Naungana na Dr Slaa na watanzania wote wanaopenda amani na majirani zake. Aidha, sikuiona busara ya Rais Kikwete kumtaka hadharani Rais Kagame na Rwanda kuzungumza na wauaji wale. Wengi wetu humu hamjui uzito wa kilichotokea mwaka 1994 ambapo mpaka leo watu 1 millioni wahakuweza kuwa accounted for. Katika nchi yenye watu 10 million, hiyo ni idadi kubwa mno na ni kubwa hata hivyo kwa standard yoyote. Nadhani Rais wetu angeweza tu kuongea na Kagame kwenye mikutano yao ya ndani uwezekano wa kukaa na wale nk. Rwanda ni nchi ndogo sana na Tanzania ambapo pia wanaishi Wanyarwanda wengi tu mpaka ndani ya seriklai na majeshini, hakuna haja ya ugomvi. Tofauti ingekuwa kama wanataka meter kadhaa ya ardhi yetu. Nadhani Rais wetu ashughulike zaidi na matatizo ya ndani Tanzania na umasikini wa watanzania walio wengi kuliko hilo la Rwanda. Kwangu anaona ni ku divert attention juu ya matatizo ya ndani na serikali yetu kuwa adiu wa raia wake. Kwangu adui ni Malawi anayetamani ziwa letu la Nyassa. Hakuna haja ya Tanzania kuwa na uadui na jirani. Ukimgusa Kagame, unamgusa Museveni. Hilo yujue. Kenya atasimamia pale maslahi yake yatakapokuwa pindi vurugu zikitokea. Congo na wacongo wala haitabiriki na kwa hiyo sio wa kutilia maanani sana. Kule Congo kuna Wanyarwanda kama milioni 5, na Rais Joseph Kabila pia ni Mnyarwanda kwa hiyo lolote laweza kutokea. Watanzania tuwe waangalifu sana na ukanda huu wa maziwa makuu. Kuna mambo mengi yaliyojificha. Tujenge Tanzania na tudumishe ujirani wetu. Kama Kikwete binafsi na tatizo na Kagame binafsi wayamalize wenyewe. Vita ya Kagera 1979 bado inaumiza Tanzania na sio jambo jema kupigana bila sababu. Wamarekani wasitutumie kwa maslahi yao. Asanteni.