Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

....Dr.Slaa yuko sahihi kabisa....naunga mkono kabisa hoja yake....watanzania tuache unafiki.....Ni unafiki mkubwa kujifanya unajali matatizo ya rais wa Rwanda na wapinzania wake....wakati nchini mwako TZ unawakandamiza wapinzani wako wakubwa kisiasa.....turejee matatizo yaliyopo TZ kati ya wapinzani wa JK na serikali yake (haswa chadema)...na tujiulize JK anayashughuikiaje matatizo yaliyoyopo kati yake na wapinzani wake kisiasa.....tuache unafiki wabongo...."charity begins at home"....
 
Sijawahi ona Padri mzandiki kama Dr Slaa! Anataka kutusahaulisha kuwa Rais Kikwete hakai na wapinzani wakati yeye dr slaa na viongozi wa chadema waliwahi kukaa ikulu kwa masaa 6 wakijadili namna ya kuunda mfumo wa kukusanya maoni ya kuunda katiba mpya kwa uwazi! Leo anasema Rais hawasikilizi wapinzani! Ee Mungu tuepushe kiongozi huyu asije akashika madaraka makubwa ya Taifa letu kwa mapenzi yako Mungu! Amen
 
namuunga mkono dr.slaa,kuna watu wanafiki kama .....na hata humu mtandaoni kuna wanafiki wengi sana kama mleta mada....
 
Never expecting such a low comment coming from Dr SlaaNi upuuzi kufanya cheap politics kwenye issues ambazo hazi hitaji siasaHivi Dr anadhani yeye hawezi kumshauri mtu kwenye mambo ya ndoa kwasababu ya mahusiano yake mabovu kwenye mahusiano yakeHivi Dr Slaa anajua JK alikua anaongea kama nani?Watu kama Ben Saanane wameonyesha ni jinsi gani wameshikiwa akili zao wala hawamaanishi wanachoongea zaidi ya kuongea wanavyopenda mabosi waoLabda nimkumbushe Dr Slaa kwamba waswahili wanasema kuchamba kwingi..................
Hapo mkuu naona ume hit a bull's EYE - well said "Kufanya cheap politics kwenye issues ambazo hazi hitaji siasa" Personally have a feeling Dr.Slaa & Co have no slightest idea how ruthless/dangerous M7 and PK are, these guys are capable of wreaking havoc in Eastern and Central Africa region at opportune time, don't U underrate their resolve....
 
Mr. man nafikiri kama nni shule pole sana. lkn tunajua si tatizo lako kwani ni pamoja na malezi yako. jaribu kuiga umakini kwa watu wengine kwani kwenda shule haikusaidia. kumbuka mbali unakaa vijiweni bado unaweza kunufaika ukibadiriha hiyo lugha yako ya mitaani. shame on you:

Wewe ndio uone aibu kwa kukubali kuwa upande mmoja na hawa mambulula waliokubali kutumika kwa kulipwa buku 7 tu kwa siku huku maharamia wanaowatumia wakichota matrilioni. Thamini Utanzania wako na kugoma kutumika kama msaliti dhidi ya nchi yako.
 
sio mbaya tutamchagua 2015 ili na yeye afanye maamuzi ya busara kama haya anayoyatolea ushauri.
 
ivi kweli mbulula kama huyu slaa anaweza fikia mahali akaitetea rwanda dhidi ya Tanzania? au kwakuwa 2010 kulikuwa na tetesi wanapata ulinzi toka rwanda kipindi cha kampeni? inawezekana slaa anatumika kuichafua amani,maneno ya Mwigulu hapa yanaanza kuleta maana kuwa huyu mzee ni chinjachinja,EWE MWENYEZIMUNGU ILINDE NCHI YETU,KWANI HATUNA PA KUKIMBILIA,SLAA ATAENDA KULIBERALIWA LONDON KWA RAFKI ZAO,AMEEN...
 
kwakweli captain huyu babu anaisaliti Tanzania kwa ajili ya tamaa za madaraka.

Wewe ni second mzizi mkavu,na wewe pia ulikuwa unaisubiri hii siku!! Imefika!! Enjoy!!namlaumu Dr slaa kujiingiza kwenye misa ya wafu.
 
Mkuu MziziMkavu, Kuna mtu ame temper na Detials zako za Kuingia JF ama ????!!!!! This is too low especially kwa Mtu Kama wewe. Hivi kwa Mfano kukawa na Ugomvi wa Ndani Baina yako na Mumeo lets say, na pia kuna Shoga yako naye ni Maswaibu kama yako. Lets say ukamshauri shaga yako akae Meza Moja na Mumewe wayamalize Mambo yao na shoga yako akawa Mbogo na Kutukana matusi ya Ndani. Akatokea Jirani yako na Kukwambia, "Acha unafiki, unamshauri shoga yako apatane na Mumewe ilhali wewe mwenyewe huna uhusiano Mzuri na Mumeo. Hivi hii itatafsiri kuwa Jirani yako anaunga Mkono Matendo ya Shoga yako ???????????? NB. Umeniudhi ndo maana nimetumia Mfano wa "Mumeo" na sio Mkeo
 
Last edited by a moderator:
Naanza kupata hisia kuna zaidi ya Kauli? Kuna nini nyuma ya Pazia wakati JK anaelekea kwa kauli yake tayari amenyoosha mikono yake!

UOTE=Rock City;6999326]

Dr. Slaa, tunatarajia kwa nafasi yako una-access ya mambo mengi kuliko haya unayoyaongelea hapa kwa juu juu....! Sidhani kwamba unaanza kupata hisia kuna kitu kiko nyuma ya hili, bali unajua kinachoendelea. Naimani hata leo wewe ungekuwa Rais wetu msimamo wa Tanzania kwa kile kinachoendelea Congo ungebaki hivyo, na hata Rais ajaye atakuwa na msimamo huo. Tumehangaika na Burundi, tumeyamaliza na sasa tunakaa na majirani zetu vizuri. Sasa majirani zetu wa Congo nao wanahitaji msaada, na ili kutoa msaada lazima chanzo cha fujo za Congo pia kishughulikiwe, na chanzo cha matatizo ya Congo ni proxy forces za Rwanda zinazokuja na majina mengi kila kukicha kwa kisingizio cha FDLR FOCA...! Sasa kuambiwa hadharani bila kificho ukweli kuwa ongea na FDLR iweje iwe nongwa.....? Inakuwa nongwa kwa vile ukimaliza tatizo la FDLR mambo ya visingizio vya Banyamulenge, CNDP, M23 na Raia Mutomboki yote yatakwisha na wananchi wa Kivu na nchi jirani waishi kwa amani na matumaini....! Kagame alijisikia vibaya mara tu baada ya Tanzania kukubali kuchangia battallion kwenye UN Intervention Brigade, kwa vile equation ilivyo ni kuwa M23 = RDF, kwa hivyo kupambana na M23 ni kupambana na RDF.....!
 
Mzizimkavu,

This is too cheap. Kumbe kukosoa udhaifu ni kuunga mkono upande wa pili! Wenye kujua principles watanielewa. Ukifanya makosa lazima tutakuambia, ndio maana wakati wa EPA tuliwasema hadharani, bila kumumunya maneno. Wangapi wakati ule walituunga mkono! Tusingelikuwa majasiri tungekata tamaa. Tulishikilia, na hata sasa ninaamini kauli ya JK haina uhusiano na kuunga mkono upande wa pili! Hata wakati wa EPA tuliambiwa hatuna uzalendo, tunaaibisha Taifa, oh tutakosa misaada, oh! Oh! Oh, Taifa lisilo na watu wenye principle au misimamo linaenda kaburini.



QUOTE=MziziMkavu;6999416]

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli yake ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake ...


Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo.

Slaa aliyasema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani na hajachukua hatua dhidi ya wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi...


"Alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda na badala yake amempandisha cheo,” alisema Slaa.


Kauli Dk Slaa imekuja siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza kuwa Tanzania haina mgogoro na nchi ya Rwanda, kutokana na kauli za kejeli na matusi zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa nchi hiyo dhidi yake na Tanzania.



Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kuitaka Rwanza imalize ugomvi na waasi kwa njia ya mazungumzo ya amani...

Rais Kikwete aliutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.


Kitendo cha Dr Slaa kumkingia kifua Kagame kinatia shaka uzalendo wake na chama chake kwa taifa hili ...

Sote tumekuwa tukishuhudia matusi ya Kagame dhidi ya Tanzania.Iwaje Rais Kikwete aonekane mbaya kwa kumjibu Kagame, tena kwa lugha ya kizalendo??


Kagame amekuwa akituhumiwa na jumuiya mbalimbali za kimataifa kwa kutoa misaada ya kivita kwa waasi wa M23 ambao wamekuwa wakiua raia na kuwabaka wanawake....


Kauli ya Dr Slaa ina mambo mengi yaliyojificha na huenda yeye na chama chake ni wafuasi wa karibu wa M23 kama ilivyo kwa Kagame.

Kuwa mpinzani, haimaanishi ukosoe kila kitu.

chanzo.
WANYARWANDA WAANZA KUREJEA MAKWAO BAADA YA RAIS KIKWETE KUWAPA SIKU 14 ZA KUONDOKA
[/QUOTE]

Wanasiasa kama wewe ni hasara tupu kwa Taifa. Rais hajachukua hatua kuhusu mauaji ya Mwangosi kwani hujui kama kesi ipo mahakamani? Unajifanya kusikitika mauaji ya Mwangosi wakati wewe ndio chanzo.
 
Mzizimkavu,

This is too cheap. Kumbe kukosoa udhaifu ni kuunga mkono upande wa pili! Wenye kujua principles watanielewa. Ukifanya makosa lazima tutakuambia, ndio maana wakati wa EPA tuliwasema hadharani, bila kumumunya maneno. Wangapi wakati ule walituunga mkono! Tusingelikuwa majasiri tungekata tamaa. Tulishikilia, na hata sasa ninaamini kauli ya JK haina uhusiano na kuunga mkono upande wa pili! Hata wakati wa EPA tuliambiwa hatuna uzalendo, tunaaibisha Taifa, oh tutakosa misaada, oh! Oh! Oh, Taifa lisilo na watu wenye principle au misimamo linaenda kaburini.



QUOTE=MziziMkavu;6999416]
Dr. Slaa nakubaliana na wewe kuhusu ugomvi huu. Japo napinga jina lako kupitishwa kugombea Urais 2015 kama ninavyopinga Lipumba, Lyatonga na Maalim Seif (you had your chance, its time for somebody else) Lakini umesema vizuri sana kuhusu hili. Mimi hapa JF nimeshaitwa majina yote mabaya kuhusu msimamo kama huu wa kupinga huo ugomvi wa Jikoni. Kwa mtizamo wangu, nilitegemea Mh JK angezungumzia ongezeka la kasi na la kutisha katika biashara ya madawa ya kulevya.



Nyie sijui
Fitinamwiko na menzio mzizimkavu ndio huwa mnawachagulia Watanzania nani awe Rais wao? Au ndio ulevi umeanza acheni ujuha usiokuwa na maana
 
Rock City,
Usiwadanganye Watanzania. Tishio la Tanzania halijadiliwi katika Mtandao. Ni muhimu Kama mtu huelewi jambo aka kimya. Kama kungelikuwa na Tishio la Watanzania kushikamana, kwa mujibu wa Katiba, Bunge japo Kamati ya Ulinzi ingelihusishwa. Pili Taifa kujulishwa juu ya Tishio Hilo. Hapo ungelizungumzia Uzalendo. Hapa tulipo tatizo ni kuwa Mambo yanajadiliwa kwa ushabiki, na kinachoonekana dhahiri nimkulinda " dhaifu" kwa udhsifu wake. Hamsaidii, mien mwenzenu ushauri mzuri. Narudia, nchi haitaenda vitamin tu kwa kauli ya marais wawili, ambao kimsingi wanajibizana wao. Simamia principle, mtu ukikosea na ulimi huteleza omba msamaha. Dhambi ni nini kuomba msamaha! Kwa hakika aliyejifanya mpatanishi kwa majirani wakati kwake kuna bomoka, safari hii kapatikana. Hakuna pa kujifichia. Nilikwisha sema, iwapo Kagame atashambulia Tanzania kwa ajili ya kiongozi mwenzake, watanzania kwa ujumla wetu tutanyanyuka na kuilinda nchi yetu. Naanza kupata hisia kuna zaidi ya Kauli? Kuna nini nyuma ya Pazia wakati JK anaelekea kwa kauli yake tayari amenyoosha mikono yake!

UOTE=Rock City;6999326]

Akili yako ni nzuri kweli we mzee?
 
dr naomba unijibu kwa nn huoni busara katika ushauri wa jk!Ni mazingira ambapo ulitolewa au ushauri wenyewe!!na je kama ni ww,ungetoa ushauri gani kwa kagame kuhusu waasi!?
 
Yericko, soma makala hadi mwisho. Naona unamshambulia mleta habari na si mwandishi wa habari.


Tena Ajabu Dr Slaa kajibu vema na kuweka sawa,
kinachomfanya yy kuja juu kwa lugha za matusi na hasira utadhani katukanwa au kakashifiwa yeye nini?
Kuna vijana wanajipendekeza ndan ya chadema na kwa viongoz utadhani waungu wao,tena kwa sababu zisizo za msingi na maana,
kichefu chefu sana
 
Wewe ndio uone aibu kwa kukubali kuwa upande mmoja na hawa mambulula waliokubali kutumika kwa kulipwa buku 7 tu kwa siku huku maharamia wanaowatumia wakichota matrilioni. Thamini Utanzania wako na kugoma kutumika kama msaliti dhidi ya nchi yako.

Mr. man ningekuwa na uwezo pamoja na ruhusa ningependa kujua elimu yako au IQ yako lkn haiwezekani. Lkn basi hata hivyo ninaona tunavyoendelea na mjadara huu utabadirika tu. Sitaka tamaa nitakusaidia hata ikiwezekana ili niweze kuongeza IQ yako. Nafikiri unaanza kuelewa maana yake. Karibu sana
 
Ingekuwa busara viongozi wa vyama wakakaa kimya kwenye hili suala na kuwaachia viongozi wa serikali, maana hili suala la kitaifa zaidi.
 
Dr.W.Slaa,

Mimi nadhani kwenye hili sakata la malumbano ya kagame dhidi ya Kikwete usilifanye la kwao, kwani nimeona hoja yako inaonyesha wazi kuwa malumbano hayo ni baina ya Kikwete (umeuvua uhusika wake kama kiongozi wa nchi) na Kagame.

Hili suala halipaswi kufanywa ni jambo binafsi la Kikwete, Dr Slaa unapaswa uelewe kuwa kikwete akitoka nje ya mipaka ya Tanzania ana kuwakilisha mpaka wewe huko ughaibuni, hivyo anapotokea mtu yeyote na kumkashfu au kumtangazia uhasama Kikwete basi ujue mpaka wewe umejumuishwa.

Ningependa kuona kwenye hili suala tushikamane kama watanzania na tuwe kitu kimoja, si vyema kuingiza tofauti zetu za kisiasa na kiitikadi kwenye mambo yanayo gusa usalama na ulinzi wetu, hapa ikitokea vita sidhani kama kuna mtu atakumbuka u-CCM au u-CHADEMA, ila utasikia watu tukililia taifa letu Tanzania.

Jambo lingine, Dr Slaa una mdhihaki kikwete kuwa ana jipendekeza kufatilia mambo ya watu wengine ilhali ya kwake yamemshinda, sidhani kama ulikuwa makini wakati ukieleza haya, ila angalau ungejisumbua kidogo kuzijua nafasi za kikwete zaidi na urais tu, ni mwenyekiti wa mambo ya usalama (SADC) kwenye nchi za kusini mwa Afrika, hivyo kushauri Rwanda ni sehemu ya majukumu yake, na hata wewe sidhani kama umezuiliwa kwenda kufanya majadiliano na Kikwete, kama amewahi kufanya hivyo wenda unaweza ukawa na hoja ya msingi.

napenda mabadiliko...naipenda tanzania sina budi kuunga mkono kauli ya rais wangu JK dhidi ya gaidi kagame...
pia kwa upande mwingine dr Slaa yupo sawa kwa jinsi nilvyo muelewa.
 
Last edited by a moderator:
Mr. man ningekuwa na uwezo pamoja na ruhusa ningependa kujua elimu yako au IQ yako lkn haiwezekani. Lkn basi hata hivyo ninaona tunavyoendelea na mjadara huu utabadirika tu. Sitaka tamaa nitakusaidia hata ikiwezekana ili niweze kuongeza IQ yako. Nafikiri unaanza kuelewa maana yake. Karibu sana

Ichunguze kwanza yako kwa kutetea maharamia wanaoiangamiza nchi kila leo. Halafu kajifunze kuandika badala ya kuandika mjadara na kubadirika. Kama ungekuwa na elimu ya kweli usingeandika mjadara na kubadirika. Thamini Utanzania wako kwa kutetea nchi yako badala ya kutetea mafisadi.
 
Back
Top Bottom