Mkuu, inaelekea una tatizo binafsi na waziri wa elimu. Kuna msemo wa kiingereza usemao - "All work and no play makes Jack a dull boy". Ulizia maana yake.
Hivi unafahamu kuwa Mtaka aliongea kitu anachokifahamu consequence yake?

Unadhani Mtaka, Chalamila, Diallo hawana akili kiasi hicho? unadhani wewe hakuna tatizo? Unadhani wewe hawa jamaa wako peke yao?
 
Yeye mkubwa aliwaheshimu wadogo?
Tusichokijua hapa ni kuwa kila RC /DC kwenye eneo lake amewekewa malengo ya kutimiza kwenye kila idara, nj pamoja na elimu.

Sasa mkuu wa mkoa kaweka mikakati yake, waziri anakuja kuwaambia wananchi kuwa hiyo mikakati si sahihi. Huyu mkuu wa mkoa au wilaya atafanikiwaje?

Vitabu kapewa vichache, walimu pungufu, majengo mabovu, madawati hakuna na hata walimu wachache waliopo wamekata tamaa ya kazi.

Waziri aje na suluhusho halisi badala ya kushikilia sheria na kanuni ambazo hazileti tija.
Kisha tujiulize hapa;
Nani ameingilia madaraka ya mwenzake?
Shule zote za Msingi na Sekondari zipo chini ya Wizara ya Tamisemi.
Waziri wa Elimu kutoa agizo la ratiba ya masomo, hakuiingilia Tamisemi?
Mkuu wa Tamisemi katika Mkoa ni RC, ambaye Elimu ya Msingi na Sekondari ipo chini yake.
Mnyukano wa Wizara unazidi kuifanya Elimu kuwa yatima.
 
Jidanganye, wote unaowaona ni ma Prof hasa waliopita PCB na PCM walitumia mtindo huo. Nani kakueleza kuwa hakuna kukariri Newton 3rd law wewe.
Ndiyo maana miaka 60 baadaye hatujafika mbali. Wamekariri, hawakuelimika.
 
Wakati huo tukumbuke. Muda wa kazi wa mwalimu ni saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:30 mchana (masaa 8 kwa siku na masaa 40 kwa wiki). Kwa mujibu wa standing orders for public servants. Mwalimu pia anajitolea kugika shuleni saa 12 asubuhi afundishe remedials.. Ni haki kabisa wanafunzi watoke saa 9 na nusu ili mwalimu pia aweze kwenda nyumbani. Tatizo la nchi hii wazazi wanataka walimu wabebe majukumu yote ..Ndio maana wanataka watoto wakae sana shulem Bila kuwaza kuwa pia unaviolate mkataba wa mwalimu. Masharti ya kulipwa overtime ukiyaangalia hayawezi kuruhusu malipo lwa mwalimu. Masaa ya masomo yanaruhusu mwalimu kumaliza syllabus na hivo hakuna haja ya kuwepo part time payments na haziwezi kuwa approved kwa sababu muda unatosha.
Nadhani ni wakati sasa wazaI wajipange jinsi ya kuhandle watoto wao baada ya muda wa kazi ili na mwalimu apate haki yake ya kukaa kazini masaa 8 tu..tena mara kibao tunakaa 10 hours maana tunafika 12 asubuhi baadhi ya shule
 
wajuzi watujuze kwanza watoto wa RC mtaka wao wanasoma wapi shule gani anuai....? au kiongozi yeyote cabinet minister , RC au mtunga sera yeyote mwenye kutembelea kiyoyozi au bendera yeye watoto wake wao wanasomea wapi shule gani za kata au serikali msingi na sekondar?
Ndio maana anataka kinachofanyika huko private kifanyike serikalini ili hawa maskini nao wafaidi
 
In Africa it's dangerous to be right when your master is wrong RC Mtaka kasimama na wananchi na katupa jiwe gizani huu ndo ukweli ambao wananchi wengi wanapiga kelele viongozi pelekeni watoto wenu shule za kata
Kwani jinai kupeleka shule zisizokuwa za kata ?
 
..Nakubaliana na wewe.

..Naamini na wewe utakubaliana na mimi kwamba " makambi ya kukariri mitihani " ni matokeo ya elimu hafifu / duni inayotolewa ktk shule nyingi hapa nchini.

..Kwenye nchi za wenzetu wanafunzi hawapigi kambi kukariri mitihani, bali hupiga kambi kwa ajili ya klabu za debate, sayansi, mashindano ya hesabu, michezo, etc etc.

Cc Chige, Augustine Moshi , Nguruvi3
Unajua hili suala la kambi nimekuwa nikijiuliza sana kwamba hivi huwa kinafanyika nini huko makambini!! Lakini ninachoona ni kama kile kinachoitwa kunenepesha ng'ombe siku mnada!!!

Lakini cha ajabu, inaelekea huu mtindo unasaidia sana wanafunzi kufaulu mitihani, lakini am sure, uchukue wanafunzi wote waliofaulu mtihani waliofanya november kisha uwape mtihani ule ule mwezi mmoja baadae, usishangae ukakuta nusu ya wale ambao mwanzoni walifaulu, hivi sasa wakafeli kwa sababu kama ulivyosema, inaonesha wazi kwamba wanasomea mitihani!

Miaka ya 90, pale Mgulani Primary School kulikuwa na teacher mmoja maarufu sana kama Mwalimu Imma!!! Pamoja na umaarufu wake kwenye ufundishaji wa tuisheni, lakini pia karibu na mitihani alikuwa na kitu kinachofanana na hizi kambi, na kweli, over 90% ya wanafunzi wake walikuwa "wanafaulu"!!

Cha ajabu, at least wale ninaowafahamu mimi, wengi wao walikuwa wanaishia Form IV kwa kile ninachodhani walienda sekondar sio kutokana na uelewa wao bali kutokana na ujanja ujanja wa kusomea mitihani, na matokeo yake, unaingia sekondari wakati hauna msingi imara wa elimu ya awali.
 
Huna hoja
 
Nashauri huyu RC apandishwe cheo na kuwa waziri wa elimu, sayansi na teknolojia.
Tutafika mbali.
Wasipobadili huo mtindo wao wa kufaulisha shule nzima darasa la7 hatutafika mbali. Wanafunzi wanafaulishwa tu hata uwezo hawana,kuandika na kusoma vizuri hawajui. Halafu ndiyo uje utegemee kufika mbali?

Warudishe ule mfumo wa zamani hata kama shule itafaulisha darasa la saba mwanafunzi mmoja tu sawa cha msingi ana sifa hizo.

Sekondari waende watu wenye kujielewa wala hawatotumia nguvu katika hilo suala la muda.

Wenye kujielewa hata kama akiambiwa mwisho wa masomo saa8 atabaki kujisomea mwwnyewe bila usimamizi wa mtu na nyumbani hasimamiwi na wazazi kusoma ni yeye mwenyewe.

Vitu vingine .mtakuwa mnawalazimisha hata wasiopenda kusoma matokeo yake wanafanyia fujo wenzao kwa kupiga story badala ya kusoma kwenye huo muda wa ziada.
 
Mtaka na Busara ndogo ya kuchonganisha na kuchanganya wananchi. Kwani kusoma international school kuna tatizo gani versus shule za kata? Mtoto gani anapelekwa shule na bendera? Hayo ma personal conflict yenu kamalizieni huko. Kweli Ndalichako hana uwezo wa kuwa waziri lakini ndio kakalia kiti na ndie waziri. Sasa unakataaje maamuzi yake hadharani? Mkagombanie hukohuko ndani sio hadharani. Mnatuchosha!
 
Bora tu amechanwa, yuko bize kupromote watoto wa masikini wapate mimba wakiwa shuleni.
 
Back
Top Bottom