Au sio, nenda tu Mkuu ila ipo siku huko mbeleni hata miaka 10 huko utakumbuka majina ya ID zote zilizokushauri katika huu uzi.
Kwa kifupi ukishakuwa nae karibu itafika mahala baba wa mtoto wake huwa anaibuka na kutaka kuwa nae karibu pia, ndugu za baba wa mme wake huibuka na kumsonga au kumjali zaidi kwa kumshirikisha mambo mbalimbali mazuri juu yake na mtoto wake, utasikia tunataka kumkatia mtoto Bima ya Afya, tunataka kumnunulia kiwanja kwa jina lake, tunataka kufanya hiki na kile hapo ndio utaanza kuona anaanza kuwaelewa na kubadilika na ww utaona husikilizwi tayari mgogoro.
Nimewah kuwa na singo maza na mtoto wake bahati nzuri alikuwa kwa mama wa baba walie zaa nae,
Gues what walipohisi ana mtu, huyo mama mkwe akipiga simu ni maongezi ya masaa 2, kule mtoto kila dakika wanajaza vocha kwenye simu na kumlazimisha aongee na mama yake.
Yani akinywa chai simu, akimeza chai simu, akivaa nguo simu, akicheka simu, akitoka na wenzie simu simu simu simu simu simu...
Wakimaliza baba mtu ulieambiwa walikosana nae anaanza nae, akiblokiwa huku anaibukia kule na akiibuka anamwambia nataka tujadili hatma ya mtoto..😀😀😀😀😀😀