Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Hivi kujenga nguzo toka Zambia na kuziingiza kwenye Gridi ya Taifa haiwezi kuwa na njia mbadala na ikatumia muda mfupi au from Msumbiji? au Maybe kutoa Umeme Zaire kupeleka Kigoma-Mza-Mara-Kagera kusupplement unao toka Uganda na kuanza ku-project matumizi yetu yanayo ongezeka, badala ya kuazima au kununua koroboi toka kwa Mwanakijiji halafu bidha zetu zikishindwa kwenye soka la kimataifa tunaanza lalamika due to un-necessary production cost caused by our in-efficiency
 
Aina zake sizijui lakini walinunua turbines tatu, moja ya MW 35 ndiyo ilikuwa mpya na ndio ambayo Rostam alikuwa ameshapiga deal na Ngeleja ili atubambikie tena kwa Bilioni 70.

Ngeleja ashukuru Shelukindo alipreempt na kufanya JK aseme acheni upumbavu la sivyo kazi alikuwa hana na labda tungemwona Kisutu siku si nyingi.

Halafu Ngeleja asivyokuwa na aibu anajifanya shujaa eti Tanesco hawaruhusiwi kununua wakati ni Sunday tu alisema serikali inanunua na kina Shelukindo walikuwa wanapewa taarifa tu.


Mitambo ya Dowan ni simple Cycle na bei ya MW35 MPYA NI $11 MILLIONS
 
Kwa nini Stieglers gorge isitumike kuzalisha cheap huropower, then tujenge grid ambayo nasi tutasupply umeme nchi za jirani? Stiglers gorge ina potential ya kuzalisha up to 1000MW.....far more the national power supply needed.

Wanasema sasa hivi tunatatizo linalo hitaji uvumbuzi wa haraka, hivyo wanaangalia supply inayo wezekana in six month to a year, in the long run hiyo Project ya Stiggler ndio yenyewe na mingine mingi tu iliyo within the country
 
Hivi kwa nini MASHANGINGI huwa hawanunui yaliyotumika walau miaka 5 kutoka JAPAN au German? Yangelikuwa yanacost kwenye $40,000 na siyo $100,000.
Ila ikija kwenye mitambo, wanaenda kununua kwa KUINAMA (Mitumba). Sasa ngoja wainame KEKO waone kazi. Kibaya zaidi utaona watu na akili zao hapa na pale wakiLAANI Wahindi na Wazungu. Kwa nini tusijilaane wenyewe? Narudia tena ombi langu, waachiani Wahindi na Wazungu kama wapo. Msalaba tuanze kuubeba wenyewe MIPINGO. Kila kitengo tunaongoza sisi, sasa Mhindi imekuwaje alaaniwe kwa UJINGA na TAMAA zetu? FREE JEETU PATEL and his co. Weka ndani MIPINGO wote na filisi mali zao ili wajue na wakariri maneno ya Marehemu Tupac "CALL tHE COP WHEN YOU SEE PATEL..." Maana ukizubaa, utashangaa mwenzio katengeneza mamilioni na wewe unaishia KEKO.
Mipingo kila siku ni kisingizio tu. Ukame, umeme, maji, mafuriko, MWANAMKE, Umande, Joto, Wahindi, Wazungu, Wachina, Wakoloni, Utumwa, ..... can you add more? Bara la Africa twalimaliza wenyewe na vitamaa vyetu vya kupewa SHANGA na KIOO na hawa matajiri na sisi tunaachia kila kitu. Hadi wake zetu, looohhhh!!!!!!
Sasa hizi mashine Mitumba ilikuwa tuuziwe. Tumepika kelele wameacha. Kama ingeshinikizwa basi ilitakiwa kujua "kipi kilimsukuma huyu Kigogo kutaka kununua mashine chakavu?" Lakini, aka, ssaa hivi anapeta tu ndani ya AC na bia mkononi.
 
Kwa nini Stieglers gorge isitumike kuzalisha cheap huropower, then tujenge grid ambayo nasi tutasupply umeme nchi za jirani? Stiglers gorge ina potential ya kuzalisha up to 1000MW.....far more the national power supply needed.

mpango wa stigler's gorge umekuwepo kwa karibu miaka 30 sasa. Angalia sehemu ya hotuba ya Mhe. Satano (kikao cha Novemba 2007)

Pili, nataka niipongeze sana Serikali katika uamuzi wake wa kuamua baada ya kuona matatizo ya umeme yanavyozidi kuwa makubwa yaliyotupelekea mpaka tukajiingiza kwa hawa wenzetu wa Richmond na Serikali ikafikia uamuzi wa kuendeleza ule mpango wa Stigler¿s Gorge Hydropower Project wa Rufiji.

Mheshimiwa Spika, nataka kusema kwamba mchango mkubwa wa matatizo yetu ni nini katika suala zima la umeme. Mimi nadhani ni matatizo ya kutofanya wakati mwingine maamuzi sahihi kwa wakati husika na kuyafanyia kazi. Huu mradi wa Stigler¿s Gorge Hydropower Project ni mradi ambao umekwishafanyiwa project, ni mradi ambao umekwishafanyiwa utafiti mwaka 1978 mpaka 1980 na kampuni moja ya NOPLAN ambayo ilikuwa imepewa kazi hii au ilikuwa commissioned na Rufiji Basin Development Authority (RUBADA). Sasa hawa walipofanya ule utafiti katika mwaka huo wa 1978 mpaka 1980 walidhamiria baada ya kufanya utafiti wao wakaona kwamba upo uwezekano wa kujenga power stations tatu ambapo moja ilikuwa inaweza kutoa megawatt mia nne; ya pili ingetoa megawatt mia nane na ya tatu ingetoa megawatt mia tisa, ambazo zote kwa ujumla wake zingetoa megawatt elfu mbili mia moja. Hiyo ni kazi iliyofanywa na Awamu ya Kwanza mwaka 1978 mpaka 1980 na gharama za mradi huu mwaka 1985 ilikuwa ni dola za Marekani milioni elfu moja na mia mbili. Kimsingi mradi huu kama utachukua njia ya mkato kutoka Chalinze ni kilomita 165 tu unafika kwenye huu mradi.

Mheshimiwa Spika, nadhani tulishindwa kufanya yale maamuzi ama ni kwa sababu ya mashinikizo ya wenzetu wakitumia kigezo cha mazingira lakini ukweli ni kwamba walitushinikiza wakati hata wao wenyewe mpaka tunavyoongea sasa hivi wameshindwa kusaini Mikataba ya Kyoto. Sasa nadhani haya ndiyo yaliyotufikisha mahali mpaka tukajikuta tuna matatizo ya umeme na tukaanza kutafuta vitu gani viweze kutusaidia. Ripoti ya Kamati imeonyesha kwamba Richmond ile shughuli nzima imetumia Shilingi bilioni 172.9/=. Hizo ni hela nyingi sana, ni asilimia kumi na tano ya zile fedha ambazo tungewekeza wakati ule ambapo tungeweza kupata mradi wa kudumu, lakini hizi hazipo na wale wameshindwa kazi. Hilo ni la kwanza, kwamba tunatakiwa tufike mahali tufanye maamuzi yanayotusaidia sisi na wananchi wetu kwa ujumla.
 
Hizi short term measures ziko cost effective?

Hiyo argency ya upatikanaji wa umeme inatoka wapi wakati msimu wa mvua umekaribia? August, September, October na November kulikuwa na ulazima wa kuangalia hizo short term solutions, not now.....huo ni ufisadi unapikwa hapo.

Ndi hivyo Mama wenzetu wenye akili saana hawaoni hivyo, nafikiri University of Dar es laam na wasomi mbali mbali wanatakiwa waanzishe makala katika magazeti mbali mbali ili kuufahamisha umma, alternatives zilizopa na more cost effective, ama sivyo Ma-lecture wetu wa Chuo wa Uchumi na Science ni fake? na fani zingine, maana naona wana mwachia Nchi Makamba nae bahati Mbaya/nzuri Shule yake ni ya CCM Kivukoni ya akina chitalilo
 
Angalia bei za Turbine mpya.
Asante kwa kunionyesha bei kaka. Naomba kama utaweza umuandikie Mheshimiwa Ngeleja mwenyewe na umtumie E-mail (I beleive itakuwepo kwenye Website ya Bunge) ili ajionee bei ya vitu vipyaa kabisa na vyevye waranty. Na naamini atakuwa anasoma hapa au kuna watu wake wanasoma. Kama kuna mtu anamjua Ngeleja mwambie asome post namba 51 na aifungue link iliyowekwa chini, please.
 
Mitambo ya Dowan ni simple Cycle na bei ya MW35 MPYA NI $11 MILLIONS

...jamaa alitaka kutubamiza kwa almost 70m USD..tena used,i wonder kama tuna watu pale wanafanya kazi au ni 10% tuu,huwezi amini huyo waziri ana timu ya washauri kuanzia engineers,finance,economy etc lakini hebu angalia maamuzi ambayo wanakuja nayo,huyu Ngeleja nina wasi wasi kama kichwa kiko sawa...angalia anavyobabaika kununua hiyo simple machine je serious policy za umeme ataweza...JK pls fire this azz hes just useless!
 
Wabongo bana yaani bado tu kuna ishu ya umeme....inasikitisha na kuchekesha...
 
Serikali yasitisha kuinunua Dowans
Mwandishi Wetu
Daily News; Wednesday,December 17, 2008 @21:15


Serikali imesimamisha mpango wake wa kununua mtambo wa kufua umeme wa Kampuni ya Dowans ambayo mkataba wake umefutwa. Uamuzi huo umetokana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kupinga mpango huo kupitia kikao kilichofanyika kati yake, Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme (Tanesco) Jumapili iliyopita.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema pamoja na kwamba kikao hicho kilielezwa faida ambazo walidhani zingepatikana kutokana na kununua mtambo huo, lakini wameona kuwa penye mjadala lazima pawapo makubaliano.

Ngeleja aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, alisema wametafakari maoni ya Kamati hiyo ya Bunge na kujiridhisha kwamba ni vyema Tanesco wasishiriki kwenye zabuni ya ununuzi wa mtambo huo wenye mashine tano.

Akinukuu hoja za Kamati ya Bunge, Waziri huyo alisema wizara yake ina imani kubwa na kamati hiyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kwa ustawi wa taifa. Alisema wamekubali ili kwenda pamoja katika kukabili changamoto zinazokabili utoaji huduma ya umeme na siyo kuwakanganya wananchi kwa mijadala.

Kwa mujibu wa Ngeleja, pamoja na faida au sababu zilizoelezwa katika kikao hicho kuhusu ununuzi wa mtambo huo, kamati ilipinga kwa kusema kuwa kufanya hivyo ni kukiuka maelekezo ya Bunge na Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa vile mitambo hiyo siyo mipya.

“Serikali tayari imeshaiagiza Tanesco kutoshiriki kwenye zabuni ya kununua mtambo wa Dowans,” Ngeleja aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake na kusema walidhamiria kutumia Sh bilioni 70 katika ununuzi. Katika kuelezea mchakato wa kutaka kununua mtambo huo, Ngeleja alisema kabla ya wizara yake kuiruhusu Tanesco, ilipata kwanza ushauri kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.

Alisema waliona pia ni busara kuishirikisha Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ili kushauriana juu ya suala hilo. Alisema, “Serikali ilifanya hivyo kwa nia njema na kwa kutambua umuhimu wa dhana shirikishi kati ya Serikali na Bunge na hasa kwenye maamuzi muhimu na nyeti yanayohusu maslahi ya taifa.”

Miongoni mwa sababu ambazo serikali ilitarajia kuzipata kutokana na kununua mtambo huo ni pamoja na kuziba pengo la uhaba wa umeme unaolikabili taifa. Kwa mujibu wa Ngeleja, kuna ongezeko la mahitaji ya umeme kwa wastani wa megawati 70 kwa mwaka.

Alisema mtambo huo wa Dowans wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 112.2 ni sawa na mbadala wa umeme wote unaozalishwa na mabwawa ya Mtera, Hale na Nyumba ya Mungu kwa pamoja. Faida nyingine ilikuwa ni kupunguza gharama za kununua umeme kama kampuni binafsi itanunua mitambo hiyo na kuiuzia Tanesco kwa utaratibu wa Capacity Charge.

Awali akielezea hali ya uzalishaji umeme nchini, alisema haikidhi mahitaji yaliyopo. Wastani wa uwezo uliopo wa mitambo ya kuzalisha nishati hiyo ni megawati 542 ikilinganishwa na wastani wa mahitaji ya megawati 570. Alisema mfumo wa umeme wa gridi ya taifa unaendeshwa katika hali ya kutokuwa na nafasi ya kupumua; jambo linalosababisha kukatika kwa umeme mara kwa mara itokeapo hitilafu ndogo kwenye mifumo ya usafirishaji na usambazaji.
 
Wabongo bana yaani bado tu kuna ishu ya umeme....inasikitisha na kuchekesha...

after almost 50 yrs of independence and all these technology out there,only 12% of Tanzanians has electricity...sad sad indeed,mimi naamini tatizo kubwa lipo kwenye energy policy zetu ambazo zinaipa TANESCO monopoly ya kuzalisha,kuuza na kusambaza,sehemu kama za kusini hawana sababu ya kutokuwa na umeme kabisa maana kuna gas ya kutosha kuzalisha umeme na watu wa kufanya hiyo kazi wapo ila serikali kwa sababu ndio yenye uwezo pekee wa kununua na kusambaza ilikataa na hairuhusu hao jamaa kusambaza na kuzalisha,bunge wamepelekewa bill mpya kubadili hii policy lakini walichofanya wanajua wenyewe na badala ya kuangalia ukweli wanachanganya new bill na rushwa za IPTL & Richmond,hope serikali inge invest kwenye kujenga GRID kuachia wengine wazalishe na kusambaza ingesaidia sana!
 
after almost 50 yrs of independence and all these technology out there,only 12% of Tanzanians has electricity...sad sad indeed,mimi naamini tatizo kubwa lipo kwenye energy policy zetu ambazo zinaipa TANESCO monopoly ya kuzalisha,kuuza na kusambaza,sehemu kama za kusini hawana sababu ya kutokuwa na umeme kabisa maana kuna gas ya kutosha kuzalisha umeme na watu wa kufanya hiyo kazi wapo ila serikali kwa sababu ndio yenye uwezo pekee wa kununua na kusambaza ilikataa na hairuhusu hao jamaa kusambaza na kuzalisha,bunge wamepelekewa bill mpya kubadili hii policy lakini walichofanya wanajua wenyewe na badala ya kuangalia ukweli wanachanganya new bill na rushwa za IPTL & Richmond,hope serikali inge invest kwenye kujenga GRID kuachia wengine wazalishe na kusambaza ingesaidia sana!

Unajua kuna mambo mengine msipoyaweza wala hamna ubaya wowote lakini mnaposhindwa hata kujipa zile huduma za msingi kwa uhakika inasikitisha sana. Ndio maana maswali na kujihoji huwa hakuishi. Arrrggggh yaani karaha karaha karaha and more karaha. Sijui zitaisha lini hizi karaha.
 
Kununua mitambo ya second hand isiyoukuwa na warrant ni uki-hiyo wa hali ya juu sana unaofanywa na kuoneshwa na viongozi wetu. Viongozi hawa wanawaaibisha waliowapa nyadhifa hizo kwamba hawakuwa na uwezo bora wa kufikiria watu mbadala zaidi ya hao wanaovurunda mchana hadi usiku na kusababisha wana JF na wabunge kuwapigia kelele miezi nenda rudi.

Hivi ni lini viongozi wetu watakuja na sera ambazo zitapelekea nchi kuwa inajitegemea katika mambo yote? Umeme ukizalishwa wa kutosha viwanda vyote nchini vitafanya kazi, nyumba zote zitapewa nishati 24/7, hata hao wawekezaji itakuwa haina maana kuwapa tax holiday au incentive yeyote ile ili waje kuwekeza kwetu, waambieni akina Ngereja wafumbue macho na waangalie mifano ya nchi kama Thailand wanao -export mchele dunia nzima, waangalie Philippines ambao pamoja na rushwa zao , wamesambaza umeme nchi nzima hadi kwenye nyumba za nyasi ingawaje maji kwao ni tatizo. Nchi zote hizo haziwapi wawekezaji incetive zozote ili wawekeze kwao... Wana umeme wa kutosha na soko la watu lipo, sasa shida iko wapi.

Tanzania tutuwasubiria hadi tutawangoja akina Ngejeja kufanya madudu yao mpaka siku wakitoka madarakani, sijui ni lini majitu haya yakawa na akili yakinifu ya kupambanua na kupembua mambo yanayotufaa kwa maendeleo yetu ikiwa kama yanang'ang'ania kununua mitambo chakavu..

Inafaa sasa wizara ya nishati ije na sera ambazo zitalenga ku-electrify nchi nzima kwa either kutumia umeme wa maji au Nishati ya nyuklia maana hii mitambo ni short term measures tu, mitambo yeyote ile inayofanya kazi 24/7 kutoa GE ina warrant ya miaka 2 na kama ni standby warrant yake ni miaka 5, sasa kwa nini tusifikirie nishati nyingine.
Ngereja na malima Amkeni , mumezidi ukihiyo... Mnatia aibu wasomi wenzenu kwa kufanya au hata kutikisa kiberiti katika mambo mnayo champion yafanyike.... mimi binafsi mmenisababishia kichefu-chefu kila nikisia jina lenu likitajwa, Amkeni na muone mambo....
 
Who is the power behind Dowans calling shots in govt?

CHARLES RUMISHA
THIS DAY
Dar es Salaam


TANZANIANS sighed with relief when Energy and Minerals Minister William Ngeleja announced that the government has directed TANESCO to ditch the talks with the infamous Dowans Holding over the procurement of its derelict power generating plant.

The past few weeks have been a testing moment, or simply put, a test of wits between the government and the parliamentary select committee on energy and minerals over the buying of the Dowans generator.

In the view of the select committee, the plant could not be purchased because it was second-hand, and therefore contradicting the Public Procurement Act.

Also, the committee stood put on its rejection because the parliament had censored the entire Richmond-Dowans-government deal and demanded the perpetrators to be fired and taken before a court of law.

As good citizens of this land, we were all in shock and had a lot of unanswered questions hovering over our sober minds.

How could the government pay 70bn/- to Dowans for its used power plant? Had Dowans, whose proprietors the government said had not been identified now emerged from Mars, earned credence and are seriously negotiating with the very government it had swindled and embarrassed?

To many Tanzanians there was no way Dowans Holding could be separated from Richmond. There are many unanswered questions on their association.

Taxpayers were still bitter on the 153m/- daily capacity charges that Dowans collected. We are not sure if the tax-man remembered to collect the revenues from the disbursement! But, most importantly, it has never been clarified on who paid the letter of credit that was guaranteed to Richmond by the government


It is undeniable that Dowans, which inherited the power generating assignment from the briefcase company, accomplished the task in default; thus perfecting a typical hoodwinking that in all essence was illegal and undesirable.

Richmond and Dowans, the former a brief-case company, and the latter a registered firm that inherited an illegal contract from Richmond in bizarre circumstances, raised eyebrows to the extent that the parliament formed a probe team to straighten out the entire tangle.

After the parliamentary probe team, led by Harrison Mwakyembe (Kyela MP), tabled its findings, the House affirmed inter alia that the deal was dirty, the government had been conned by the brief case company and that the entire deal was floppy and corrupt.

Parliament passed 23 resolutions on Richmond, demanding the government to take stern action including abrogating the contract with Richmond-Dowans and putting to task all those who collaborated in the scam.

The Prime Minister of the time, Edward Lowassa and two ministers resigned and a few months later the government cancelled the controversial Richmond-Dowans contract.

After the dust that the scam had raised settled, Tanzanians felt relieved and the parliament regained its position in society. The JK government received new baptism and people kept waiting for the culprits to be either sacked or taken to court.

As if opening up an old wound, reports emerged that TANESCO was negotiating with a censored company to purchase the Dowans plant.

The news was like a bolt from the blue because the House was waiting to know what the government had done on its recommendations.

We began wondering if the minerals and energy ministry had suffered a curse, or was it led by big headed people who no longer respected the rule of law and the wish of the people.

Indications were that the lackluster and laissez faire tradition in the ministry had recaptured its seat.

Thank God sanity has reigned and the whole shabby deal dropped. Albeit we want to insist that it is time the government skirted around silly and embarrassing actions.

The TANESCO Board of Directors, the government negotiation team and the ministry lawyer cannot be absolved of the heinous crime of treachery.

We assert that it was shameful for the ministry to open new avenues with a firm that had been censored by parliament and declared illegal.

We want to state categorically that the Public Procurement Act prevents government from buying second-hand items. Who are those powers behind government forcing public institutions to break the law?

But, most importantly, since TANESCO and the government negotiation team have talked face to face with representatives of Dowans over the purchase of the latter’s plant, it’s the right time Tanzanians were told the powers behind Dowans.

Tanzanians want to know the power behind Dowans that calls shots in government; earns favours and cash, tramples the law and just walk off scot-free.

We want to emphasize that public servants have obligations to the public and not to any other forces. It is indeed a bizarre situation to see the ministry of energy collaborating with Dowans, a firm that has much to account to the taxpayers for the millions it has pocketed before the abrogation of the contract.

While many Tanzanians are anxiously waiting for the suspects of the Richmond scam to get a sack while others are sent to court, we believe it was inappropriate, totally shameful and illegal for a public institution like TANESCO to sit face to face with Dowans holding to negotiate over the purchase of its used plant.

Where has the civil service lost its morals and respectability Can’t people draw a lesson from the stunning events witnessed in the last four weeks at Kisutu Resident Magistrate’s Court?
 
Dowans ‘sale’ put on hold
By DAILY NEWS Reporter
Daily News; Friday,December 19, 2008 @21:15


The Commercial Court of the High Court of Tanzania has given a court injunction to stop the process of the selling of the gas turbines owned by the Messrs Dowans after being asked by the Tanzania Electric Supply Company Ltd (Tanesco).

The ruling was reached on Wednesday after Tanesco asked to court to impose the injunction on the sale following the case filled in Paris Chamber of Arbitration by Dowans in late November.

A press release by the power supply company said that Tanesco asked the court to stop the process, which begun in November 3 with newspaper announcements, so as they can be used to pay for case costs if the company wins the Paris case.

“The gas turbines will be held until the case is closed so as they can be used to pay for case costs if Tanesco wins the case,” said the statement, signed by the company’s Communications Manager, Ms Badra Masoud.

On November 27 this year, Tanesco was served with court documents informing it the Dowans has filled the case in Paris claiming that the former cancelled its contract before its expiry date and that it has not paid it capacity charge.

Before the Paris case, the state’s power utility firm expressed interest in buying the gas tribunes, which are laying idle since cancelation of the contract last August in the light of non-existence reserve power supply to cope with rising demand.

However, the Minister for Energy and Minerals, William Ngeleja, announced on Tuesday that the government, after consultation with the Attorney General's (AG) office and Parliamentary Committee on Energy and Minerals, directed Tanesco to drop its plans to purchase the gas turbines.

The Minister explained that the move would be in contravention of public procurement regulations and that ‘the purchase could spark off confusion and misunderstanding.’

Dowans has two sets of gas turbine with total capacity of 100 mw. One of 65 mw said to be second hand and that of 35 mw is reported to be new, which are in Ubungo, dare s Salaam.
 
Taarifa za ndani ni kuwa Rostam/Lowassa wametushinda kwenye deal la Dowans kwa kutumia mahakama. Dowans wamefungua kesi uchwara huko Paris wakipinga kutokulipwa capacity charges na Tanesco. Kwa kumshirikisha MD wa Tanesco na kina Ngeleja, Tanesco wamefile kesi kuzuia Dowans kuuza mitambo yao kwa kisingizio eti Tanesco wakishinda kesi wawe na mali za Dowans.

Wananchi tumefurahi na kusema du Dowans wamewekwa pabaya!! But is it true???

Kwani kama Tanesco wakishinda kesi huko Paris si wataambiwa tu msiwalipe hao dowans?? The most expense ni lawyers fees ambazo Dowans watatakiwa kuwalipa Tanesco.

Sasa je ikiwa Dowans watashinda itakuwa vipi??? Tanesco itabidi ilipe capacity charges through the Paris case, then Dowans wataclaim kuwa High Court sababu ya kesi ya Tanesco walizuia mitambo kuuzwa therefore by default sababu ya muda kupita Tanesco will be liable to buy the plant or pay the total cost of missed opportunity.

Upside ya Tanesco through High Court is so low compared to the downside which is high.

Tanesco ondoeni hiyo injuction sababu mnarisk award ya @ most 1 million USD lawyer fee to almost 100million USD ya cost ya Dowans plant.

Rostam/Lowassa wanajua hamna mnunuzi yeyote duniani anayeweza kununua hiyo mitambo na hawana pa kuipeleka, kwa kuogopa kulazimishwa kutoa mitambo kwenye ardhi ya Tanesco wamewatumia viongozi uchwara through Mahakama.

Dowans suffers another setback

2008-12-20 11:46:03
By Guardian Reporter

The Commercial Division of the High Court has restrained Dowans from selling its turbines, following an application for court injunction filed by the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO).

Dowans had advertised on November 3, this year an intention to sell their turbines but the High Court restrained them temporarily on Thursday, pending determination of complaints filed by Dowans at the Paris Chamber of Arbitration.

Tanesco Communications Manager Badra Masoud said yesterday in a statement that Dowans had filed its complaints with the Paris Chamber of Arbitration, claiming that the state run power utility firm had illegally terminated its contract with Dowans.

Masoud said Dowans had claimed that Tanesco had not paid Dowans the outstanding capacity charges as agreed in the contract.

Tanesco, represented by Rex Attorneys, filed an application with the Commercial Division of the High Court seeking the court injunction.

Masoud said they took the option because should Tanesco win the case, Dowans` property would be attached in case it failed to pay legal costs.

The government, working on the recommendations of House Committee on Energy and Minerals, had directed Tanesco to abandon negotiations on purchase of Dowans power generators as they were too old.

Minister of Energy and Minerals William Ngeleja said recently that Dowans` generators were able to operate continuously for 12 to 13 years but thereafter, the refurbishing would be quite expensive and take a long time.

The minister said the government would purchase similar plants directly from manufacturers, although the process could take time.

Dowans and Tanesco entered into the contract after Richmond Development Company LLC failed to generate 100MW of electricity as stipulated in the June 23, 2006 agreement, which was signed after power-generation dams ran dry following prolonged drought.

Revoking the contract some few months ago, Tanesco said its contract with Richmond had no legal mandate and its transfer from Redvo to Richmond, later on to Dowans Holding SA Limited and eventually to Dowans Tanzania Ltd., did not conform to the original terms and was therefore illegal.

SOURCE: Guardian
 
Last edited by a moderator:
Naona Gemu la RICMOND bado bichi, hivi kwanini Muungwana asiwaweke Rostam na Edo kwenye kachumba kadogo kwa kuhujumu uchumi?
 
Moelex23,
Sasa je ikiwa Dowans watashinda itakuwa vipi??? Tanesco itabidi ilipe capacity charges through the Paris case, then Dowans wataclaim kuwa High Court sababu ya kesi ya Tanesco walizuia mitambo kuuzwa therefore by default sababu ya muda kupita Tanesco will be liable to buy the plant or pay the total cost of missed opportunity.

Duh, na hii inaweza kuwa mabillioni ya fedha!..
Lakini bado dawa ipo, kifupi nadhani sasa hivi tumepata sababu ya kuwafikisha mahakamani Rostam/Lowassa kwa kesi ya ndani - UFISADI watiwe Lupango na isitolewe hukumu hadi hiyo kesi ya Paris ijulukane.
Kwa kila ndululu watakayo zawadiwa huko nasi huku ndani tunawafunga ktk Ufisadi!.. Kesi mbili tofauti lakini matokeo yake ni kifo chao.
 
...naona tricky za IPTL zinajirudia tena hapa,sitashangaa TANESCO wakishindwa kesi walipa kodi tukaishia kulipa mamilioni,hili shirika(Tanesco limetia hasara wananchi kuliko umeme linaozalisha...damn,ruhusu private company wafanye kazi ya kuzalisha/kuuza/kusambaza umeme,serikali inachoweza kufanya vizuri kwenye sekta ya umeme ni kusaidia kujenga infrastructure za kusambaza huo umeme maana sio rahisi kwa investors kupeleka nyaya zao mpaka vijijini ambako hakulipi,mabilioni yaliyotumika kwenye uzembe wa IPTL na Dowans ni tosha kabisa kusambaza infrastructure to the half of the country,kuzalisha umeme sio issue maana tuna gas nyingi sana na technology ipo all over,acha private investor wanunue mitambo yao na wanunue gas kutoka kwa wazalishaji na walipie kwenye grid ili kusambaza product zao,sijui kwanini ni ngumu sana kuelewa kitu rahisi kama hiki tunabaki kulalamika tuu na kula hasara kutoka Tanesco kila siku,kama sio ukichaa ni nini? matatizo mengine ni ya kujitakia,Tanzania hatuna tatizo la umeme,tatizo ni sisi wenyewe ambao hatuoni the obvious!
 
Moelex23,


Duh, na hii inaweza kuwa mabillioni ya fedha!..
Lakini bado dawa ipo, kifupi nadhani sasa hivi tumepata sababu ya kuwafikisha mahakamani Rostam/Lowassa kwa kesi ya ndani - UFISADI watiwe Lupango na isitolewe hukumu hadi hiyo kesi ya Paris ijulukane.
Kwa kila ndululu watakayo zawadiwa huko nasi huku ndani tunawafunga ktk Ufisadi!.. Kesi mbili tofauti lakini matokeo yake ni kifo chao.

...hakuna haja ya kukomoana hapa,kama serikali wana kesi wapeleke mahakamani kwa kufuata utaratibu sio kuangalia Paris wameamua nini na sisi ndio tuamue,unachotaka kufanya seems ni kukomoa sio kutaka haki ipatikane,haya mambo ya ujanja ujanja na mikato hayasaidii na hayana tofauti na ufisadi wa aina nyingine hata kama tumeibiwa!
 
Back
Top Bottom