Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba awataka Watanzania kuacha tabia ya kuhifadhi fedha nyumbani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
2 (1).jpg
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewataka Watanzania kutumia benki kuhifadhi fedha zao ili kuhakikisha usalama wa fedha zao na usalama wao na kuacha tabia ya kuhifadhi fedha nyumbani.

Dkt. Nchemba aliyasema hayo Jijini Dodoma wakati akizindua Tawi la Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) kwa niaba ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo na kushindwa kutokana na majukumu mengine ya Kitaifa.

Dkt. Nchemba alisema ni vema Wananchi wakajenga utamaduni wa kutumia benki kwa kuwa uendeshaji wa uchumi wa kisasa unategemea zaidi matuminzi ya utaratibu wa kibenki ambao kwa sasa umerahisishwa na unapatikana kwa urahisi.

“Utaratibu wa kuchimbia fedha ni utaratibu wa kizamani, benki sasa zipo kiganjani kwanini uchimbie fedha? Popote ulipo unawezakupata huduma za benki,” alisisitiza Nchemba.
1 (2).jpg

3 (2).jpg
Dkt. Nchemba alisema Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na benki zote hapa nchini kama utekelezaji wa sera jumuishi za masuala ya kifedha na kiuchumi zinazolenga kuwasogezea wananchi huduma karibu hasa hizi za kifedha.

‘’Naomba kutumia fursa hii kuwaomba wafanyabiashara, watumishi wa umma na binafsi, viongozi wa Serikali wa ngazi mbalimbali na wananchi kwa ujumla kuiunga mkono na kuitumia Benki ya PBZ katika shughuli zetu za kiuchumi, kwani benki hii imekuwa ikitoa huduma zake kwa uaminifu mkubwa na kwa riba nafuu.’’

Akitoa salamu za Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Zanznibar, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Ali Suleiman Amir alisema Serikali imeamua kuhakikisha huduma za fedha zinawafikia wananchi wote kwa urahisi.

Aliipongeza Benki hiyo kwa kuendelea kutimiza azma ya Serikali kwa kufungua matawi yao katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Mtendaji wa PBZ, Dkt. Muhsin Salim Masoud, alisema kuwa Benki hiyo ina vituo vya kutolea huduma takribani 45 ambapo vituo 34 vipo Zanzibar na vituo 11 vikiwa Tanzania Bara huku akiahidi kuongeza vituo vya kutolea huduma ili kuwafikia watanzania wengi zaidi.

‘’Katika mpango kazi wetu, mwakani tutafungua kituo katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Mwanza, Arusha na Tanga ili kuwafikia Watanzania wengi na kuwapatia huduma za kifedha kwa gharama nafuu sana," alibainisha Dkt. Masoud.

Aliongeza kuwa Benki hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kupata tuzo ya mlipaji kodi bora Zanzibar iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuongezeka kwa faida, kufuatia juhudi mbalimbali zilizofanywa kuhakikisha wateja wanapata huduma kwa weledi.

‘’Mafaniko ya Benki hii yametokana na Sera nzuri za Fedha hapa Nchini, Sera nzuri za Benki ya PBZ, mahusiano mazuri ya wateja, huduma zenye gharama nafuu na juhudi za wafanyakazi wa Benki yetu," alisema Dkt. Masoud.

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ni Taasisi ya kifedha inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa asilimia mia moja. Benki hiyo ilianzishwa mwaka 1966 kwa lengo la kutoa huduma za kifedha kwa wananchi ambapo kwa sasa inamtaji wa takribani bilioni 150.
 
Waweke pesa benki kwa kipato kipi?Huo ushauri unatakiwa uendane na kuweka mifumo bora ya fursa za kiuchumi kwa wanannchi,80% ya watanzania vipato vyao kwa mwezi ni chini yaMilion moja.Hiyo hela ya kuweka benki zilizojaa tozo inatoka wapi?
 
Mbowe anazificha Nairobi, Lissu anakusanya anapeleka Marekani ambako yeye na watoto wake wana uraia.
 
Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ni Taasisi ya kifedha inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa asilimia mia moja. Benki hiyo ilianzishwa mwaka 1966 kwa lengo la kutoa huduma za kifedha kwa wananchi ambapo kwa sasa inamtaji wa takribani bilioni 150.u

Wamekusikia!
 
Waweke pesa benki kwa kipato kipi?Huo ushauri unatakiwa uendane na kuweka mifumo bora ya fursa za kiuchumi kwa wanannchi,80% ya watanzania vipato vyao kwa mwezi ni chini yaMilion moja.Hiyo hela ya kuweka benki zilizojaa tozo inatoka wapi?
Mtego wa TOZO huo kimbia🏃🏃
 
Juzi nilifanya malipo ya bili kama tatu hivi kupitia crdb nikakuta elfu 12 zimetumika kama malipo ya haraka za kulipa bili.

Benki ukiweka 10,000 usihesabie kama una elfu kumi bali una elfu 6.
 
Back
Top Bottom