Rais Samia: Tunaendelea kuimarisha miundombinu ya barabara na madaraja

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,093
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea na juhudi mbalimbali za kuimarisha miundombinu ya Barabara na Madaraja Nchini kwani ndio kilio cha wananchi kwa sasa.

Rais Samia amesema hayo wakati akizungumza na wananchi eneo la Itigi baada kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Makongolosi – Rungwa – Itigi - Mkiwa Kilomita 413 kwa kiwango cha lami; Sehemu ya Doroto – Noranga – Itigi - Mkiwa yenye urefu wa kilomita 56.9

Ameitaja baadhi ya Miradi ya barabara na madaraja iliyokamilika hivi karibuni katika Ukanda wa Kati ambayo ni Daraja la Sibiti (m 82); (Singida/Simiyu), Manyoni – Itigi – Chaya (km 85); (Singida), Tabora – Koga – Mpanda (km 360); (Tabora) na Tabora – Nyahua – Chaya (km 166.5); (Tabora)

Miradi mingine iliyokamilika ni Nzega – Tabora (km 116); (Tabora), Tabora Ndono – Urambo (km94); (Tabora), Urambo – Kaliua – Kazilambwa (km 86.9); (Tabora), Dodoma – Mayamaya – Mela (km 47); (Dodoma), Mwigumbi – Maswa (km 50.3) (Simiyu), Maswa – Bariadi (km 50) (Simiyu) na Bariadi – Lamadi (km 71.8) (Simiyu)

Naye Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kuwa, kuhusu Daraja la Sanza Daraja la Sanza na Maingilio yake yenye urefu wa kilomita 14.5 kwa kiwango cha lami, ambalo linaunganisha Mkoa wa Singida na Dodoma kupitia wilaya ya Manyoni eneo la Heka na Bahi eneo la Sanza, ambalo Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Dr. Pius Chaya amemuomba Mhe Rais na amekuwa akilipigania muda mrefu tayari kibali kimetolewa na usanifu na upembuzi yakinifu umefanyika na Mkataba wa Ujenzi umeshaandaliwa na unasubiri utiaji saini ili kazi iweze kuanza.

IMG-20231016-WA0002.jpg
IMG-20231016-WA0001.jpg
IMG-20231016-WA0000.jpg
 
Sijui kwa nini serikali inajenga michirizi ya barabara bdala ya kujenga barabara bora, barabara zinazojengwa ni nyembamba sana, inahitajika kujengwa barabara Pana kama za wenzetu walioendelea,bila hivyo ajali zitazidi kutumaliza na uchumi utazidi kudumaa.
 
Sawa pia, Tunashukuru kwa taarifa. Japo Miundombinu hiyo imechelewa sana, ila wanasema "kawia ufike".
 
Ni bora kujenga barabara bora chache kuliko utitiri huu ambao unaonekana ni uchafu, angalia kilichofanyika kwenye T1 ndani ya mikumi national park hadi ule mlima wa kuondokea mikumi towards iringa, ni vurugu tupu zimefanyika pale
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom