Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Nyie sijui
Fitinamwiko na menzio mzizimkavu ndio huwa mnawachagulia Watanzania nani awe Rais wao? Au ndio ulevi umeanza acheni ujuha usiokuwa na maana
Kusema maoni yangu ni kutekeleza uhuru wangu kama vile wewe unavyotoa ya kwako. Nilipinga na Napinga kitendo cha Nyerere kutupangia Nkapa then JK kuongoza Tanzania. Imani yetu kwa Mwalimu ndiyo imetuingiza katika haya majanga ya Ufisadi na madawa ya kulevya. Tuna watanganyika wengi na wazuri, let us give them a chance
 
Wanasiasa kama wewe ni hasara tupu kwa Taifa. Rais hajachukua hatua kuhusu mauaji ya Mwangosi kwani hujui kama kesi ipo mahakamani? Unajifanya kusikitika mauaji ya Mwangosi wakati wewe ndio chanzo.[/QUOTE]

Ok! Vipi kuhusu mabomu?? Hakuona umuhimu wa kuongea na hasimu wake kabla ya kutuma kikosi cha mauaji??haya ya mazungumzo yana fit upande wa rwanda tu? Mwangosi aliuliwa na polisi mbele ya kamanda wao!au sio? Dialogue haikuwepo miaka hiyo? Mtwara wanataka tu kujua manufaa ya gesi itakayopatikana kwao!jibu ni mazungumzo rahisi tu ya kuwaelewesha wana mtwara A B c ,badala ya majibu wamepelekewa jeshi la wabakaji wauaji!!! Na wewe umeona ni sawa tu?????eti?
 
Duuh.. kweli this's too low coming from u MziziMkavu.. Maana according to ur bandiko hapa Dr. Slaa amesema haoni busara kwa kauli ya JK kumuambia PK azungumze na magaidi wakati huku anashindwa kulifanya lile analolishauri kwa mwenzie.. Unaita huko ni kukosa uzalendo..? Hivi kweli kichwa cha habari kinaendana na maudhui..?
Mzizi Mkavu anaunyemelea u DC kaambiwa kutakuwa na mabadiliko ya ma DC hivi karibuni! uroho mbaya ona sasa unauza mpaka utu wako!
 
Wanasiasa kama wewe ni hasara tupu kwa Taifa. Rais hajachukua hatua kuhusu mauaji ya Mwangosi kwani hujui kama kesi ipo mahakamani? Unajifanya kusikitika mauaji ya Mwangosi wakati wewe ndio chanzo.[/QUOTE] Su unaposema kuwa Chanzo ni Dr. Slaa unamaanisha kuwa Lile Bomu lilitoa uhai wa Mwangosi lilifyatuliwa na Dr Slaa ? Ficha Upumbavu wako
 
Mzizimkavu,

(This is too cheap. Kumbe kukosoa udhaifu ni kuunga mkono upande wa pili! Wenye kujua principles watanielewa. Ukifanya makosa lazima tutakuambia, ndio maana wakati wa EPA tuliwasema hadharani, bila kumumunya maneno. Wangapi wakati ule walituunga mkono! Tusingelikuwa majasiri tungekata tamaa. Tulishikilia, na hata sasa ninaamini kauli ya JK haina uhusiano na kuunga mkono upande wa pili! Hata wakati wa EPA tuliambiwa hatuna uzalendo, tunaaibisha Taifa, oh tutakosa misaada, oh! Oh! Oh, Taifa lisilo na watu wenye principle au misimamo linaenda kaburini.)
Mzizimkavu,

Ni ukweli kwamba pande zote mbili kuna tatizo, Kikwete anatatizo la kuropoka hovyohovyo mmbo yake bila kujipanga, lakini Kagame amekosea sana namna alivyolihandle hili swala. Pamoja na kwamba haya mambo yanaweza kutatuliwa kidiplomasia, lakini kwa namna moja au nyingine hili swala litawacost sana wanyarwanda na rwanda kwa ujumla. Inawezekana Kagame amekuwa akitoaa matamko yake out of frustration, lakini ameonyesha dharau ya hali ya juu kwa Tanzania. Hapaa ndo penye tatizo.
 
Wanasiasa kama wewe ni hasara tupu kwa Taifa. Rais hajachukua hatua kuhusu mauaji ya Mwangosi kwani hujui kama kesi ipo mahakamani? Unajifanya kusikitika mauaji ya Mwangosi wakati wewe ndio chanzo.
Su unaposema kuwa Chanzo ni Dr. Slaa unamaanisha kuwa Lile Bomu lilitoa uhai wa Mwangosi lilifyatuliwa na Dr Slaa ? Ficha Upumbavu wako[/QUOTE]
Upumbavu mwingine haufichiki mkuu.
 
kama kweli slaa unamuunga mkono kagame katika hili basi jua unapotea,jkbalichofanyavni kutoa ushauri tu na ushauri unaamua mwenyewe kuuchukua au laa sasa tatizo liko wap?
slaaa unapotea.
 
Ni kawaida mpinzani siku zote kukosoa kwa kila jambo kwa hilo sishangai
 
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli yake ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake ...

Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo.

Slaa aliyasema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

"Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani na hajachukua hatua dhidi ya wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi...

"Alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda na badala yake amempandisha cheo," alisema Slaa.

Kauli Dk Slaa imekuja siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza kuwa Tanzania haina mgogoro na nchi ya Rwanda, kutokana na kauli za kejeli na matusi zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa nchi hiyo dhidi yake na Tanzania.

Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kuitaka Rwanza imalize ugomvi na waasi kwa njia ya mazungumzo ya amani...

Rais Kikwete aliutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.

Kitendo cha Dr Slaa kumkingia kifua Kagame kinatia shaka uzalendo wake na chama chake kwa taifa hili ...

Sote tumekuwa tukishuhudia matusi ya Kagame dhidi ya Tanzania.Iwaje Rais Kikwete aonekane mbaya kwa kumjibu Kagame, tena kwa lugha ya kizalendo??

Kagame amekuwa akituhumiwa na jumuiya mbalimbali za kimataifa kwa kutoa misaada ya kivita kwa waasi wa M23 ambao wamekuwa wakiua raia na kuwabaka wanawake....

Kauli ya Dr Slaa ina mambo mengi yaliyojificha na huenda yeye na chama chake ni wafuasi wa karibu wa M23 kama ilivyo kwa Kagame.

Kuwa mpinzani, haimaanishi ukosoe kila kitu.

chanzo.
WANYARWANDA WAANZA KUREJEA MAKWAO BAADA YA RAIS KIKWETE KUWAPA SIKU 14 ZA KUONDOKA
UKWELI NI HUU

ASEMA HERI KUPATANISHA KAGAME NA WAASI KULIKO KUTAKA ‘WAYAMALIZE'KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema Rais Jakaya Kikwete alipaswa kuwapatanisha Rais Paul Kagame na waasi wa FDLR badala ya kumtaka rais huyo wa Rwanda akutane na waasi hao, jambo ambao limeibua hisia hasi na kuhatarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Alisema haoni mantiki ya Rais Kikwete kumtaka Rais Kagame akae na wafuasi wa FDLR, wakati yeye mwenyewe ndani ya nchi yake akishirikiana na Waziri Mkuu wake, Mizengo Pinda, wameviagiza vyombo vya dola kuwapiga wapinzani.
"Rais Kikwete anakosa mamlaka ya kimaadili ya kumwambia Kagame atekeleze kitu ambacho yeye mwenyewe hatekelezi nchini kwake. Yeye alipaswa kumwita Kagame na waasi ili awapatanishe. Ni vigumu kuwaambia watu waliopigana na kuuana kaeni meza moja mzungumze. Badala yake yeye, kama alikuwa na nia njema, angewaita na kuwapatanisha," alisema.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam baada ya kutakiwa kutoa maoni yake juu ya hotuba aliyoitoa Rais Kikwete juzi. Alisema uhusiano wa Rwanda na Tanzania unapita katika kipindi kigumu kutokana na viongozi hao kutoleana maneno yasiyofaa.
Dk. Slaa alisema Rais Kikwete hivi sasa anapaswa kukutana na Rais Paul Kagame wazungumze na kumaliza tofauti zao ili kuepusha nchi zao kuingia kwenye vita.
Alisema kama viongozi hao hawatachukua hatua madhubuti na maneno baina yao yakaendelea, kuna kila dalili ya kuzuka kwa vita baina ya mataifa haya mawili siku za usoni.
"Mimi sipendi nchi zetu ziingie vitani kwa sababu ya kauli za viongozi wawili, hapa tunazungumzia kushambulia na kushambuliwa, hawa marais wawili wangekutana kumaliza tofauti zao, maana wananchi wa mataifa haya ni ndugu," alisema.
Akitoa hotuba ya mwisho wa mwezi, Kikwete alisema: "Katika kipindi cha miezi miwili sasa hususan tangu mwishoni mwa mwezi Mei, 2013, uhusiano kati ya nchi yetu na Rwanda unapitia katika wakati mgumu. Kauli za viongozi wa Rwanda dhidi yangu na nchi yetu ni ushahidi wa kuwepo hali hiyo."
Katika hotuba yake ya juzi, Rais Kikwete alisema katika kipindi cha miezi miwili kuanzia Mei mwaka huu, uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda unapitia katika wakati mgumu kutokana na kauli za viongozi wa Rwanda dhidi yake.
Hata hivyo Rais Kikwete aliwahakikishia Watanzania kuwa serikali anayoiongoza inapenda kuwa na uhusiano mzuri na nchi zote jirani, kwa sababu kila mmoja anamhitaji mwenzake, hivyo lazima uhusiano na ushirikiano mwema uendelezwe.
Slaa apinga utoaji wa fedha
Katika mkutano wake wa ufunguzi kwa BAVICHA, Dk. Slaa alisema serikali imekuwa ikitoa fedha kwa Watanzania kama karanga badala ya kuwekeza kwenye ajira za vijana.
Alisema serikali imetumia zaidi ya sh bilioni saba kulipa posho na tiketi za ndege kwa ajili ya baadhi ya wageni waliotoka nje kuja kuhudhuria mkutano wa ‘Smart partnership' na tangu ufisadi huo ufanyike hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika.
"Rais wetu anagawa fedha za nchi kama njugu kujitafutia umaarufu badala ya kuwekeza kwa vijana ili kupunguza tatizo la ajira ambalo tumekuwa tukilizungumzia kila mara, uchumi wetu upo mahututi (ICU), lakini tunakubali kupoteza mabilioni kwa ajili ya kujipendekeza, Rais Obama alipokuja nchini tulipoteza pesa nyingi sana, lakini sisi Watanzania tumepata nini? Tujiulize.
"Rais wetu amewahi kutoa shilingi trilioni 1.7, siku tatu kabla ya kikao cha bajeti, kinyume kabisa cha utaratibu, lakini hao wameshazoea, na ndiyo maana mapendekezo ya CCM kuhusu rasimu ya Katiba mpya yanakataza uwazi na uwajibikaji," alisema.
Dk. Slaa alisema Rais Kikwete alitangaza kutoa sh bilioni moja kila mkoa, lakini mpaka hivi sasa watu waliozipata fedha hizo ni wachache kuliko kiwango kilichotolewa, jambo linalozua utata kuwa zimeishia mifukoni mwa wajanja wachache.
Awaasa vijana
Dk. Slaa alisema adui wa kwanza wa uchumi wa Tanzania ni elimu duni na vijana wamekuwa wakipata elimu hiyo ambayo imeshindwa kuwasaidia kujitegemea na kujiajiri.
Aliongeza kuwa Chadema wanahitaji kubadili mfumo wa elimu na kuufumua ili uendane na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, hivyo kufungua fursa za kujiajiri.
"Nawaasa vijana mfanye kazi kwa bidii, acheni kulalamika juu ya ugumu wa maisha, uongozi mbaya na mambo mengineyo yaliyopo kwenye jamii, vijana mmepata hasara kwa kutozingatia muda," alisema.
Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashariki, Dk. Kamilius Kasala, ameukosoa mpango wa kukuza pato kuelekea mwaka 2025, ambapo alisema matazamio ya serikali hayawezi kuwa na matunda ifikapo mwaka huo, kwakuwa takwimu zinaonyesha thamani ya fedha inazidi kuporomoka na kutengeneza uchumi tegemezi
 
napenda mabadiliko...naipenda tanzania sina budi kuunga mkono kauli ya rais wangu JK dhidi ya gaidi kagame...
pia kwa upande mwingine dr Slaa yupo sawa kwa jinsi nilvyo muelewa.

well said mkuu! Hapa kwenye ishu ya kitaifa huyu Slaa asituyumbishe kabisa!jitu linawaza tamaa ya madaraka tu!
 
kwa hyo yeye alitaka jk asuport vita iendelee hajui kama fdlc wengine hawakushiriki katika mauaji yale 1994,sijaona alichokosea jk katika hilo kwa kuwa ule ulikuwa ni ushaur tu.. na kwa kuwa slaa amekosa uzalendo hapaswi kuwa rais tegemezi wa 2015
 
ASEMA HERI KUPATANISHA KAGAME NA WAASI KULIKO KUTAKA ‘WAYAMALIZE'KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema Rais Jakaya Kikwete alipaswa kuwapatanisha Rais Paul Kagame na waasi wa FDLR badala ya kumtaka rais huyo wa Rwanda akutane na waasi hao, jambo ambao limeibua hisia hasi na kuhatarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Alisema haoni mantiki ya Rais Kikwete kumtaka Rais Kagame akae na wafuasi wa FDLR, wakati yeye mwenyewe ndani ya nchi yake akishirikiana na Waziri Mkuu wake, Mizengo Pinda, wameviagiza vyombo vya dola kuwapiga wapinzani.
"Rais Kikwete anakosa mamlaka ya kimaadili ya kumwambia Kagame atekeleze kitu ambacho yeye mwenyewe hatekelezi nchini kwake. Yeye alipaswa kumwita Kagame na waasi ili awapatanishe. Ni vigumu kuwaambia watu waliopigana na kuuana kaeni meza moja mzungumze. Badala yake yeye, kama alikuwa na nia njema, angewaita na kuwapatanisha," alisema.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam baada ya kutakiwa kutoa maoni yake juu ya hotuba aliyoitoa Rais Kikwete juzi. Alisema uhusiano wa Rwanda na Tanzania unapita katika kipindi kigumu kutokana na viongozi hao kutoleana maneno yasiyofaa.
Dk. Slaa alisema Rais Kikwete hivi sasa anapaswa kukutana na Rais Paul Kagame wazungumze na kumaliza tofauti zao ili kuepusha nchi zao kuingia kwenye vita.
Alisema kama viongozi hao hawatachukua hatua madhubuti na maneno baina yao yakaendelea, kuna kila dalili ya kuzuka kwa vita baina ya mataifa haya mawili siku za usoni.
"Mimi sipendi nchi zetu ziingie vitani kwa sababu ya kauli za viongozi wawili, hapa tunazungumzia kushambulia na kushambuliwa, hawa marais wawili wangekutana kumaliza tofauti zao, maana wananchi wa mataifa haya ni ndugu," alisema.
Akitoa hotuba ya mwisho wa mwezi, Kikwete alisema: "Katika kipindi cha miezi miwili sasa hususan tangu mwishoni mwa mwezi Mei, 2013, uhusiano kati ya nchi yetu na Rwanda unapitia katika wakati mgumu. Kauli za viongozi wa Rwanda dhidi yangu na nchi yetu ni ushahidi wa kuwepo hali hiyo."
Katika hotuba yake ya juzi, Rais Kikwete alisema katika kipindi cha miezi miwili kuanzia Mei mwaka huu, uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda unapitia katika wakati mgumu kutokana na kauli za viongozi wa Rwanda dhidi yake.
Hata hivyo Rais Kikwete aliwahakikishia Watanzania kuwa serikali anayoiongoza inapenda kuwa na uhusiano mzuri na nchi zote jirani, kwa sababu kila mmoja anamhitaji mwenzake, hivyo lazima uhusiano na ushirikiano mwema uendelezwe.
Slaa apinga utoaji wa fedha
Katika mkutano wake wa ufunguzi kwa BAVICHA, Dk. Slaa alisema serikali imekuwa ikitoa fedha kwa Watanzania kama karanga badala ya kuwekeza kwenye ajira za vijana.
Alisema serikali imetumia zaidi ya sh bilioni saba kulipa posho na tiketi za ndege kwa ajili ya baadhi ya wageni waliotoka nje kuja kuhudhuria mkutano wa ‘Smart partnership' na tangu ufisadi huo ufanyike hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika.
"Rais wetu anagawa fedha za nchi kama njugu kujitafutia umaarufu badala ya kuwekeza kwa vijana ili kupunguza tatizo la ajira ambalo tumekuwa tukilizungumzia kila mara, uchumi wetu upo mahututi (ICU), lakini tunakubali kupoteza mabilioni kwa ajili ya kujipendekeza, Rais Obama alipokuja nchini tulipoteza pesa nyingi sana, lakini sisi Watanzania tumepata nini? Tujiulize.
"Rais wetu amewahi kutoa shilingi trilioni 1.7, siku tatu kabla ya kikao cha bajeti, kinyume kabisa cha utaratibu, lakini hao wameshazoea, na ndiyo maana mapendekezo ya CCM kuhusu rasimu ya Katiba mpya yanakataza uwazi na uwajibikaji," alisema.
Dk. Slaa alisema Rais Kikwete alitangaza kutoa sh bilioni moja kila mkoa, lakini mpaka hivi sasa watu waliozipata fedha hizo ni wachache kuliko kiwango kilichotolewa, jambo linalozua utata kuwa zimeishia mifukoni mwa wajanja wachache.
Awaasa vijana
Dk. Slaa alisema adui wa kwanza wa uchumi wa Tanzania ni elimu duni na vijana wamekuwa wakipata elimu hiyo ambayo imeshindwa kuwasaidia kujitegemea na kujiajiri.
Aliongeza kuwa Chadema wanahitaji kubadili mfumo wa elimu na kuufumua ili uendane na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, hivyo kufungua fursa za kujiajiri.
"Nawaasa vijana mfanye kazi kwa bidii, acheni kulalamika juu ya ugumu wa maisha, uongozi mbaya na mambo mengineyo yaliyopo kwenye jamii, vijana mmepata hasara kwa kutozingatia muda," alisema.
Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashariki, Dk. Kamilius Kasala, ameukosoa mpango wa kukuza pato kuelekea mwaka 2025, ambapo alisema matazamio ya serikali hayawezi kuwa na matunda ifikapo mwaka huo, kwakuwa takwimu zinaonyesha thamani ya fedha inazidi kuporomoka na kutengeneza uchumi tegemezi
 
Dr.W.Slaa,

..u definetely need to do more research kuhusu mgogoro wa DRC kabla ya kuanza kuchukua upande wa Kagame au Kikwete.

..ningeshauri uwe na timu ya vijana wako wanaofanya kazi ya utafiti na kukupatia taarifa ya mambo mbalimbali.

..zaidi timu hiyo inatakiwa ukishauri kuhusu misimamo na mitizamo ambayo unapaswa kuchukua huku ukizingatia sera rasmi za CDM.

..I think u r doing too much. U have too much on your plate. kwa nafasi kama yako unahitaji timu ya wataalamu kukushauri, kukuelekeza, na kukuongoza, kwani masuala ambayo unashughulika nayo ni mengi.

cc😡Jasusi, Kitila Mkumbo, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Kosa kubwa la Rais Kikwete ni kutamka maneno hayo hadharani angeweza kumwita kagame wakaongea naye badala ya kukimbilia kutoa matamko hadharani ni kama anamwona kagame hana akili

na kweli kagame hana akili kama nyie mnaomtetea na akina slaa
 
Nimimi tu sielewi au? Kichwa cha habari hakina uhusiano na habari yenyewe
 
Dr.W.Slaa,

Mimi nadhani kwenye hili sakata la malumbano ya kagame dhidi ya Kikwete usilifanye la kwao, kwani nimeona hoja yako inaonyesha wazi kuwa malumbano hayo ni baina ya Kikwete (umeuvua uhusika wake kama kiongozi wa nchi) na Kagame.

Hili suala halipaswi kufanywa ni jambo binafsi la Kikwete, Dr Slaa unapaswa uelewe kuwa kikwete akitoka nje ya mipaka ya Tanzania ana kuwakilisha mpaka wewe huko ughaibuni, hivyo anapotokea mtu yeyote na kumkashfu au kumtangazia uhasama Kikwete basi ujue mpaka wewe umejumuishwa.

Ningependa kuona kwenye hili suala tushikamane kama watanzania na tuwe kitu kimoja, si vyema kuingiza tofauti zetu za kisiasa na kiitikadi kwenye mambo yanayo gusa usalama na ulinzi wetu, hapa ikitokea vita sidhani kama kuna mtu atakumbuka u-CCM au u-CHADEMA, ila utasikia watu tukililia taifa letu Tanzania.

Jambo lingine, Dr Slaa una mdhihaki kikwete kuwa ana jipendekeza kufatilia mambo ya watu wengine ilhali ya kwake yamemshinda, sidhani kama ulikuwa makini wakati ukieleza haya, ila angalau ungejisumbua kidogo kuzijua nafasi za kikwete zaidi na urais tu, ni mwenyekiti wa mambo ya usalama (SADC) kwenye nchi za kusini mwa Afrika, hivyo kushauri Rwanda ni sehemu ya majukumu yake, na hata wewe sidhani kama umezuiliwa kwenda kufanya majadiliano na Kikwete, kama amewahi kufanya hivyo wenda unaweza ukawa na hoja ya msingi.

Kwenye hili sakata, kwa hali ilivyo, ccm hakuna mwanasiasa makini anayeweza kushughulika na Kagame. Kikwete haliwezi! Tena wasijefanya makosa kumkabidhi mwigulu au nape, hawa ndo kabisa, ni vilaza tu. Hili swala wawakabidhi makamanda tu, kina Dr Slaa na Mbowe, uone kashikashi lake.
 
Utawezaje kuona boliti kwenye jicho la mwenzako wakati kwenye jicho lako hulioni. Mia
 
Hii ni trick thread kwa watu w pre-defined views, hii ni thread ambayo ni angle nyingi ya kutazama jambo.Watatokwa povu sana watu humu..watatukana wengine,watapinga wengine, watatamani hata kuwaua wengine.Ila kuna naman JK hakustahili jiingiza kwa staili ile, na kuna sehemu ya kuangalia sababu ya nchi kuingia vitani, na kuna sehmu ya kutazama reaction ya Kagame na kuna maeneo ya kuangalia kwanini viongozi wote wawe wajinga kiasi hiki..kwanini washindwe chukua hatua stahiki, kwanii hadi leo hawajaweza kuwa na mauzngumzo binfsi,hata ktk njia za kusoma , au hata ktk njia za jumuia ya africa mashariki, etc.

Kwa ujumla viongozi wetu wa africa bado ni shida, na bado wanaongozwa kwa fikra za kijuju za watu wa magaharibi.
 
Wanasiasa kama wewe ni hasara tupu kwa Taifa. Rais hajachukua hatua kuhusu mauaji ya Mwangosi kwani hujui kama kesi ipo mahakamani? Unajifanya kusikitika mauaji ya Mwangosi wakati wewe ndio chanzo.

Ok! Vipi kuhusu mabomu?? Hakuona umuhimu wa kuongea na hasimu wake kabla ya kutuma kikosi cha mauaji??haya ya mazungumzo yana fit upande wa rwanda tu? Mwangosi aliuliwa na polisi mbele ya kamanda wao!au sio? Dialogue haikuwepo miaka hiyo? Mtwara wanataka tu kujua manufaa ya gesi itakayopatikana kwao!jibu ni mazungumzo rahisi tu ya kuwaelewesha wana mtwara A B c ,badala ya majibu wamepelekewa jeshi la wabakaji wauaji!!! Na wewe umeona ni sawa tu?????eti?[/QUOTE]

Mwangosi aliuwawa na polisi ndio, lakini mwenye uwezo wa kutoa hukumu ni mahakama na siyo Kikwete. Kama mahakama itaona Kamuhanda anahusika basi itampa hukumu. Huo ndio utawala wa sheria. Rais hawezi kufanya maamuzi kwa sababu tu eti Chadema mmesema. Mahakama zipo zitafanya kazi yake. Ni upuuzi kusema Kikwete katuma kikosi cha mauaji kurusha bomu bila kuwa na ushahidi. Ningewashauri wewe na Chadema kama mna ushahidi fuateni misingi ya kisheria mpeleke huko ushahidi wenu ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria. Hizo porojo zenu za kusema tume ya kijaji hazina maana wala tija kwa taifa. Kabla hujailaumu serikali kuhusu Mtwara, jiulize kwanza ni uharibifu kiasi gani uliofanywa na vijana wa Mtwara kabla ya polisi na jeshi kuamua kutumia nguvu. Kudai haki hakukupi ruhusa ya wewe kuvunja haki ya mwingine. Yawezekana wananchi wa Mtwara walikuwa sahihi kudai haki yao ila njia waliyotumia siyo sahihi na ndio maana nguvu iliyowekwa kisheria imetumika.
 
Back
Top Bottom