Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli akiwa Misungwi; Nimebaki mimi tu kwa sababu hamnipendi, hamjanipitisha bila kupingwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,038
Dkt. Magufuli asubuhi hii amefanya mkutano wa kampeni katika jimbo la Misungwi jijini Mwanza na kuwataka Watanzania tupendane.

Dkt. Magufuli amewasihi wananchi kutobaguana kwa misingi ya chama cha siasa, dini au kabila kwa mustakabali mwema wa taifa letu.

Kadhalika Dkt. Magufuli amewataka wanamisungwi kuchagua Rais, mbunge na diwani kutoka CCM ili waendeleze maendeleo yaliyo katika ilani ya uchaguzi.

Source: Channel Ten

Maendeleo hayana vyama!

==============

Rais Magufuli leo Jumanne anaendelea na kampeni za kuwania Urais na kuwanadi Wabunge na Madiwani wa chama anachokiongoza. Amepita Misungwi jimbo lilikuwa linaongozwa na waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Charles Kitwanga ambalo kwa sasa CCM ilimpitisha ndugu Mnyeti, Hii ni sehemu ya hotuba yake fupi.

DKT MAGUFULI: Ninachowaambia mimi niko nyumbani, ninawashukuru sana watu wa Misungwi mmepitisha mbunge bila kupingwa, mmepitisha madiwani bila kupingwa, hongereni sana. Nimebaki mimi tu kwa sababu hamnipendi, hamjanipitisha bila kupingwa, wangapi mtanipitisha bila Kupingwa? Asanteni sana.

Nataka nieleze ukweli, mlikuwa na mbunge hapa, Kitwanga alikuwa ananisumbua sana baadhi ya miradi. Ni lazima tujue historia ilikotoka, mahali tulipo na tunapoenda na Mnyeti atakuwa Mbunge.

Katika mipango ambayo imefanyika hapa ni mingi, hata hili barabara halikuwepo, katika kipindi cha miaka mitano tulilifanya na alienisumbua ni Kitwanga, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Nataka niyazungumze haya, bahati nzuri katika kazi zetu huwa sio za maisha. Palikuwa na Nyerere akamaliza muda wake, akaja Mwinyi akamaliza miaka yake kumi, akaja Mkapa akamaliza miaka yake kumi, akaja Kikwete miaka yake kumi na mimi mkitipisha hapa imebaki miaka mitano tu watakuja na wengine.

Hapa tuna mradi mkubwa wa maji ambao utagharimu bilioni 12 utakaonufaisha watu zaidi ya sitini na nne elfu.

Tumeanza vizuri, naomba mtuamini, naomba muendelee kuiamini CCM na hasa mnaona kazi nyingine ambayo inafanyika hapo Kigongo-Busisi, tunatengeneza daraja ambalo halijawahi kuonekana Tanzania na Afrika mashariki, daraja la kilomita 3.2.

Sasa msiache mkanichagua, yakaja mengine yakafuta haya mamiradi kwa sababu gharama ya daraja hili ni bilioni 699, bilioni 700 tunaziweka hapa. Ninachowaomba ndugu zangu wa Usagara na Misungwi endeleeni kushikamana, muwe wamoja. Haya mambo ya siasa yaliyokuwa yanawatenganisha myaache na bahati nzuri ndoa ya Mnyeti, alieiandaa ni Kitwanga.

MNYETI: Mheshimiwa Rais ni kweli kama ulivyosema, ndoa yangu aliiandaa mzee Kitwanga, namheshimu sana, nampenda sana siku zote.

MAGUFULI: Nampongeza Mnyeti kwa kushinda, nawapongeza waheshimiwa madiwani. Ninafahamu kuna appeal zitatokea tokea lakini tusubiri hilo ni kazi la tume pia nawapongeza wananchi wa hapa kwa kushikamana, maendeleo hayana chama.

Nina mke wangu nae nilimuoa Misungwi, mke wa Kitwanga hebu njoo hapa bwana.

MAMA JANETH MAGUFULI: Tunamuombea kura Rais, wabunge, madiwani, mtawachagua? Basi tunawashukuru sana asanteni.

MAGUFULI: Jamani nawapenda, nitakuja siku moja tufanye mkutano hapa.

Rais Magufuli leo Jumanne anaendelea na kampeni za kuwania Urais na kuwanadi wabunge na madiwani wa chama anachokiongoza. Amepita Misungwi jimbo lilikuwa linaongozwa na waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Charles Kitwanga ambalo kwa sasa CCM ilimpitisha ndugu Mnyeti, Hii ni sehemu ya hotuba yake fupi.

DKT MAGUFULI: Ninachowaambia mimi niko nyumbani, ninawashukuru sana watu wa Misungwi mmepitisha mbunge bila kupingwa, mmepitisha madiwani bila kupingwa, hongereni sana. Nimebaki mimi tu kwa sababu hamnipendi, hamjanipitisha bila kupingwa, wangapi mtanipitisha bila Kupingwa? Asanteni sana.

Nataka nieleze ukweli, mlikuwa na mbunge hapa, Kitwanga alikuwa ananisumbua sana baadhi ya miradi. Ni lazima tujue historia ilikotoka, mahali tulipo na tunapoenda na Mnyeti atakuwa mbunge.

Katika mipango ambayo imefanyika hapa ni mingi, hata hili barabara halikuwepo, katika kipindi cha miaka mitano tulilifanya na alienisumbua ni Kitwanga, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Nataka niyazungumze haya, bahati nzuri katika kazi zetu huwa sio za maisha. Palikuwa na Nyerere akamaliza muda wake, akaja Mwinyi akamaliza miaka yake kumi, akaja Mkapa akamaliza miaka yake kumi, akaja Kikwete miaka yake kumi na mimi mkitipisha hapa imebaki miaka mitano tu watakuja na wengine.

Hapa tuna mradi mkubwa wa maji ambao utagharimu bilioni 12 utakaonufaisha watu zaidi ya sitini na nne elfu.

Tumeanza vizuri, naomba mtuamini, naomba muendelee kuiamini CCM na hasa mnaona kazi nyingine ambayo inafanyika hapo Kigongo-Busisi, tunatengeneza daraja ambalo halijawahi kuonekana Tanzania na Afrika mashariki, daraja la kilomita 3.2.

Sasa msiache mkanichagua, yakaja mengine yakafuta haya mamiradi kwa sababu gharama ya daraja hili ni bilioni 699, bilioni 700 tunaziweka hapa. Ninachowaomba ndugu zangu wa Usagara na Misungwi endeleeni kushikamana, muwe wamoja. Haya mambo ya siasa yaliyokuwa yanawatenganisha myaache na bahati nzuri ndoa ya Mnyeti, alieiandaa ni Kitwanga.

MNYETI: Mheshimiwa Rais ni kweli kama ulivyosema, ndoa yangu aliiandaa mzee Kitwanga, namheshimu sana, nampenda sana siku zote.

MAGUFULI: Nampongeza Mnyeti kwa kushinda, nawapongeza waheshimiwa madiwani. Ninafahamu kuna appeal zitatokea tokea lakini tusubiri hilo ni kazi la tume pia nawapongeza wananchi wa hapa kwa kushikamana, maendeleo hayana chama.

Replica, Magufuli anajua pa kuanzia kampeni zake mfano katika miradi mikubwa aliyotekeleza na maendeleo kwa ujumla Sasa sijui wenzetu huwa wanaanzia wapi manake hawana reference.
 
Hivi huyu jamaa ana akili kweli au ndio ukichaa umeshika kasi? Tangu dunia iumbwe huyu ndio kiongozi "Hamnazo" kuwahi kutokea! Hajui nini anaongea ana hana kumbukumbu sijui alifauluje mpaka akafika PHD. Huyu ni wakuonewa huruma!
Hahaha Unamwones Huruma Eeeh ,Au Anakunyoosha Mpka Hujielewi ,unabaki unajifariji kwa Matusi YANI KAMA UNAMCHUKIA MAGU JIANDAE MIAKA 5 TENA YA MAUMIVU YA MOYO MAANA MTAKUFAWENGI BAVICHA KWA PRESSURE
 
Back
Top Bottom