Serikali kupitia TANROADS imemkabidhi Mkandarasi kazi ya ujenzi wa Barabara ya Kimara-Bonyokwa-Kinyerezi kwa kiwango cha lami

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imemkabidhi Mkandarasi kazi ya ujenzi wa Barabara ya Kimara – Bonyokwa – Kinyerezi kwa kiwango cha lami; Sehemu ya kwanza yenye urefu wa kilomita 6 pamoja na ujenzi wa daraja la Kinyerezi lenye urefu wa mita 25.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa kwenye hafla iliyofanyika kwenye eneo la mradi tarehe 9 Machi 2024, Mkuu wa Mkoa wa Dar - es Salaam Mhe. Albert Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusikia kilio cha miaka mingi cha wakazi wa Jimbo la Ubungo na Segerea ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia ubovu wa barabara hiyo ambayo wamesema ilikuwa kikwazo cha maendeleo katika eneo hilo.

RC Chalamila amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya kizawa ya Nyanza Road Works iliyopewa kazi ya ujenzi wa barabara hiyo kufanya kazi usiku na mchana ili ikiwezekana hata kabla ya mienzi 16 ambayo iko kwenye mkataba iwe imekamilika na kuhakikisha anazingatia viwango na thamani ya fedha iliyoelekezwa na Serikali katika utekelelezaji wa mradi huo ( value for Money).

Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mha. Mohamed Besta; Mkurugenzi wa Miradi TANROADS Mha. Japharson Nnko amesema mkataba wa ujenzi wa Barabara hiyo ulisainiwa tarehe 9 Februari mwaka huu 2024 na kilichofanyika ni kumkabidhi rasmi mkandarasi eneo la mradi ili aanze kazi baada ya kuwa amekamilisha taratibu zote zinazotakiwa.
 
Hapo panatakiwa iunganishwe ringroad kutoka Tegeta mpaka Mbwamaji.

Yani mtu awezekutoka Tegeta mapaka Kimara mpaka Kinyerezi mpaka Airport mpaka Mbwamaji kwa kutumia barabara hiyo bila kuingia kati huku.
 
Hongera wakazi wa Kimara Bonyokwa,

Bado barabara ya Mbezi -Mpigi Magohe- Bunju, itakayopita Mabasi ya kwenda mikoani iliyoagizwa na Mh Magufuli ijengwe lakini mpaka leo bado na wananchi wa huko wanapata tabu ya usafiri kwa nauli kupanda na magari kuharibika kutokana na ubovu wa barabara.
 
Good news
 
Ahsante
 
Hapo panatakiwa iunganishwe ringroad kutoka Tegeta mpaka Mbwamaji.

Yani mtu awezekutoka Tegeta mapaka Kimara mpaka Kinyerezi mpaka Airport mpaka Mbwamaji kwa kutumia barabara hiyo bila kuingia kati huku.
Ipo barabara inatokea tegeta unapitia madale unatokea mbezi mwisho unapitia malamba mawili mpaka kinyerezi lami tupu
 
Back
Top Bottom