Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Sio hongo, mimi bado ni Rais, natangaza tenda ya barabara za mjini Itigi KM 10

Sio rushwa ni utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu nliyopitishwa na bunge la june mwaka huu

Utekelezaji wa bajeti huwa hausimami kwa sababu ya uchaguzi

Hata bajeti ya tume ya mwaka huu wanayotumia ni iliyoidhinishwa na bunge la June
Pesa amesema atatoa yeye!Sasa hapo unaweza kujiuliza nini kipo nyuma ya pazia!
Halafu mbona,mnajihi?Wenyewe mnajua ni rushwa ndio maana mnajaribu kupotosha!shwain!
 
Acha kutetea mjinga,kazi za rais ni kuidhinisha pesa za ujenzi wa barabara au kupiga simu Tanroad wewe ni hovyo kama unae mtetea alivyo wa hovyo pia
Sasa simu aliyopewa Raisi kazi yake nini kucheza game au?
 
Dkt. Magufuli anaendelea na kampeni na leo yuko Itigi mkoani Singida. Akiwa huko akaongelea uzuri wa nyumba za Singida na kusikitika zinavyopigwa vumbi ndipo ghafla akaitwa meneja wa Tanroad mkoa wa Singida mbele ya hadhara ya kampeni. Mazungumzo yao yalikuwa hivi.
=======

Dkt Magufuli: Ahadi yangu ya mjini ilikuwa kilomita 8 sasa ntatengeneza 10 pamoja na hii barabara niliyokuja nayo, nasema kwa dhati, sisemi kwa sababu ya kura. Nasema kwa sababu hii ni haki yenu.

Huu mji umependeza sana, mmejenga nyumba nzuri sana. Haiwezekani nyumba nzuri nzuri ziwe zinaendelea kupigwa mavumbi, nasema hapana kabisa lazima tutengeneze lami na mimi lazima niwaahidi ukweli. Mheshimiwa mkuu wa mkoa sijui yuko wapi? Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Singida hili ndio liwe la kwanza kushughulikiwa, asante sana.

Na regional manager wa Tanroads yupo au msaidizi wake? Njoo hapa, chukua mic

Dkt. Magufuli: Regional manager

Regional manager: Ndio mheshimiwa

Dkt. Magufuli: Pamoja na wa Tarura, nataka mkae hapa, kuanzia leo sisi tukiondoka.

Regional manager: Ndio mheshimiwa

Dkt. Magufuli: Mchague baadhi ya barabara zitakazotosha kwenye KM 10(Regional manager: Ndio mheshimiwa Rais).

Dkt Magufuli: Tangaza tenda mwezi huu, pesa usiulize, mimi nitatoa pesa kwa ajili ya kutengeza barabara hii. Itigi Oyee, (Wananchi: Oyee kwa shangwe). Kwa hiyo mjulishe chief executive wa Tanroard, mjulishe na waziri wa ujenzi, tunaanza mara moja, wala tusichelewe na hii wala sio hongo, mimi bado ni Rais kwa hiyo natoa maagizo. Tangaza tenda ya barabara za mjini Itigi kilomita 10, zitengenezwe kwa kiwango cha lami.

Regional manager: Ndio mheshimiwa Rais.

Dkt. Magufuli alifunga suala hilo na kuendelea na kampeni kwa kuelezea ubaya wa kugawa nchi katika majimbo na kuwataka wana-Itigi wawafundishe kwa kuwanyima kura wanaotaka kufanya hivyo.

Ni kweli bado ni Rais,ni kweli kuwa anaweza hata kutengua wajumbe wa NEC,ni kweli kuwa anaweza ku saini na mtu akanyongwa LAKINI kwa hili ni ushawishi wa kutaka kupata kura.NEC msaidieni kuhalalisha hili au mkatazeni.This time anapambana na mtu anayeweza kuzungumza masaa sio yule wa dakika kumi.
 
Hapo JPM amekosea Kama anataka kufanya kazi za serikali wakati huu wa kampeni arudi ikulu avae suti yake aanze ziara za kiserikali then akimaliza arudi upya kuvaa sare za chama aanze kuomba kura kwa wananchi kwa kutoa ahadi kwamba mkinichagua nini atafanya, Mimi CCM na nampenda JPM sitaki aharibikiwe Kama hao wanaompamba na mwenzao anaharibu kama issue ya majimbo aliyoianzisha Bashiru wakati rasmu ya Warioba imependekeza hilo swala. Sasa hivi ajitahidi kunadi sera zake na ahadi zaidi Kama ni vijembe achombeze vile vya utani lakini siyo kwenye Mambo makubwa.
 
Tena ajitahidi akiwa kwenye kampeni aseme Mimi nimgombea wa kiti cha uraisi hayo ya uraisi awaachie mashabiki Kama wanavyofanya kwa wagombea wengine itamuongezea kura za huruma.
 
Rais wa Nchi, Mgombea Urais na mwenyekiti wa chama. Yaani hata NEC yenyewe muda wote hawajui anapokuwa jukwaani anakuwa amevaa cheo kipi kwa wakati huo.

Huyu kabla NEC hawajatangaza matokeo lazima atoe presidential order.
 
Sio rushwa ni utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu nliyopitishwa na bunge la june mwaka huu

Utekelezaji wa bajeti huwa hausimami kwa sababu ya uchaguzi

Hata bajeti ya tume ya mwaka huu wanayotumia ni iliyoidhinishwa na bunge la June
Mbona anasema Pesa atatoa yeye wala wasiulizr zitatoka wapi kwa mini asiseme ni budget inatekelezwa
 
Napata taabu sana anapoitwa subordinate ili aanze utekelezaji wa mradi na kuagizwa awaeleze mabosi wake maagizo aliyopokea hadharani. Kwani huwa kuna haraka gani, no structures?
 
IMG_20200922_173958.jpg

Weaker minds wanalirudisha Taifa letu nyuma...
 
View attachment 1577338
Mgombea wa Urais wa JMT kupitia CCM, Dkt. Magufuli

Dkt. Magufuli anaendelea na kampeni na leo yuko Itigi mkoani Singida.

View attachment 1577339
Magufuli akiwa na Mwigulu na wanaCCM wakiserebuka

Akiwa huko akaongelea uzuri wa nyumba za Singida na kusikitika zinavyopigwa vumbi ndipo ghafla akaitwa meneja wa Tanroad mkoa wa Singida mbele ya hadhara ya kampeni.​

Mazungumzo yao yalikuwa hivi.
=======
View attachment 1577341
“Nyomi” ya CCM Itigi

Dkt Magufuli: Ahadi yangu ya mjini ilikuwa kilomita 8 sasa ntatengeneza 10 pamoja na hii barabara niliyokuja nayo, nasema kwa dhati, sisemi kwa sababu ya kura. Nasema kwa sababu hii ni haki yenu.

Huu mji umependeza sana, mmejenga nyumba nzuri sana. Haiwezekani nyumba nzuri nzuri ziwe zinaendelea kupigwa mavumbi, nasema hapana kabisa lazima tutengeneze lami na mimi lazima niwaahidi ukweli. Mheshimiwa mkuu wa mkoa sijui yuko wapi? Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Singida hili ndio liwe la kwanza kushughulikiwa, asante sana.

Na regional manager wa Tanroads yupo au msaidizi wake? Njoo hapa, chukua mic

Dkt. Magufuli: Regional manager

Regional manager: Ndio mheshimiwa

Dkt. Magufuli: Pamoja na wa Tarura, nataka mkae hapa, kuanzia leo sisi tukiondoka.

Regional manager: Ndio mheshimiwa

Dkt. Magufuli: Mchague baadhi ya barabara zitakazotosha kwenye KM 10(Regional manager: Ndio mheshimiwa Rais).

Dkt Magufuli: Tangaza tenda mwezi huu, pesa usiulize, mimi nitatoa pesa kwa ajili ya kutengeza barabara hii. Itigi Oyee, (Wananchi: Oyee kwa shangwe). Kwa hiyo mjulishe chief executive wa Tanroard, mjulishe na waziri wa ujenzi, tunaanza mara moja, wala tusichelewe na hii wala sio hongo, mimi bado ni Rais kwa hiyo natoa maagizo. Tangaza tenda ya barabara za mjini Itigi kilomita 10, zitengenezwe kwa kiwango cha lami.

Regional manager: Ndio mheshimiwa Rais.

View attachment 1577336
Magufuli akinadi sera za CCM Itigi, Singida

Dkt. Magufuli alifunga suala hilo na kuendelea na kampeni kwa kuelezea ubaya wa kugawa nchi katika majimbo na kuwataka wana-Itigi wawafundishe kwa kuwanyima kura wanaotaka kufanya hivyo.

Ilegal directive
 
Magufuli na mchaka mchaka wa LISSU. DADEKI..
Kwisha abari yake, Chali,.. anaucheza mziki wa LISSU penda usipende.
Usiishie hapo waahidi kuwakamata
Waliomshambulia mtoto wao wana Singida, kinyume cha hapo kwendraaaa, hakuna kura kwa muuaji kama wewe

#NIYEYE kiboko ya ViChaa na WendaWazimu. ✌🏽✌🏽✌🏽
 
Daah! Procurement officer & Paymaster...

Anakosea! Mbona ka anafanya kusudi!

Everyday is Saturday.............................. :cool:
 
Back
Top Bottom