Kumuenzi Magufuli: Tujikumbushe 'spana' za JF zilivyomsaidia Hayati Magufuli na Taifa. Je, Samia pia tumsaidie kwa 'spana' au tumkune tu tusimpare?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
51,023
115,153
Wanabodi,

Leo siku ya Machi 17 ndio siku Taifa tulipotangaziwa kifo cha Shujaa wetu JPM, hivyo katika kumkumbuka, na kumuenzi, mnaonaje tukijikumbusha baadhi ya mabandiko ambayo tulimshauri JPM na ushauri huo ukafanyiwa kazi, kwa kutaja bandiko husika, ulishauri nini, na nini kilikuja kufanyika kwa ushauri huo, na jee kulimsaidia JPM? na kulisaidia taifa?

Kwa vile JPM alikuwa ni mbabe kwa kufanya baadhi ya mambo kibabe, hadi kutafsiriwa ni dikiteta, hivyo baadhi ya ushauri kwa JPM pia ulitolewa kibabe kwa kumpiga spana za kutosha, ila tukubali tukatae, baadhi ya spana za JF zilimsaidia sana JPM na kulisaidia sana taifa!.

Kumuenzi JPM, naomba tujikumbushe baadhi ya mabandiko, tuliwahi kushauri nini kwa kuandika nini na kutoa ushauri wa nini kifanyike, na kufuatia ushauri huo, nini kilifanyika na jee kilimsaidia JPM? kilimsaidia kivipi?. Jee kililisaidia taifa?, kililisaidia kivipi?
 1. Naanza na bandiko hili la August 2014 kutangaza ujio wa JPM nikieleza kwanini ni JPM Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli bandiko hili liliwaandaa Watanzania kwa 2015 with what to expect kwa JPM, hivyo ilipokuja kutokea kweli, it was not a surprise.
 2. Elections 2015 - Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo, Vunja Kambi, Jisalimishe! kwa vile uteuzi wa Magufuli uliwaumiza watu ya kambi ya Lowassa, hapa niliwashauri wavunje kambi na kukubali matokeo.
 3. ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!, Tushukuru Kwa Yote!, Life Goes On!. baada tuu ya uchaguzi, bandiko hili lilisaidia sana kuwapooza watu.
 4. Kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi Mkuu wa 2015 nikapandisha bandiko hili Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him! lilisaidia sana kuandaa watu kisaikolojia
 5. Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!, hapa tulimshauri kuifuta katiba na kutawala kwa kutumia presidential decrees. Hapa ni baada ya JPM kuifuta predicts ya Uhuru kwa tamko tuu la mdomo, Bandiko hili liliwaibua watendaji wa Ikulu wakaandaa a decree ikawa backdated na kutolewa 3 days later. Hivyo bandiko hili limeisaidia serikali.
 6. Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake! hapa nimetoa angalizo muhimu la karma kwa serikali yetu, na it's consequences
 7. Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote bandiko hili limesaidia kutujulisha Watanzania kuwa Rais wa JMT akiamua, anauwezo wa kufanya chochote regardless ya katiba, sheria, taratibu na kanuni. Rais wa JMT hapangi mishahara ya watumishi wa umma, na kwa majibu wa kanuni, mshahara ukiishapangwa na kulipwa kwa kipindi cha miezi 3 mfululizo, hauwezi kupunguzwa unaweza tuu kuongezwa!. Huyu jamaa aliweza kupunguza!. Mpaka leo sijui alitumia sheria gani, kanuni gani na taratibu gani kuipunguza mishahara, hivyo aliipunguza!. Bandiko hili japo halikusaidia kitu lakini limetujulisha kuwa rais wa JMT ana inherent powers to do anything!.
 8. Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa kiuchumi? bandiko hili lilisaidia sana kuyarekebisha hayo yaliyozungumzwa humo hivyo kumsaidia na kulisaidia taifa.
 9. Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki 'Separation of Powers'? bandiko hili limesaidia sana, baada ya bandiko hili, safari za mhimili wa Mahakama zilipitia kwa CJ na zile za Bunge kwa Spika,, majina yalipelekwa Ikulu for procedures tuu na sio kuomba kibali!.
 10. Pongezi Dkt. Magufuli kutenganisha shughuli za Chama na Serikali, Utabarikiwa na Tanzania itabarikiwa! baada ya bandiko hili, vikao vya CCM ikulu vilisitishwa sasa vikawa vinafanyika CCM Lumumba.
 11. Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya Woga, Kutasaidia?!. bandiko hili lilisaidia sana, zile ziara za ku terrorised zilikoma.
 12. Hii Tumbua Tumbua ya Rais Magufuli, Hivi Kikwete Anajisikiaje?!. Anajisikia Sifa Au Anajuta?!.
 13. Je, Kila utumbuaji ni wa haki, au kuna kumkomoa Kikwete?!
 14. Je, inawezekana huu ndio mwisho wa utumbuaji wa papara na kukurupuka?! Mkuu kutumbuliwa soon! uzi huu ulisaidia kupunguza utumbuaji wa papara
 15. Could There Be A Double Standards Kwa Viongozi Wadanganyifu?!. Wengine Fired, na Wengine Spared?!. bandiko hili limesaidia kupunguza double standards kwenye utumbuaji.
 16. Kanda ya Ziwa na kuongea kwa ukali: Ukali wa Rais Magufuli ni asili tuu ya wasukuma, sio udikteta! bandiko hili limesaidia kumuona Blaza ni mkali sana.
 17. Je, huu sio uvunjaji wa haki za msingi za binadamu unaofanywa na serikali ya Magufuli?
 18. Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020? bandiko hili lilisaidia sana kujua uchaguzi Mkuu wa 2020 utakuwaje, hivyo matokeo ya uchaguzi wa 2020 hayakuwa a surprise.
 19. Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! . bandiko hili liliwasaidia wasaidizi wa rais kutimiza wajibu wao.
 20. Je, aachwe aseme tu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara? bandiko hili lilimuelezea kiongozi wetu kama ni msema chochote, lilisaidia kumbadilisha na wale waalimu 4 liliowateua walianza kutimiza wajibu wao kikamilifu.
 21. Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni Yake au ni ya Wale Wazee wa..?!. bandiko hili lilimuibua Waziri wa Afya kumuweka sawa bosi wake kuwa kauli hiyo ilikuwa ni ya Utani tuu kwa watani zake Wazaramo.
 22. Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila... bandiko hili lilimfanya Mkuu akawa anasikiliza ushauri wa wasaidizi wake.
 23. Je, maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu au vitu? Wachumi tusaidieni, uchumi wa Awamu ya 5, unalisaidia Taifa au utaliangamiza? hapa tulizungumzia maendeleo ya watu na vitu
 24. Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows! bandiko hili lilisaidia sana kuachana na maigizo ya ziara za kushtukiza. Baada ya bandiko hili hakukutokea tena maigizo ya ziara za kushtukiza
 25. Tuache Siasa ktk Uchumi: Wachumi tuelimisheni Dhambi ya Fixed Deposit na Faida ya Fedha Kukaa tu BoT bandiko hili lilisaidia taasisi za umma kuruhusiwa kuendelea kutumia mabenki ya kibiashara.
 26. Tusikalie kumlaumu tu Rais Magufuli na Serikali yake wanapofanya mabaya, kwenye mazuri pia tupongeze! bandiko hili limesaidia sana kuonyesha the human part of JPM, kuna watu kazi yao ni kulaumu tuu, kulalamika na kuangazia mabaya tuu na madhaifu mazuri hawakuoni.
 27. Magufuli is getting better and better, he is changing for the better. Hongera sana! kuna watu walimdhania Rais Magufuli ni static, bandiko hili limesaidia kuowaonyesha watu JPM alikuwa dynamic changing for the better.
 28. Magufuli is Doing Good For This Nation, Tumuassess kwa Positive Attitude, Kwa Mazuri Tumpongeze, Tumuunge Mkono Kumsupport, lakini kwa Mabaya Tumkosoe Luna watu wanaangalia mabaya tuu na negativity, mazuri na vitu positive hawaoni!, bandiko hili limewasaidia changing mind set zao na kumuangalia JPM with a positive attitude.
 29. Kiukweli nimeguswa sana na uchapakazi wa Rais Magufuli!. Je, kuna uhusiano kati ya kabila la mtu, na uchapakazi wake?. Je, 2020 kuna haja ya... bandiko hili limetusaidia kuangazia uchapakazi wa viongozi wetu kutokana na makabila yao.
 30. Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli bandiko hili ni darasa la ukosoaji ambalo limesaidia sana jinsi ya kumkosoa Mkuu wa nchi na ukabaki salama.
 31. Magufuli ni Rais wetu, asiabudiwe, asiogopwe, bali aheshimiwe kuna watu walimuogopa JPM mpaka kama kutaka kumuabudu!. Hivyo bandiko hili limesaidia kujilisha JPM ni human being aheshimiwe, asiabudowe.
 32. Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio Mungu! Na Kwenye Utawala ni Katiba! hapa ni kuzuia JPM asiabudiwe.
 33. Kati ya wakosoaji wa Rais Magufuli na Serikali yake, na wasifiaji nani wanamsaidia zaidi? Ijue nafasi ya JamiiForums bandiko hili limesaidia kuelimisha umma kuwa kati ya wasifiaji na wakosoaji, wanaomsaidia zaidi zaidi rais ni wakosoaji na sio wasifiaji.
 34. Magufuli kama Nyerere: Ni mtu wa watu, hapapasi, hamung'unyi, ni kazi tuu, ila pia sio kama Nyerere! bandiko hili limesaidia kumuona JPM kama Nyerere fulani hivi hivyo kumfanya akubalike zaidi.
 35. Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti huyu, ana hoja ya Msingi! bandiko hili limesaidia hadi Mzee Baba akasema ataleta Salary Slip yake!.
 36. Thinking Aloud: Hongera JF kulisaidia Taifa, "Atakuwa anaingia JF in person na kutusoma!". 2021 let's be more responsible, more strategic hapa ni kuwajulisha wana JF kuwa Blaza alikuwa anaingia mwenyewe humu JF na kutusoma. Ile siku amemtumbua Nape, saa 5:51 usiku kuna mtu nikapandisha bandiko Mwakiembe amegomea uteuzi. Bandiko lile likafutwa saa 6:29 usiku!. Kesho yake baada ya kumwapisha Mwakyembe, akamuita kuzungumza kidogo ili waliosema amegoma washushuke!.
 37. Magufuli amecapture attention ya Watanzania, Watu wako makini na shauku ya leo anatumbuliwa nani?!.
 38. Hakika Pasco alikuwa sahihi kuhusu Magufuli
 39. Udikiteta ni dhana tu au ni real? Lets call a spade a spade. Dikteta ni mtu mwenye tabia hizi
 40. Kauli huumba! Je, ni kweli Magufuli ni dikiteta? Kama ni kweli, ni kosa la nani kati yake na aliyetoa kauli hii?
 41. Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia!. Akishika Chama, Watakoma
 42. Nimetishwa, kushitushwa na kuogopeshwa na kauli hii ya Rais Magufuli. Alimaanisha nini?
 43. Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?!
 44. Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya Kujenga Nidhamu au Udikiteta Tuu?!.
 45. Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A ...
 46. Magufuli amecapture attention ya Watanzania, Watu wako makini na ...
 47. Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha Upinzani ...
 48. Kama Magufuli Anaangalia Clouds TV na Kuipongeza, Kunatuma Ujumbe ...
 49. Baraza Jipya: Pongezi kwa JamiiForums, WanaJF watatu(VERIFIED ...
 50. Rais Magufuli na serikali yake wakosolewe kwa hoja sio kwa viroja - Jicho letu, Star TV bandiko hili limetufundisha ukosoaji kwa hoja.
 51. Kama kikokotoo kipya ni matokeo ya actuarial valuation ya mifuko, kosa la Irene Isaka ni lipi hadi atumbuliwe? Tusishangilie tuu...mwishowe...
 52. Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi
 53. Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...
 54. Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade ...
 55. Kutoonyesha Hisia/Huruma wala pole za sauti si Udikteta bali ni ...
 56. Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili ...
 57. Gwiji wa Sheria na Katiba, Prof. Issa Shivji, Agoma Kuzungumzia
 58. Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu
 59. UDIKTETA: Hongera Sana TWAWEZA, TZ hakuna Udikteta! Ila
 60. https://www.jamiiforums.com/threads/pongezi-rais-magufuli-na-awamu-yake-ya-tano-wafanya-maajabu-vita-dhidi-ya-umasikini-tanzania-yaongoza-dunia-kupunguza-umasikini-uliotopea-wb.1671617/
 61. Kwa Uamuzi Huu, Pongezi Sana Rais Wetu Magufuli, Utabarikiwa na Mungu, na Taifa Pia Litabarikiwa!
 62. Tusikalie kumlaumu tu Rais Magufuli na Serikali yake wanapofanya mabaya, kwenye mazuri pia tupongeze!
 63. Pongezi Rais Magufuli na Awamu Yake ya Tano, Wafanya Maajabu Vita Dhidi ya Umasikini, Tanzania Yaongoza Dunia Kupunguza Umasikini Uliotopea-WB.
 64. "Pongezi Rais Magufuli Kuwa Mkweli Daima. Tuanzishe Church of Africa, Tuoe Wake Wengi, Tuzae Watoto Wengi?"
 65. Magufuli kama Nyerere: Ni mtu wa watu, hapapasi, hamung'unyi, ni kazi tuu, ila pia sio kama Nyerere!
 66. Pongezi kwa Rais Magufuli Kusitisha Bomoa Bomoa Kwa Kuongeza Kigezo Cha "Human Face" He's So Human!
 67. Magufuli is getting better and better, he is changing for the better. Hongera sana!
 68. Pongezi Rais Magufuli. Ameonesha uzalendo wa hali ya juu uliotukuka!, amebadilika, amejishusha, uchumi wa Tz kupaa!
 69. Life After Life: Je, wajua Magufuli huko alipo anayaona yote? Je, tuendeleze 'double standards' ya 'cherry picking' au tuiachie Karma iwashughulikie? kuna watu wanadhani kwa vile JPM ametangulia, that is the end of him!, hawajui kuwa there is life after life, JPM yupo na anayaona yote!.

Na mwisho kwa vile sasa Samia ndie Rais wetu, JF tunapaswa kuendelea kutimiza wajibu wetu kwa jamii kwa kumsaidia Samia, awasaidie Watanzania.

Kwa vile JPM alikuwa ni rais mbabe vivyo hivyo ushauri ulitolewa kibabe, lakini Samia ni rais mtaratibu, muungwana na mstaarabu kama Mwarabu, jee licha ya utaratibu, uugwana na ustaarabu wake, jee huyu Mama naye tumpige spana za kutosha kama za JPM? au huyu mama twende naye taratibu kama alivyo, kwa Mama iwe ni kumkuna tuu, na tusimpare kama alivyo shauri mwenyewe, kuwa ukinikuna vizuri nitakukuna ila ukinipara, nitakuparua?

Mabandiko mengi ya kuwakumbuka marehemu huishia kwa RIP kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi kwavile wanakuwa hawajui marehemu yuko wapi,, lakini mimi kwa vile tayari nimeisha kulishwa JPM yuko wapi Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani bado kuna haja ya kuendelea kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi huku tayari najua yuko peponi?.

Pumzika Magufuli Pumzika! Tutakukumbuka Daima!, na sasa tushughulike na Mama, na sio tumshughulikie!.

Paskali!
 
Wakati mwingine huwa nafikiri hamjui who is raisi Samia, jibu la hilo swali lingewasaidia kuelewa mlipo na mnapoenda kama nchi, …
 
Back
Top Bottom