Huu uzi unaonesha umuhimu wa kuangalia siasa za ndani na maslahi mapana ya nchi. Tuchukulie mfano mzuri Marekani, ndani ya mwezi mmoja wamekuja marais 3 Tanzania, na marais hawa wanatoka vyama tofauti. Wanaweza kuja kwa mgongo wa taasisi zao za kusaidia watu lakini hapo hapo kwenye kujenga mazingira mazuri kwa nchi yao kufaidika kwa kuwa karibu na Tanzania.
Linapokuja swala la maslahi ya taifa kama hili la DRC na Rwanda tulitakiwa (kama taifa) kuwa na kauli moja. Dr Slaa hakutakiwa kuongea hayo maneno hadharani. Lakini pia, nilitegemea katika sintofahamu inayoikabili Tanzania kwa kipindi hiki, basi viongozi wa juu toka vyama vikubwa vya siasa nchini wangekutakana na kuwekana sawa kuhusu 'Tanzania'. Kama ni ushauri wangepeana humo ndani lakini nje ya nchi lazima tuwe kitu kimoja.
Kagame amefanya kazi kubwa kuinua nchi yake, lakini Kagame ana upande wa pili ambao ni 'shameful' kwa Afrika. Miaka nenda rudi sisi Waafrika tumekuwa tunalalamika kuwa machafuko yanayotokea barani kwetu yanafanywa na wazungu ili waibe rasilimali zao. DRC imakuwa ni kielelezi cha jinsi gani sisi Waafrika ni wanafiki. Kagame anang'aka, si kwa sababu kaambiwa aongee na wabaya wake, lakini anajua msimamo wa Tanzania kuhusu DRC unamuumbua. Angalia pato la taifa la Rwanda lina nini ndani yake? wana-export madini bila aibu, na sasa anajua Bandari ya Dar itakamata madini yake amekimbilia Kenya.
Na iweje Kagame hakumjibu Kikwete pale pale kwenye kikao badala yake ameenda kupiga kelele nyumbani kwake? Huo ujasiri anaotamba kuwa nao aliusahau wapi siku hiyo ya kikao?