Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Jamani,

Sikuwa na maana hakuna mwanamke fisadi. Kwa ujumla wanawake sio mafisadi kama sisi wanaume.

Kwa asilimia zaidi ya 90 ufisadi TZ unafanywa na wanaume.

Mkuu Mtanzania una hoja, ila jiulize wanaume wakishaiba wanapeleka wapi? Nani ndio wa kwanza kumsifia mwanaume anapofanikiwa? Tena sifa hizi ni continuous, multidimensional and importantly specific!
 
Wana JF tusiende mbali sana na original thread - shelukindo kulipua bomu la Dowans an Richmond.

Ngeleja, mbona umepotea njia?! unataka kutumbukia kwenye shimo walimotumbukia wenzako? na wewe ni fisadi? huwezi hata kidogo kusoma alama za nyakati?! nakusikitikia sana kama mafisadi wameshakurubuni kumbuka watakuacha peke yako.
yaani pamoja na report ya Dr. Mwakyembe na yote yaliyotokea leo unadiriki kusema openly kwamba serikali inataka kununua mitambo ya dowans (richmond)!

sitaki kukuambia ujiuzuru ila fikiria tu mwenyewe utoe uamuzi wa busara kwa faida ya nchi yetu.
 
Kwenye hili mimi nakubaliana na Ngeleja na naamini huenda ningelikuwa mimi pia ningelipendekeza kununua hiyo mitambo baada ya kuangalia options zingine zote ikiwemo suala la maintenance. Hiyo mitambo ingeweza kupatikana kwa bei ya chini sana kwasababu kwa hapo ilipo hao jamaa hawana uwezo wa kuipeleka kwingine kokote.

Lakini pia naelewa wasiwasi wa wana JF mbalimbali juu ya kuwatajirisha hao hao ambao wametuibia mwanzoni. Naelewa pia kwamba kununua mitambo kama hiyo kunaweza kukuletea matatizo makubwa sana kisiasa. Ila tu kwenye biashara unachoangalia ni value for money kwa upande wako na wala sio nani anakuuzia.

Ndio maana naona kuongoza Tanzania ya sasa ni balaa tupu, huenda tukaishia kuwa na viongozi wafuata upepo ili kukwepa mashambulizi ya kisiasa. Hakuna anayetaka kuitwa fisadi wakati hajafanya lolote baya kwa jamii.

Pole sana kijana Ngeleja, inabidi mkiamua kununua basi baraza zima la mawaziri lipige kura ili usije ukaingia pabaya hata kama una nia njema.
 
Malizia basi!

Kwa asilimia zaidi ya 90 ufisadi unafanywa na wanaume nyuma yao wakiwepo wanawake!

au unataka kusema asilimia 90 ya wanawake hawajaolewa? au hujajua ndoa mkuu

wanawake chanzo cha almost kila kitu wataalamu wanasema ni source ya uovu uwao wote! mi simo nimesikia hivyo. wanasema hakuna dhana ya mwanaue na kila anachofanya kama mwanamke hayupo!

Mkuu Waberoya,

Mali nyingi za wizi zinaenda kwa nyumba ndogo. Msiwalaume bure wanawake kwenye ndoa.

Mwisho mtasema hata watoto ni mafisadi kwasababu wanafaidi hizo pesa kutoka kwa baba zao.

Wanaume wanaiba kwa tamaa na ego zao na wala sio kwa kusukumwa na wanawake.

Wanaume Afrika tunachemsha sana, afadhali hao dada zetu.
 
Kwenye hili mimi nakubaliana na Ngeleja na naamini huenda ningelikuwa mimi pia ningelipendekeza kununua hiyo mitambo baada ya kuangalia options zingine zote ikiwemo suala la maintenance. Hiyo mitambo ingeweza kupatikana kwa bei ya chini sana kwasababu kwa hapo ilipo hao jamaa hawana uwezo wa kuipeleka kwingine kokote.

Lakini pia naelewa wasiwasi wa wana JF mbalimbali juu ya kuwatajirisha hao hao ambao wametuibia mwanzoni. Naelewa pia kwamba kununua mitambo kama hiyo kunaweza kukuletea matatizo makubwa sana kisiasa. Ila tu kwenye biashara unachoangalia ni value for money kwa upande wako na wala sio nani anakuuzia.

Ndio maana naona kuongoza Tanzania ya sasa ni balaa tupu, huenda tukaishia kuwa na viongozi wafuata upepo ili kukwepa mashambulizi ya kisiasa. Hakuna anayetaka kuitwa fisadi wakati hajafanya lolote baya kwa jamii.

Pole sana kijana Ngeleja, inabidi mkiamua kununua basi baraza zima la mawaziri lipige kura ili usije ukaingia pabaya hata kama una nia njema.

Sikubaliani kidogo na wewe kwenye hili kaka, Kuna watu humu walishasema bei ya kitu kipya kabisaa na kina waranty ya hata 5 years ni ya chini kuliko hilo limtambo walilonunua. Kwa sababu kina Ngeleja wakinunua huo halafu baada ya miezi miwili ukaharibika itakuwa ni too expensiv kutafuta wataalamu wa kuja kuutengeneza na ndio utaanza ufisadi mwingine wa kuajiri watu kutoka nje watengengeneze, na nje kwa kweli mara nyingine ni too expensive kutengeneza kitu na ni bora ununue. Wangechukua kitu brand new na chenye waranty kwa miaka kadhaa, kwamba ikiharibika wanatengenezewa bure. Gari BMW wanakutengenezea bure mpaka 50,000 miles ndio uwe mtambo mkubwa hivyoo. Hapo tutakula hasara nyinginee, hilo ni bomu linalosubiri kulipuka. Ukinunua tuu (umelala nalo)
 
Ngeleja anaonekana ana uwezo finyu wa kufanya maamuzi mazito kuhusiana na wizara yake. Uamuzi wake wa kununua turbines zilizokwishatumika kwa shilingi 70 billioni ni uamuzi wa kushangaza sana ambao ungelitia hasara kubwa Taifa. Si ajabu bei ya turbines mpya haitofautiani sana na hiyo bei aliyotaka kununulia mali za Rostam Aziz au hata ni ndogo. Pia Turbines mpya life span yake ni kubwa ukilinganisha na hizo ambazo zimekwishatumika. Sijui aliahidiwa kitu gani na fisadi RA mpaka afanye maamuzi yasiyo na maslahi kwa Taifa. Wizara imemshinda huyu naye inabidi JK amuondoe katika baraza la Mawaziri pamoja na Masha.
 
Kwenye hili mimi nakubaliana na Ngeleja na naamini huenda ningelikuwa mimi pia ningelipendekeza kununua hiyo mitambo baada ya kuangalia options zingine zote ikiwemo suala la maintenance. Hiyo mitambo ingeweza kupatikana kwa bei ya chini sana kwasababu kwa hapo ilipo hao jamaa hawana uwezo wa kuipeleka kwingine kokote.

Lakini pia naelewa wasiwasi wa wana JF mbalimbali juu ya kuwatajirisha hao hao ambao wametuibia mwanzoni. Naelewa pia kwamba kununua mitambo kama hiyo kunaweza kukuletea matatizo makubwa sana kisiasa. Ila tu kwenye biashara unachoangalia ni value for money kwa upande wako na wala sio nani anakuuzia.

Ndio maana naona kuongoza Tanzania ya sasa ni balaa tupu, huenda tukaishia kuwa na viongozi wafuata upepo ili kukwepa mashambulizi ya kisiasa. Hakuna anayetaka kuitwa fisadi wakati hajafanya lolote baya kwa jamii.

Pole sana kijana Ngeleja, inabidi mkiamua kununua basi baraza zima la mawaziri lipige kura ili usije ukaingia pabaya hata kama una nia njema.

Mtanzania-M,
Mie sidhani kama hilo ni tatizo. Badala ya Waziri kushughulikia huo UNUNUZI, heri awaachie TANESCO wenyewe wafanye huo ununuzi. Wao waje tu waangalie kama mkataba umefanywa bila ufisadi. Pia sijui kama unajua kuwa Mlodi Bernard kwa sasa yupo kwenye shirika linalosimamia matumizi ya fedha za serikali. Pia wanaweza kuchukua maoni ya watu kama "walimu wa UDSM, DIT, TCA, MTC etc" na kila atakayeweka maoni yake basi aweke sahihi yake. Heri kuwalipa hawa watu hata dola 10,000 kuliko baadaye kusikia zimeibiwa dola milioni 10,000.
Hii kitu kwenye ujenzi ipo sana. Uki-design daraja au jengo na hilo jengo likaanguka basi wahusika mna hali mbaya. Mtabebwa kuanzia Designer hadi wajenzi. Sasa ili kujihami hasa kwa kwa wale structure Engineers, huwa wanashirikisha watu wengi kuipitia na kuweka sahihi kwenye michoro. Likianguka basi itajulikana kuwa kulikuwa na sababu ambayo kwa wahandisi wote, hili jambo lilikuwa JIPYA. Hii ya kufanya MIKATABA ya SERIKALI inakuwa SIRI-KALI basi huanza kuleta UTATA. Kama mkataba wa mauzo utawekwa wazi kwa wabunge, waandishi wa habari kwenda kuuona hata kabla ya manunuzi, itapunguza au kuondoa kabisa UTATA huo.
 
Sikonge,

Kwenye hili unafikiri hao Tanesco watakubali tena? Hii imeshakuwa biashara kichaa, kila mtu anaikimbia.

Huyo kijana kapewa wizara ngumu sana kwa Tanzania ya leo.
 
Mkuu Waberoya,

Mali nyingi za wizi zinaenda kwa nyumba ndogo. Msiwalaume bure wanawake kwenye ndoa.

Mwisho mtasema hata watoto ni mafisadi kwasababu wanafaidi hizo pesa kutoka kwa baba zao.

Wanaume wanaiba kwa tamaa na ego zao na wala sio kwa kusukumwa na wanawake.

Wanaume Afrika tunachemsha sana, afadhali hao dada zetu.

Mtz.
Umeleta hoja nzuri sana inayonishawishi kuchangia ila nachelea kuvuruga mtiririko wa mada kuu.Laiti kama tungeanzisha thread nyingine ya kuangalia athari za matarajio ya kijinsia basi mjadala ungenoga kweli.
 
hana lolote huyu naye

miaka nenda rudio bado yumo tuu. I was so keen on hayo mabomu mimi nilitegemea mabomnu yafuatayo:

1) Mwanae wa kiume BARAKA kuzaa watoto wawili na dada yake

2) DEGREE feki ya baraka

HAMNA MPYA HAPO inawezekana ndio jua la bongo linamzidi huyu mzee
 
Kuna press conference au? Hayo mambo ya kuwaweka wawekezaji kwenye "tension and suspense" kunadhoofisha uwekezaji nchini!

Utafiti unaonyesha kwamba wawekezaji kwenye sekta ya madini hapa Tanzania ume-stagnate kwa karibu miaka miwili kutokana na hiyo kamati ya kuchunguza mikataba ya madini. Maana hawaelewi mwelekeo utaofuata baada ya hapo!

Ukichanganya na financial meltdown ndio kabisa, vijikampuni vidog vidogo vya exploaration vyote vimesimamisha shughuli zao na kupunguza wafanyakazi!

Masaki hujaacha bado kusimama nao hao jamaaa zako ambao mnakaa nao Masaki ?
 
Hivi kama Raisi yupo serious na kupiga vita Rushwa nk , mbona hili suala lina jirudia rudia, na hili ni shirika la umma kwanini mambo yake wajidai ni internal. Tatu kuzuia ni bora kuliko kutibu au huo msemo umebadilika siku hizi?
Tanesco: `Talks` with Dowans internal affair

2008-12-15 11:46:50
By Angel Navuri

The anticipated transactions between the government and the private power generation company Dowans for the acquisition of the latter`s gas turbines are an internal affair, according to the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco).

Tanesco Communications Manager Badra Masoud said in an exclusive interview with this paper at the weekend that the matter was still at the level of internal communication and details could not be made public yet.

``This is not the right moment to announce agreements reached so far, so just be patient and give time to the government to complete the negotiations,`` she pleaded.

When contacted for clarification on the secrecy in the matter, Energy and Minerals minister William Ngeleja said briefly that the national power utility firm (Tanesco) had all the information regarding the plan.

In September this year the government expressed interest in purchasing Dowans` turbines but it did not rule out the possibility of entering into another contract with the controversial Dar es Salaam-based power plant in the wake of the latest national energy crisis.

�Purchase or no purchase depends on various factors such as price, purchasing process and need.

We`re examining all options,`` noted Tanesco managing director Idris Rashidi in an interview earlier this year.

Tanesco`s statement was part of a clarification outlining intentions by the government to hire or make an outright purchase of the turbines from Dowans after the malfunctioning of gas-powered turbines operated by Songas knocked off 110 MW from the national power grid.

Dowans, of the United Arab Emirates, was discreetly drafted in to save the situation after Richmond Development Company Limited had failed to meet the deadline set to supply power.

The development touched off intense scrutiny over RDC\'s credibility and its ability to deliver on the sensitive project at a time of great need.

Dowans finally yielded the 100mw but at a time when heavy rains had resuscitated the hydro-power stations for Tanesco to supply enough of its own energy.

The government then directed Tanesco to terminate the previous contract for the 100 MW emergency power supply by Dowans, which inherited the deal signed by the controversial RDC.

The equally controversial contract between Tanesco and Dowans was terminated with effect from August 1, this year, after much legal wrangling.

The public power utility has an installed capacity of 1,212 MW, of which 562 MW is from hydro dams. Projections indicate that annual demand will rise to more than 1,100 MW by 2010.

Tanzania experienced massive power cuts in 2006 after prolonged drought caused a drastic decline in water levels at power production dams, necessitating the signing of the power purchase agreements with Richmond and subsequently Dowans.

The controversial transactions resulted in a scandalous implication and the resignation of immediate former Prime Minister Edward Lowassa and two senior cabinet ministers - Nazir Karamagi and Dr Ibrahim Msabaha.

SOURCE: Guardian
 
Bunge lashtukia Dowans

na Edward Kinabo

KAMATI ya Kudumu ya Nishati na Madini ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imefichua siri ya serikali kuanza mchakato wa kununua mitambo chakavu ya kuzalisha umeme kutoka kwenye Kampuni ya Dowans, kwa gharama ya sh bilioni 70.

Kutokana na kugundua nia hiyo ya serikali, kamati hiyo imekataa kuunga mkono uamuzi huo kwa kuwa utakiuka utekelezaji wa maazimio yaliyopitishwa na Bunge Februari 2008, kuhusu Kampuni ya Richmond na Dowans.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jana katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo, William Shellukindo, alisema juzi Desemba 14, 2008, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, aliitisha kikao cha dharura na kamati hiyo, kwa lengo la kutoa taarifa ya hali ya dharura kuhusu tatizo la umeme nchini.

Shellukindo ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, alisema Ngeleja alitoa maelezo juu ya uamuzi wa serikali kushiriki zabuni ya ununuzi wa mitambo ya Kampuni ya Dowans ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa megawati 10 za umeme, na kuomba kamati hiyo ibariki uamuzi huo.

Akiwa na mjumbe mmoja wa kamati hiyo, Chritopher ole Sendeka (Mbunge wa Simanjiro), Shellukindo alisema kamati yake imeshtushwa kupewa taarifa hiyo ikiwa ni siku mbili tu kabla ya zabuni hiyo kufungwa, Desemba 16, 2008.

"Kamati imeshtushwa kupewa taarifa ya maamuzi mazito ya serikali kama hayo ya kushiriki zabuni ya ununuzi wa mitambo ya Dowans siku ya Jumapili Desemba 14, 2008, ikiwa ni siku mbili tu kabla ya zabuni hiyo kufungwa (Desemba 16, 2008)," alisema Shellukindo.

Alisema kamati hiyo ilipata taarifa juu ya ununuzi wa mitambo ya Dowans mwanzoni mwa Oktoba 2008, ilipotembelea TANESCO lakini taarifa hiyo ilikanushwa na TANESCO.

"Kamati inashangazwa kuona suala hili la ununuzi wa mitambo ya Dowans likiibuka tena baada ya kamati kumshauri Waziri wa Nishati na Madini Novemba 7, 2008 mjini Dodoma, kuwa hatua yoyote ya kununua mitambo hiyo itakuwa batili na inakiuka maamuzi ya Bunge," alisema Shellukindo.

Alitoa msimamo kuwa, kamati yake haitapenda kujihusisha na uamuzi huo wa serikali kwani unavunja kanuni ya 53 (8) na 54 (4) za kanuni za kudumu za Bunge (toleo la 2007), ambazo zote zinakataza kurudiwa kwa mjadala wa jambo ambalo tayari lilishatolewa uamuzi na Bunge.

Alisisitiza kuwa, kamati yake haiwezi kubariki uamuzi huo wa serikali kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha Bunge ambalo lilishaagiza mkataba kati ya Richmond na serikali ambayo ilirithiwa na Dowans uvunjwe.

Alipoulizwa kamati yake itafanya nini ikiwa serikali bado itaendelea na azima ya kununua mitambo hiyo ya Dowans alisema: "Wakifanya hivyo tutakutana bungeni."

Alipoulizwa iwapo serikali ilikuwa haijui kama ni makosa kununua mitambo hiyo alisema:

"Kusema hawajui si sawa, wana kumbukumbu zote. Wana ripoti zote, ile ya Richmond na maazimio ya Bunge ambayo Waziri Mkuu alikuja akatueleza utekelezaji wa awali wa maamuzi hayo. Wakati mwingine unaweza kuficha utendaji mbovu kwa kufanya kila kitu kionekana kama kinatokea kwa dharura. Walikuwa wapi tangu Januari wasitafute njia nyingine mbadala?" alihoji Shellukindo.

Aliishauri serikali kuendelea kutafuta namna bora ya kushughulikia dharura hiyo ya umeme kwa mujibu wa sheria zilizopo ili kuiepusha nchi na maamuzi ya zimamoto ambayo uzoefu unaonyesha huliingizia taifa hasara kubwa kama ilivyoelezwa kwenye azimio namba 19 la kamati teule ya Mwakyembe.

"Kwa mfano sisi tuliwaambia kama mnataka megawati 10, tuna IPTL. IPTL inazalisha megawati 100. Wakatuambia kuna kesi mahakamani, nasi tukawaambia serikali iombe kibali mahakamani cha kutumia IPTL, kutokana na hiyo dharura wanayosema imetokea," alisema Shellukindo.

Aliikumbusha serikali kutekeleza maazimio yaliyopitishwa na Bunge Februari 2008 kuhusu Richmond na Dowans kama alivyoahidi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwenye hotuba yake ya utekelezaji wa awali wa maazimio ya Bunge ya Agosti 28, 2008, hasa azimio namba 18 lililotaka wamiliki wa Richmond Development Company LLC na Richmond Development Company (T) Ltd, wafunguliwe kesi ya jinai mara moja kwa udanganyifu na ujanja wa kuiibia serikali.

"Kwa kuwa suala hili bado linashughulikiwa na serikali na hatujui hatima na mipaka ya utekelezaji wake katika mahusiano ya Richmond na Dowans; kamati bado inaendelea na msimamo wake iliyokupatia waziri Novemba 7, 2008.

"Hali hii inaweza kusababisha mgongano mkubwa kati ya serikali na Bunge linalowakilisha wananchi na hivyo kuwafanya wananchi kukosa imani na serikali yao," ilisema taarifa ya maoni ya kamati hiyo kwenda kwa Waziri wa Nishati na Madini.

Naye mjumbe wa kamati hiyo, Ole Sendeka, alisema uamuzi huo wa serikali pia unakwenda kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma ambayo hairuhusu serikali kununua mitambo chakavu na kusisitiza kuwa mitambo ambayo serikali imeamua kuinunua ni chakavu.

Uamuzi huo wa Wizara ya Nishati na Madini wa kushiriki kwenye zabuni ya ununuzi wa mitambo chakavu ya Kampuni ya Dowans, umefichuka siku chache tu tangu Rais Jakaya Kikwete, awasifie Waziri wa wizara hiyo, William Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima, kwa kazi nzuri wanayofanya kwenye wizara hiyo.
 
Back
Top Bottom