Dkt. Mwigulu Nchemba ateua wadau watakaotoa elimu ya mlipa kodi; wamo Hamisa Mobetto, Edo Kumwembe na Mbwana Samatta

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
3,994
2,000
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amewateua Mbwana Samatta, Hamisa Mobeto na Edo Kumwembe kuwa mabalozi wa kuhamasisha ulipaji kodi. Mbali na hao amewateua wanasiasa wengine kuwa mabalozi wa elimu ya kodi, ili kuhakikisha wananchi wanalipa kodi bila kushurutishwa.

=========

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya uteuzi wa watu mbalimbali watakaotoa elimu ya mlipa kodi kwa Watanzania wakiwemo

Mbwana Samata, Edo Kumwembe na Hamisa Mobeto.

IMG_20210622_124216.jpg
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,951
2,000
Bure?

Au ndio Matumizi ya Hizo Kodi zetu tutakazotoa?

Sidhani kama hawa wadau wanafanya haya mambo kwa Uzalendo.

Hizi Promo hawa watu hawafanyi bure, na huku kupeana shavu bila transparency utasikia kila tangazo la sekunde kadhaa watu wamelipwa pesa ya mlipa kodi mmoja ya miaka 30.
 

Compact

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
4,401
2,000
Hivi kweli Hamisa akakueleze kuhusu elimu ya Mlipa kodi? Kweli?

Kwani elimu ya mlipa kodi inahitaji mvuto wa ngozi na makalio ili mtu aweze kuelewa vema?

Si kuna vijana wengi tu wamesoma Chuo cha Kodi, wapewe hilo chapuo.

Wakawaeleweshe watu mtaani na kuwajibu kwa ufasaha. Pengine makali ya kukosa ajira yangepunguzwa kidogo.

Upuuzi!.
 

Rugaiyulula

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,500
2,000
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba amefanya uteuzi wa watu mbalimbali watakaotoa elimu ya mlipa kodi kwa Watanzania wakiwemo;
Mbwana Samata, Edo Kumwembe na Hamisa Mobeto.

View attachment 1826377
Mwigulu bwana, sasa kati ya hao nani anajua maswala ya kodi au uchumi?????? Kama hawajui watatoaje elimu gani, mpria, utangazaji, comedy au ulimbwende????
Nadhubuti kusema ni yale yale ya Kigwang`ala, wasanii na utalii kumbe tulipigwa hadi basi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom