RC Mtaka Yeye anataka Wanafunzi kuruhusiwa kubaki Shuleni au kuweka Kambi za Kujisomea zaidi ili kuongeza Ufaulu wao na Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako anasema muda ukifika Watoto warejee Makwao na hakuna cha kuweka Kambi au Twisheni kwani Elimu wanayopewa Darasani na Walimu inatosha.

Kwa mengi zaidi juu ya 'Mtifuano' wao huu hawa 'Wateule' wa Rais Samia usikose Kununua Gazeti la Nipashe la Kesho Jumatano tarehe 14 July, 2021 na 'Zogo' lao hili Kamili lipo katika Ukurasa wa Pili.

Nilichovutiwa zaidi na 'Mtifuano' wao huu ni kwamba RC Mtaka anauamini sana Ubongo wake japo hana 'Doctorate' huku Waziri Profesa Ndalichako akiiamini zaidi 'PhD' yake na Uprofesa wake na Kukaa Kwake katika Sekta ya Elimu kama Mdau na Mwandamizi pia.

Na Mimi GENTAMYCINE ambaye hata sina Masters kama ya RC Mtaka na 'Doctorate' kama ya Profesa Ndalichako bali nina 'Kadigrii' kangu haka Kamoja tu nawaona Wote hawa hawana Hoja ya Msingi na kuna mahala wamekosea hivyo kunisaidia kujua kumbe ni kweli Viongozi wengi Tanzania Wamesoma tu ila hawajaelimika na hawawezi Kuisaidia nchi Kifikra.
 
Mkuu wa mkoa hana facts ni siasa tu watoto wanahitaji kupumzika bhana.Mbona Tabora girls na tabora boys zimeshika namba 3&4 kitaifa bila makambi.Aaacha kuja mikakati isiyo na takwimu za ukweli
Umeshawahi fika hizo shule ndugu? Sasa subiri nikumegee siri ya shule za mtindo huo:
Kwanza hizo ni boarding schools tena vipaji maalum na huko ni zaidi ya makambi, vijana wanasoma haswa, yani kusoma kwa kwenda mbele. Shule za day mbona wanacheza tu. Nenda hizo shule ndo utajua maana ya kutoboa Ozone.

Pili RC yupo sahihi sana na MESSAGE SENT AND DELIVERED. Sasa waziri akitaka akae chini abadili iyo sijui ni sheria au sera ya kutoka saa 9 au aendelee kujidai na PhD yake wakati ubunifu zero.

Tatu, watanzania tuache unafiki.. Vijana wa shule za day wengi haswa vijijini wakirudi nyumban hawawezi shika madaftari tena mpaka kesho yake shule maana kazi majumbani ni nyingi mno. Angalau basi wakikaa huko shule watapata kitu.

Tukiendelea kujifanya tunawachekea hawa wanaojiita wazalendo uchwara hili taifa litapotea. Tuwaambie ukweli na waamue kushupaza shingo au watusikilize wananchi tulio wengi.

MWISHO: SIRI YA KUFAULU NI KUSOMA KWA BIDII, USIPOSOMA UTAFELI TU. HAKUNA BLA BLA
 
Kwani Wanafunzi wenyewe wanasemaje? Warudi majumbani au wabaki shule WAJIFUE kujiandaa na mitihani!?
Wanafunzi wa kweli Tanzania ( hasa kwa Primary, Ordinary na Advanced level ) tuliishia mwaka 2000 tu Mkuu na kuanzia hapo hadi leo hii hakuna Wanafunzi bali kuna Wahudhuriaji tu wa Madarasani Mashuleni.
 
Hilo ni kweli Mkuu kwa sababu ya anguko la elimu. Kwa maoni yangu Wanafunzi wengi ambao wanapenda shule na kutaka mafanikio ya kielimu kipindi kile wangechagua kubaki shule.

Wanafunzi wa kweli Tanzania ( hasa kwa Primary, Ordinary na Advanced level ) tuliishia mwaka 2000 tu Mkuu na kuanzia hapo hadi leo hii hakuna Wanafunzi bali kuna Wahudhuriaji tu wa Madarasani Mashuleni.
 
Antony mtaka ana wazo zuri lkn nikumbushe tu, hao wagogo tangia mji waonupewe hadhi ya jiji na serikal.kuhamia hapo mtumba bac wao wanahisi they are first class ..,

Nakushauri MTAKA achana na hao wagogo ktk swala ilo la elimu kuongeza ufaulu watakushinda tu....siunaona yaan wakat ww una waambia kitu reality yenyewe yapo busy kuku record maana yake walidhamiri kukuchongea kwa wakuu
 
Wewe kwa akili hizi ni Sifuri, Kuna mkoa unaitwa "Songea"

Wana ccm mna matatizo makubwa sana

Unatetea mambo wakati wewe una elimu ya kuunga unga na elimu ya shule za kata

Mkuu wa mkoa anataka kuboresha, wewe unataka watoto wawe Vilaza kama wewe
Huyu kweli kiazi!! Mkoa wa Songea silui aliukuta nchi gani!
 
Mtaka Hana adabu kabisa. Kungelikuwa Samia I would have fired him. Angelitafuta forum ya staha kusema aliuoyasema na si kubwatuka
Nitashangaa kama hataondolewa kimsingi amemtukana rais na kwa ile kauli amedharau mamlaka na hadi gender
 
Ukisoma usiku kucha unapata muda wapi wa kutafakari? Ni kukariri, siyo kuelimika.
Jidanganye, wote unaowaona ni ma Prof hasa waliopita PCB na PCM walitumia mtindo huo. Nani kakueleza kuwa hakuna kukariri Newton 3rd law wewe.
 
Mko wengi wewe na nani? Watu mbona mnajipa mamlaka ya kuwawakilisha wengine
Acha uongo, hata makonda alikuwa akipinga kauli ya waziri. Kumbuka issue yake na Dr.Mpango
Sikusema wote, ila wengi. Kama wewe si mmoja wao basi tulia tu mkuu. Ninaoungana nao wamenielewa.
 
Mikoa ambayo hakuna makambi wanafunzi hawafaulu?
Uko sahihi, wanafaulu. Lakini mazingira yao ni rafiki na wazazi wanahangaika kivyao. Mfano mkoa wa Dsm, tuition kwa mtoto toka awali hadi form 6. Kuna haja gani ya kambi wakati mambo yanaenda?

Lakini maeneo ya vijijini mwanafunzi anamtegemea mwalimu tu. Akisafiri wiki basi hasara ya kudumu. Atafidiaje? Kambi au masomo ya muda wa ziada ndo suluhisho.
 
Mtaka yupo sahihi kuhusu Kambi zake. Lakini approach ya kumjibu waziri, yaani mteule wa rais hivi kuna mushkeli kidogo. Labda yupo undercover ili kumexpose waziri kurahisisha uamuzi wa mamlaka
nakuelewa mkuu, kama viongozi tena wateule wa raisi wanashindwa kuongea na kujadiliana kwa pamoja kuhusu jambo dogo kama hili mpaka wanaishia kutumia majukwaa kujibizana ni tatizo kubwa. Kuna moja hapa wendo kuna mmoja siyo mwenzetu - yupo kwa nia ya kutuvuruga na mwingine ni mwenzetu ila amezidiwa ameona sasa liwalo na liwe.
 
Back
Top Bottom