Dr Slaa,
Mimi sileti ushabiki mzee wangu,ninachojaribi kukweka sawa hapa ni kwamba kuna mambo ya msingi ambayo sisi kama taifa tunatakiwa kuwajibika regardless tuna yetu ya ndani ambayo tunaweza kuyatatua muda wowote,au kwa maana nyingine mtoto huwezi kususa na kuacha wajibu wako wa msingi wa kulinda nyumba,kuua nyoka anayehatarisha usalama wa nyumbani,au kwenda machungani eti kwa sababu,eti kwa sababu baba ni mlevi-anatumia pesa yote aliyopata mnadani/gulioni kulewea,au huwezi kutoboa ngalawa unayosafiria eti sababu nahodha amekutusi 'two wrongs don't a right'.
Alichokifanya JK ni kujaribu kutoa suggestion tu,katika kujaribu kuokoa nyumba ya jirani inayowaka moto(nadhani hata ukilala njaa,ikitokea ajalia ya moto kwa jirani huwezi kukaa bila kusaidia eti kwa kuwa umelala njaa,lazima utoe msaada hata wa mawazo tu).
Lakini matusi aliyeyatoa PK ni dhahiri huyu mtu ni mshari,ametumia nguvu kubwa mno kujibu swala dogo kwa jazba kubwa,sasa hapo umeona anaashiria nini huyu kama sio chokochoko za wazi.hana nia nzuri huyu na usalama wa maziwa makuu huyu nyoka,na akitoka Kivu atakuja Kigoma akiendelea kuchekewachekewa.
Mimi ni Chadema damu, lakini sibezi mafanikio yaliyofikiwa na CCM maana huwezi kusema hawajafanya kitu kabisa,vilevile siwezi kuacha kulaani usafirishaji wata wanyama pori,ufisadi wa ccm amabo wewe ndio uliyeuibua na kutujuza watanzania wote,rushwa katika vyombo vya serikali kama police,police kutumia nguvu kupita kiasi,usafirishaji wa madawa ya kulevya ulioibuka n.k.LAKINI LINAPOKUJA SWALA LA KUSHAMBULWA KWA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MTU WA NJE,IWE KWA RAIA,IWE KWA KIONGOZI,IWE KWA JK,IWE KWA DR.SLAA,sitaangalia mapungufu aliyo nayo mtu huyo, nitashika mtutu kumshambulia adui kwanza,nikimalizana nae ndipo narudi kumwambia ndugu yangu-mtanzania huyo kuwa aliteleza kama ameteleza kweli na siku nyingine asirudie.
Hata wewe mathalani siku ukiwa magogoni pale,ukakwaruzana na mtu yeyote wa nje,nitakutete kwa nguvu zote bila ya kuhoji umefanya kosa lipi,halafu baadae ndipo nitarudi kwako na kukuuliza umefanya nini,lakini wakati huo adui atakuwa tayari keshakiona cha mtema kuni.
Mwisho angalia attachement ya UN inavyoonyesha kwa ushahidi PK yupoje
Asante mzee kwa uungwana wako wa kujibu ,nisamehe kama nilitumia lugha kali kidogo maana nilihamaki,lakini Mungu ibariki Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Kusema ukweli
Nyamafu,
Hapo ndo umeona JK amekaa anajadiliana na Upinzani. Ushabiki umelewesha kiasi cha kutoelewa kila kitu kina mazingira yake! Hayo yalikuwa matembezi ya Hiari ya CCBRT na CCBRT ni chombo cha huduma kwa walemavu. Tunachoxungumzia hapa ni lini JK kakutana kujadili mgogoro na wapinzani wake na hapa ninamaanisha Chadema. Kikao pekee ni cha Kujadili Katiba Mpya, ambako hata yaliyojadiliwa hakuyatekeleza ilivyokubaliwa
Mkuu sema kweli kisa kinachokufanya uichukie CCM kwa kweli visa ni kwamba
1. Ufisadi(ujangili,wizi,uporaji,ulanguzi,uhujumu uchumi,mauaji,utesaji,wapiga dili) mfano madini(almasi,Dhahabu,tanzanite coper nk) yanapigwa dili kwa kigezo cha uwekezaji/twiga wameporwa njenje kweupe wakapanda lidege la kijeshi Quartor kwenda Doha,Tembo/kifaru wanaelekea kupotea katika ardhi ya tanzania badala ya kupambana na hali hii ccm iko busy kuiangamiza chadema ili inchi hii ipigwe dili la kufa na kupoa. Jamani tulikatae hili watanzania tupambane kuiondoa ccm ccm ni adui No.1 Tanzania.
2. Watanzania tukae macho tutambu7a uhuni unaofanywa na majangili ya ccm leo yanapita mitaani yakihubili udini na ukanda Niwaombe watanzania kwamba leo tunataza na kushangilia pale tunaposikia viongozi(majangili) ya ccm yakihubili udini bila kutafakari kwamba siku limebuma wote ni wahanga isipokuwa majangili(ccm) yenye mipesa uswizi na ulaya .Hivyo tukatae kwa nguvu zote.
3. Dalili za hili ni nyingi sisi waislam tuposhap sana tunaposikia na kuhubiliwa udini hatulazi damu wote hujingiza mkenge upande ambao shehe anahubili. Hili naliona si zuri ni lazima watanzania tutafakari mahubili yanayokuwa yanafanywa na wanasiasa hususani ya ccm Tafakari kabla ya kuchukua hatua . Mara nyingi sana tumekosea kwa kusikiliza na kuamini maneno ya udini yanayosambazwa na ccm kwa lengo la kuifight chadema. hapo mwanzo walitumia njia hi hi kuifight CUF
4 Leo wanaanza kutumia vijana kwa kuwateka na kuwanunua wakachafue mikutano ya chadema.