Dilemma ya kumpenda mwanamke mwenye mtoto

Dilemma ya kumpenda mwanamke mwenye mtoto

Mmh aisee..
Mbona hii ni hatari sana ndugu yangu?

Ilikuwaje na hatma yako na yule mwanamke ili ishaje?

Kuna mtu juu kule alicomment kuwa ukioa singo mama unakuwa umeingia kwenye familia nyingine na ninaona kabisa point yake kupitia stori yako.

Duh kweli ni changamoto mkuu, je uliacha a na yule mwanamke? Au ulitafuta mbinu ya kukabili hiyo changamoto?
Tokea mwanzo wa Dunia hakuna suluhu ya hilo jambo tofauti na kujivua gamba na kutafuta mwanamke asie na mtoto.

Kwa sababu mwanzoni atakuwa anakuunga mkono anawalaumu pia ila kadri siku zinavyo enda hasa hutumika kipengele cha mtoto anaumwa au kapata tatizo fulani, lazima mama wa mtoto aende maana huyo ni mwanae ana uchungu nae pia, akienda lazima akutane na baba wa mtoto na mashangazi na mawifi. Atashauriwa sanaaa hata kama ana moyo wa chuma lazima yamuingie.

Akirudi mnaanza kugombana nyie kwa nyie na atakuambia live una roho mbaya unachukia mtoto wake, atakuambia una wivu sana, atakuambia baba wa mtoto wake kabadilika kawa mwema kwa sasa.

Anyway niishie hapo utajua mwenyewe bwana
 
Wanabodi..

Ni heri mmeamka salama kwenda kuyakabiri majukumu ya siku hii ya leo.

Ningelipenda kuwasumbua kidogo. Je hii ni sawa au nataka kuingia kwenye mtego?

Kuna binti nimetokea kumpenda sana, ila bahati mbaya ama nzuri tayari ana mtoto Au amezaa na mtu mwingine.

Binafsi nimependezwa naye katika kila angle, na niko radhi kulea mtoto wake na kumpenda maana ukipenda boga huna obligation ya kulipenda pia uwa lake.

Naona kabisa yeye kuwa na mwanae sio tatizo kwangu, ila nimekuwa Niki Sikia kuwa kupenda singo mama ni kujichimbia kaburi mapema, ila mbona anaheshima, ni mstaarabu ana utii na mwerevu?

Je, eti kisa watu wanasema kuwa single mama ni vichomi na mimi niache mtu ni naye mpenda kwa dhati?

Je, niko delusional ama ni ufwate moyo wangu? Na wenye experience Naombeni uzoefu ndugu zangu.

Asanteni.
Huna akili.
 
Hahaha, aisee ila mapenzi bwana, kwanini yawatese watu namna hii?
Kuna jambo huliewi, mwanamke anapozaa na mwanaume tayari kuna damu zimeungana na hilo agano ambalo hudumu muda wote, ndio maana sio rahisi kwa mwanamke kumsahau mwanaume aliyezaa naye hata kama kuna ugomvi mkubwa wa kutoana roho, kusahau ni ngumu.

Katika mazingira hayo ya kutosahau mwanamke hujikuta anakuwa mrahisi pale mzazi mwenzake anamhitaji ndipo mgogoro unapoanza, ndio maana inashauriwa Mwanamke aolewe na aliyemzalisha au Lah asikimbilie kuzaa haraka kama hana uhakika na huyo mwanaume.

Ndio maana wajumbe wamekushauri kuwa fuata moyo wako
 
Au sio, nenda tu Mkuu ila ipo siku huko mbeleni hata miaka 10 huko utakumbuka majina ya ID zote zilizokushauri katika huu uzi.



Kwa kifupi ukishakuwa nae karibu itafika mahala baba wa mtoto wake huwa anaibuka na kutaka kuwa nae karibu pia, ndugu za baba wa mme wake huibuka na kumsonga au kumjali zaidi kwa kumshirikisha mambo mbalimbali mazuri juu yake na mtoto wake, utasikia tunataka kumkatia mtoto Bima ya Afya, tunataka kumnunulia kiwanja kwa jina lake, tunataka kufanya hiki na kile hapo ndio utaanza kuona anaanza kuwaelewa na kubadilika na ww utaona husikilizwi tayari mgogoro.

Nimewah kuwa na singo maza na mtoto wake bahati nzuri alikuwa kwa mama wa baba walie zaa nae,

Gues what walipohisi ana mtu, huyo mama mkwe akipiga simu ni maongezi ya masaa 2, kule mtoto kila dakika wanajaza vocha kwenye simu na kumlazimisha aongee na mama yake.


Yani akinywa chai simu, akimeza chai simu, akivaa nguo simu, akicheka simu, akitoka na wenzie simu simu simu simu simu simu...


Wakimaliza baba mtu ulieambiwa walikosana nae anaanza nae, akiblokiwa huku anaibukia kule na akiibuka anamwambia nataka tujadili hatma ya mtoto..😀😀😀😀😀😀
😅😅😅
 
Vitu vingine fanya research mwenyewe
Kabla hujapata ushauri kutoka kwa watu wenye trauma na single mother

But kwenye wengi kuna mengi fatilia comment halafu changanya na za kwako kila la kheri

Halafu hapo unaposema upo tayari kumlea mtoto kwani baba ake yupo wapi?


Hii ni point kubwa.

Hilo swali yeye mwenyewe angetakiwa amuulize huyo dada nani atakuwa na wajibu wa kumlea huyo mtoto.
Jibu la binti litaonyesha future ya hiyo ndoa yao.

Binti lazima aseme wazi kwamba jukumu na wajibu wa kumtunza huyo mtoto ni la Baba mzazi na yeye(mwanamke) na sio la huyo mtoa mada.
Ingawake mtoa mada afanye kwa hiyari. Binti akisema hivi ninampa 20% ya mwanamke mzuri.

Lakini mambo ya kupenda boga sijui ua ni kuyafanya mapenzi kama Msalaba wa Yesu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom