata kujiuliza kama Taliban ni nini? Ni Serikali au ni nini? Na kwa nini Marekani pamoja na huko nyuma kuitambua Taliban kama kikundi kinachosapoti ugaidi (na hivyo wao pia magaidi) hivi sasa kuonyesha nia ya kuzungumza nao? Halafu tukubali kwamba, Tanzania haiwezi kumshauri Marekani kwa sababu mgogoro wa Marekani na maadui zake hauiathiri Tanzania Directly kama namna mgogoro wa majirani wa Tanzania (Rwanda, Burundi) unavyoathiri Tanzania kwa kila nyanja. Mwita Maranya najua sote ni waathirika wa yule mama aliyeua Ukonga yetu lakini sitakuwa mtumwa wa kukubali kauli iliyokosa substance kwa kuwa tu ni chama kimoja. Hii ni tabia ya kulindana, tabia ambayo siku zote tunagombana na wana Lumumba humu JF.

Yaani wewe ndugu yangu mwanaukonga mwenzangu nimesoma hoja yako nilipoimaliza nikakuhurumia huenda hujui kinachoendelea duniani.

Jana Marekani imetangaza kufunga ofisi zake za balozi zipatazo 21 katika nchi za Afrika Kaskazini pamoja na Middle East kufuatia kitisho cha mashambulizi ya Al Qaeda. Sasa sijui unaizungumzia al qaeda ipi iliyodhoofika lakini hapo hapo inaweza kuwa kitisho kwa nchi kubwa super power kama marekani hadi inaamua kufunga balozi zake.

Kwahiyo ndugu yangu hoja yangu iko palepale kwamba Kikwete angekuwa muungwana sana kama angetoa ushauri ambao yeye mwenyewe ana u-practice. Wananchi wa Mtwara tu ameshindwa kuongea nao na kuwatumia batallion ya JWTZ sasa huo uungwana/huruma kwa majirani zake ameutoa wapi?
 
slaa amesomea wapi? Halafu na wewe msomi wa india unajisifu ni msomi wakati watu wananunua degree kama njugu huko india.acha zarau kijana wakati elimu ulio nayo ni ya kidosi.

Kama kununua ni rahsi kihivyo mbona wewe umeshindwa kununua?
 
Dr.slaa kama wewe uliweza kumuiba Josephine Akiwa mke wa mtu, wanjanja nao watakuibia uanze kulalamika Kama kagame. Funga domo Lako slaa na acha upuuzi na lugha za kizembe kwa amirijeshi mkuu. Indoa njaa zako na endelea kumbaka mke aw watu.
 
Hakuna kigeni hapo, Marekani amemshauri Karzai aongee na Tarbani na sasa wanafanya hayo maongezi huko Doha. Sasa nini kosa la Kikwete kumshauri Kagame afanye hivyo. Diplomasia ya Kikwete inaingia akilini kwa mantiki ya kuwa hawa watu wamekuwa wakiuana kwa muda mrefu bila mafanikio kama huko Afghanistan. Unadhani Wahutu waliowengi Rwanda wana raha au wanaunga mkono yanayofanywa na Kagame, la hasha isipokuwa hawana jinsi kwani nguvu yote ya serikali ipo kwa Wtusi walio wachache. Fikiria katiaka kuzuia mauaji ya Kimbali Kagame aliua Wahutu wangapi? Huwezi kuwa na action plan kama mtu hajawa na nia ya kutaka maongezi, yabidi akubali kwanza and then mnaangalia jinsi gani ya kuendesha hayo mazungumzo, mfano mzuri ni wa Kerry, amewashawishi Wapalestina na Waizlaeri kuongea na sasa wanaweka utaratibu wa jinsi gani ya kuendesha maongezi na mambo gani yanayopaswa kuwepo katika maongezi. Kikwete yupo, sasa hihi tu, tatizo ni kwamba watoto hatuna nidhamu, mamako ukimkuta na mwanaume wa nje hata kama ni dhahiri huwezi kuthubutu kumuita Malaya kwakuwa ni mamako, na huyu ni Rais hata kama hukumchangua ni Rais wa nchii yetu na ni Kichwa cha nchi, zote twapaswa kuwa nyuma yako kuhusu masuala mazito ya kitaifa hata kama anakosea anatakiwa asikosolewe hadharani, tuwe wazalendo hata kama Mzee anakwenda kombo, nchi yetu hii

Kinadharia ushauri wa Kikwete unaweza kuonekana kama mzuri lakini haukuwa na action plan au road map ya utekelezaji kushauri bila action plan ni sawa na kuropoka hasa unapomshauri mkuu wa nchi nyingine.

Kama Kikwete ataanzisha vita na Kagame binafsi nitakuwa wa mwisho kwenda vitani, kwa sababu naamini Kikwete hakuwa sahihi kuwaambia Rwanda wakutane na waasi alichotakiwa ni ku-mediate mkutano kwa kuwakutanisha mahasimu na sio kuwaambia wakutane, kwanza wakutane wapi na nani awe mlalamikaji na mlalamikiwa.
 
CCM otewalipo + Kikwete + Mwiguru =janga la taifa
Vijana wa bavicha siku moja slaa atawambia mle tope mtakula kwa sababu mnamwabudu hata akikosea nyie mnaona yuko sawa kwa hilinbabu kachemka,kwani wapi jk alitangaza vita,haya matoto ya bavicha yanatumika vibaya hata kufikili hayawezi tena.
 
Wewe mtu usiyeshaurika leo ndio unazungumzia umuhimu wa kuomba msamaha?!!!

By the way, kwenye swala hili unajiabisha tu. Watanzania hawako radhi kulaghaika na porojo zako, wakati wamesikia maneno aliyoyatoa Kagame juu ya nchi yetu na Rais wake. Kama una deal na Kagame basi jua umeshapotea. Wewe na rafiki yako Kagame wote tutawadefeat...

Kagame ni muuaaji, hujui hilo?

Lini uliomba appointment na Rais kujadili swala la kitaifa ukakataliwa?

Tuondolee unafiki wako hapa hivi vita ikitokea utabeba silaha kwenda kupigana wewe?Au unajifanya Mzalendo hapa JF tu?Dr Slaa amekosea wapi?Aliichokiongelea ni kama tahadhari tu kwamba kauli za kiuhasama za Viongozi hawa zisije zikatuingiza katika vita kamili akimlenga zaidi Rais ajitathmini upya kutokana na kauli zake.Na hata hapa sioni kama kabadili msimamo wake isipokuwa tu umetoa ufafanuzi wa kina juu ya Uzalendo wake kwa Tanzania maana kuna Magamba walishaanza kupotosha kauli zake kwasababu zao za kisiasa.
 
Back
Top Bottom