Martin Maranja Masese amchambua Hayati Magufuli (JPM) mwanzo mwisho

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,018
144,377
“MAGUFULI ALICHELEWA KUWA RAIS WETU.”

Tulitakiwa kuwa na JPM kabla ya miaka 20 iliyopita. Magufuli alichelewa kuwa Rais wetu kwa katiba ya kifalme/kisultan tuliyonayo. Miaka 5 na miezi 5 ilituonesha rangi za udikteta. Ingawa rangi hiyo haikufika kwa mtu mmoja mmoja, wapo walioguswa

Bado tulihitaji kuwa na JPM kwa miaka mingi au tuseme kwa lugha rahisi kabisa, JPM alichelewa kuwa Rais wetu. Ndiyo. Kabla ya JPM, kuna masuala mengi ya hovyo hatukuwahi kuyaona au kupitia katika siasa za nchi yetu, lakini katika uwepo wake tumeona masuala mengi ya kuogofya.

JPM alikuwa daktari bingwa wa propaganda. Aliweza kuwaaminisha watu uchumi wetu ni imara na ukuaji wake ni wa kadi kubwa, watu waliamini ingawa bado walikuwa maskini wa kutupwa, hawana huduma za kijamii katika maeneo yao, hawana miradi ya maendeleo na kipato chao ni duni.

JPM aliweza kuwaaminisha watu ndiye mtetezi wao, mtetezi wa wanyonge. Akawapa jina hilo, umaskini ukatiwa nakshi-nakshi. Watu wakaamini, na kumuita Rais wa wanyonge, na kila alipokwenda hakusita kueleza kwa sauti kwamba haoni mwingine wa kumaliza kazi yake isipokuwa yeye.

Watu hawakujali, hata kuhamisha Serikali Dodoma bila bunge kuketi na kupitisha fedha hizo, ununuzi wa ndege bila bunge kurudhia, ujenzi wa uwanja wa ndege Chato bila bunge kuketi na kuridhia matumizi ya fedha za umma. Watu waliaminishwa kwamba Magufuli hakosei, wanyonge waliamini

Waliothubutu kuhoji walionekana ni wenye chuki na JPM, wakaitwa majina mabaya. Wakaambiwa ni vibaraka wa mabeberu. Walioendeleza ukosoaji walitafutwa na kuitwa wachochezi, wakashtakiwa kwa makosa ya uchochezi, madawa ya kulevya, uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, ugaidi.

Ni wakati wa Magufuli, miili ya binadamu ilionekana katika mifuko ya sandarusi ikiwa imefungwa, ikielea katika Pwani ya bahari ya Hindi na hata katika michirizi ya mto Ruvu. Tulipouliza, tulipewa majibu kwamba hao ni wahamiaji haramu. Wahamiaji haramu ndiyo walistahili kuuwawa hivyo?

Upendeleo ulishamiri. Ubaguzi wa kisiasa ulikuwa ni dhahiri. Magufuli aliwahi kufika Vwawa, Mbozi na kuwaambia wananchi kwamba walichagua upinzani (CHADEMA) sasa wasitarajie kamwe atawapa maendeleo, wamuulize masuala ya maendeleo huyo mbunge waliyemchagua kutoka upinzani.

JPM alifanikiwa katika masuala yake mengi, yenye ubaguzi. Wakazi wa Kimara, Dar es Salaam walibomolewa makazi yao kupisha ujenzi wa barabara. Lakini wakazi wa Mwanza akaagiza kusitishwa kwa ubomoaji wa nyumba za wananchi zaidi ya 2,000 wanaodaiwa kuvamia eneo la Uwanja wa Ndege Mwanza, kituo cha polisi na (JWTZ)

JPM akiwa Kinyerezi anazindua mradi wa umeme alisema hawezi kupeleka chakula kwa mtoto wa kambo (upinzani) na wakati nyumbani kwake wanahitaji hicho chakula. Akiwa na maana kwamba walipochagua wapinzani ni watoto yatima hawezi kuhangaika nao kamwe. Huu ulikuwa ubinafsi.

Tundu Antiphas Mughwai Lissu, ameshambuliwa kwa risasi nyingi, Dodoma siku ya 07.09.2017 akitoka katika shughuli zake za bunge, tena akiwa Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania (TLS). Waliomshambulia hadi sasa wanaitwa “wasiojulikana”. Ni wakati wa JPM wauaji hao walipewa jina hilo, JPM hakuwahi hata kukemea kundi hilo. Hatari sana.

Picha za gari la Tundu Lissu aina ya Toyota Land Cruiser VX, zilizopigwa baada ya tukio hilo, zilionyesha likiwa na matundu zaidi ya 25 ya risasi; kwenye tairi la mbele upande wa abiria, na sehemu mbalimbali za upande huo ambao ndiyo aliokuwa amekaa mbunge huyo. Unyama.

Ben Saanane hajulikani hata alipo hadi leo. Ni marehemu au bado yupo hai? Sasa awepo hai tangu 2016 kwamba wanamtunza? Siyo Kweli. Ben Saanane alikuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Magufuli. Alikosoa vilivyo pia upatikanaji wa Ph.D ya Magufuli. Nyakati hizo ndizo alizopotezwa.

Wakati ndugu wa karibu na viongozi wa Chadema wakitumia kila mbinu kujua aliko Ben, Desemba 24, 2016 siku moja kabla ya sikukuu ya Krismas, mtu asiyejulikana aliingia katika akaunti yake ya Facebook na kufuta baadhi ya maandishi yake yaliyokosoa viongozi wa juu serikalini.

Akwilina Akwilini, mnakumbuka kisa cha binti huyu wa chuo cha NIT? Akiwa katika daladala akitoka chuoni, alilelengwa na risasi iliyotupwa na Askari Polisi waliokuwa wakizuia Maandamano ya wafuasi wa CHADEMA eneo la Mkwajuni, Kinondoni, Dar es Salaam wakiongozwa na Freeman Mbowe

Kilichofuata? Freeman Mbowe na viongozi wenzake wa CHADEMA walishtakiwa kwa makosa mengi ikiwepo la kusabsbisha mauaji ya Akwilina Akwilini. Walihukumiwa kwenda gerezani au kulipa faini. Watanzania walichangia faini hizo, Shilingi 350 milioni. Muuaji wa Akwilina akabaki mtaani.

Wanasiasa wa upinzani walifanya biashara ya kisiasa. Walisema wanaunga juhudi za JPM mkono. Wabunge waliacha ubunge na kuomba ubunge. Madiwani pia na hata mameya. Ilifanyika biashara haramu kuaminisha macho ya umma kwamba JPM anakubalika na wanasiasa wa upinzani. UONGO.

Ni wakati wa JPM tumeshuhudia COVID-19, janga kubwa la Dunia, likiumiza watu na kuondoka na maisha ya watu, lakini ilikuwa ni jinai kwa mamlaka za afya kutoa takwimu za ugonjwa. Waliacha. Uchumi uliharibika kutokana na COVID-19 lakini ilikuwa jinai wahusika kusema vinginevyo.

Ni wakati wa JPM kulikuwa na jaribio la kufuta Tanganyika Law Society (TLS) ambayo imeanzishwa kwa Sheria. Kisa? Ni wakati ule Tundu Lissu aligombea u-Rais wa TLS, awali ilionekana ni taasisi ambayo watawala na dola waliitumia kwa matakwa yao. Ujio wa Tundu Lissu uliwakera.

Ni katika utawala wa JPM, Mbunge halali wa watu wa Singida Mashariki, Rais wa chama cha Mawakili, Tundu Antiphas Mughwai Lissu alishsmbuliwa kwa risasi nyingi Mji wa Serikali Dodoma akitoka bungeni na wahalifu hawajawahi kutafutwa kamwe kama alipigwa risasi mnyama.

AZORY Gwanda? Ni kati ya wengi waliotoweshwa na kupotezwa kabisa. AZORY alikuwa mwandishi wa habari, akiandaa makala kuhusu mauaji yaliyokuwa yakifanyika katika eneo la MKIRU (Mkuranga, Kibiti, Rufiji). Raia wengi waliuwawa na habari za kwanini wanauwawa hazikuwahi kujulikana

AZORY Gwanda akachukua jukumu la uandishi wa habari za uchunguzi, akaandaa makala. Vikosi vya usalama vikamkamata, vikaenda naye hadi shambani kwa mkewe, akawapa funguo za nyumbani, wakafanya upekuzi, wakabeba vifaa kazi na kuondoka na AZORY hadi leo tangu mwaka 2017

Mdude Mpaluka Said Nyagali, ni mfano mzuri wa madhila ya utawala wa kidikteta. Ametekwa mara mbili kwa sababu za kumkosoa JPM. Ameteswa na kushtakiwa kwa kesi ya madawa ya kulevya. Alishinda kesi Mahakamani na ikaonekana ni kesi ya uongo kumuumiza Mdude Nyagali.

Gavana wa benki kuu alijitokeza hadharani akadiriki kuita hazina ya taifa kwamba ni chungu cha Rais. Huu ulikuwa ni mwisho kabisa wa kuona wataalam wetu, wasomi na wabobezi wamefika mwisho wao wa kufikiri kwa kutumia kichwa sasa wanatetea nyadhifa zao kwa kumlamba miguu mtawala

Mawaziri walianza kumuita JPM kwa jina la “Mheshimiwa Mungu” hadharani. Mkuu wa Mkoa wa Tabora akasema “Mungu sasa amshukuru JPM kwa niaba ya watu wa Tabora”. Wote hao ni wakristo. Walifikia kiwango cha mwisho kabisa cha upambe. Na JPM hakuwahi kuwakanya wapambe wake.

Paul Makonda akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akivamia Kituo cha luninga cha Clouds TV kwa mitutu ya bunduki na Askari, siku mbili baadae, JPM anasema hawezi kupangiwa mamlaka yake, hivyo Makonda achape kazi na asisikilize maneno ya wananchi. Kiburi cha hali ya juu

Lengai Ole Sabaya amekuwa mfungwa. Ametumikia kifungo katika gereza la Kisingo. Kifungo cha miaka 30 gerezani (kabla ya kukata rufaa), alihukumiwa kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha. Alipata pia kesi ya uhujumu uchumi. Huyu alikuwa ni mteule wa JPM.

Unaweza kuona aina ya wateule wake. Makonda na Sabaya walikuwa na hulka, silka na tabia nyingi zenye kufanana. Kulikuwa na Mrisho Gambo, Simon Odunga akiwa DC wa Rorya, na Alexander Mnyeti pia na wateule wengine wengi. Hawa walisadifu sifa za aliyewateua. Aliwapenda na kuwasifu hadharani.

Mbaya zaidi, uchaguzi mkuu wa 2020, uliharibiwa na mamlaka za serikali tena chini ya utawala wa JPM, wagombea wa upinzani walienguliwa, maeneo mengi CCM wakajitangaza washindi, wagombea wa upinzani hadi sasa wanazo kesi za uhujumu uchumi, mauaji na wapo gerezani kutokana na uchaguzi huo.

Unakumbuka JPM aliwaita wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa (hawa ni watendaji wa vijiji na mitaa) Ikulu ya Dodoma? Baadae alikutana na wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo ya uchaguzi (Wakurugenzi watendaji wa halmashauri) na kilichofuata sote tunakumbuka. Uharibifu.

Ni uchaguzi huo umelifanya bunge kuwa la chama kimoja. Bunge halina hata kambi rasmi ya upinzani bungeni. Walipogundua kwamba hata kamati za PAC na LAAC lazima ziongozwe na wabunge wa upinzani, wakawaomba ACT wapokee ofa na wale wabunge 19 wakaingizwa bungeni. Haramu.

JPM akiwa madarakani, wabunge 19 wasiokuwa na uwakilishi wowote wa chama cha siasa au kutokana na takwa lolote la katiba, waliapishwa, wakaitwa wabunge halali kwa kuapishwa na hadi sasa wapo bungeni. Kuonyesha kwamba kuna mkono wa DOLA, Spika wa bunge, Job Ndugai alisema hakuna wa kuwagusa.

Ni matendo ya aibu kubwa sana yenye kuonyesha alama kubwa za udikteta. Mambo mengi sana yalitokea, mambo yasiyopendeza. Ni wakati wa JPM tunaelezwa fedha za Plea-Bargain zimepotea na kuna akaunti nyingine za fedha hizo zimefunguliwa China kwa siri. Huu ni uhujumu uchumi. Unabisha?

Ni wakati wa JPM, ukaguzi wa CAG, ndani ya (TANROADS) akabaini TZS 129 bilioni zilitumika kununua mtambo wa sukari ambao hata hivyo mtambo wenyewe (ambao haujulikani kazi yake), haujafika nchini.. Unajiuliza, TANROADS na kununua mtambo wa sukari wapi na wapi. Mambo ya ovyo yalifanyika.

Pia CAG akabaini kuna manunuzi ya TZS 68 bilioni nje ya mfumo hapo TANROADS. Pia CAG akasema kuna Shs. 54 bilioni ongezeko gharama ujenzi uwanja wa ndege CHATO (nje ya bajeti), ambao sasa ni mapango ya kujificha kunguru. Kwanini nisiseme mtu huyu alichelewa kuwa Rais wetu? Ndiyo!

Katika eneo hilo, CAG akaendelea kusema, kuna TZS 69.6 hasara za kuchelewa kuwalipa wazabuni katika ujenzi wa miundombinu ya barabara, na hasara ya Sh72.2 bilioni Barabara za chini ya kiwango. Jumla ya Shs. 362 bilioni mwaka 2020/2021 pekee hapo TANROADS zilipotea kwa Ubadhirifu tu..

CAGReport ukurasa wa 400, Aya ya 12.3.4 inaeleza, CAG alipofanya ukaguzi maalum kiwanja cha ndege Mtwara alikuta vibali vya kazi vya muda mfupi kwa wageni (CTA) visivyo halali vilivyotolewa na Idara ya UHAMIAJI na kusababisha hasara ya $1.732 million (TZS 4.041 billion).

CAG anaeleza kuna mtandao wa maafisa 32 wa uhamiaji wameghushi hati za kusafiria feki na wakapiga TZS 2.42 bilioni. Taarifa inafafanua wageni wa kigeni 21,208 walipewa stika za kughushi, Mtandao wa maafisa hao wakafuta taarifa (ushahidi) katika mfumo wa utoaji stika hizo.

Ufisadi huu wa TZS 2.42 bilioni umefanyika ndani ya siku 180) katika uwanja wa ndege wa KIA kuanzia 1/1/2019 hadi 30/6/2019 kwa mtandao wa maofisa hao wa uhamiaji kucheza na mfumo wa maombi ya viza (VAS). Huu ni wakati tulielezwa kwamba JPM amefanikiwa kumaliza ufisadi.

Taarifa ya stika 21,208 za viza za wageni waliowasili Tanzania kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) zilifutwa katika kanzidata za VAS ambazo zilihusu wageni waliowasili nchini Tanzania lakini maofisa hao 32 wakawapa stika za kughushi kujipatia TZS 2.4bn

Taarifa ya CAG, 2020/2021 iliweka wazi kuwa kuna hasara ya TZS 3.9 ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Hayo yalitokea wakati tukiwa na Rais John Magufuli, na tukielezwa nidhamu ya utumishi imekuwa kubwa na hakuna ufisadi. Ni katika nyakati hizi tulikuwa tukielezwa uadilifu na nidhamu kwa watumishi ni mkubwa sana.

Hasara hiyo iliyotokana na mchakato wa kubadili noti chakavu ambapo ni mtandao wa wafanyakazi sita wasio waadilifu ndani ya benki kuu ya Tanzania (BOT) ndiyo waliohusika na mchezo huo haramu uliofanyika kati ya Januari 2017 hadi Desemba 2019.

Noti chakavu ni noti halisi yenye kukosa sifa za kufanya malipo halali. BoT ilipokea noti TZS bilioni 4.17 ili zitolewe noti mpya. Ni utaratibu wa kawaida wa benki kuu, kupokea fedha chakavu.

Katika ukaguzi huo wa (CAG) ilibainika, Noti 1,427 zenye thamani ya TZS milioni 14.27 zilikuwa safi na zinafaa kwa matumizi, noti zenye thamani ya TZS 161.87 milioni zilikuwa chakavu, noti 399,392 zenye thamani ya TZS bilioni 3.99 hazikuwa na vigezo vya kupewa noti mpya na zilipewa noti mpya kwa njia ya udanganyifu.

Udanganyifu huo uliofanywa na maofisa wawili na watunza fedha wanne wa Benki kuu ya Tanzania (BoT), ikiwemo kukata vipande vya noti ya Shs 10,000 ili wapate noti mpya, na pia kutohifadhi daftari la wateja waliokuwa wanabadilisha fedha chakavu katika benki kuu ya Tanzania.

Yaani watumishi wa benki ya Tanzania wakapoteza ushahidi. Maharamia hao waliamua kupoteza nyaraka halali za serikali ili kuficha uhalifu wao. Watumishi hao walifanya kazi wakati wa JPM na Gavana wa BoT alikuwa mteule wa JPM, Glorious Luoga.

Na katika kitabu cha mahudhurio (Attendance Register) ya wateja kuna wateja 24 waliokuwa wakifika katika benki kuu ya Tanzania (BoT) mara kwa mara kwa ajili ya kufanya miamala ya noti chakavu, na wao wamehusishwa katika mtandao huo (genge la Uhalifu) katika kushirikiana na wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutekeleza mpango huo.

Siyo hoja yangu kusema JPM alihusika na ufisadi huo moja kwa moja. Hapana. Nataka kusema, alifanikiwa kwa kiwango kikubwa kuwafanya watumishi wa umma kuwa na nidhamu ua woga tu. Waliiba na kupora hadi benki kuu. JPM alikuwa na wapambe tu ambao walimfichia 'White'. Hawakumueleza ukweli.

Mambo hayo ya kukosoa ufisadi huo yangefanyika na wanasiasa katika mikutano yao ya hadhara au katika michango ya wabunge bungeni. Hilo halikuwezekana. JPM alifanikiwa kulifanya bunge kuwa chombo chake cha pongezi. Nje akazuia shughuli za kujadiliana majukwaani. Watu wakawa mateka.

JPM akiwa Singida, July 2016 alizuia shughuli za mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa. JPM alikuwa Alpha na Omega. Kitu ambacho aliamua hakuna wa kupinga. Akitokea wa kupinga angelionyeshwa shimo la kaburi lake.

Wakati JPM anapiga marufuku mikutano ya hadhara alisema “mimi (Rais) pekee ndiye natakiwa kuzunguka nchi nzima kila jimbo kufikisha maendeleo niliyowahidi watanzania wote. Wengine kama umechaguliwa fanya mkutano jimboni kwako”.

CHADEMA walikuwa wameandaa maandamano ya UKUTA 01.09.2016, siku hiyo Singida JPM akawaeleza wananchi "wanaotaka kuandamana au kufanya mikutano kiholela kwanini wanasubiri mwezi wa 9? Wafanye hata leo wajue mimi ni nani. Siwezi kugeuza nchi hii ya siasa, nataka nchi ya maendeleo tu. Siasa zikekwisha wakati wa kampeni, muda huu ni kazi tu"

Roho mbaya, chuki na wivu? Hii inaweza kuwa tafsiri halisi kwa the jinsi JPM alimfanya Freeman Mbowe. Club Billicanas ilivunjwa. Shamba la Green House Hai likaharibiwa. Akaunti zake za kifedha zikafungwa. Freeman akashtakiwa kwamba kasabaisha kifo cha Akwilina. kesi hii ilimuweka gerezani FAM miezi 4.

Akwilina ambaye alikuwa ndani ya daladala akitoka chuo cha usafirishaji (NIT) kwenda nyumbani, risasi ya Polisi ikamfuata, na kumuua, kesi akapewa Freeman Mbowe na wenzake, wakahukumiwa kwenda gerezani au kulipa faini ya Sh.350 milioni. Wananchi tulichanga fedha hizo za kulipa faini.

JPM alipofariki, Mahakama Kuu, ikabatilisha hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kesi ya Jinai iliyokuwa ikimkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake 7 na kuamuru warejeshewe fedha walizolipa kama faini, kiasi cha TZS 350 milioni. Uamuzi huo ulitolewa 25.07.2021 na Jaji Irvin Mgeta.

Tumesahau haraka hivi? Ni JPM alimueleza Spika Job Ndugai kwamba huko bungeni awashughulikie wabunge wa upinzani, wasiseme au kukosoa serikali yake, na awatoe awatupe nje, na huku nje watamkuta, atawashughulikia. Kwanini sasa leo tusiseme JPM alistahili kuwepo miaka 20 iliyopita? CHUKI!

Ukurasa wa 34 katika ripoti ya CAG kwa ripoti kuu ya Serikali Kuu 2016/2017 unasomeka hivi: “Kati ya shilingi bilioni 25,307.48 zilizokusanywa, shilingi bilioni 23,792.30 zilitolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi, matumizi mengine, matumizi ya maendeleo na fedha kwa ajili ya kulipa madeni yatokanayo na amana za Serikali pamoja na riba.”

CAG anatuambia kuwa serikali ya Magufuli, inayojinasibu siku zote kuwa ni serikali ya wanyonge, ilikusanya TZS bilioni 25,307.48 kutoka vyanzo vyote vya mapato, misaada, mikopo na kutumia TZS bilioni 23,792.30 katika matumizi yake kwa bajeti ya mwaka 2016/2017.

Maana yake, na kwa hesabu rahisi, ni kuwa katika pesa zote zilizokusanywa na kutimiwa (TZS 25,307.48-23,792.30 = 1,515.18) zaidi ya shilingi za Kitanzania trilioni 1.5 haikutumika na haileweki sehemu ilipo mpaka ukaguzi unamalizika na ripoti kutolewa kwa umma.

JPM ametusaidia sana wanasiasa wa upinzani. Sasa tumefahamu umuhimu wa kuondokana na katiba hii mbovu inayompa mamlaka ya kikatili Rais. Ni lazima tupate katiba inayoendana na matakwa ya umma katika mfumo wa kisiasa wa vyama vingi na siyo Rais. Katiba mpya ni muhimu sasa.

Mwenyekiti wa UVCCM wakati fulani, Heri James alisema Jukwaani kwamba wao (CCM) ndiyo wanaamua wapi wapeleka maendeleo na wapi wasipeleke na wasipopeleka hakuna kitu watafanywa na yeyote. Hili lilipaswa kukemewa na JPM kama kweli siyo kweli. Lakini ndiyo ulikuwa mtazamo wa JPM.

JPM ametusaidia sasa tunafahamu kwamba kuna wanasiasa wanafiki, waongo na wazandiki katika siasa za nchi yetu, ambao wapo tayari kuuza UTU wao, kwa watawala ili watimize haja ya nafsi na matamanio yao. Wanapenda kuwa na vyeo bila kujali mahitaji ya wananchi. Wabinafsi.

JPM ametusaidia kuwafahamu ‘political mercenaries’ ambao Mwalimu Nyerere alisema tuwatambue kwa jina la “Malaya wa kisiasa”. Wanayo bei. Wanajiuza. Hawana uvumilivu na hawa ndiyo wengi walihamia CCM wakisema wanaunga mkono juhudi za Rais. Hii ni shukrani kwa JPM .

Wafanyabiashara, ambao walikuwa ni tabaka kubwa linalounga na kufadhili shughuli za CCM, waliguswa, Walipewa mashtaka ya uhujumu uchumi, walifilisiwa. Hili ni moja kati ya makundi yaliyoguswa moja kwa moja. Hata wavuvi waliona moto. Nenda Chato, waulize wavuvi, JPM safi??

JPM ametuonyesha kwamba kwa katiba hii ukiwa na wapambe wengi bungeni, unaweza kuamua kujiongezea muda wa kubaki madarakani kisheria kabisa kwa Bunge kupitisha mabadiliko ys sheria na kuondoa ukomo wa muhula na Muda wa kuwa Rais. Tulianza kusikia minong'ono na vitendo.

JPM kwa muda wa miaka 5 na miezi 5 tu, alitufungua jicho, tulipaswa kuwa naye kwa miaka 20 kabla ili atusaidie kuwafungua watu akili, macho, masikio. Alituonesha mkono wa chuma ukiwa madarakani, tusirudi huko, tuitengeneze katiba ya nchi yetu, asipatikane Magufuli mwingine, mwanamke au mwanaume.

MMM, Martin Maranja Masese

Chanzo; Mtandao wa X
 
Huyu hamna kitu , ukitaka kujua hamna kitu weka ubaya wa Mbowe katika Chama chake

Hivyo huyu ni Chawa wa Mbowe kama walivyo Chawa wa Mama huko CCM
 
Wewe unayesubiri kufa kwa nini unahangaika na mtu aliyekwishakufa miaka mltatu iliyopita?
 
Wakati Rais wa awamu ya tano hayati Magufuli akitangaza kwamba Tanzania inaenda kutekeleza mradi wa kufua umeme wa bwawa la mwl nyerere kwa gharama yoyote bila kuangalia makunyanzi ya mtu yoyote, kuna watanzania wenzetu walipinga mradi huo na kutusaliti kwa wazungu ili mradi huo ukwame!.
Mungu saidia Magufuli hakulegeza kamba wala kukata tamaa na mradi huo ukaendelea na sasa umekamilika na mashine moja imefungwa hivyo kupelekea kupungua kwa kiasi kikubwa kwa mgao wa umeme uliokuwa unatesa wananchi na kuuwa uchumi wa nchi yetu.

Sasa ili kukomesha tabia ya watanzania wenzetu kusaliti na pia ili kuongeza uzalendo kwa nchi yetu wanasiasa waliohamasisha wananchi kupinga mradi huo wasiruhusiwe kutumia umeme kutoka bwawa la mwl nyerere.

Wanasiasa hao ni Tundu Lisu, Nape Nnauye, January Makamba, God bless Lema, John Heche, Freeman Mbowe, Sugu, Peter Msigwa, Martin Maranja Masese. Na wengine wengi ambao tutaendelea kuwataja.
 
Mimi msomaji sana lakini nimeshindwa kumaliza.
Lakini ni kwamba unajisumbua kabisa kumlaumu Magufuli.Tatizo ni kwamba sisi watumishi wa umma tuliobaki tumeshindwa kufikia viwango alivyoviacha.
Kwa kifupi ni kwamba unajisumbua kabisa kumlaumu Magufuli.Tatizo ni kwamba sisi watumi
 
Back
Top Bottom