Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Gas Turbine Price

Simple Cycle price range from $501,000.00 for 0.5mw (514kw) to $26,000,000.00 for 100mw.( 102,000 kw)

For combine Cycle with heating system and chiller the price range from $6million for 8mw to $50million for 100mw


Mitambo ya Dowan ni simple Cycle pia ni chakavu (used) walichokifanya kabla ya kuleta Tanzania walifanyia overhaule zionekane mpya, na wataalamu wetu wanataka 10% kwa kusema ni mpya kumbe ni za miaka 47. See attached price range you can get some idea.

Kwa nini serikali wanataka kununua mitambo ya dowan ya simple cycle 100mw kwa $70million na ni michakavu (20 years old) japo wamezifanyia overhauled.
 

Attachments

Kwenye hili mimi nakubaliana na Ngeleja na naamini huenda ningelikuwa mimi pia ningelipendekeza kununua hiyo mitambo baada ya kuangalia options zingine zote ikiwemo suala la maintenance. Hiyo mitambo ingeweza kupatikana kwa bei ya chini sana kwasababu kwa hapo ilipo hao jamaa hawana uwezo wa kuipeleka kwingine kokote.

Lakini pia naelewa wasiwasi wa wana JF mbalimbali juu ya kuwatajirisha hao hao ambao wametuibia mwanzoni. Naelewa pia kwamba kununua mitambo kama hiyo kunaweza kukuletea matatizo makubwa sana kisiasa. Ila tu kwenye biashara unachoangalia ni value for money kwa upande wako na wala sio nani anakuuzia.

Ndio maana naona kuongoza Tanzania ya sasa ni balaa tupu, huenda tukaishia kuwa na viongozi wafuata upepo ili kukwepa mashambulizi ya kisiasa. Hakuna anayetaka kuitwa fisadi wakati hajafanya lolote baya kwa jamii.

Pole sana kijana Ngeleja, inabidi mkiamua kununua basi baraza zima la mawaziri lipige kura ili usije ukaingia pabaya hata kama una nia njema.

Ili kuwa na uwazi ktk kufanya mambo, ni vema serikali ikawa na wajibu kuhakikisha kuwa inaponunua mali yeyote inaangalia value for money na pia ni lazima kuangalia nani anauza. Haiwezekanani kununua hata haramu ati kwa kua ni bei poa. Ili mradi DOWANS hawakuja kama watu safi, ni dhahiri kuna siri zingine za kutuingiza kwenye mkenge tutaziona, ama huyo Ngereja ataziona endapo tutanunua hizo machine. Ngereja ni highest risk taker kwa hilo, na si vema kutuweka wananchi wote kwenye hiyo risk na tungetegemea kama kiongozi atuongoze kutuondolea risks kwani gharama ya hizo risks ni kubwa. DOWANS sio fair player, labda wazalishe na watuuzie umeme. Kwanza kwa sasa tumeshika makali yeye kashika mpini, hivyo atuuzie umeme cheap with no conditions, na tutanunua 'as per our demand', na ni kama anataka lakini pango la kiwanja lazima alipie. La sivyo, waachie machine zao wauze kwa bider yeyote, huwezi jua ndani ya machine wamefunga parts toka wapi - TAPELI NI TAPELI TU. Tunaweza bambikiwa hata parts toka China bila jua, tutapojua DOWANS atakua tayari ana kinga ya mkataba wa mauzo na pesa ipo kibindoni.
 
Gas Turbine Price

Simple Cycle price range from $501,000.00 for 0.5mw (514kw) to $26,000,000.00 for 100mw.( 102,000 kw)

For combine Cycle with heating system and chiller the price range from $6million for 8mw to $50million for 100mw


Mitambo ya Dowan ni simple Cycle pia ni chakavu (used) walichokifanya kabla ya kuleta Tanzania walifanyia overhaule zionekane mpya, na wataalamu wetu wanataka 10% kwa kusema ni mpya kumbe ni za miaka 47. See attached price range you can get some idea.

Kwa nini serikali wanataka kununua mitambo ya dowan ya simple cycle 100mw kwa $70million na ni michakavu (20 years old) japo wamezifanyia overhauled.
 
kuwa na wazo tu la kununua hiyo mitambo ni kosa lisilisameheka!!! someone has to be accountable for that!!!
 
kuwa na wazo tu la kununua hiyo mitambo ni kosa lisilisameheka!!! someone has to be accountable for that!!!
 
Hatimaye serikali imeamua kutonunua mitambo ya Dowans SA kwa mujibu wa waliosikiliza BBC. Tovuti ya GlobalPublishers katika taarifa yao leo iliyoambatana na picha wamesema kuwa:

1229518579_waziriwanishati.jpg


Picha hiyo ina maelezo yafuatayo:
Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa William Ngereja, leo alielezea azma ya Serikali kununua mtambo wa kuzalisha umeme Megawati 112 .5 kutoka kampuni ya Dowans ili kuongeza nguvu ya nishati hiyo kufuatia ongezeko la watumiaji wa Nishati hiyo. kulia ni Naibu wake Mheshimiwa Adam Malima.
My Original story (now corrected?)
ili kusaidia kupunguzo tatizo la nishati nchini. Uamuzi huo umetangazwa leo rasmi na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. William Ngeleja pamojana Naibu Wake Mhe. Adam Malima.

Uamuzi huo umekuja licha ya pingamizi kubwa la Kamati ya Bunge inayoongozwa na Mhe. Shelukindo na licha ya taarifa ya kuufunua mchezo "uliochezwa" iliyoandikwa kwa kifupi tu kwenye "kijarida kimoja" uchwara ambacho kimelinganishwa na "radio mbao" kinachotoka kila jumanne kwenye mtandao!

Uamuzi huo yawezekana kuhitimisha mjadala wa wa Richmond na Dowans uliodumu kwa muda mrefu nchini. Kampuni ya Dowans kutoka Saudi Arabia, Afrika ya Kusini na Costa Rica ndiyo ilirithi mkataba usiokuwa halali wa Richmond.

Baadhi ya watumishi wa Richmond ndio pia walikuwa watumishi wa Dowans na mmoja wa maafisa wa juu wa Tanesco wakati wa mchakato wa Richmond ndiye alikuja kuwa mmoja wa wahandisi waandamizi wa Dowans.

Tetesi ya kijarida hicho (ambacho inadokezwa kinatarajiwa kuifunua zaidi Dowans wiki ijayo) zinasema kuwa kampuni ya Dowans inauhusiano na Afisa mmoja wa Kijeshi kutoka kutoka nchi moja ya Mashariki ya Kati mwenye uhusiano wa karibu na mmoja wa Wafanyabiashara maarufu nchini ambaye amekuwa akitajwa tajwa kwenye tuhuma za ufisadi na kuhusishwa sana na mkataba wa Richmond. Mfanyabiashara huyo ambaye ana nafasi ya uongozi wa kisiasa amekuwa akikanusha kuhusika na makampuni hayo!

Wachunguzi wa mambo ya nishati na siasa wanadokeza kuwa mfupa ambao ulimshinda Lowassa inaonekana Mhe. Ngeleja ameuweza.

Habari ndiyo hiyo!

I hate to be the bearer of bad news.. or is it?
 
Last edited by a moderator:
hivi kwa nini viongozi pamoja na mameneja bongo wanapenda kununua takataka? yaani mara nyingi watu wakitumwa kununua vitu wananunua vya zamani halafu kwa bei kubwa. Wana JF ambao wanajua bei ya mtambo mpya kama huo kutoka makampuni kama GE watuwekee bei ya mtambo hapa.
 
Kwa mujibu wa bbc leo jioni, Serikali amesitisha kuwania zabuni ya kununua mitambo hiyo. Waziri Njeleja ameeleza kwamba Serikali imekubaliana na ushauri wa kamati ya bunge. Pia imeelezwa kwamba endapo ingenunua ingekuwa imekiuka sheria ya manunuzi.

Swali la kujiuliza ni je Serikali haina macho? credibility yao ipo wapi? yaani mpaka kamati ya bunge ipige kelele! lol
 
Kwa Tanzania sita amini hadi baada ya muda ili nami nijiridhishe kwamba wamesitisha maana jamaa wana mabavu na kufunikiana mambo ni kawaida yao .
 
nimesikiliza bbc swahili wamesema hawato nunua maana itakuwa ni kukiuka Procurement act na mambo ya Bunge, labda niwe sikusikiliza vizuri, Ngeleja alikuwa anahojiwa, na akaelezea kuhemewa kwa TANESCo, kwamba uzalishaji wake hautoshelezi mahitaji, nakuongelea mradi wa 45mw na huu utakuwa nafikiri wa Binafsi na mradi mwingine wa Gesi asilia by mid next year kwa Private public Partnership. Lakini mimi ningependa kujiuliza au kila siku najiuliza nini ni energy Policy ya nchi yetu? ni huu umeme wa koroboi, maana ukianza kuchukua 45 kwa huyu 45 kwa huyu, ni kitu cha kuchekesha kwa nchi kama tanzania, na kama kweli tuko serious kwenda huko tunako kwenda, tukiwa katika hali ya bora zaidi ya kiushindani.
Naona tatizo kubwa la uzalishaji wa umeme tanzania ni kuweka maslahi binafsi mbele kuliko maslahi ya taifa na ndio maana watu wanashindwa kufanya upembuzi yakinifu na kuja na mradi moja mkubwa utakao kuwa na manufa kwa taifa, mahali popote wanapo pata nafasi ya kuwekeza,. basi inakuwa nafasi ya mafisadi kufanya vitu vyao, kwa kutumia sura ya usamaria wema au vinginevyo.
 
Yawezekana mko sahihi kabisa, waliotoa taarifa awali (global publishers) wao ndio walioripoti hiyo kwanza. Nimeomba mod wasahihishe, lakini kwanini kila kitu kiwe hadi kuwe na pressure!? Dowans tumeipigia kelele kwa karibu mwaka mzima, walikuwa wanafikiria nini hata kuifikiria?
 
...yaani serikali ilitaka kununua mtambo used? hivi kuna shida gani kununua moja kwa moja from GE or any credible company kitu mpya yenye warrant ya nguvu,yaani ajabu kweli kweli kununua kwa hawa matapeli mitambo used bei mara 10,hawa watu sijui ni tamaa au ushamba tuu? na hii sheria ya kuifanya TANESCO pekee ndio yenye uwezo wa kuzalisha na kuuza inabidi hiyo policy ibadilike maana hawawezi na wanao suffer ni sisi wananchi na uchumi wetu,huko kusini nasikia kuna company ya wazungu ina uwezo wa kuzalisha mpaka 300MW lakini serikali imewakataza kwa madai haiwezi kununua huo umeme na haiwezi kuwaruhusu wao kuuza kwa wananchi...najiuliza serikali ipo pale kutukomoa kwa urasimu wake au kusaidia wananchi wake,sheria ya umeme lazima ibadilike kama tunataka kuondoa hili tatizo!
 
Yawezekana mko sahihi kabisa, waliotoa taarifa awali (global publishers) wao ndio walioripoti hiyo kwanza. Nimeomba mod wasahihishe, lakini kwanini kila kitu kiwe hadi kuwe na pressure!? Dowans tumeipigia kelele kwa karibu mwaka mzima, walikuwa wanafikiria nini hata kuifikiria?
Nik kweli kwenye taarifa za saa 2 usiku huko nyumbani Waziri Ngeleja amesema serikali wameiamuru Tanesco kutoshiriki kwenye zabuni ya ununuzi wa mitambo hiyo kufuatia ushauri wa kamati ya bunge.

Nadhani uamuzi wa awali ulichochewa na ushawishi wa watu fulani ambao wanaaminika kuimiliki Dowans; bila shaka ni mzimu wa Richmond bado unaiandama serikali.
 
Hawa hawa si walikuwa wanajadiliana na IPTL ili wainunue mitambo yake, au mchakato huo umeisha kimyakimya?
 
Yawezekana mko sahihi kabisa, waliotoa taarifa awali (global publishers) wao ndio walioripoti hiyo kwanza. Nimeomba mod wasahihishe, lakini kwanini kila kitu kiwe hadi kuwe na pressure!? Dowans tumeipigia kelele kwa karibu mwaka mzima, walikuwa wanafikiria nini hata kuifikiria?

Global Publishers sio magazeti ya udaku haya? Mwanakijiji bwana! Sometimes unakuwa kama sio mwenyewe vile!
 
Ngeleja kastuka mapema. Keko (baada ya kumaliza uwaziri wake) ilikuwa inamchungulia angeendelea kutimiza azma yake ya kununua Richmond/Dowans. Kosa lake lingefananafanana na akina Mgonja et al la kukiuka ushauri halali wa kamati ya bunge na kwenda kinyume cha procurement act na hivyo kuliingizia taifa hasara. Bila shaka, ama yeye mwenyewe au wapambe wake walisoma maoni kwenye tovuti ya Tanzania Daima ambako alichambuliwa kwa undani sana. Bila shaka JF nayo imechangia kiasi kikubwa. Swali langu ni kwanini mawaziri wetu wanakurupuka tu kutangaza kitu bila kuchuja chuya na mchele kwanza! Yaani Ngeleja hajui Procurement Act mpaka kamati ya bunge imuambie! Ngeleja hajui kama mitambo ya Dowans ni chakavu kwa mujibu wa sheria za manunuzi ya serikali na hata kwa hali halisi - Iliwasumbua Dowans wenyewe wakati inafanya kazi! Napata picha kuwa mawaziri wetu ama hawasomi, au hawana washauri wazuri, au hawawasikilizi washauri wao, au donda lilelile la ufisadi (10 percent). Bado safari ni ndefu.
 
hivi kwa nini viongozi pamoja na mameneja bongo wanapenda kununua takataka? yaani mara nyingi watu wakitumwa kununua vitu wananunua vya zamani halafu kwa bei kubwa. Wana JF ambao wanajua bei ya mtambo mpya kama huo kutoka makampuni kama GE watuwekee bei ya mtambo hapa.


Angalia bei za Turbine mpya.
 

Attachments

Kokolo.. nakumbuka uliandika a while ago kuhusu jambo hili. Hivi tunajua ni mitambo ya aina gani waliyonayo Dowans na imegharimu kiasi gani?

Aina zake sizijui lakini walinunua turbines tatu, moja ya MW 35 ndiyo ilikuwa mpya na ndio ambayo Rostam alikuwa ameshapiga deal na Ngeleja ili atubambikie tena kwa Bilioni 70.

Ngeleja ashukuru Shelukindo alipreempt na kufanya JK aseme acheni upumbavu la sivyo kazi alikuwa hana na labda tungemwona Kisutu siku si nyingi.

Halafu Ngeleja asivyokuwa na aibu anajifanya shujaa eti Tanesco hawaruhusiwi kununua wakati ni Sunday tu alisema serikali inanunua na kina Shelukindo walikuwa wanapewa taarifa tu.
 
Back
Top Bottom